tcra

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (pia huitwa kwa Kiingereza: Tanzania Communications Regulatory Authority ambapo mara nyingi huitwa kwa kifupi: TCRA) ni taasisi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yenye majukumu ya kusimamia sekta za mawasiliano na utangazaji.

TCRA Ilianzishwa kwa Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Na. 12 ya mwaka 2003 kusimamia huduma za kielektroniki na posta na masafa ya mawasiliano nchini Tanzania. Mamlaka ilianza kazi tarehe 1 Novemba 2003 na inafanya shughuli za zilizokuwa Tume ya Mawasiliano Tanzania (TCC) na Tume ya Utangazaji Tanzania (TBC).

Mamlaka ya TCRA ni kusimamia sekta ya posta, mawasiliano ya kielektroniki na utangazaji katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiwa ni pamoja na:
  • Kuzifanya shughuli za TCRA kuwa za kisasa kwa kutumia teknolojia sahihi;kuimarisha tafiti zenye ubora katika huduma zinazodhibitiwa, uwezo na umahiri wa watumishi.
  • Kukuza ufanisi; kuaminika na kuhakikisha usalama wa miundombinu ya mawasiliano na matumizi yake.
  • Kukuza ufanisi na unafuu wa huduma za Mawasiliano na kuongeza upatikanaji wa huduma za Posta na TEHAMA katika maeneo yasiyohudumiwa ipasavyo na yale yasiyo na huduma kabisa.
  • Kulinda maslahi ya wadau na kukuza uelewa wa haki na wajibu wao.
  • Kufuatilia utendaji wa huduma zinazosimamiwa na kuhakikisha utekelezaji wa Sheria na Kanuni kwa viwango vinavyostahili.
  • Kuratibu utekelezaji wa ahadi za kisekta kitaifa, kikanda na kimataifa.
  • Kufikia kiwango cha juu ya kuridhisha wateja kama ilivyoainishwa kwenye Mkataba wa Huduma kwa Mteja wa TCRA.
  • Kuendelea kuzingatia matakwa ya kisheria na kiusimamizi.

Sera zinazoathiri utendaji kazi wa TCRA ni pamoja na:
  • Sera ya Taifa ya Mawasiliano ya mwaka 1997
  • Sera ya TEHAMA ya mwaka 2003
  • Sera ya Taifa ya Posta ya mwaka 2003
  1. ANT DRUGS

    Uozo Vodacom na TCRA

    Morning wakuu!Naomba niende kwenye mada yangu moja kwa moja. Siku ya jumatatu tarehe 30/11/2020 niliishiwa muda wa maongezi na nikaamua kujiunga kifurushi cha TSH 2,500/ ambapo nilipewa dk50 kwenda mitandao mwingne na dk180 voda kwenye voda tu. Maana yake nilikuwa na jumla ya dk230,cha...
  2. Kelela

    Msaada: Leseni ya Maudhui ya Mtandaoni TCRA

    Wataalamu naomba kujua, Kama una YouTube Channel na Blog ambayo maudhui yake yanafanana na Channel. Je unatakiwa kusajili leseni mbili tofauti? au Ni leseni moja tu inajitosheleza? Maana leseni kwa mwaka ni Tsh 500,000 - 1,000,000
  3. Miss Zomboko

    Watu 2 wahukumiwa kwa hatia ya kusambaza Huduma ya Internet bila kibali na kuisababishia hasara TCRA

    Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemuhukumu Mhandisi Baraka Mtunga (43) na Rajabu Katunda (42) kulipa faina ya Sh. Milioni 1.5 kwa kila mmoja baada ya kupatikana na hatia ya kusambaza Huduma ya Internet bila kibali na kuisababishia hasara Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) zaidi ya Sh...
  4. mgt software

    Kushindwa kwa TCRA kudhibiti Simu feki ni ushahidi kuwa TRA na TBS zimesinzia Kabisa

