Salam kwako Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan.
Kila mwaka tarehe 1 Mei ni sikukuu ya wafanyakazi duniani ambapo wafanyakazi wote husheherekea siku hiyo kwa mambo mbalimbali na katika desturi yetu hapa Tanzania kunakuwa na maadhimisho ya kitaifa na mara zote anayekuwa mgeni rasmi ni Rais kwakuwa ndiye mwajiri Mkuu.
Mwaka huu sherehe za Mei Mosi kitaifa zitafanyika katika Mkoa wa Arusha katika uwanja wa Shekhe Amri Abeid Karume Stadium. Sherehe hizi huambatana na kauli mbiu mbalimbali toka sekta tofauti lakini kunakuwa na kauli mbiu kuu inayobeba sherehe yenyewe.
Sherehe hii ni ya wafanyakazi wote na wewe Mheshimiwa Rais ndiye mgeni rasmi. Nasikitika kuona baadhi ya wafanyakazi wanabagiliwa kwenye sherehe hizo kwa kutopewa nafasi kama wafanyakazi wengine.
Sherehe hizo zinaandaliwa na shirikisho la wafanyakazi TUCTA na kupewa dhamana ya kuandaa, washiriki ni wafanyakazi wote na siyo wale wa shirikisho pekee. Zipo taasis na vyama vya wafanyakazi ambavyo havipo kwenye shirikisho hilo TUCTA lakini wapewa nafasi ya kushiriki na kutambulika.
Nasimama na walimu zaidi ya 1,000 wa Mkoa wa Arusha ambao wamebaguliwa kwenye sherehe hizo kwasababu tu wao ni wanachama wa CHAKUHAWATA na ni chama kilichopo kwa mujibu wa sheria na kinafanya kazi zake kwa uhalali na kwa mujibu wa sheria. Ubaguzi huu upo nchi nzima lakini nazungumzia Arusha kwakuwa ndipo sherehe inafanyikia kitaifa.
Inawezekana wewe Mheshimiwa Rais kama mgeni rasmi usijue hilo Ila naomba nikujulishe hili ili ulikemee. Walimu ambao ni wanachama wa CHAKUHAWATA ni watumishi pia na wapo chini yako. Wote ni watoto wako, kama ulivyosema huna upendeleo naomba walimu hawa wapate nafasi kwenye maadhimisho ya Mei mosi 2024 na miaka mingine bila kubaguliwa kwa aina yeyote.
Naomba kuwasilisha kwa niaba Yao.
===
Pia soma:
Dkt. Mpango: Serikali imepokea hoja ya kuboresha kikokotoo kwakuwa wafanyakazi hawaridhishwi na kanuni zake