Yaliyojiri Ikulu Dar: Rais Magufuli amtaka CAG Kichere kutojifanya Muhimili mwingine, amwambia anaweza kuondolewa hata akiwa na mwaka mmoja

Anamuapisha CAG mteule, anasema maneno ya msingi sana.

1. Usiende kujifanya na wewe ni Muhimili, Mihilimi ni mitatu tu. (ASSAD alijiona muhimili eeh)

2. Una nidhamu sana, unatenguliwa hapa, na pale, lakini haulalamiki

3. Una elimu nzuri na uzoefu wa kazi.
Assd alikuwa anavimbishiana kifua na Spika Ndugai kumbe Ngosha anawaangalia tu akisema hiiiiiii.
 
Jiwe anapenda sana kuogopwa na kuabudiwa! Sijui hata hao watoto wanaishije na baba kama huyu!
 
Nakumb
Mkuu naona una copy na ku paste , taifa letu lina wanasheria lukuki, utata sakata la CAG, ni fursa nzuri kufungua hoja madai katiba bora.
Wote mnakumbuka shangazi fatma karume alifungua kesi juu ya ukiukwaji wa katiba uteuzi wa mwanasheria mkuu was serikali, kilichomkuta ni kufungiwa uwakili Tanganyika. Km taifa tunasafari ndefu juu ya utawala was sheria
 
Shall be eligible maana yake eligible sio mtu mmoja pekee, wakitoke eligible wengine wewe wa wakati huo unawapisha na wao waifanyie kazi sifa hiyo ya kustahiki.
 
Binafsi natoa pongezi kwa Ikulu kufanya uteuzi,pia nawatakia kazi njema wateule wote katika kulihudumia taifa.
Kama mpenda maendeleo,macho yangu yatatazama sana kwa Kamishna wa Kazi na CAG maana napenda matumizi mazuri ya Raslimali watu na Fedha.
Amani na Utulivu Daima.
 
Nipo siti ya mbele hapa kusikiliza sababu za kushindwa kumwongezea CAG awamu ya pili.
Limekupita hata baada ya kukaa kiti cha mbele kweli ww bongo lala kweli! Muda wake umekwisha na Tz ina watu zaidi ya mil 54! Hivyo tupo wengi sana tunaoweza kufanya kazi ya CAG!
 
Inasikitisha sana, katika kila idara nyeti serikalini anaweka watu ambao watakuwa ni wenye kukubaliana na yale ayatakayo hata kama yako kinyume na sheria.

Tuliamini ya kuwa katiba ni sauti ya uma lakini si kwa utawala huu dhalimu. Pamoja na Katiba yetu kuwa na mapungufu mengi lakini bado ilipaswa kuheshimiwa.

Kwa sasa nchi inaongozwa bila ya kuzingatia misingi ya katiba, alitakalo yeye ndilo alifanyalo bila kujali matokeo yake.

MUNGU INUSURU TANZANIA
 
ataondoka 2035, atakuja mwengine, at that time yeye atakuwa THE HAGUE
Nani wa kumpeleka huko mwenyekiti wa SADC, angalia anavyopanga team yake, kuanzia bungeni, mahakamani na serikalini.

Usije ukashangaa sasa ATCL ikakaguliwa an report ya manunuzi ya ndege kwa cash ikatolewa.

Stone is building fortress wall around him.
 
Hakuna aliye huru awamu hii,kila kiongozi analazimishwa kupiga 'kagoti flani'...najiuliza wanavyompamba na kumwogopa hivi ikiibuka ile 666 kunamtu atapinga kweli!??
Ogopa mtu anakwambia kuna 'mwenye' serikali sio kuna 'wenye'... inamana serikali ni yake sio ya wananchi...basi nchi ni yake pia maana anaamua apendavyo!!! Aibu ajabu,bora tungekuwa hatujawahi onja demokrasia.
Shida ni lugha,unaweza kuta anamaanisha kile ambacho ungependa kukisikia.
 
Kuna ma CAG wawili leo

kasema Assad anamaliza mkataba wake leo saa sita usiku

Kichere anamtaka aripoti kazini mapema kesho asubuhi

lakini kamuapisha leo! Sasa leo sijui nani kalipwa mshahara leo?

hahaahaaaaa

Halafu Kichere akifika kesho asubuhi anatakiwa aanze kusafisha ofisi, watu wa Hazina watamwambia machafu chafu yako wapi... hahahahaaaaaaa....

Yani kam-maindi Assad vibaya mno lakini alishindwa kumchomoa, japo kamchimbia biti Kichere kwamba anaweza kumpangurua anytime!
 
Hivi Dodoma kashindwa kabisa kwenda uko? Nashindwa kuelewa kabisa ilikuwa ni siasa au mkakati nilitegemea mambo kama aya yafanyike Dodoma maana juzi tu kasema kashaamia uko.
Umeangalia kila kona umekosa cha kupinga umerukia Dodoma nyie watu wa ajabu sana
Ikulu haijaisha,kashauriwa tu si vizuri kupishana kwenye Corridor na mafundi,soon atakwenda naona roho inakuuma sana
 
November 4 , 2019
Dar es Salaam, Tanzania

Majaji 12 wapya wa Mahakama Kuu walioteuliwa, wala viapo vyao leo katika Ikulu ya Dar es Salaam nchini Tanzania mbele ya Mh. Rais John Pombe Joseph Magufuli.

Walioteuliwa ni;

Dkt. Zainabu Diwa Mango, Kabla ya uteuzi huu Dkt. Zainab Diwa Mango alikuwa Wakili wa Serikali Mkuu katika Ofisi ya Taifa ya Mashtaka.

Edwin Elias Kakolaki, Kabla ya uteuzi huu Edwin Elias Kakolaki alikuwa katika Ofisi ya Kupambana na Kuzuia Dawa za Kulevya Nchini.

Dkt. Deo John Nangela, Kabla ya uteuzi huu Dkt. Deo John Nangela alikuwa katika Ofisi ya Tume ya Ushindani (Fair Competition Commission – FCC).

Fredrick Kapela Manyanda, Kabla ya uteuzi huu Fredrick Kapela Manyanda alikuwa katika Ofisi ya Taifa ya Mashtaka.

Elizabeth Yoeza Mkwizu, Kabla ya uteuzi huu Elizabeth Yoeza Mkwizu alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani.

Augustine Karichuba Rwizile, Kabla ya uteuzi huu Augustine Karichuba Rwizile alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama.

Ephery Sedekia, Kabla ya uteuzi huu Ephery Sedekia alikuwa Katibu wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (Attorney General – AG).

Angaza Mwaipopo, Kabla ya uteuzi huu Angaza Mwaipopo alikuwa katika Ofisi ya Rais, Ikulu.

Joachim Charles Tiganga, Kabla ya uteuzi huu Joachim Charles Tiganga alikuwa Naibu Msajili Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Kassim Ngukali Robert, Kabla ya uteuzi huu Kassim Ngukali Robert alikuwa katika Ofisi ya Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu cha Wizara ya Fedha na Mipango.

Said Mashaka Kalunde, Kabla ya uteuzi huo, Said Mashaka Kalunde alikuwa katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Angela Antony Bahati, Kabla ya uteuzi huo, Angela Antony Bahati alikuwa Katibu Msaidizi wa Tume ya Kurekebisha Sheria.

Maneno ya Jaji Mkuu wa Tanzania:

Jaji Mkuu wa Tanzania awataka Majaji walioapishwa kufuata Sheria Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma, amewataka Majaji 12 wa Mahakama Kuu walioteuliwa na baadaye kuapishwa na Rais John Magufuli, kutekeleza majukumu yao kwa kufuata sheria na kamwe wasifanye upendeleo.

Akizungumza wakati wa hafla ya kuwaapisha Majaji hao pamoja na viongozi wengine Ikulu jijini Dar es salaam, Jaji Mkuu amesisitiza kuwa Majaji hawana Polisi wa kuwachunga, hivyo vi vema wakajichunga wenyewe na kujitathmini kila wakati wakifanya kazi zao.

Jaji Mkuu amesema kuwa mashauri bado ni mengi yanayohitaji kufanyiwa kazi haraka, hivyo ni vema wakahakikisha wanayafanyia kazi na kuhakikisha hukumu zinatoka kwa wakati.

Amemshukuru Rais Magufuli kwa kuiongezea Mahakama Kuu Majaji 12, na kuongeza kuwa kwa sasa Mahakama Kuu itakuwa na Majaji 78 kutoka 66 waliokuwepo hapo awali. Amesema kuwa kwa ongezeko hilo, Jaji mmoja wa Mahakama Kuu kwa sasa itakua na uwezo wa kushughulikia mashauri 220 kwa mwaka, badala ya mashauri 518 ambayo walikuwa wakiyashughulikia kabla ya ongezeko la Majaji hao 12.

Halfa ya kuwaapisha Majaji hao pamoja na viongozi wengine, pia imehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, - Job Ndugai.
 
Back
Top Bottom