Zimbabwe Election: Progress & Results

Zimbabwe Election: Progress & Results

Kuna habari za uhakika vile vile ZANU-PF wanafanya mkutano kesho utakaosimamiwa na R. Mugabe kupanga strategy ya kuwamaliza wapinzani.

Kwa kweli mambo ni magumu sana na kuna watakaopoteza maisha big time, na wanaokwamisha utangazaji wa kura ni Mugabe na wapambe wake wa karibu maana wengi walikuwa wananyanyasa wananchi na watashitakiwa kwa kuvunja haki za binadamu bila kusahau wakuu wa polisi na jeshi ambao wengi wanagwaya. Sasa ndio tuone what next - huwezi kusema re-run election wakati hutangazi matokeo - Miujiza hii!
 
Ni vema unyamaze hata hujui unaongea nini hapa.
Ninyi ndo mmelelewakwenye chupa za Thermos, raha yenu ni kuhimiza ujoto mlouzoea usibadirike.

Ni vema kuheshimu mitazamo ya wengine hata kama inapingana na mtazamo wako.

Majibu mengine ni sawa na kujidharilisha tu...
 
Nakumbuka ile quote yako ya waafrika ndivyo tulivyo. This one caught me by suprise

I was just being sarcastic..
'member Rev. Wright when he said no no no not God Bless America; God Damn America...
I say no no no..not Waafrika Ndivyo Tulivyo bali Waafrika Sivyo Tulivyo....recent case in point...the elections in Zimbabwe that were held a week ago
 
Jongwe bwana anazeeka vibaya sasa! Kura zilipoanza kumwendea vibaya alijaribu kuchonga mbinu za kuleta utaratibu wa muafaka kama ule wa Kibaki na Odinga, lakini yeye akitaka upatikane kabla ya fujo ili aonekane bingwa! Alipotuma "feelers" ikamrudia feedback kuwa kuna uwezekano wa kuzungukwa na kina Tsvangirai. Na hii suala la muafaka fulani wala si siri, Askofu Tutu ndiye aliye-broker hii dili, lakini yeye alitaka Mugabe aachie madaraka kwa "heshima", kwamba Mbeki akaongee naye kama "kaka" kumshawishi hivyo, kwa hiyo angetoa tangazo kuwa anajiuzulu, hatashiriki re-run. Kisha hiyo re-run ingekuwa kati ya Tsvangirai na Makoni, halafu iundwe serikali ya umoja. Lakini watu wa usalama, wakikumbuka kiapo walichosema kuwa hawatakubali mshindi zaidi ya Mugabe, na wanasiasa wa ZANU-PF wanaohofia nafasi zao, kwa pamoja wakamletea Mugabe kitisho kipya. Wakamtishia kuwa hata wakifanya vipi, Makoni hawezi kumshinda wala kumkaribia kwa kura Tsvangirai. Pia wakamtisha kuwa kina Tsvangirai wakiingia madarakani watamgeuzia Mugabe kibao, na hapo hata walio marafiki zake watashindwa kumtetea kwa kuwa then itakuwa kila mtu na lwake. Politburo ya ZANU-PF ikaamua kwa pamoja itasimama na Mugabe hadi mwisho, watafanya hiyo re-run! Mazingira yanawekwa ya kubakisha ushindi kwa Mugabe!

Kuna madai kuwa Mugabe aliwahi kusema licha ya degree saba alizo nazo (zote kasomea, hakuna honorary wala usanii), ati pia anayo degree ya violence!

Jongwe bwana!
 
Nimesoma kwenye yahoo news ofisi za MDC zimevamiwa...

MDC na hotel walioko foreign journalists.... mpaka sasa hivi sijui nini kinaendelea uko Zimbabwe(nimeshapoteza interest) mpaka watakapotangaza mshindi wa urais.
 
Ninadhani walikuwa wanataka kupata data zilizotumika ku-compile results ili wazibebe na watumie ubabe kumtangaza Mugabe kwamba ndiye mshindi! Afrika bana .... bado tuna safari ndefu sana ili kufikia demorasia ya kweli.
 
