Kitila Mkumbo
JF-Expert Member
- Feb 25, 2006
- 3,353
- 1,935
Nimejaribu kusoma hapa na pale kuhusu uchaguzi wa kesho Zimbabwe. Inafurahisha kwamba angalau watu wengi sasa hatimaye wameweza kuona ubaya wa Mugabe na inaonekana kesho wameamua liwe na lisiwe hawatampigia kura Mugabe. Katika somasoma yangu pia nimegundua kuwa bado kuna watu wa kutosha, japokuwa si kwa kiwango cha kumpa ushindi Mugabe, ambao bado wanampenda Mugabe. Sasa mimi najiuliza hivi hawa watu wanataka Mugabe awafanyeje ndio wamchukie maana ameshawatenda kila aina ya ubaya unaoweza kufikiria? Ninaamini kwa haya aliyokwisha kuyafanya Mugabe ingekuwa ni kwa wenzetu wazungu, hata kura za watoto na mke wake asingezipata. Sasa mimi ndio najiuliza sisi waafrika tuna matatizo gani inapokujwa kwenye kuchagua viongozi?
Ok, kwa Tanzania watu wanaoendelea kuipigia kura CCM wanatoa visingizio kwamba wapinzani wapo wachache wenye uwezo na hawana sera. Haya, na huko Zimbabwe? Mbona upinzani wameshusha kila aina ya sera na kila mwanasiasa hodari yupo kwenye upinzani, iweje basi watu waendelee kumpigia kura Mugabe na CCM ( or sorry I mean, ZANU-PF) yake?
Kibaya zaidi ni kwamba jeshi eti limesema halitatambua mshindi mwingine zaidi ya Mugabe! Sasa najiuliza tena hawa wanajeshi wa nchi zetu mafunzo yao yakoje kiasi kwamba wanashindwa kuelewa wajibu wao kwa kiwango hiki? Halafu lijamaa (Mugabe) limesema eti ikibidi litatumia style ya Kibaki huko Kenya, na limewaonya MDC ole wao wafuata mtindo aliotumia Odinga, watakiona cha mtema kuni-hii hapa soma: http://www.guardian.co.uk/commentisfree/2008/mar/28/zimbabwe
Sasa mimi ndio najiuliza, sisi wabongo (Waafrika) tuna matatizo gani hasa kwenye mambo haya ya kuchaguana?
Je, tunahitaji nadharia (theories) maalumu kwa ajili ya kuelewa siasa za Afrika?