Kwa muundo huu wa tume huru ya uchaguzi, CCM wataachia ngazi asubuhi na mapema kabisa hata kabla ya kura moja haijapigwa

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,174
Wameuza nchi, wamekuwa na kiburi, majivuno na madharau sasa wakati wa kuwatimua CCM madarakani ni huu na mwarobaini wao ni marekebisho ya katiba na sheria za uchaguzi kama tunavyopendekeza hapa chini baada ya kudadavua ukakasi uko wapi.


Ukiufuatilia kwa karibu mjadala wa vuguvugu la kudai katiba mpya umejikita kwenye mchakato wa kuibua uongozi bora kwa kuhakikisha wapigakura badala ya wanasiasa, vyombo vya usalama au vyombo vya khabari vinatuchagulia viongozi wetu.

Hii inajengwa na imani ya kuwa wapigakura wana masilahi makubwa ya kuwapata viongozi bora kuliko taasisi nyingine zozote zile.

Tutaangazia mfumo wa katiba ya Kenya na tutalinganisha na watanzania kuona ni kwa namna ipi tutaweza kuibua viongozi wenye vipaji na kutunasua kutoka hapo tulipo.

KATIBA YA KENYA YADADAVULIWA.

TUME HURU YA UCHAGUZI (IEBC)

1) Tofauti na katiba yetu, katiba ya Kenya imeweka msisitizo uwajibikaji ni kwa wananchi wa Kenya na hivyo demokrasia yao ni kwa manufaa ya wananchi wakati sisi demokrasia yetu ni kwa manufaa ya vyama vya siasa na ndiyo maana tunakwama kwa sababu zifuatazo:-

2) Nje ya vyama vya siasa wagombea na wapigakura hawana sauti ya kusikilizwa,

3) Wagombea binafsi wamepigwa marufuku,

4) Chama cha siasa kinao uwezo wa kuwatimua uanachama wanachama ambao ni tishio kwa waliopo madarakani na hivyo kuwapora haki ya wahanga ya kugombea au kushiriki kikamilifu kwenye shughuli za kisiasa.

5) Wanaoteuliwa kugombea nafasi za uongozi wa umma kupitia vyama vya siasa mara nyingi maoni ya wapigakura hayazingatiwi,

6) Tume ya uchaguzi huteuliwa na Rais na hivyo kumpa fursa pana ya kuigeuza Tume tajwa kuwa idara ya Chama chake cha siasa kwa kuishindilia na makada wa chama chake,

7) Tofauti na katiba ya Kenya, Katiba yetu haijatoa maelekezo ya kina Tume ya uchaguzi itekeleze vipi majukumu yake kwenye maeneo ya umuhimu wa kitekinolojia katika kuandikisha wapigakura, uhesabu wa kura, uhakiki wa kura mbele ya mawakala wa vyama vyote shiriki vya siasa, usafirishaji wa matokeo na uchapishwaji wa matokeo ya kila kituo kwenye tovuti ya Tume ya uchaguzi. Haya mazingira yametoa mwanya kwa dola kupitia vyombo vya usalama kutengua matokeo sahihi na kuweka ya kwao yanayokinufaisha chama tawala,

8) Katiba ya Kenya na maamuzi ya kimahakama yanaonyesha fomu za vituo vys kupigia kura ndizo ushahidi ambao wapaswa kutumika katika kupinga matokeo ya uchaguzi wakati katiba na sheria za uchaguzi wa Tanzania zimeyatambua matokeo ya majimbo bila ya kujali yanaweza kuwa yamechakachuliwa na hivyo kutowakilisha maamuzi ya wapigakura kwenye vituo vya wapigakura,

9) Tofauti na Katiba na sheria za uchaguzi wa Kenya, Tanzania tunazo sheria za uchaguzi zinazokinzana na katiba ya nchi hii ambayo inaitambua Tume ya uchaguzi kama chombo pekee cha kusimamia chaguzi zao wakati sisi tumeilazimisha Tume ya uchaguzi kukasimu mamlaka yake ya kikatiba kwa chombo batili cha serikali za mitaa,

10) Muundo wa wajumbe wa Tume ndilo eneo linalotatiza pengine kuliko maeneo yote kwa nchi zote mbili. Katiba ya Kenya imeweka sifa za makamishina wa Tume ya uchaguzi kuondoa migongano ya kimasilahi sisi katiba yetu imegusia kijuujuu tu na hakuna msisitizo na hivyo kuacha mianya wa makada wa chama tawala kujaza makada wake ndani ya Tume na hivyo kupoteza hadhi ya Tume tajwa kuwa huru na ya haki. Sifa za ujaji wa mahakama kuu hakuzuii kuwa kada wa chama cha siasa kama tulipomwona Jaji Mkuu Augustine Ramadhani alivyojaza fomu ya kugombea Urais kupitia CCM mwaka 2015 mara tu baada ya kustaafu na kutuacha na maswali mengi yasiyo na majibu mojawapo ni lini alijiunga na CCM ili aweze kugombea. Ilikuwa ni baada au kabla ya kustaafu? Kama ni kabla ya kustaafu basi hakuwa na sifa ya kuwa Jaji wa Mahakama zetu na maamuzi yote aliyoshiriki hususani ya mgombea huru kuwa ni batili,

11) Tume kujitegemea kwa kuwa na mtandao wake wenyewe nje ya Tume ya uchaguzi kwa kiasi kikubwa unaipa jamii imani ni Tume huru kulikoni kuiita huru kama alivyopendekeza aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Jaji mstaafu Damian Lubuva wakati kimuundo na kiuendaji haiko huru.

12) Katika Mapendekezo ya rasimu ya Warioba ambayo yaliridhiwa na Bunge haramu la kikatiba yalikuwa na kamati ya uteuzi wa makamishina wa Tume ya uchaguzi ikiashiria umuhimu wa Tume huru lazima taasisi ya Urais isishiriki katika kuiteua. Kamati hiyo ya uteuzi wa Tume tajwa kwa bahati mbaya ilikuwa imeundwa na Majaji wakuu Tanganyika na Zanzibar na manaibu wao pamoja na Maspika wa Tanganyika na Zanzibar na manaibu wao, Mwanasheria Mkuu na mwakilishi mmoja wa vyuo vikuu, Tume ya uchaguzi inayotokana na Kamati batili ya uteuzi nayo ni haramu tu,

13) Mabadiliko ya sheria ya Kenya ya Tume ya uchaguzi (2023) yanayoruhusu Tume ya uteuzi wa makamishina wa Tume ya uchaguzi ina muundo ufuatao:-

14) Wajumbe 2 wa jinsia ya kike na wajumbe 2 wa jinsia ya kiume kutoka Tume ya Huduma ya Bunge. Hawa wote ni wabunge ambao upo uwezekano wa chama tawala kuwateua wengi wao au wote kutoka chama tawala na vyama vya upinzani vimekuwa vikilalamikia hili na kuwa moja ya sababu zao za maandamano,

Wajumbe 2 kutoka Muungano wa taasisi za kidini,

Mjumbe 1 kutoka Chama cha mawakili wa Kenya,

Jumla ya idadi ya kamati ya uteuzi ni 7 ambao wao wenyewe watamteua Mwenyekiti wao na naibu wao wakisaidiwa na secretariat ya bunge katika kutekeleza majukumu yao.


12. Katika Mapendekezo ya rasimu ya Warioba ambayo yaliridhiwa na Bunge haramu la kikatiba yalikuwa na kamati ya uteuzi wa makamishina wa Tume ya uchaguzi ikiashiria umuhimu wa Tume huru lazima taasisi ya Urais isishiriki katika kuiteua.

Kamati hiyo ya uteuzi wa Tume tajwa kwa bahati mbaya ilikuwa imeundwa na Majaji wakuu Tanganyika na Zanzibar na manaibu wao pamoja na Mwanasheria Mkuu na mwakilishi wa vyuo vikuu. Maspika, majaji tajwa ni wateule wa Rais



MAPENDEKEZO YETU BAADA YA UCHAMBUZI TAJWA.

1) Tume huru ya uchaguzi siyo kwa jina lake tu bali kimuundo wake hauingiliwi na taasisi ya Urais na pia ni jinsi inavyofanya kazi,

2) Mabadiliko ya Katiba yanahitaji kuanzisha Kamati ya Uteuzi wa Tume ya uchaguzi ambayo itaondoa ushawishi wa chama tawala pungufu kubwa la rasimu ya Warioba ambayo ilijenga mazingira Kamati ya uteuzi kuundwa karibu yote na wateule wa Rais au chama chake cha siasa na hivyo kugeuza Kamati ya Uteuzi kuwa kijiwe cha chama tawala kuwarubuni wapigakura patakuwepo Tume huru ya Uchaguzi kumbe wanawarushia changa la macho tu. Ujumbe wa maspika na manaibu wao ambao ni wana masilahi mazito ya kugombea kwenye chaguzi zetu kama Rais kunaharamisha uhuru wa kamati ya uteuzi na pia Tume ya uchaguzi watakayoshiriki kuiunda hivyo kubatilisha kila kitu.

