LHRC yawataka TCRA na Makampuni ya Mawasiliano kutoa ufafanuzi kuhusu hali ya kukatika kwa mtandao nchini

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,811
4,533
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimetoa wito kwa Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) na Makampuni ya Mawasiliano ikiwamo TTCL, Vodacom, Tigo, Airtel kutoa taarifa rasmi kwa wateja kufafanua kuhusu changamoto inayowakabili watumiaji wa mitandao.

1604285731734.png

Mtandao ni anasa, watu mfanye kazi.
Tumeamua kufanya kazi na kuachana na mitandao inayotweza utu wa mtanzania. Malaika wamekuja kuifungilia mbali
Mitandao hiyo unayoita anasa wengine imetusaidia kujenga nyumba, kusafiri dunia, kuajiri watu zaidi ya 10 ambao na wao wana familia zina wategemea.

Kaa na umaskini wako mwenyewe, nenda kalime maana ndiyo biashara mnaziweza, hizi za kidijitali achia watu smart, baki na ushamba wako
 
Mtandao ni anasa, watu mfanye kazi.
Tumeamua kufanya kazi na kuachana na mitandao inayotweza utu wa mtanzania. Malaika wamekuja kuifungilia mbali
Wewe unahisi hiyo simu yako unavyopokea na kutuma tu sms ndio unaona umuhimu siyo.

Wengine ili tuweze kuishi na kufanya kazi tunawategemea waliopo mitandaoni, au hujawahi sikia online business?

Naomba JF Moderator kabla ya kuruhusu matumizi ya anayetaka kujiunga humu, muweke questionnaires ili akishindwa abakie huko
 
Nakuunga mkono mkuu, imeshakuwa kero bado najiuliza watafanya hivi hadi lini
 
Waturudishie na fedha zetu tulizowalipa kwa ma-bundle ya, mfano, mwezi. Haiwezekani inilipie mwezi, halafu video hazifunguki, halafu mwezi unapita na kulipia tena. Nalipia nini sasa? Sio wizi huo?
 
Back
Top Bottom