benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,504
- 3,034
Mbunge wa zamani wa Nyamagana kupitia CHADEMA EZEKIEL WENJE amenukuliwa akisema kuwa kama Rais wa Awamu ya Tano, Marehemu Dkt John Pombe Magufuli angekuwa hai basi asingekubali hali aliyoiita "ufisadi" huu uliotajwa kwenye ripoti ya CAG.
Nimeshangazwa sana na kauli hii ya Wenje na nimejiuliza kama ni amekuwa MSAHAULIFU, AMEKUWA MNAFIKI au UWEZO WAKE WA KUFIKIRI umepungua tangu aende kuishi Ughaibuni akiukimbia utawala wa huyuhuyu Magufuli anayemhubiri leo.
Wenje anasahau kuwa
1. MAMBO YOTE YA "PLEA BARGAINING" YALIANZISHWA NA JPM, hivyo leo tunapowasema kina Biswalo, kina Dotto James, Baba yao alikuwa JPM
2. Tunamkumbusha tu kuwa ni JPM huyuhuyu ambaye aliuminya uhuru wa CAG, (Sote tunakumbuka yaliyomkuta ASSAD), alimuondoa CAG kinyume na Katiba kwa kufichua madudu ya Serikali yake na pengine kama huyo JPM angakuwa hai leo RIPOTI YA CAG Isingetoka na taarifa kama hizi (INGEFICHA MENGI)
3. Ni wakati wa JPM tuliona TTCL eti ikitoa gawio kwa Serikali lakini leo kutokana na kukua kwa uwazi na ukweli tumeambiwa inaendeshwa kwa hasara na ina madeni hewa ya karibu Bilioni 21.
CAG amefichua uchafu na makosa anasatahili pongezi lakini, WENJE kuja na porojo za JPM ni kutufanya Watzania hatuna kumbukumbu kama yeye suala ambalo hatuwezi kulikubali