Yaliyojiri Ikulu Dar: Rais Magufuli amtaka CAG Kichere kutojifanya Muhimili mwingine, amwambia anaweza kuondolewa hata akiwa na mwaka mmoja

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,454
3,417
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, leo Novemba 4, 2019 kuanzia majira ya saa tatu na nusu (3:30) asubuhi atawaapisha viongozi mbalimbali aliowateua hivi karibuniWanaoapishwa ni pamoja na;
1. Charles Edward Kichere kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (Controller and Auditor General – CAG)

2. Katarina Tengia Revocati kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe.

3. Mhandisi Aisha Amour kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kuwait.

4. Kanali Francis Ronald Mbindi kuwa Kamishna wa Kazi katika Ofisi ya Waziri Mkuu

Aidha, Mhe. Rais Magufuli anawaapisha Majaji 12 wa Mahakama Kuu
*****

1.jpg

IKULU: Charles Kichere akiapa kuwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) akichukua nafasi ya Prof. Mussa Assad aliyekuwa CAG kwa miaka mitano - CAG Kichere alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe na awali alikuwa Kamishna Mkuu wa TRA

UPDATES:
Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma: Leo ni siku ya shukrani na tunamshukuru Rais kwa kutuongezea nguvu kazi. Tumeweza kupata watu bora Namshukuru pia Msajili Mkuu wa Mahakama kwa utumishi uliotukuka Mahakamani na naamini akifika Njombe atafanya kazi zaidi

1572857501332.png

Prof. Juma: Asante Rais kwa kutuongezea Majaji 12, tukiondoa Majaji 2 wenye majukumu maalumu, nguvu kazi inabaki ni Majaji 76 - Majaji 2 watastaafu mwisho wa mwaka na watabaki 74 na mzigo kwa kila Jaji kwa sasa ni mashauri 518 na uwezo wa kila Jaji ni mashauri 220

Prof. Juma: Majaji tumejiwekea utaratibu wetu katika utendaji. Mfano, kila mwaka tunatakiwa kutoa mashauri angalau 220 kila Jaji, kuangalia hukumu zinatoka kwa wakati - Tuna mfumo wa kujiangalia wenyewe na kwa kujiangalia tunakuwa tunarudisha imani tuliyopewa na Katiba
*****

Spika Job Ndugai: "Mlioteuliwa leo mmepata imani ya Rais Magufuli. Na kwa vile Watanzania walimuamini Rais Magufuli, basi mmepata imani ya Watanzania. "Ndugai akitoa neno kwa wateule walioapishwa na Rais leo. "Nakupongeza sana Mhe.rais kwa teuzi hizi, nawapongeza sana walioapishwa leo, mna imani ya watanzania, mnalo jukumu kubwa, tunawategemeeni sana"

Spika Job Ndugai: "Niwapongeze walioteuliwa, mmepewa imani kubwa kwa walioteuliwa. Kwa kuwa sisi sote tulimpa imani kubwa Mhe. Rais Dkt. Magufuli mjue pia mna imani ya watanzania wote. "CAG Kichere karibu sana, sisi Bunge tunaanza shughuli zetu kesho za kuangalia mipango ya Taifa ambayo inaweka vipaumbele ambavyo vitaisaidia Serikali kuona ni aina gani ya Bajeti ya Serikali ambayo itakuja 2020/21, wewe CAG ndio jicho letu tunakutegemea."

1572858364252.png

Spika Job Ndugai: "Hivi karibuni Mhe. Rais alitembelea Gereza la Butimba na kutoa maagizo, hata mimi huwa natembelea sana Gereza la Kongwa, nawaomba majaji mkafanye kazi yenu ili kila mtu apate haki yake, anayestahiki kukaa gerezani akae asiyestahiki atolewe na arudi uraini. "Jicho ndiyo kila kitu kwa Binadamu bila jicho hujui unaenda wapi kwahiyo wewe CAG ni jicho letu tunakutegemea kushauri kuona namna ya kurekebisha na taaarifa yako inapojadiliwa Bungeni huwa ni taarifa nzito, tunaahidi kukusaidia kazi yako ni nzito."
*******

1572857611489.png

Rais Magufuli: Nawapongeza wote mlioapa leo. Zingatieni viapo vyenu mlivyovisoma leo. Pia, mkamtangulize Mungu katika kazi zenu - Nimeambiwa mmoja wa Majaji walioapa leo alifiwa na mke wake wiki iliyopita. Kassim pole sana, roho ya Marehemu ipumzike kwa Amani

