Arusha ipo karibu na Nairobi yenye gereji za kisasa; kwanini bado hata matajiri wanasita kununua magari mapya ya Ulaya (0 km)?

Arusha ipo karibu na Nairobi yenye gereji za kisasa; kwanini bado hata matajiri wanasita kununua magari mapya ya Ulaya (0 km)?

mkata uzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2025
Posts
1,910
Reaction score
5,451
Kenya watu wanaojiweza wana magari latest kwasababu huduma za gereji zipo za uhakika.

Arusha hadi Nairobi ni safari ya masaa tano tu unaweza kwenda na kurudi kwa mafuta lita 50 kwenye chombo kama BENZ gl 300.

kwanini hata matajiri bado wanasita kununua vitu latest vya ulaya ?
 
Gari ni Toyota Mkuu, ndio durable sana niliwahi kuwa na Volvo Yani ni Kichomi sensors kibao Gari inazima
Toyota ni gari durable kwetu kwasababu tumezoea MITUMBA,

Gari umeenda kuinunua 0KM wewe ndie mtumiaji wa kwaza, kukiwa na gereji nzuri na ukizingatia sevisi kuna uhakika wa kudumu nayo vizuri kabisa hadi kilometa elf 70
 
Kenya watu wanaojiweza wana magari latest kwasababu huduma za gereji zipo za uhakika.

Arusha hadi Nairobi ni safari ya masaa tano tu unaweza kwenda na kurudi kwa mafuta lita 50 kwenye chombo kama BENZ gl 300.

kwanini hata matajiri bado wanasita kununua vitu latest vya ulaya ?
Hatab hivyo kwa hapa Tz, huduma za Magari na ufundi Arusha inaongoza, yaanu pale kuna watu utadhani waaamesomea Toyota Japani.

Wanawexa kuigeuza Fuso kuwa scania, Lori kuwa Bus
 
Toyota ni gari durable kwetu kwasababu tumezoea MITUMBA,
Kwamba hizo Toyota mpya haziuzwi, ni lazima kununua pre owned tu?

Gari umeenda kuinunua 0KM wewe ndie mtumiaji wa kwaza, kukiwa na gereji nzuri na ukizingatia sevisi kuna uhakika wa kudumu nayo vizuri kabisa hadi kilometa elf 70
Kwanini hizo za Ulaya ni mpaka ununue mpya ndio idumu hadi 70,000 km? Tena hapo uzingatie gereji NZURI, na service ya uhakika.

Huoni hapo unataja sifa za magari ya Ulaya kutokuwa durable and reliable?
 
Kwenye vita ya Ukraine kuna silaha nyingi sana za makers tofauti. Kati ya hizo kuna self propelled howitzer moja ni ya Ujerumani inaitwa Panzerhaubitze 2000 (Pz2000). Hiyo SPG yenye uwezo mkubwa zaidi, range kubwa na accuracy kubwa kuliko SPG zote zilizotolewa kwa msaada Ukraine.

Ilipofika wakati wa Ukraine kuweka order hawakuichukua Pz2000 sababu ina sensors nyingi mno kama magari ya Kijerumani yalivyo. Mnakuwa kwenye mapigano ghafla sensor ya oxygen inakufa silaha inagoma kufanya kazi. Iko too complicated kufanyia service mpaka mwanzoni walikuwa wanapeleka Poland kwenye service center. Wakati SPGs nyinginezo kama Caesar ya Ufaransa na Archer ya Sweden zinafanya kazi kwa kuvumilia shida. Mwishowe Ukraine wakanunua hizo.

Yaani niwe safari ya kwenda vacation Serengeti, alafu gari lizime kisa sensor ya kipuuzi nianze kuagiza fundi Nairobi. Eti kisa nina hela. Watu wenye hela hawataki usumbufu na kupotezewa muda. Umemuona jana mayor wa mji mmoja kule Ufilipino alikuwa kwenye Toyota LC200 series iko blast proof amepigwa RPG-7 nadhani ile, ila kapona na gari hakijaharibika. Hiyo reliability ndio watu wanataka, sio vimulimuli.
 
Kenya watu wanaojiweza wana magari latest kwasababu huduma za gereji zipo za uhakika.

Arusha hadi Nairobi ni safari ya masaa tano tu unaweza kwenda na kurudi kwa mafuta lita 50 kwenye chombo kama BENZ gl 300.

kwanini hata matajiri bado wanasita kununua vitu latest vya ulaya ?
Exposure. Utakuta mtu kanunua gari japani lakini ukimwambia agiza spare japan anaogopa, anaishia kutafuta bongo ambayo anaweza asipate nakuishia kusema hayo magari achana nayo
 
Maamuzi ya kununua gari Ulaya au Japani, inategemea kipato cha muhusika. Sasa naona mchina kaingia na gari za umeme, sijui itakuwaje.

You are what you think you are. Ukisema mtumba wa japan ni bora, upo sahihi. Ukisema gari za ulaya ni bora Zaidi kuliko Japan upo sahihi pia.
 
Toyota ni gari durable kwetu kwasababu tumezoea MITUMBA,

Gari umeenda kuinunua 0KM wewe ndie mtumiaji wa kwaza, kukiwa na gereji nzuri na ukizingatia sevisi kuna uhakika wa kudumu nayo vizuri kabisa hadi kilometa elf 70
Sio kwasababu tumezoes mitumba ila practicality yake, unlike magari mengine, toyota imetenengezwa with durability in hand.
Haswa kwa mazingira ya porini hayahitaji gari soft, ndio maana akina cruiser , landrover defender na heavyduty suv zingine zinatamba

australia, even us wanasifis toyota likija suala la practility, upande wa pickup or offroad experience
 
Maamuzi ya kununua gari Ulaya au Japani, inategemea kipato cha muhusika. Sasa naona mchina kaingia na gari za umeme, sijui itakuwaje.

You are what you think you are. Ukisema mtumba wa japan ni bora, upo sahihi. Ukisema gari za ulaya ni bora Zaidi kuliko Japan upo sahihi pia.
Umeme bado haujafikia durability ya diesel vehicles, plus miundombinu na garage za kuhudumia gari ya umeme bongo bado sanaaaaa
 
Tukiachana na matajiri ambao matumizi yao yapo tagged na matumizi ya makampuni yao, si rahisi ukutane na tajiri anayependa gari linalotengenezwa kwa gharama kubwa. Gharama ya kumiliki gari inapokuwa kubwa na wenyewe wanalikimbia gari, hata akiwa nalo linakuwa si kwa matumizi heavy, ni mara moja moja tu kwa heshima.
 
Back
Top Bottom