Koba,
Mkuu wangu umenielewa vibaya sana pengine jinsi navyoandika. Hata siku moja sijasema Mugabe ni kiongozi bora ama ndiye anayetakiwa na wananchi wa Zimbabwe..Na huyo Morgan bila kificho nimesema hafai kwa sababu ndiye mgombea pekee ambaye nyie mnamweka mbele.
Tatizo langu kubwa ni reality yenyewe, nadhni kuna sehemu nimeomba sana watu wamchague Simba ambaye sii popular na uwezekano wa kushinda haupo.
Nachotazama mimi ni mbele siku zote, napima vitu na kuvitazama pande zote mbili kisha kujiuliza what if?..
Simpendi Mugabe na nimeshasema sana kuwa pamoja na wazo la kuchukua ardhi lilikuwa zuri lakini hakuwa na akili ya kufikiria matokeo ya kitendo hicho kama vile Bush alivyovamia Iraq na Afghanstan bila plan B. Initial idea inaweza kuwa nzuri lakini unaposhindwa ku control kile ulichoazimia na matokeo yake yakawa na madhara kuliko ugonjwa wenyewe tena basi imetokana na kutokuwa na upeo mkubwa ndicho kinachoharibu sifa zote za kiongozi huyo...
Hivyo basi maadam Bush anashindwa Iraq haina maana Wairaq wanamwona Saadam ni mbora.. ndivyo navyomwona Morgan kuwa ni kibaraka wa waingereza na nasema hivi sio kwa sababu Mugabe kasema ila ndio ukweli hata kuanzishwa kwa chama hicho kunajulikana. Ni moja ya strategy ya nchi za magharibi (UK and USA) siku zote kumtafuta adui yako ndani pindi wanaposhindwa kukamata uchumi wa nchi ambayo wana interest zao.
So simpendi kweli Morgan lakini haina maana nampenda Mugabe just because kuna wagombea wawili wenye nafasi ya kuchukua madaraka.
Ni kweli pia Uingereza imeupa uchaguzi wa Zimbabwe kipaumbele utadhani news zao zinatoka Zimbabwe kila siku sii chini ya 15 minutes kuhusu Zimbabwe tu jambo ambalo hawakulifanya ktk chaguzi za nchi nyinginezo.. Siwalaumu kwani wanalinda interest zao, hii ni reality na fact ni kwamba Morgan ni mtu wao.
Nachosema mimi kama Mugabe angeachia ngazi na kumwachi mtu mwingine ndani ya ZANU- PF, Je, mngekubali mabadiliko hayo hata kama matokeo ya kiuchumi nchini yangeendelea kuwa mabaya!...
Wakuu tatizo la Zimbabwe kiuchumi ni ZANU-PF na policy yake ya ardhi ambayo Mugabe kama rais anaendelea kuitumia kwa sababu majority ya Wazimbabwe ambao mwaka 1980 walikuwa vijana wadogo wanamapinduzi, wapiganaji wakiwa na umri usiozidi miaka 20, leo hii ndio wapo ktk Uongozi, wazazi, Professional, wanajeshi na kadhalika na hawa kamwe hawatakubali nguvu zao za kuikomboa Zimbabwe wabakie Utumwani na maskini..
Kifupi mkuu nitasema NDIVYO TULIVYO! ni reality amabyo haiwezi kuepukwa iwe kwa Mugabe ama Morgan..
Hakuna spin hapa, nilichoandika jana ndicho kinatokea leo na kesho.. mwisho wa yote majeshi wanachukua nchi mkuu, sio Morgan.
 
Kuna habari za uhakika vile vile ZANU-PF wanafanya mkutano kesho utakaosimamiwa na R. Mugabe kupanga strategy ya kuwamaliza wapinzani.

Kwa kweli mambo ni magumu sana na kuna watakaopoteza maisha big time, na wanaokwamisha utangazaji wa kura ni Mugabe na wapambe wake wa karibu maana wengi walikuwa wananyanyasa wananchi na watashitakiwa kwa kuvunja haki za binadamu bila kusahau wakuu wa polisi na jeshi ambao wengi wanagwaya. Sasa ndio tuone what next - huwezi kusema re-run election wakati hutangazi matokeo - Miujiza hii!

Pamoja na hayo, watu wasiojulikana (huenda ni polisi au Maafisa usalama) wamevamia Ofisi za MDC na kuzipekua usiku. Kwasasa Bw. Mogan Tsvangirai amejificha pamoja na viongozi wa juu wa MDC. Hata mkutano wao waliokuwa wamepanga kuongea na Waandishi wa habari wameufuta.

Kuna uvumi kuwa Mugabe anataka kutangaza hali ya hatari. Kwasasa hali ni mbaya. Mungu awaponye wazimbabwe, uroho wa Mugabe unaendelea kulitia aibu bara la Afrika.
 
mkuu Mkandara tunaposema Morgan ni kibaraka....tunatafsiriwa kuwa tunamsapoti Mugabe kitu ambacho si kweli.....WE ARE AGAINST MORGAN.....APATIKANE MTU MZALENDO KWA AJILI YA ZIMBABWE...MUGABE NI MZEE...NANI ELSE...?
NDO MAANA NILIWAHI KUSEMA ....BTN TWO EVILS CHOOSE THE LESSER....!
 
wazimbabwe kweli ni wana demokrasia ingekuwa nchi nyengine pasingekalika saaa hii tungekuwa tunasikia mauaji na kuharibu mali za nchi na wananchi
 
Morgan might not be as bad as Bob, or at least he hasn't had the chance to prove himself so, but his decision making process is highly suspect.He conducted meetings with Mugabe or his people and lacked the integrity to come clean.

He is offering some controversial concessional deals like a handsome retirement packages to the Mugabe military men, essentially cowardic bribery to have them keep a low profile. He is hardly the Lech Walesa he is made out to be.

Right now some people are feeling Morgan ascended due to the 'Anybody But Mugabe' phenomena.The fact that Mugabe harangued him in the most unbecoming fashion built political sympathy for him and demonized Bob.

He has a chance to redeem himself before his base, Zimbabweans and the world is hugely dissapointed.Time will tell.
to
 
Mgogoro wa Zimbabwe ulianza baada ya Mugabe kutangaza na kutekeleza sera ya ardhi. Nchini Zimbabwe ardi ni tatizo kubwa sana. Wakati wa kupigania uhuru, ZANU-PF walitumia sera ya ardhi kupata wafuasi wengi. Haya yanapatikana ktk nchi nyingi za Kiafrika. Wazungu wanamiliki kwa kiasi kikubwa sana ardi ktk bara la Afrika, hilo halina ubishi.
Ingekuwa aibu kubwa sana kwa Mugabe kuondoka madarakani bila kutekeleza kile wananchi wengi wa Zimbabwe walichokipigania.
Ikumbukwe kuwa, hapo awali kulikuwa na makubaliano kati ya Uingereza na Zimbabwe wakati wa kukabidhi uhuru, nalo lilikuwa ni suala la ARDHI ambapo Waingereza walikubali kutoa fidia kwa wananchi wa Zimbabwe.
Ktk hali ya kustaajabisha, makubaliano hayo yalikiukwa na Uingereza kwa UBABE wao.
Mugabe alipoanza kutekeleza sera yake ya mageuzi ya ardhi, zoezi zima likageuzwa na kuwa ni ukiukwaji wa haki za binadamu. Vyombo vya habari vya kimataifa vikatumika kwa nguvu na gharama zote kuhakikisha kuwa, suala la ardhi linafunikwa na kutubatiza na suala la haki za binadamu.
Hata hivyo, SIKUBALIANI na Mzee Mugabe kwa maamuzi yake ya kuendelea kugombea urais wa nchi hiyo ilhali kuna Wazimbabwe wengi ambao wana uwezo wa kuongoza nchi.
Uwezo wa Morgani kuongoza Zimbabwe ni MDOGO sana. WAZIMBABWE WAPO KTK MATATIZO TAYARI. Mugabe ameishaapa kutomwachia nchi Morgani.
 
Nyani Ngabu,
Mambo bado hayajawaka vizuri Zimbabwe, subiri matokeo ya uchaguzi yatangazwe ndipo utaona "reaction" ya wananchi. Nadhani Zimbabwe WAMELIKOROGA tayari, wanasubiri KULINYWA sasa.
 
Morgan might not be as bad as Bob, or at least he hasn't had the chance to prove himself so, but his decision making process is highly suspect.He conducted meetings with Mugabe or his people and lacked the integrity to come clean.

He is offering some controversial concessional deals like a handsome retirement packages to the Mugabe military men, essentially cowardic bribery to have them keep a low profile. He is hardly the Lech Walesa he is made out to be.

Right now some people are feeling Morgan ascended due to the 'Anybody But Mugabe' phenomena.The fact that Mugabe harangued him in the most unbecoming fashion built political sympathy for him and demonized Bob.

He has a chance to redeem himself before his base, Zimbabweans and the world is hugely dissapointed.Time will tell.
to

Too early to speculate the leadership of Morgan. We should give the man a chance to show his credentials. So far he has shown an incredible level of resilience, which is an important attribute of a leader and a fighter. I have particularly admired this man for having been able to calm down his supporters even after all signs point out that he may have won the presidential election. This explains his level of selfless and love of life for his people. We didn't see this level of restraint in Kenya's odinga, following the aftermath of their elections, whose consequence we all well remember.

In any case, for the level that Mugabe has reached, even a primary school leaver would be a better option than him!
 
wazimbabwe kweli ni wana demokrasia ingekuwa nchi nyengine pasingekalika saaa hii tungekuwa tunasikia mauaji na kuharibu mali za nchi na wananchi

Hongera tena Mkuu naona hii post imeanza kuifukzia namba ya 3000. Mawazo yangu mimi naona Wazimbabwe ni wavumilivu kinyume ya hili na sisi WTZ pia tuwana demokrasia kama kigezo ni uvumilivu.
 
Koba,
Mkuu wangu umenielewa vibaya sana pengine jinsi navyoandika. Hata siku moja sijasema Mugabe ni kiongozi bora ama ndiye anayetakiwa na wananchi wa Zimbabwe..Na huyo Morgan bila kificho nimesema hafai kwa sababu ndiye mgombea pekee ambaye nyie mnamweka mbele.

Tatizo langu kubwa ni reality yenyewe, nadhni kuna sehemu nimeomba sana watu wamchague Simba ambaye sii popular na uwezekano wa kushinda haupo.

Kifupi mkuu nitasema NDIVYO TULIVYO! ni reality amabyo haiwezi kuepukwa iwe kwa Mugabe ama Morgan..
Hakuna spin hapa, nilichoandika jana ndicho kinatokea leo na kesho.. mwisho wa yote majeshi wanachukua nchi mkuu, sio Morgan.

Mkandara....pamoja na ukweli kwamba umpendi Mugabe wala Morgan lakini sasa hali ilivyo ni kwamba kati ya hao mmojawao atakuwa Rais wa zim, kwa hiyo ungekuwa wazi kusema kwamba afadhali ya Mugabe kuliko Morgan...maana hapa hakuna options nyingine labda hiyo ya jeshi unayoisema....hapa ni kama mama mjamzito yuko kwenye uchungu na lazima ajifungue hakuna jinsi...kwa mfano kama ulikuwa unataka mtoto atakayezaliwa awe wa kiume au kike na ghafla muda mfupi kabla ya kujifungua unagundua jinsia ya mtoto siyo uliyokuwa unaitaka hata ufanyaje lazima huyo mama ajifungue. Hii ndo hali ilivyo ZIM... kwa sasa ni kati ya Mugabe na Morgan...na si vinginevyo...kwa hiyo utamke kabisa kwamba afadhali ya Mugabe....hakuna njia nyingine zaidi.

Mimi nasamaje...bora achukue huyo Morgan...maana si lazima uwe kibaraka wa USA au UK...tunayoyaona hapa kwetu ni matokeo ya nini? EPA, Richmonduli nk...ni matokeo ya watu kulewa madaraka na kutokuwa na wasiwasi kwamba siku moja wananchi wa Tanzania wanaweza kuongea tofauti na matakwa na matarajio yao...sasa mwache Morgan achukue nchi bwana....
 
Back
Top Bottom