Msaada: Leseni ya Maudhui ya Mtandaoni TCRA

Kelela

Senior Member
Nov 7, 2020
186
269
Wataalamu naomba kujua, Kama una YouTube Channel na Blog ambayo maudhui yake yanafanana na Channel. Je unatakiwa kusajili leseni mbili tofauti? au Ni leseni moja tu inajitosheleza?

Maana leseni kwa mwaka ni Tsh 500,000 - 1,000,000
 
tcra wameamua mkuu kufanya kazi ya tra hapo vyote utatakiwa kuvilipia
Dah hii mifumo mingine itaendelea kuwainua walio juu na kuwadidimiza walio chini.
all in all hatuna namna, wacha tuishi wanavyotaka.

Tanzania nchi yangu, Nakupenda kwa moyo woteeeee!
 
"Maana leseni kwa mwaka ni Tsh 500,000 - 1,000,000"

Mambo ya jiwe haya!Mliambiwa mchague mabadiliko mkabisha
 
Dah hii mifumo mingine itaendelea kuwainua walio juu na kuwadidimiza walio chini.
all in all hatuna namna, wacha tuishi wanavyotaka.

Tanzania nchi yangu, Nakupenda kwa moyo woteeeee!
Mkuu wewe jilipue weka kitu online ila usiweke taarifa zako binafsi ikifika wakati channel imekuwa maarufu ndio unaenda kwa hao majambazi wa tcra kuisajili
 
Wataalamu naomba kujua, Kama una YouTube Channel na Blog ambayo maudhui yake yanafanana na Channel. Je unatakiwa kusajili leseni mbili tofauti? au Ni leseni moja tu inajitosheleza?

Maana leseni kwa mwaka ni Tsh 500,000 - 1,000,000
Hiyo Channel yako na blog inaingiza kiasi gani mpaka ukatoe kiasi chote hicho Kwasababu ya leseni.
 
Wataalamu naomba kujua, Kama una YouTube Channel na Blog ambayo maudhui yake yanafanana na Channel. Je unatakiwa kusajili leseni mbili tofauti? au Ni leseni moja tu inajitosheleza?

Maana leseni kwa mwaka ni Tsh 500,000 - 1,000,000
Mkuu. Blog na YouTube channel ni biashara mbili tofauti. Kila moja ina kodi yake kwa mwaka.

Kujua tembelea website ya TCRA nenda kwenye kusajili Blog au YouTube utaona gharama.

However, mfumo huu umekaa kimkakati, kwanza kukwamisha vijana wanaotafuta vijisenti mtandaoni. Ila lengo mahususi ni kudhibiti contents hasa za taharuki, habari za uongo na kuikosoa serikali bila uthibitisho.

Kama una lengo la kupost hard news na masuala ya siasa chukua tahadhari mapema nenda kasajili. Ila kama unaganga njaa tu nakushauri ujilipue.
 
Back
Top Bottom