BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

Sensa ya mwaka 1957 ya kikoloni kipengele cha kuonesha dini kilikuwepo na ndio kinachoonesha takwimu waislamu wangapi na wakristo wangapi, na ukiangalia mwaka huo 1957 waislamu walikuwa ni 65%.

Baada ya hapo sensa zote zilizofuata kipengele cha dini kilifutwa; ajabu leo hii watu wanasema wakristo wapo wengi kuliko waislamu kwa takwimu zipi ikiwa kipengele cha kuorodhesha watu dini zao hakipo.

Pili ni kwanini wanaogopa kuhesabu watu kwa kutumia kigezo cha dini? Wengi watasema wanaogopa udini, hii hoja ni dhaifu maana nchi nyingi duniani sensa zinahebabiwa kwa mtindo wakujua idadi ya watu na dini zao ni asilimia ngapi katika nchi hizo.
Kwani hata waislamu wangekuwa 99% ina implication gani kwa maendeleo ya taifa? Itasaidia kujenga shule zaidi, hospitali, maji safi, barabara umeme, n.k?

Mbona watanzania mnaacha kufuatilia na kushuguligikia mambo ya maana mnakeshea ujinga? Sasa hivi tulitakiwa tunaumiza kwa miaka 50 ya uhuru wetu mbona hali inazidi kuwa duni? Kwa rasilimali tulizo nazo madini, ardhi, watu, maji, bahari, milima mbuga za wanyama, amani, maziwa, mito hali nzuri ya hewa mbona umaskini unatumaliza! Mnakalia kutokwa mishipa ya shingo kutaka kujua waislamu na wakristu wepi wengi!! Au mnataka kutangaza taifa la kiislamu muwafukuze wakristu?

Mtanzania amka, umaskini, magonjwa, ujinga havichagui dini hata mnekuwa waislamu peke yenu isingewasaidia!!
 
Hivi katika nchi hii, dini zinazotambulika kisheria ni uislamu na ukristo? kwa nini dini nyingine hazizungmziwi hapa,mfano dini za kimila sijasikia zikizungumziwa kabisa.

Niliwahi kwenda Polisi, katika kuandikisha malezo yangu nikaulizwa dini yangu, nikajibu kuwa sina dini, mimi ni mpagani, lakini yule askari alilazimisha kwamba lazima nina dini, baada ya kubishana sana akaniuliza dini ya wazazi wangu nikamwambia nao hawana dini, yule askari akasema haiwezekani na mwishowe akanipachika dini ambayo si yangu...
 
Tukimaliza kuhesabu Waislam, watasema tuhesabu na wasiosali swala tano, wasiofunga mwezi Mtukufu, wasiovaa hijab, wenye wake wawili, n.k. Hii ni kwa sababu ikiwa mtu unang'ang'ania kipengele cha dini katika sensa, ina maana unataka kufanya mipango fulani iendane na jinsi watu walivyo waaminifu katika dini yao.

Jamani hawa wananifanya nijione siko Tanzania!

Hoja wa dini fulani kuwa inataja idadi ya waumini wake ni ya kitoto kwa sababu kuna baadhi ya madhehebu yana utaratibu wake wa kufanya sensa ya waumini wake.
 
Wengi mnapindisha pindisha! Lakini lengo kuu la kujua idadi yao ni kutaka kuibadili nchi iwe ya kiislamu, wakishajua idadi yao wataanzisha lingine la kutaka ipigwe kura ya kutaka nchi iwe ya kiislamu au la na hapo ndiyo katiba mpya inafuata. Mark my words!!
 
Baada ya kujua idadi ya wana imani fulan!, nini kitafata?
 
Sensa ya mwaka 1957 ya kikoloni kipengele cha kuonesha dini kilikuwepo na ndio kinachoonesha takwimu waislamu wangapi na wakristo wangapi, na ukiangalia mwaka huo 1957 waislamu walikuwa ni 65%.

Baada ya hapo sensa zote zilizofuata kipengele cha dini kilifutwa; ajabu leo hii watu wanasema wakristo wapo wengi kuliko waislamu kwa takwimu zipi ikiwa kipengele cha kuorodhesha watu dini zao hakipo.