    Wana JF, Vyombo muhimu vya serikali vyote kwa pamoja vimeshindwa kudhibiti Simu feki hivyo kuongezeka kwa uharifu pamoja nakuikosesha serikali mapato. Kazi ya kudhibiti bidhaa feki ni ya TBS kazi ya kukagua uingiaji bidhaa halali kutoka viwanda vinavyotambulika na kutoza kodi ni TRA. Tra...
  5. Roving Journalist

    Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) yatembelea Ofisi za Jamii Forums

    Kamati ya Maudhui ya TCRA ikiongozwa na Makamu Menyekiti wake, Ndugu Joseph Mapunda, imetembelea ofisi za Jamii Forums ikiwa na lengo la kujifunza mambo kadha wa kadha kuhusu Taasisi na kujionea namna huduma inavyotolewa kwa wananchi. Kamati hiyo ilipokelewa na watendaji wa Jamii Forums...
  6. Jidu La Mabambasi

    TCRA, mmeshakuwa irrelevant

    Katika dunia hii ya teknolojia, alternatives to communication zinajitokeza kila uchao. Kwa sababu za kisiasa tu TCRA imeamua kuminya upatikanaji na upashanaji wa habari kwa waTanzania. Hili ni kosa la kimsingi, kwa sababu yoyote ile. Teknolojia hailali, watu wamekwisha anza kutumia njia...
  7. Suley2019

    LHRC yawataka TCRA na Makampuni ya Mawasiliano kutoa ufafanuzi kuhusu hali ya kukatika kwa mtandao nchini

    Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimetoa wito kwa Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) na Makampuni ya Mawasiliano ikiwamo TTCL, Vodacom, Tigo, Airtel kutoa taarifa rasmi kwa wateja kufafanua kuhusu changamoto inayowakabili watumiaji wa mitandao.
  8. M

    GE2020 TCRA, hamuwaoni TBC wanavyopiga kampeni wazi siku ya Uchaguzi?

    Kwa wote mnaoangalia TBC, wana “Mchambuzi wa Masuala ya Siasa” anamwaga sifa kemu kemu kwa Dkt. Magufuli ambaye ni mgombea Urais kupitia CCM. Mchambuzi wao huyu anaonekana wazi kuwa amekuja kuhamasisha watu kumpigia kura Ndg. Magufuli na mbaya zaidi anamkandia Mzee Mwinyi na kueleza mazuri ya...
  9. Kirchhoff

    TCRA mnaniharibia Kazi kuzima mitandao ya Kijamii. Mitambo ya Kiwanda inakufa

    Hakika Kitendo chenu Cha kuzima WhatsApp kimeniuzi na kuniumiza sana. Nimepata hitilafu kwa mitambo ya kiwanda. Nikiwa napokea maelekezo ya Nini cha kufanya kupitia Whatsapp ghafla mmeifungia. Mmenipa hasara kubwa sana. Ninyi mngeacha WhatsApp. Mtu akivunja sheria mumuadhibu.
  10. Komeo Lachuma

    TCRA huu wizi wa Makampuni ya simu mbona mmeufumbia macho? Angalieni Airtel

    Wananchi tumekuwa tukilalamika sana kuhusiana na wizi unaofanywa na mitandano ya simu. Mmeziba masikio yenu kwa Vigondo. Hamsikii.Na macho yenu mmeyavalisha miwani ya Mbao. Hamuoni. Airtel kwanza wana utaratibu ambao mimi nmeshindwa uelewa.napotaka kuangalia data bundle iliyobaki sipewi majibu...
  11. mgt software

    TBS, TCRA na TRA washindwa kuisaidia Serikali kuondoa spea feki za Simu. Mafundi simu waishia lockup wasijue lakufanya

    Wana Jf Serilikali kupitia ajent zake za kitaifa kwa pamoja wanaungana kuikosesha mapata serikali na kuleta mtafaruku mkubwa kati ya mafundi simu na wateja wao. TBS, TCRA na TRA zilivyoshindwa Nazi zao kila moja nitaelezea makosa yao TBS wameshindwa kuajiri vijana wenye weledi kutambua vitu...
  12. Kurzweil