Rais Magufuli: Ndugu zangu Majaji kafanyeni kazi ya haki. Judgement huwa inatolewa na Mungu tu ila kwa hapa Duniani mpo ninyi - Katoeni hukumu kwa haki ila haki hizo pia msizicheleweshe kwa sababu changamoto zipo sehemu mbalimbali, Waheshimiwa wamesema hapa

Rais Magufuli: Nakumbuka Jaji, aliyekuwa kwenye Fair Competation (si ni wewe?), huyu wakati akifanya kazi alishaamuliwa kufukuzwa kwasababu alisimamia haki - Walikuwa wanamshangaa kuona Mchaga asiyependa rushwa. Kwasababu pale kwenye Fair Competation kuna kazi

Rais Magufuli: Nendeni mkatimize wajibu wenu, mkawatumikie Watanzania hasa wanyonge ambao haki zao zinapotea - Mkienda kufanya kazi vizuri mtaipunguzia Tume ya Haki za Binadamu mzigo. Kafanyeni kazi

Rais Magufuli: Kamishna wa Kazi nawe kasimamie kazi hivyo hivyo, pale kuna changamoto nyingi. Kawanyooshe Wizara ya Kazi - Malata alifanya kazi nzuri ndio maana nimekaa naangalia muda wote nikaona panafaa Mwanajeshi wenye Qualification. Usiende pale kazi zikawa za hovyo

Rais Magufuli: Kwa CAG mpya nakutakia kazi njema. Usiende huko ukajifanya Muhimili. Mihimili ni mitatu tu na umeiona hapa Mahakama, Bunge na Sisi wa Serikali - Katika Kiapo chako ni Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali, kwa hiyo mwenye Serikali yupo

Rais Magufuli: Kafanye kazi zako za ukaguzi vizuri bila kuonea mtu. Unapopewa kazi na Mihimili mingine kama Bunge, katekeleze. Usibishane nao - Ukipewa maagizo na Mahakama katekeleze, wewe ni Mtumishi. Lakini pia kasimamie hiyo ofisi, kasimamie watendaji wako

Rais Magufuli: Kuna baadhi ya watendaji wako wanapopewa jukumu la kwenda kukagua kwenye Balozi wanalipwa fedha hapa na wakifika kule wanaomba pesa - Sitaki nikutajie majina yao, wewe nenda kule kachambue mwenyewe kwenye ofisi hii. Ofisi ya CAG sio Clean kama mnavyofikiria

Rais Magufuli: Nenda ukapange nafasi za watu wako ili mauchafuuchafu haya ukayasafishe. Najua una Qualification nzuri tu na hatufanyi makosa ktk kuteua - Form 4 umetoka na Div. I, Form 6 Div. I. Hii ni kuonesha wewe ni Kipanga sio Kilaza. Ukachukua Shahada ya Sheria na Account

Rais Magufuli: Tunakuamini. Pia, una heshima, umetolewa kwenye Ukamishna Jenerali wa TRA hukusema neno, 'You're humble, very polite' ukaenda ukafanya kazi huko - Wapo wengine ukiwateua wanafikiri ni nafasi zao. Unampa U-DC ukimtoa ananza kulalamika, wakati hakulalamika ukimteua

Rais Magufuli: Nataka nikuambie mapema, Katiba inazungumza na Sheria inazungumza. Unaweza kukaa miaka mitano ya Mkataba wako ila unaweza hata kukaa mwaka mmoja. Kwasababu taratibu za kukutoa zipo na zinafanywa na Rais. Sikutishi ila wewe nenda kafanye kazi.

Rais Magufuli: Duniani humu huwezi kupewa Mamlaka ya Kuteua halafu usipewe Mamlaka ya Kutengua. Ukishindwa hivyo hufai kuwa Rais na hufai kuwa kiongozi. Mwenzako aliyekuwepo amemaliza kipindi chake cha miaka 5 na kinaisha leo usiku nafikiri saa 6. Kuanzia kesho uende ofisiniFor the English Audience

President Magufuli swears in various newly appointed officials. The officials include Controller and Auditor General (CAG) Charles Kichere, Njombe Regional Administrative Secretary Katarina Tengia Revocati, Tanzania's Ambassador to Kuwait Aisha Amour, Labour Commissioner in the Prime Minister’s Office Colonel Francis Ronald Mbindi and 12 judges of the High Court of Tanzania.

Apart from wishing all the appointed officials well, President Magufuli called upon the CAG to be professional, and to respect the three pillars of government; executive, legislature and judiciary urging him not to disagree when given directives and instead, comply.

Apart from that, President Magufuli also ordered the CAG to 'clean up' audit office.

"The Constitution is clear. You can be there for 5 years or you can be there for 1 because the procedures for appointing and removing the CAG from office are well articulated. This isn't a threat, just work hard". Said President Magufuli in part.

On the other hand, Speaker of Parliament Job Ndugai assured the new CAG his full support.

The Presidents appointment has received mixed reviews where as some are applauding Kichere's new position claiming that he is well experienced and as CAG, he can do lot more for the benefit of the country, while others claim that the CAG was threatened publicly so he isn't in the position to go against the government.

 
Kicheere anaenda kukagua madudu yake TRA.

Wakati akitumbuliwa TRA tuliambiwa ali 'under perform'.

Sasa hivi kapewa kazi ya kukagua taasisi ambayo mwaka wa fedha uliopita yeye ndie alikuwa Mtendaji Mkuu wa Taasisi hiyo.

Siye Team TANROAD tunamtakia kila la kheri.
 
Rais Magufuli ateua CAG, Balozi, Kamishna wa Kazi na Majaji 12.
By Mtinge Blog - November 3, 2019054


Rais Dkt. John Magufuli leo tarehe 03 Novemba, 2019 amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi imewataja walioteuliwa kama ifuatavyo;

Rais Magufuli amemteua Charles Edward Kichere kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (Controller and Auditor General – CAG).

Kichere anachukuwa nafasi ya Prof. Mussa Juma Assad ambaye kipindi chake cha miaka 5 katika nafasi hiyo kinakwisha kesho tarehe 04 Novemba, 2019. Kabla ya Uteuzi huo Kichere alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe.

Rais Magufuli amemteua Katarina Tengia Revocati kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe. Kabla ya uteuzi huo Katarina Tengia Revocati alikuwa Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania na anachukua nafasi ya Charles Edward Kichere ambaye ameteuliwa kuwa CAG.

Rais Magufuli amemteua Mhandisi Aisha Amour kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kuwait. Kabla ya Uteuzi huo, Mhandisi Aisha Amour alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro.

Rais Magufuli amemteua Kanali Francis Ronald Mbindi kuwa Kamishna wa Kazi katika Ofisi ya Waziri Mkuu. Kanali Francis Ronald Mbindi anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Gabriel Pascal Malata ambaye hivi karibuni aliteuliwa kuwa Naibu Wakili Mkuu wa Serikali (Deputy Solicitor General)

Aidha, Rais Magufuli amefanya uteuzi wa Majaji 12 wa Mahakama Kuu.

Walioteuliwa ni;

Dkt. Zainabu Diwa Mango, Kabla ya uteuzi huu Dkt. Zainab Diwa Mango alikuwa Wakili wa Serikali Mkuu katika Ofisi ya Taifa ya Mashtaka.

Edwin Elias Kakolaki, Kabla ya uteuzi huu Edwin Elias Kakolaki alikuwa katika Ofisi ya Kupambana na Kuzuia Dawa za Kulevya Nchini.

Dkt. Deo John Nangela, Kabla ya uteuzi huu Dkt. Deo John Nangela alikuwa katika Ofisi ya Tume ya Ushindani (Fair Competition Commission – FCC).

Fredrick Kapela Manyanda, Kabla ya uteuzi huu Fredrick Kapela Manyanda alikuwa katika Ofisi ya Taifa ya Mashtaka.

Elizabeth Yoeza Mkwizu, Kabla ya uteuzi huu Elizabeth Yoeza Mkwizu alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani.

Augustine Karichuba Rwizile, Kabla ya uteuzi huu Augustine Karichuba Rwizile alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama.

Ephery Sedekia, Kabla ya uteuzi huu Ephery Sedekia alikuwa Katibu wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (Attorney General – AG).

Angaza Mwaipopo, Kabla ya uteuzi huu Angaza Mwaipopo alikuwa katika Ofisi ya Rais, Ikulu.

Joachim Charles Tiganga, Kabla ya uteuzi huu Joachim Charles Tiganga alikuwa Naibu Msajili Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Kassim Ngukali Robert, Kabla ya uteuzi huu Kassim Ngukali Robert alikuwa katika Ofisi ya Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu cha Wizara ya Fedha na Mipango.

Said Mashaka Kalunde, Kabla ya uteuzi huo, Said Mashaka Kalunde alikuwa katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Angela Antony Bahati, Kabla ya uteuzi huo, Angela Antony Bahati alikuwa Katibu Msaidizi wa Tume ya Kurekebisha Sheria.