Pili ni kwanini wanaogopa kuhesabu watu kwa kutumia kigezo cha dini? Wengi watasema wanaogopa udini, hii hoja ni dhaifu maana nchi nyingi duniani sensa zinahebabiwa kwa mtindo wakujua idadi ya watu na dini zao ni asilimia ngapi katika nchi hizo.
Hujasoma majibu ya NBS kwenye hii hoja nadhani.

Yanasema hivi 'serikali haiwezi kuweka vipengele vya kabila na udini katika sensa kwa sababu haipangi mipango yake ya maendeleo kwa kufuata vipengele hivyo'

...Hivi kuna busara kubwa zaidi ya hii jamani? Kenya wanauana hapa kila siku kisa ukabila tu na upuuzi... kwanini tunatamani kujenga utengano kati yetu!??
 
Sensa ya mwaka 1957 ya kikoloni kipengele cha kuonesha dini kilikuwepo na ndio kinachoonesha takwimu waislamu wangapi na wakristo wangapi, na ukiangalia mwaka huo 1957 waislamu walikuwa ni 65%.

Baada ya hapo sensa zote zilizofuata kipengele cha dini kilifutwa; ajabu leo hii watu wanasema wakristo wapo wengi kuliko waislamu kwa takwimu zipi ikiwa kipengele cha kuorodhesha watu dini zao hakipo.

Pili ni kwanini wanaogopa kuhesabu watu kwa kutumia kigezo cha dini? Wengi watasema wanaogopa udini, hii hoja ni dhaifu maana nchi nyingi duniani sensa zinahebabiwa kwa mtindo wakujua idadi ya watu na dini zao ni asilimia ngapi katika nchi hizo.
hivi hamwezi kuhesabiana ninyi kwa ninyi? mbona kila kanisa linajua lina waumini wangapi active na inactive, ninyi mmeshindwa nini?
 
Sensa ya mwaka 1957 ya kikoloni kipengele cha kuonesha dini kilikuwepo na ndio kinachoonesha takwimu waislamu wangapi na wakristo wangapi, na ukiangalia mwaka huo 1957 waislamu walikuwa ni 65%.

Baada ya hapo sensa zote zilizofuata kipengele cha dini kilifutwa; ajabu leo hii watu wanasema wakristo wapo wengi kuliko waislamu kwa takwimu zipi ikiwa kipengele cha kuorodhesha watu dini zao hakipo.

Pili ni kwanini wanaogopa kuhesabu watu kwa kutumia kigezo cha dini? Wengi watasema wanaogopa udini, hii hoja ni dhaifu maana nchi nyingi duniani sensa zinahebabiwa kwa mtindo wakujua idadi ya watu na dini zao ni asilimia ngapi katika nchi hizo.
Mkuu ndo maana CCM wana promote hoja za udini kwa makusudi wakijua kuwa kuna wapumbavu wengi tu ambao watajikita kujadili udini wakiacha mambo ya msingi ikiwamo jinsi raslimali za nchi znavyoibwa, kwa kweli katika hilo wamefanikiwa kutukamata sisi wengine ambao kila jambo ni lazima kwanza tuliangalie kwa mtazamo wa dini
 
A massive failure to a failed state leader.... ukiona wananchi wako wanashindwa hata kuamini serikali kwenye sensa basi jua huna mamlaka ya kutawala
 
....da,, akili ni muhimu sana. Lengo la sensa si kuongeza makanisa wala misikiti. Si kutoa ruzuku, ila anaepandikiza hii mbegu na wanaoacha ikuwe karibu na nyumba yetu, hakika lazima tuzalishe ufa kama si kubomoa ukuta...
 
Kwani kuna tatizo gani kuweka dini kwenye sensa, mbona nchi nyingi duniani wameweka sehemu ya dini, kama Uingereza, Misri, Israel, na hakuna tatizo lolote.
 
habari kwa wanajamii wote.leo kwa mshituko nimesoma tamko la BAKWATA kuhusiana na sensa ya 2012. wanataka watu tuhesabiwe kwa idadi ya dini zetu.
swali kwenu BAKWATA mnataka kujua mko wangapi ili iweje? mbona hamwishi vituko ?
 
Idadi ya mahudhurio ya makanisani, misikitini, mahekaruni, kwenye majumba ya ufalme ya mashahidi wa Munyazi Mungu (Yehova), n.k. Visihusishwe na sensa ya watu na makazi. Chokochoko zingine mbona zina-create unnecessary inconvenience bila sababu?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom