Rufiji,
Sina hakika kama unafahamu mazingira halisi ya Operation Sangara. Umstushwa na hii picha baadaya ya kuonyeshwa kwenye mtandao. Hata tungelizishikia bango zitafikaje vijijini? Ni dhahiri huna touch na reality ya vijijini! Ungelituuliza tunaofanya Operation Sangara tungelikupa picha kamili. Nenda Handeni hata dishi za Satelite (kuona TV) ziko katikati ya mji tu, tena nyumba za vigogo. Nenda kijiji chochote iwe Handeni au Kilindi ambapo hata simu ya kawaida ya Kigaganjani au haipo au lazima upande juu ya mti mrefu au mlima kupata mtandao. Magazeti yako Handeni mjini tu, tena ya siku ya baadaye. Hivyo, Operation Sangara katika vijiji vingi nchini, (siyo Tanga tu) ndiyo njia pekee ya kupeleka elimu kwa wananchi walio wengi. Ni bahatimbaya kila kinachosemwa kwenye Operation Sangara hakiwafikii ndugu zetu mlio mbali kwani waandishi wanaandika wanayopenda kuandika. Lakini ingelifaa siku mmoja kuwekewa live kila kinachowekwa katika hotuba za Operation Sangara ndipo muweze kuthamini operation Sangara na muweze kuelewa vizuri. Kwa mtu ambaye hayuko on the ground ni rahisi sana ku comment kama ilivyo kwa mtu anayetazama mpira wa miguu kutoka nje, na asiweze kuelewa mpiga penalty anashindwa kuingiza mpira kwenye goal!!! Tunahitaji kutafakari sana siyo tu hali ya elimu ya wananchi wetu lakini pia namna ya kufikisha elimu hiyo kwa wananchi wetu zaidi ya asilimia 80 wanaoishi vijijini. Isitoshe, ni vema kufahamu kuwa Tanzania ina vijiji zaidi ya 12,500 kabla ya ( uandikishaji uliofanyika kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa). Ni vema mtu makini akafikiria jinsi ilivyo ngumu kufikia vijiji hivyo katika muda mfupi. Hata ungelitembea bila kulala, bila kula unahitaji siku 12,500( ongeza na vijiji vilivyoongezeka). Mwaka mmoja una siku 365(6). Sasa fikiria unahitaji kusafiri miaka mingapi kufikia vijiji vyote. Rahisi kuwa critical, lakini ngumu sana kutoa "solution" sahihi kukomboa taifa hili.
Watu wapenda demokrasia ya kweli na mabadiliko wanapaswa kuendelea kuwaelimisha wananchi wengi ambao bado hawajapata uelewa na mwanga wa kutosha. Wengi wanahofia mabadiliko ya uongozi kutoka CCM kwenda chama cha upinzani bila hata kuwa na sababu za msingi. Utasikia wanasema:
"Tumeizoea CCM, hata kama ni mbaya",
"Wapinzani wataweza kutawala?",
"Na wenyewe si wataiba tu kama hawa waliopo?",
"Wanasiasa wote ni wezi tu",
"Wote wanatafuta ulaji tu, si maslahi ya walio wengi".
Haya yote ni majibu ya watu waliokata tamaa.
Wanahitaji kuondolewa kwenye kukata tamaa, na waelezwe kuwa
wanaweza kuchukua hatua ambazo hatimaye zitaleta mabadiliko chanya kwenye maisha yao na manufaa chanya kwa nchi.
Waelimishaji wa demokrasia/elimu ya uraia wanaweza kuwa ni taasisi mbalimbali.
Serikali haipendi vyombo vingine isivyoweza kuvidhibiti na kuvielekeza nini cha kufanya/kusema viwaelimishe wananchi kuhusu suala zima la demokrasia na elimu ya uraia.
Taasisi huru ni muhimu sana ili kuelimisha watu kwa uhuru bila kuingliwa na Serikali.
Mifano: MNF, LHRC, LEAT...
Serikali inawajibika kwa wananchi wake, hivyo inapaswa kuulizwa maswali (magumu bila shaka!) kuhusiana na utendaji wa viongozi (wanasiasa na watendaji), hasa kuhusiana na vipaumbele katika suala la matumizi.
Hapa ndipo linapokuja suala la matumizi mabaya ya fedha za umma...
Ununuzi na ukarabati (kutokea kwenye msingi??) wa nyumba ya Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania halikuwa suala la kupewa kipaumbele.
Si tayari alikuwa akiishi kwenye nyumba nzuri tu?
Gharama iliyotajwa (nasisitiza ILIYOTAJWA) imezidi hata gharama za nyumba za Ben Bernanke ambaye ni Mwenyekiti wa Benki Kuu ya Marekani (Chairman of the US Federal Reserve), au Mervyn King, Gavana wa Benki Kuu ya Uingereza.
Wananchi wengi wanadhani kuwa hata wakipiga kura vipi, bado itatangazwa kuwa CCM imeshinda. Hii ndio maana ukiwauliza watu ambao hawaendi kupiga kura swali kuwa je kama wangepiga kura wangepiga vipi, wengi wangepigia kuleta mabadiliko (upinzani). Ila wanadhani kuwa hata wakipiga kura vipi, matokeo yanakuwa yameshapangwa.
Hivyo uhamasishaji ni muhimu sana.
Watu waelimishwe kuwa:
1. Ukipiga kura
unaongeza uwezekano wa kuchaguliwa mgombea unayemtaka, na kupunguza uwezekano wa kuchagiliwa mgombea usiyemtaka.
2. Kupiga kura ni
SIRI YAKO. Hakuna atakayejua umemchagua nani, labla useme wewe mwenyewe. Hivyo usimchague mgombea asiyefaa, hata awe amekupa rushwa ( ya pesa, pilau, vinywaji, nk). Kwanza
hawezi kujua kama hukumpigia (Hili ni muhimu kulisema kwani bado wapo wengi tu wanaowaogopa viongozi).
3. Wananchi wakielimika na elimu ya demokrasia na uraia, watawatosa
viongozi wachafu pamoja na
viongozi wasiochukua hatua kwa viongozi wachafu. Hii itawashtua hata viongozi wapya watakaochaguliwa (kuwa nao wakiboronga tu, watapigwa chini next time).
Swali kwa Dr.,
Je mkimaliza ziara mkoa fulani mnaacha tasks kwa waliobaki (viongozi wa Chama mikoani na wilayani etc. kuendelea kuelimisha na kuhamasisha wanachama wa zamani, wanachama wapya mliopata, na wananchi kwa ujumla wake?
Kuhusu vijiji 12,500...
Mnaweza kugawana wewe ukaenda nusu ya mikoa na Mbowe nusu ya mikoa iliyobaki, mkaelimisha (pamoja na wengine) kisha mkaacha tasks huko. Mkifika kila wilaya itakuwa safi sana.
One of the solutions ni kuelimisha na kuhamasisha viongozi kwa kila ngazi (Mikoa/Wilaya/Tarafa/Kata/vijiji na Mitaa) kuhusu umuhimu wa kupiga kura ili kuleta mabadiliko. Viongozi hao nao waendelee hivyo hivyo.
Tahadhari ni kuwa msiwaachie viongozi VIGEUGEU (nadhani hapa inaeleweka) watoe statements kwa niaba ya Chama, la sivyo mtaumia.