Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 40,949
- 74,431
Dhamira ya Mugabe ilikuwa nzuri sana tokea zamani kwa mustakabali wa raia wa Zimbabwe. Tatizo lililotokea Zimbabwe halina tofauti kabisa na hali ya kwetu. Kuwa hiyo nia njema aitakayo mtu haipaswi kufikiriwa njia za kuifuata kwa mawazo ya mtu mmoja bali kwa kufuata sheria na kanuni mnazojiwekea huku ikishirikisha watu na vyombo mbalimbali kama sera ya nchi.
Mugabe alikuwa anafanya maamuzi jinsi anavyojisikia au anavyo shauriwa na mkewe tena bila woga. Hivyo nia yake njema ikawa ni ubabe na mipango duni mbele ya jamii na mwisho akaitia umasikini mkubwa Zimbabwe huku yeye na familia yake wakiwa matajiri sana. Walianza kuficha utajiri wao (kama hapa kwetu) lakini utajiri ukikomaa moyoni ni vigumu tena kuuficha.
Tujifunze hata sisi kutoka Zimbabwe, haya mambo ya mimi siambiwi la kufanya kama vile Taifa ni mali yako, kuto kaa meza moja na wenye mawazo tofauti nawe, kukomesha wenye nacho nk hayatatufikisha pazuri zaidi ya nchi kiuchumi kuangukia pua na mwisho haya yanayotokea sasa