Wateule hawa wote pamoja na Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Makamishna 5 wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ambao waliteuliwa hivi karibuni wataapishwa kesho tarehe 04 Novemba, 2019 saa 3:30 asubuhi, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
 
Nafuatilia mnyukano wa kikatiba na kisheria unaoendelea baada ya Rais kuteua CAG mpya.

Huyo CAG mpya ni ACPA 1450 ila sio active member 1.7.2019, kama sio active member anakosa sifa. Hebu chungulia hapa ujionee: Orodha ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu |BODI YA TAIFA YA WAHASIBU NA WAKAGUZI WA HESABU TANZANIA (NBAA).

Aliyekuwa hafai TRA Sasa ameteuliwa kuwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali! Yajayo yanafurahisha!!
Raia wanauliza sasa Mahesabu yake akiwa TRA ana uhalali wa kuyakagua?
Je, matumizi ya ofisini akiwa RAS Njombe atakuwa na uhalali wa kuyakagua?
Hakuna rangi hatutaona at this Regime

Taarifa ya Ikulu imeeleza kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Prof. Mussa Assad amemaliza kipindi chake cha miaka mitano kwenye nafasi hiyo. Lakini Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 (ambayo ndio sheria mama) haelezi hicho kinachoitwa "kipindi cha miaka mitano"

Katiba inaeleza kuwa CAG atakoma utumishi wake atakapotimiza umri wa miaka 60. Yani akifikisha umri wa miaka 60 anapumzika bila kujalisha ametumikia nafasi hiyo kwa muda gani. Iwe miezi miwili, miaka nane, au miaka kumi.

Ndio maana maCAG wote waliotangulia wameongoza ofisi hiyo kwa vipindi tofauti. Mzee Mohamed Aboud aliongoza kwa miaka 27 tangu 1969 hadi 1996. Thomas Kiama akaongoza kwa miaka 9 tangu 1996 hadi 2005. Ludovick Utouh akaongoza kwa miaka 8 tangu 2006 hadi 2014. Sasa hii kauli ya kusema Assad amemaliza kipindi chake cha "miaka mitano" imetoka wapi?

Matakwa ya kikatiba ni umri wa miaka 60, unless aondolewe kwa kushindwa kutimiza majukumu yake. Na ikitokea hivyo Katiba imeweka utaratibu wa kumuondoa kwa kuunda tume.

Lakini taarifa ya Ikulu inaeleza Assad amemaliza kipindi chake cha miaka mitano. Je hiki kipindi cha miaka mitano Ikulu wamekitoa wapi? Kwenye sheria ipi? Kama ipo sheria hiyo ipo ni batili maana inapingana na katiba.

Na kwa kawaida unapotokea mgogoro kati ya sheria na katiba, basi Katiba ndiyo inayoshika hatamu (When a state law conflicts with a Constitution, then constitution prevails because constitution rules supreme above all state laws).
_
Prof.Assad amezaliwa tar.06 October mwaka 1961. Kwa sasa ana umri wa miaka 58. Atafikisha umri wa miaka 60 October 06 mwaka 2021. Hivyo nadhani kwa mujibu wa KATIBA Assad alipaswa kustaafu nafasi yake ya CAG akifikisha umri huo, na si kwa hiki kinachoitwa "miaka mitano". I stand to be corrected. Hoja hujibiwa kwa hoja, sio bunduki.!

1.0 Kwa mazingira haya hana sifa ya kuwa auditor kwa kuwa amesajiliwa na NBAA kama mhasibu na sio auditor. Auditor kwa sheria ilivyo anaweza akawa mhasibu ila mhasibu sio auditor. Ina maana auditor ni superior kuliko mhasibu.

2.0 Hayuko kwenye active members wa 1.7.2019 yaani (2018/2019). Hivyo hana Certificate of Practice hata ya uhasibu ya 2018/2019.

Nimeona kuna migawanyiko ya hoja, upande wa kusifu na kuabudu unaongonzwa na VIBAKA wa Lumumba wao wanatetea uteuzi huu kwakutumia Sheria iliyoanzisha hiyo Ofisi( The National Audit Act 2008) inayo-specify 5 years terms na umri ni 65 year. Na kwamba hapa Rais ndipo katumia.

Upande wa kundi jadidi lenye akili na weledi, lenye busara na hekima ya nera una hoja za kikatiba sio za kisheria. Ikulu imeeleza kuwa Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali Prof.Mussa Assad amemaliza kipindi chake cha miaka mitano kwenye nafasi hiyo.

