TCRA huu wizi wa Makampuni ya simu mbona mmeufumbia macho? Angalieni Airtel

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Oct 31, 2014
2,722
2,000
Wananchi tumekuwa tukilalamika sana kuhusiana na wizi unaofanywa na mitandano ya simu. Mmeziba masikio yenu kwa Vigondo. Hamsikii.Na macho yenu mmeyavalisha miwani ya Mbao. Hamuoni.

Airtel kwanza wana utaratibu ambao mimi nmeshindwa uelewa.napotaka kuangalia data bundle iliyobaki sipewi majibu. Napewa majibu ya salio la kawaida lililobaki. Data sipewi majibu yake. Lengo lao ni kuwa nisiweze fuatilia kiasi cha bundle kinachotumika.

Pili leo nmeshangaa simu ikiwa haipo online sijawasha data naletewa ujumbe nimetumia asilimia 90 ya GB 1 ambayo nliweka jana mchana na sijadownload chochote cha kufika hata MB 200. Huu ni wizi. TCRA sijajua kwa nini mnawaacha hawa wenye mitandao watuibie.

"Umetumia takribani 90% ya MB 1024 yako. Salio ya intaneti yako ni 87 MB. Bonyeza My Airtel - Apps on Google Play kupakua Airtel App kununua Bando mpya."

Screenshot_20201016-093804~2.png
 
Ngalikihinja

JF-Expert Member
Sep 1, 2009
22,509

View attachment 1601814
MB 1024 = 100%
10% = 102.4 MB, lakini wao wanasema umebakiwa na 87MB. 15.4MB hazijulikani ziliko
 
marxlups

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
15,011
2,000
Na ndiyo wenye mamlaka kwa sura ya kuwatetea wanyonge na sijui anayewanyonga ni nani!!!
 
2019

JF-Expert Member
Dec 31, 2018
1,581
2,000
Unatumia simu gani nikusaidie hienda ni kweli lakini kuna vitu hujajua bado!! Mm niligombana na tigo 2014 hivyo hivyo kumbe matumizi yalikua sawa...nitajie simu yako kwanza.
 
Zabron Hamis

Verified Member
Dec 19, 2016
3,527
2,000
Unatumia simu gani nikusaidie hienda ni kweli lakini kuna vitu hujajua bado!! Mm niligombana na tigo 2014 hivyo hivyo kumbe matumizi yalikua sawa...nitajie simu yako kwanza.
10% ya 1024MB ni kiasi gani. Tuanzie hapa kwanza ndio tuje kwenye ubishi wako na tigo 2014
 
1gb

JF-Expert Member
Jun 30, 2013
1,843
2,000
Kwenye suala la kuonyesha salio la data,kiukweli hilo suala limeanza hivi karibuni,najua hiyo sio bht mbaya wamefanya kwa makusudi.
Nimekua kila nikijaribu kuangalia salio la data.
Napata sms pop up.
Salio lako 0.
 
ABLE04

Senior Member
Apr 13, 2017
139
500
Nilijaribu kumtumia mtu pesa kwa Airtel Money anayetumia mtandao mwingine, kutuma Tsh 1000 ada wanasema Tsh 400....hii ni baada ya kutuma Tsh345,000 kwa kutumia M-pesa na Kukwata Tsh 8,500....hii sio fair, wanatuibia sana.
 
bg_dg_dy

JF-Expert Member
Feb 27, 2009
552
500
Usemayo ni kweli mimi nimeshuhudia, salio haiji tena. Jaribu kupiga *199*81# then chagua 6 haikupi salio lako la data bali huja sh 0.00
 
2019

JF-Expert Member
Dec 31, 2018
1,581
2,000
Vodacom nao wana wizi wao wa bundle.kuna wakati mpaka nikahisi hii simu ni fake inatumia data bila kuwasha data
mm nimewatema rasmi kwa bei kubwa kila siku nipo Halotel 3k kwa wk 3GB na dk 30 mitandao yote
 
Tella Mande

JF-Expert Member
Jun 2, 2018
247
500
Huku voda ni balaa. Nanunua GB 50 na simalizi mwezi! Na zikibakia GB 10 USUMBUGU NINAOUPATA UNATISHA. Mara uambiwe uongeze salio, mara igome tuu mpaka unaangalia salio nk.

VIFURUSHI vimevurugwa sana na vitrtengenezwa kihuni haswa. Tzs 10,000 unaambiwa mitandao yote kwa mpangilio huu.... dk 400 za usiku na dk 100 ndo za mchana pekee.
HUU NI UHUNI.

YAPO MENGI...
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom