Kinachoendelea katika nchi ya Afrika Kusini ni ishara Gani?

Kinachoendelea katika nchi ya Afrika Kusini ni ishara Gani?

kadeti

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2011
Posts
1,330
Reaction score
1,412
Ni masikitiko makubwa sana Kwa kuona zile harakati zinazofanywa na wazawa wa nchi ya Afrika Kusini dhidi ya ndugu zao Waafrika wanaotoka katika nchi mbali mbali hasa zile nchi kama Ghana, Nigeria, Ethiopian, Zimbabwe, Tanzania wanasahau kwamba bila ya hizo nchi Leo Afrika Kusini kungekuwa na historia nyingine....zaidi ya hichi wanachokifanya.

Dhambi ya xenophobia ambayo Wananchi wa Afrika Kusini wanaifanya kama wakiendelea haitakuja kuwaacha salama.

Wananchi wa Afrika Kusini kukosa kazi,kukosa maisha Bora, kukosa maji safi, kukosa ardhi nzuri yenye rutuba, kukosa mahitaji muhimu ya binadamu hayajasababishwa na kuwepo Kwa Waafrika wenzenu wanaoishi apo, kukosekana Kwa ayo maitaji ni mfumo uliojengwa tangu utawala wa makaburu...

Na kusudi waweze kuliponya Taifa na kuendelea mbele...wanapaswa kufanya yafuatayo.

1. Waache mara moja kuwabagua weusi wenzao Kwa maana wengi wao wanavibali halali vya kuishi apo.

2. Wananchi wa Afrika Kusini wapunguze uvivu wa kufanya kazi, waache kabisa tabia za kufanyiwa kila kitu na kulipiwa kila hitaji lao,km maji, umeme na matibabu....pia wapunguze km siyo kuaacha kabisa tabia za ulevi,na uzinzi vitendo ambavyo vinachochea uvunjifu wa maadili.

3. Wakubali na kuanza upya juu ya kujifunza kutoka Kwa Wageni, na wabadilishe mfumo wao wa elimu hasa kuanzia chini kabisa....waende na mfumo wa vocational training(education)

4. Serikali yao ianze kubadilisha sera zao za uhamiaji....hasa Kwa wale watu wenye maujuzi na watu wenye mitaji mikubwa kuwapa kipaumbele kuingia nchini kwao, hii itachochea ukuwaji wa huchumi na kuwa fanya Waafrika Kusini kujifunza kutoka kwao wahamiaji halali ndani ya Taifa lao....km sasa hivi apartment nyingi zilizopo ktk miji mikubwa ni ya Wageni na Wala siyo ya Waafrika Kusini, pili hata maduka makubwa na mage rage siyo ya wazawa ni ya Wageni kwaiyo Kuna vitu vya kujifunza Kwa Waafrika Kusini
 
Kwa nini haukubaliani nayo mkuu?
Mambo ya nchi kusema tuliwasaidia kupata uhuru yamepitwa na wakati hakuna nchi inayotawaliwa na wakoloni moja Kwa moja mpaka sasa uhuru ungepatikana tu ,mtu asiseme kama sio juhudi za Fulani uhuru tusingeupata Hakuna jambo la hovyo kama hili ,point yangu ni hakuna nchi Afrika inatawaliwa na wakoloni moja Kwa moja mpaka sasa tusitukuze watu bila sababu.
 
Nelsons Mandela alipewa passport ya kutembelea na Taifa la Ethiopia kipindi chote hicho kabala ya kwenda Jela.
 
Sila walizokuwa wakitumia kupigania dhidi ya Wazungu /makaburu nyingi zilitoka/zilikuwa zikiifadhiwa Zimbabwe
 
Mleta mada anataka kutuaminisha kuwa bila hizo nchi alizotaja majority rule isingepatikana nchi Afrika kusini kitu ambacho si kweli.
😆😆😆😆😆😆😆
1-SA ilikaliwa na makaburu katika ujazo "mzuri" ambapo walishindwa hata kufurukuta.Kwa ufupi SA walibanwa mnoo na kushindwa kuendesha mapambano ya Uhuru wao ndani kwa ndani.Hata kama baadhi/wachache walijumuika kwenye mapambano,hayakuleta tija kubwa kwa kiasi hitajika.
2-Wengi wa wapigania Uhuru wa SA ilibidi watoke nje ya nchi yao ili kupata mafunzo ya "ideologies" na mapambano ya kimsituni/mapigano kijeshi zaidi.
-Waliomba kwa nchi jirani msaada wa kupambana physically na wakoloni na walisaidiwa sana.
HOJA NI NINI?
-Ilikuwa kuongezewa elimu/ideas za mapambano kwa hamasa,
-kuongezewa ujuzi na silaha za mapigano,
-kuongezewa idadi ya wapambanaji/askari dhidi ya wakoloni.
-Kuandaa wasomi wa kuja kuendesha nchi.
Hivyo basi,ukiangalia nchi nyingi za Afrika zilizokuwa kwenye harakati za ukombozi zilifanikiwa miaka ya mwishoni mwa '50,60,70 nk.Lakini SA ilichelewa hata baada ya kusaidiwa.Tujiulize;Je,isingepata msaada wa nchi zingine za Afrika wangeweza hata kufanya uchaguzi huru na kuwa huru mwaka 1992?Msaada wa majirani uliwakomboa kwa haraka.Laa sivyo,wangekuwa wanajiliza na kuifuta kamasi vitongoji vya SOWETO hadi leo bila uhuru wala kupumzika.
 
Mkuu ungeona aina ya vijana kutoka Mbagala, Kigogo, Temeke na maeneo mengine ya Dar wanaoenda Afrika kusini usingelaumu wazawa kuwakataa wageni. Vijana wengi wanaoenda huko huwa ni vibaka wa hatari na wakifika huko wanachokifanya ni uhalifu. Wasauzi wanapitia madhila mengi yanayoletwa na baadhi ya wageni. Kuna dogo alikuwa kibaka hatari maeneo ya Kigogo enzi za Magu akakimbilia SA. Akaenda kuendeleza uhalifu. Mbaya zaidi hawa vijana wanakufa sana kwa kuuwawa na wasauzi pia wao kwa wao kuuana.
 
😆😆😆😆😆😆😆
1-SA ilikaliwa na makaburu katika ujazo "mzuri" ambapo walishindwa hata kufurukuta.Kwa ufupi SA walibanwa mnoo na kushindwa kuendesha mapambano ya Uhuru wao ndani kwa ndani.Hata kama baadhi/wachache walijumuika kwenye mapambano,hayakuleta tija kubwa kwa kiasi hitajika.
2-Wengi wa wapigania Uhuru wa SA ilibidi watoke nje ya nchi yao ili kupata mafunzo ya "ideologies" na mapambano ya kimsituni/mapigano kijeshi zaidi.
-Waliomba kwa nchi jirani msaada wa kupambana physically na wakoloni na walisaidiwa sana.
HOJA NI NINI?
-Ilikuwa kuongezewa elimu/ideas za mapambano kwa hamasa,
-kuongezewa ujuzi na silaha za mapigano,
-kuongezewa idadi ya wapambanaji/askari dhidi ya wakoloni.
-Kuandaa wasomi wa kuja kuendesha nchi.
Hivyo basi,ukiangalia nchi nyingi za Afrika zilizokuwa kwenye harakati za ukombozi zilifanikiwa miaka ya mwishoni mwa '50,60,70 nk.Lakini SA ilichelewa hata baada ya kusaidiwa.Tujiulize;Je,isingepata msaada wa nchi zingine za Afrika wangeweza hata kufanya uchaguzi huru na kuwa huru mwaka 1992?Msaada wa majirani uliwakomboa kwa haraka.Laa sivyo,wangekuwa wanajiliza na kuifuta kamasi vitongoji vya SOWETO hadi leo bila uhuru wala kupumzika.
Sidhani kama wangefika hadi leo wakiwa chini ya kibano kikali Cha makaburu.
 
Sidhani kama wangefika hadi leo wakiwa chini ya kibano kikali Cha makaburu.
Bado wanapaswa kuwa na kashukurani hata kadogo kwa Waafrika wenzao waliokuwa nao sambamba kwenye kilio chao.Ni kweli wasingetawaliwa milele(ingawa bado indirect wanatawaliwa na wazungu)lakini wangechelewa sana.Boers walijua kuwabana,,kuwatesa na kutowapa pumzi.Kule ndiko kungeitwa kupelekewa moto kwa zama hizi.
 
Shida yao wanapigana na adui asiye halisi. Inabidi wapigane na serikali yao na si wageni.

Wanavyowafukuza wageni serikali yao ndo inafurahi kwa sababu serikali ndo chanzo cha matatizo yao.
 
Sidhani kama wangefika hadi leo wakiwa chini ya kibano kikali Cha makaburu.
Bado wanapaswa kuwa na kashukurani hata kadogo kwa Waafrika wenzao waliokuwa nao sambamba kwenye kilio chao.Ni kweli wasingetawaliwa milele(ingawa bado indirect wanatawaliwa na wazungu)lakini wangechelewa sana.Boers walijua kuwa ana,kuwatesa na kutowapa pumzi.Kule ndiko kungeitwa kupelekewa moto kwa zama hizi
Shida yao wanapigana na adui asiye halisi. Inabidi wapigane na serikali yao na si wageni.

Wanavyowafukuza wageni serikali yao ndo inafurahi kwa sababu serikali ndo chanzo cha matatizo yao.
Hao watu ni bure kabisa.Mwingine,juzi-kati kampiga risasi mama (asiye msouth)muuza chakula barabarani kwa kudaiwa hela ya alichokula.Kwa nini asingeenda sehemu ambazo serikali yake inatoa huduma ndipo akaanzishe sakalambanda/fujo zake?Mgeni anahusikaje na ukosefu wa huduma za nchi?Au wageni ni wabia wa serikali ya South Africa?
 
Ni masikitiko makubwa sana Kwa kuona zile harakati zinazofanywa na wazawa wa nchi ya Afrika Kusini dhidi ya ndugu zao Waafrika wanaotoka katika nchi mbali mbali hasa zile nchi kama Ghana, Nigeria, Ethiopian, Zimbabwe, Tanzania....wanasahau kwamba bila ya hizo nchi Leo Afrika Kusini kungekuwa na historia nyingine....zaidi ya hichi wanchini kwao, hii itachochea ukuwaji wa huchumi na kuwa fanya Waafrika Kusini kujifunza kutoka kwao wahamiaji halali ndani ya Taifa lao....km sasahivi apartment nyingi zilizopo ktk miji mikubwa ni ya Wageni na Wala siyo ya Waafrika Kusini, pili hata maduka makubwa na mage rage siyo ya wazawa ni ya Wageni kwaiyo Kuna vitu vya kujifunza Kwa Waafrika Kusini
Africa kusini ni nchi ya kijinga. Hata mabaria wanaozamiaga sehemu za huko kama vile Durban, Kwa zulu Natal sijui wanavutiwaga na nini huko, wakati kuna nchi nyingine za Africa hapahapa zenye utulivu na good living standard
 
Huwa wanadanganyana(kupeana taarifa za uongo)na huwa wanawafuata masela wenzao wakaendeleze maisha ya hovyohovyo na ugangwe mdebwedo.Na wazulu siyo watu wale.Wanawapiga risasi wajinga kama hao kila leo.
 
Bado wanapaswa kuwa na kashukurani hata kadogo kwa Waafrika wenzao waliokuwa nao sambamba kwenye kilio chao.Ni kweli wasingetawaliwa milele(ingawa bado indirect wanatawaliwa na wazungu)lakini wangechelewa sana.Boers walijua kuwa ana,kuwatesa na kutowapa pumzi.Kule ndiko kungeitwa kupelekewa moto kwa zama hizi
Ni kweli Kwa sababu viongozi wa nchi zilizopata uhuru walifanya jitihada kubwa kuhakikisha ubaguzi wa rangi unakoma.
Hao watu ni bure kabisa.Mwingine,juzi kampiga risasi mama (asiye mouth)muuza chakula barabarani kwa kudaiwa hela ya alichokula.Kwa nini asingeenda sehemu ambazo serikali yake inatoa huduma ndipo akaanzishe sakalambanda/fujo zake?Mgeni anahusikaje na ukosefu wa huduma za nchi?Au wageni ni wabia wa serikali ya South Africa?
Unaweza ukakuta hii ndiyo mbinu inayotumiwa na serikali yao (kutengenezaa adui bandia) ili watu wasitambue kuwa chanzo halisi cha ugumu wao wa maisha ni serikali. Si unajua serikali za kiafrika zilivyo!
 
Ni kweli Kwa sababu viongozi wa nchi zilizopata uhuru walifanya jitihada kubwa kuhakikisha ubaguzi wa rangi unakoma.

Unaweza ukakuta hii ndiyo mbinu inayotumiwa na serikali yao (kutengenezaa adui bandia) ili watu wasitambue kuwa chanzo halisi cha ugumu wao wa maisha ni serikali. Si unajua serikali za kiafrika zilivyo!
Inawezekana lakini wasouth ni wakorofi na wana roho mbaya sana.
 
Back
Top Bottom