Wakili msomi Emmanuel Chengula anafafanua kwa kusema kwamba, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 (ambayo ndio sheria mama) haelezi hicho kinachoitwa "kipindi cha miaka mitano"

Katiba inaeleza kuwa CAG atakoma utumishi wake atakapotimiza umri wa miaka 60. Yani akifikisha umri wa miaka 60 anapumzika bila kujalisha ametumikia nafasi hiyo kwa muda gani. Iwe miezi miwili, miaka nane, au miaka kumi.

Ndio maana maCAG wote waliotangulia wameongoza ofisi hiyo kwa vipindi tofauti. Mzee Mohamed Aboud aliongoza kwa miaka 27 tangu 1969 hadi 1996. Thomas Kiama akaongoza kwa miaka 9 tangu 1996 hadi 2005. Ludovick Utouh akaongoza kwa miaka 8 tangu 2006 hadi 2014. Sasa hii kauli ya kusema Assad amemaliza kipindi chake cha "miaka mitano" imetoka wapi?

Matakwa ya kikatiba ni umri wa miaka 60, unless aondolewe kwa kushindwa kutimiza majukumu yake. Na ikitokea hivyo Katiba imeweka utaratibu wa kumuondoa kwa kuunda tume.

Lakini taarifa ya Ikulu inaeleza Assad amemaliza kipindi chake cha miaka mitano. Je hiki kipindi cha miaka mitano Ikulu wamekitoa wapi? Kwenye sheria ipi? Kama ipo sheria hiyo ipo ni batili maana inapingana na katiba.

Na kwa kawaida unapotokea mgogoro kati ya sheria na katiba, basi Katiba ndiyo inayoshika hatamu (When a state law conflicts with a Constitution, then constitution prevails because constitution rules supreme above all state laws).
_
Prof.Assad amezaliwa tar.06 October mwaka 1961. Kwa sasa ana umri wa miaka 58. Atafikisha umri wa miaka 60 October 06 mwaka 2021. Hivyo kwa mujibu wa KATIBA alipaswa kustaafu nafasi yake ya CAG akifikisha umri huo, na si kwa hiki kinachoitwa "miaka mitano".

Kumbuka, Kicheere alitumbuliwa June 8, 2019 baada ya kutuhumiwa na wafanyabiashara kuwafanyia bugudha na kuua biashara zao, Alikuwa kamishna wa TRA. Leo kateuliwa kuwa CAG!

Nchi ina maigizo mengi hii. Bahati mbaya wanaoigiziwa hawajui lolote. Charles Kicheere alitumbuliwa kwa tuhuma za uzembe katika usimamizi wa TRA na kubugudhi wafanyabiashara sasa ameteuliwa anakwenda kuwa Msimamizi wa uadilifu katika mifumo ya fedha na UKAGUZI.

Mtu aliyeonekana kupwaya TRA (Kicheere) anapewa sasa kwenda kusimamia UKAGUZI wa mahesabu ya serikali. Kusimamia ukusanyaji wa mapato alishindwa, tukaaminishwa hivyo, ataweza kweli kudhibiti na kukagua HESABU za umma? Anyways, tuendelee kuona maajabu!

Wakili Chengula amemaliza kwakusema, I stand to be corrected.!

Katika hatua nyingine, Mbunge Zitto Kabwe ameongeza utata wa uteuzi wa CAG mpya kuonyesha kuwa hana sifa ya kushika ofisi hiyo kubwa ya umma iliyoanzishwa na katiba ya nchi sio na sheria,

Zitto anasema, "Charles Kicheere hana sifa za kuwa CAG kwa mujibu wa Katiba. Hana record ya ku-practice Auditing. Rais Alipomwondoa Kicheere TRA alimsema kuwa hajui kazi. Leo anampatia kazi kubwa hii huku akiwaacha 4 Deputies CAG. Uteuzi huu ni wa kuficha wizi (miradi mikubwa)"

CAG Musa Asad ameonekana kushangazwa na uteuzi huo na amenukuliwa na chombo cha habari kuwa hata taarifa hizo na yeye yuko katika majukumu ya kiutendaji. Hapa ndipo mkanganyiko unapozidi.

Kwa maoni yangu, nawauliza, ni lini utawala huu uliwahi kufuata sheria na katiba ya nchi kwa 100% katika utendaji wake? Mnakumbuka kesi ya uteuzi wa AG?
 
Back
Top Bottom