09 Dec, 2019: Maadhimisho ya siku ya uhuru wa Tanganyika. Wafungwa 5,533 wapata msamaha wa Rais. Mbowe ataka maridhiano ya Kitaifa

USHAURI:
Ili kujua kama unachoandika kinachukuliwa kwa uzito na wasomaji, angalia jinsi wanavyochukulia habari unayoanzisha kwa kukujibu au kuchangia ulichopost. Kama kila unachoanzisha kinasuswa na watu jitathmini. Wengine mnaweza kujidanganya kwa kauli "Hata kama hawachangii ujumbe umewafikia", Hapana, angalia inawezekana unachopost ni pumba tupu hivyo hakuna anayehangaika nazo. Si lazima uanzishe thread, unaweza kuwa mchangiaji kwenye thread za wenye busara ili kujipa muda wa kuweza kutoa mada zenye busara.
 
The truth... just ahead
Kuna baadhi ya wanasiasa wamesema hawawezi kuhudhuria kwenye sherehe ya kumbukumbu ya uhuru wa Tanganyika kwa sababu hakuna uhuru.

Tusije kushangaaa kuona wanasiasa waliosema hawawezi kuhudhuria wanakuwa mstari wa mbele katika kuelezea na kukosoa yatakayojiri kwenye sherehe hizo katika uwanja wa Kirumba, Mwanza.

Hawa wanasiasa lazima waelewe kuwa hata kuangalia tukio la kumbukumbu ya uhuru kwenye luninga (Tv) haina tofauti na mtu ambaye amehudhuria sherehe hizo. Kama hawataki kuhudhuria kwenye sherehe hizo kwa sababu hazina maana kwa sasa basi wasiangalie hata yanayojiri kwa kutumia luninga (Tv) ili kuutendea haki msimamo wao.

Kutokuangalia yanayojiri kwa njia ya luninga (Tv) watakuwa wamelitendea haki tangazo lao la kutokuhudhuria kwenye sherehe hizo.

Nchi hii kuna baadhi ya watu utawasikia wakisema, ''Mimi huwa siangalii kituo fulani cha luninga'' lakini cha kushangaza huwa wa kwanza kuelezea tukio linalotokea kwenye kituo hicho cha luninga!
 
Kwani kuiangalia simba wakati inacheza ni lazima uwe mshabiki wake au uwe unaikubali simba? Huenda una hoja lakini umeshindwa namna ya kuiwasilisha.
 
Kiukweli mawaziri wakuu wastaafu Mzee Lowassa na Sumaye walijivuruga sana walipohamia upinzani na kuna wakati niliuliza hapa jamvini kama uamuzi wao ulikuwa sahihi.

Lakini jambo jema ni kwamba waliyagundua makosa yao na kujisahihisha na leo mzee Sumaye yupo kwenye safu ya viongozi wa taifa......akimwangalia kwa mbali mh Mbowe anayekaa safu ya wanasiasa akina Momose Cheyo na Prof Lipumba.

Maendeleo hayana vyama!
 
Siasa za kipumbavu kabisa, mtu anabuguliwa kutokana na chama anachokifuata.
Yaani mtu akiwa CCM anakuwa Ni raia daraja la Kwanza, na wapinzani Ni raia daraja la pili.
Hi dhambi uliyoasisiwa na Magufuli Mungu atamhukumu nayo
 
Back
Top Bottom