popo bawa,kwa bibi,yemen,tandale,cinza kwa remi,samaki mbezi,fundi kira,naombeni yalivyotokea

kwa bibi >>> nyumbani kwa bibi aliyekuwa akifuga nyau wengi sana maeneo fulani ya magomeni makanya
sinza kwa remi >>> nyumbani kwa marehemu ramadhan mtoro ongara a.k.a dokta remmy
mbezi samaki >>> kulikuwa na duka miaka ya mwanzo 2000 na mwishoni 1990 pale njia panda ya kwenda massana hospitali barabara ya kwenda goba
fundi kira >>> nyumbani kwa mwanasiasa maarufu mzee fundikira
 
Ubungo >>> zamani kulikuwa pori lililokuwa na miti mingi ya matunda ya mabungo. Mabungo ni mazuri sana kwa kutengeneza juisi, wenyeji wa pwani na dar wanayajua mabungo vizuri sana.

Mabibo >>> kulikuwa na mikorosho mingi sana, mikorosho hutoa matunda ya mabibo ambayo maji yake hutengenezwa pombe ya mnazi na korosho. Hii mikorosho ilisambaa maeneo ya mabibo, tabata dampo hadi kisukuru. Tulipohamia mabibo mwaka 1979 tulikuta mabaki ya mikorosho.

Mabibo farasi >>> kulikuwa na zizi la farasi enzi hizo, eneo hilo siku hizi pamejengwa sekondari ya loyola

Mabibo mpakani >>> mpaka wa kati manzese na mabibo

Mabibo makutano >>> makutano ya barabara za kwenda manzese, mabibo na mburahati

Gongo la mboto mwisho wa rami >>> barabara ya rami ya pugu (nyerere) ilikuwa ikiishia hapo.

Kunduchi >>> wavuvi wa samaki huvaa mavazi yanayoweka maungo yao uchi
 
niambieni na ya tanzania visiwani kama mkanyageni, makunduchi, kiembe samaki, mchambawima n.k
 
asili ya jina meli...
enzi za ukoloni wanajeshi walipokuwa wakiziona meli zinatia nanga walikuwa wanazikimbilia huku wakitamka mails! mails! kwa maana ya barua wabongo walivyosikia wakadhani ule mdude mkubwa wa chuma unaitwa mails.......dont quote me....l.o.l
 
Kinondoni - kiuno ndooni- mtu nalikwenda kuchota maji akaangukia ndooni, mzungu watu wakasema kiuno ndooni

magari saba - ajali ya magari saba yaliungua wakati wanasafirisha mwili

pangani - ni watumwa walikua wakitoka bwagamoyo wakifika pangani wanaambiwa pangeni msitari

bismini - ni sanamu ya busy man
 
Wakati wa biashara ya Utumwa, kulikuwa na kambo kubwa sana ya Wasafiri. Kambi hiyo walikuwa wakiuza sana Matobolwa (Viazi vitamu vinaanikwa juani, vinapikwa na kukatwakatwa na kuanikwa, vinakuwa kama BigG). Sasa jamaa wakaya hayo Matobolwa hadi wakaanza kupaita mahali hapo - Kambi ya maTOBOLwA. Baadaye ikaja kuitwa TABORA.

Chekeleni = Check Line (Angalia Train)

Mirambo ni jina la Mtemi Mirambo (Urambo) ambalo kwa Kinyamwezi haswa ni MILAMBO na ikiwa na maana ya MAITI.

Bagamoyo - Bwagamoyo, umeshakuwa mtumwa wewe na utapelekwa kuuzwa Zanzibar.

Dodoma - Idodomia - Tembo alizama na hiyo sehemu alipozamia (kudidimia) wakapaita Idodomia.

Sikonge - Sikong (soma SAIKONG) au Mikonge.......
 
Mozambique = Mussa al Bik. Huyu alikuwa mwarabu aliyekuwa na ushawishi mkubwa Msumbiji kama alivyokuwa Abushir bin Salim. Wareno wakaita eneo alilokuwa analidhibiti kwa jina lake Musabik. Bombay = Bom+bahia (kireno) yaani Good bay au Ghuba Njema.

Kwa Tanzania, majina mengi yametokana na miti, majengo au maumbile ya kijiografia ya pahala husika, kama vile Mkoroshoni, Mwembe yanga, Mwembetogwa, Mwembedezo, Majani Mapana, Mnazini, Mtufaani, Mshelishelini, Mipeani, Magorofani, Relini, Darajani n.k
 
Je na haya ya wenzetu MAYAHE wa kule visiwani mnayaonaje?

1. Mfereji wa wima
2. Mchamba wima
4. Makunduchi
5. Mwembemakumbi
6.Kwahaji tumbo.
 
Wandugu majina ya maeneo mbalimbali hapa TANZANIA na asili yake hebu tukumbushane machache kati ya haya :-

-KARIAKOO-carrier cool
-MSASANI-musa hasan
-BAGAMOYO-bwaga moyo

eti kuna maeneo mengine mnayoyajua ama ni haya haya au yapo mengine.

Sahihisho: Kariakoo - Carrier Corps
Ni sehemu ambayo walikuwa wanakaa wapagazi wakati huo. Ndiyo maana kuna Kariakoo hata Nairobi.

Saadani - Mwarabu alikuwa anaulizwa ni saa ngapi ili watu waende kuswali,
yeye aliwajibu 'saa dani', kwa maana kwamba saa ipo ndani.

Makuyuni - Penye mikuyu
Manyara - Manyero (kimbugwe), mahali wanyama wanapokunywa maji.
Serengeti - (kiMaasai) Mbuga isiyo na ukomo
 
Nimeshindwa kuzipitia sredi zote, sijuwi hii imewekwa Dar es salaam = Daari ssalaam
‎‎ (nyumba ya amani) wakati huo hata kibaka hakuna
 
Sahihisho: Kariakoo - Carrier Corps
Ni sehemu ambayo walikuwa wanakaa wapagazi wakati huo. Ndiyo maana kuna Kariakoo hata Nairobi.

Saadani - Mwarabu alikuwa anaulizwa ni saa ngapi ili watu waende kuswali,
yeye aliwajibu 'saa dani', kwa maana kwamba saa ipo ndani.

Makuyuni - Penye mikuyu
Manyara - Manyero (kimbugwe), mahali wanyama wanapokunywa maji.
Serengeti - (kiMaasai) Mbuga isiyo na ukomo

What about olduvai?
 
Nimeshindwa kuzipitia sredi zote, sijuwi hii imewekwa Dar es salaam = Daari ssalaam
‎‎ (nyumba ya amani) wakati huo hata kibaka hakuna

halafu ni kweli hakuna aliyekumbuka kweli tuna mambo mengi wtz,lol....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom