Vipindi vya Mashamsham, Mgahawa na SportsArena vimesheheni Waropokaji; TCRA ni waungwana sana vinginevyo wangeshavifutilia mbali

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,279
21,396
Tunapozungumzia uthubutu;

Tusisahau kuthubutu bila kuzingatia kanuni (Ethic's) katika kazi husika!

Wamiliki wa Wasafi wamethubutu na wanania njema ya kuleta mabadiliko kwenye media lakini malengo yao yataendelea kuwa butu kutokana na aina ya baadhi watangazaji wanaowaajili kushindana kuropoka!

Wapuuzi na waropokaji wamewapa nafasi kubwa kuibeba Media kuliko weledi! Hivyo Wapuuzi na waropokaji kwa nguvu ileile ya kuibeba Wasafi FM ndivyo watavyoindosha kwa upuuzi wao! Na kwasababu ya upuuzi wa baadhi ya watangazaji wao ni rahisi sana kuihujumu media IKAFA kupitia Uropokaji wao wenyewe!

Namna ya kuipoteza na kuihujumu wasafi ni rahisi sana kupitia Shehena ya Wapuuzi na waropokaji waliojaa kwenye vipindi vya sportsArena,Mashamsham, na Mgahawani!

TCRA inawaonea huruma wamiliki wa media kuvifutilia mbali vipindi vya namna hii lakini IPO siku huruma itakoma Endapo wamiliki wasipowachukulia hatua.
 
Kwani lazima kuwasikiliza redio mbona zipo nyingi sikiliza hata TBC au redio Uhuru
 
Mtangazaji yupo busy kuropoka kila neno ilimradi tu ss tucheke

Kulikuwa na kipindi(sijui channel gani)redioni nilikuw nasikiliz kweny daladala
kwanza wapo busy wanaongea broken swahili(kwenye L wanaweka R), wanapiga makelele tu
 
WIVU WA KIKE HUU AFU CHA AJABU UNAWEZA KUTA AMEANDIKA MWANAUME TENA ANAETEGEMEWA KUTOA USHAURI KWA FAMILIA YAKE
 
wasafi ni wa kuowaonea huruma, its high time Kusaga na mke wake waingilie kati watafute watu wanaojua kuongoza media au Ruge ndo alikuwa anamsaidia???
Wasafi wanjiona wajanja wa mjini ila kuna redio za mikoani ukisikiza utagundua kuna ueweledi na ufahamu kuliko hata hao wenye jina ,yaani majitu mazezeta yamekuwa waandishi wa habari hata majina ya miji mikuu kutamka ni shida.
 
Mimi nilipoona vipindi kama mgahawa na vinavyofanana na hivyo havinivutii nikiacha kuvisikiliza wasafi nafata sports arenna na mziku laini usiku kwahiyo ni kitu rahisi tu mda wa mgahawa we sikikiza radio station nyingine mkuu

NB:. Sports arenna haina waropokaji kama unavodai mkuu labda we si mfatiliaji wa icho kipindi
 
WIVU WA KIKE HUU AFU CHA AJABU UNAWEZA KUTA AMEANDIKA MWANAUME TENA ANAETEGEMEWA KUTOA USHAURI KWA FAMILIA YAKE
Hata shoga ukimkanya husema unamuonea Wivu!

Mahaba yasikufanye usione kosa!
 
Back
Top Bottom