    TCRA: Yatoa neno kwa Vyombo vya Habari vinavyowatumia watangazaji wasio na Taaluma ya Habari

    MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA(TCRA) YATOA ONYO KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU KUAJIRI WATANGAZAJI WASIO NA TAALUMA. Mamlaka ya Mawasiliano nchini imetoa onyo kwa vyombo vya habari hususani redio na televisheni kwa kile inachodai kuwa vyombo hivyo vimekua na tabia ya kuajiri watangazaji wasio...
  13. MamaSamia2025

    TCRA, TRA na Mamlaka zingine za Serikali hazipaswi kulaumiwa

    Natumaini mko salama. Leo tena natumia haki yangu ya kikatiba kutoa maoni yangu kuhusu mamlaka za kiserikali hasa zinazolaumiwa zaidi. Kwa muda mrefu Mamlaka hasa TCRA na TRA zimekuwa zikitupiwa lawama wanapofanya kazi zao kwa mujibu wa sheria. Binafsi naona hawastahili kulaumiwa endapo hakuna...
  14. J

    TCRA yawafungia Wasafi FM kwa kutumia lugha za matusi

    Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesitisha utoaji huduma za utangazaji kwa Wasafi FM kwa muda wa siku saba kuanzia Septemba 12 hadi Septemba 18 mwaka huu. Uamuzi huo umetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandisi James Kilaba Jijini Dar es Salaam ambapo amesema hatua hiyo ni kutokana na...
  15. J

    Clouds wamaliza adhabu ya TCRA warudi hewani kwa mbwembwe!

    Hatimaye Clouds Media Group wamemaliza kutumikia adhabu ya kifungo cha siku 7 waliyopewa na TCRA na wamerudi hewani rasmi. Kinachoendelea sasa luningani ni sherehe ya wafanyakazi baada ya kutoka kifungoni, ni full shangwe. CCM hoyeeee! Maendeleo hayana vyama!
  16. FRANCIS DA DON

    Napendekeza TCRA wapige marufuku matangazo ya BBC nchini Tanzania. Wameitukana kumbukumbu ya Mwl. Nyerere

    Eti wameonyesha kipindi cha historia ya ukombozi wa Afrika, ambapo wametaja wapambania uhuru kama akina Kwame Nkrumah, Patrice Lumumba na Nelson Mandela, Jomo Kenyatta miongoni mwa wengi. Lakini cha ajabu walipofika kwenye ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika wameishia kumtaja Mandela tu na...
  17. Miss Zomboko

    TCRA yaipiga faini ya Tsh. bilioni 11.89 Kampuni ya Intaneti ya Raha Limited kwa kuendesha shughuli zake bila kuwa na kibali

    MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeipiga Faini ya Sh.bilioni 11.89 Kampuni ya Raha Limited watoa huduma ya Internet kwa makosa mbalimbali ikiwemo kutumia masafa ya mawasiliano ya Radio katika wigo 1452-1482 MHZ bila kuwa na leseni halali kutoka TCRA tangu 24 Machi 2020. Akizungumza na...
  18. Return Of Undertaker

    TCRA, inakuwaje magazeti ya Uhuru na Jamvi la Habari hayajafungiwa kwa kuripoti habari sawa na Clouds Media?

    Hapa kuna tofauti gani au nayo ni sehemu ya kuendeleza udhalimu na kutishia vyombo vya habari kuelekea uchaguzi mkuu kutotangaza habari za upinzani.
  19. Roving Journalist

    Clouds Media wafungiwa kwa siku 7, kwa kutangaza Takwimu za Uchaguzi ambazo hazijathibitishwa na Tume

    Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imevifungia vituo vya habari vya Clouds TV na Radio kwa siku saba kuanzia kesho Agosti 28 na adhabu ya kuomba radhi siku nzima ya leo kwa kosa la kukiuka kanuni za utangazaji na kanuni ndogo za utangazaji za Uchaguzi. TCRA imesema kosa walilolifanya ni...
Back
Top Bottom