3) Tunapendekeza Kamati ya Uteuzi iwe na wajumbe wenye sifa zifuatazo:-

4) Wajumbe wa Kamati ya uteuzi wasiwe waajiriwa wa Umma au vyama vya siasa katika wadhifa wowote ule kuondoa hisia za upendeleo kwa chama tawala

5) Jumla ya wajumbe wa kamati ya uteuzi kuwa 9 tu,

Wajumbe wa kamati ya uteuzi wawe na umri kati ya miaka 45 hadi 65 tu, hii tutaondoa aina zote za watumishi wa umma hususani majaji ambao wako mstari wa mbele kupindisha haki,

6) Wajumbe kumteua Mwenyekiti na katibu wao,

7) Wataajiri secretariat yao kuwasaidia katika kutekeleza majukumu yao watumishi wasiozidi 20 tu,

8) Wajumbe wa kamati ya uteuzi wachaguliwe na wadau wa maeneo yafuatayo: Chama cha wanasheria wajumbe 2, jinsia zote kuwakilishwa yaani ya kike 1 na ya kiume 1, Wajumbe 4 wa vyama vya wataalamu nchini ambao watapendekezwa na mikutano mikuu ya vyama vyao kutoka chama cha wahandisi, madaktari, Wauuguzi na wasanii wa majengo kila kimoja mjumbe mmoja na Muungano wa vyama vya wafanyakazi nchini TUCTA itatoa wajumbe 2 wa jinsia moja ya kike na ya kiume ambao watachaguliwa na mkutano mkuu wa vyama vya wafanyakazi na hawatakuwa ni viongozi au waajiriwa wa vyama vya wafanyakazi,

9) Wajumbe wa kamati ya uteuzi wawe siyo wanachama wa vyama vya siasa kuondoa dhana nzima ya mwamba ngoma huvutia kwake,


Pia, tunapendekeza makamishina wa Tume ya uchaguzi wawe na sifa zifuatazo:-

1) Makamishina wa Tume ya uchaguzi wasiwe waajiriwa wa Umma katika wadhifa wowote ule au kwenye vyama vya siasa kuondoa hisia za upendeleo kwa chama tawala.

2) Kamati ya uteuzi itatanganza nafasi ya Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi na Naibu wake, makamishina 7 na jumla ya idadi yao kuwa 9 tu.

3) Wajumbe wa Tume ya uchaguzi watakuwa na sifa zifuatazo:-

i) Hawatakuwa wanachama wa chama cha siasa chochote kile,

ii) Wanapaswa kuwa na elimu ya Chuo kikuu kinachotambuliwa na Taasisi ya elimu ya juu nchini,

iii) Uhitimu wa elimu wa chuo kikuu usipungue miaka 10 kwa makamishina na miaka 15 kwa Mwenyekiti na Makamu wake tangia walipowakilisha maombi ya teuzi hizi,

iv) Makamishina wawe na umri kati ya miaka 45 hadi 65 tu,

v) Patakuwapo na uwakilishi wa kijinsia ya kike au kiume yenye makamishina wasiopungua 3 kwa aidha ya makamishina 7 wa Tume ya uchaguzi,



4) Makamishina watateuliwa na Rais kutokana na mapendekezo ya majina 9 ya Kamati ya Uteuzi,

5) Makamishina watathibitishwa na Bunge kabla ya kuanza kazi.

6) Ajira za Makamishina zitalindwa sawa sawa na za majaji wa mahakama kuu yaani kuwaondoa lazima Rais aunde Tume ya kuwachunguza na Mapendekezo yake ndiyo uamuzi,

7) Makamishina wasioridhishwa na maamuzi ya Tume ya uchunguzi tajwa wanayo haki ya kuyapinga mahakamani,

8) Makamishina kutumikia kwa kipindi kimoja cha miaka 7 tu na hawataruhusiwa kushika wadhifa serikalini au kwenye vyama vya siasa kwa miaka 10 tangia tarehe ya mwisho wa utumishi wao kwenye Tume ya uchaguzi.


Kwamba, Tume ya uchaguzi itakeleza majukumu yake kama ifuatavyo:-

1) Itatumia tekinolojia ya kisasa na ilyo bora katika kusajili wapigakura kila siku ya kazi na kuboresha daftari la wapigakura wakishirikiana na NIDA na RITA katika kuhakiki uraia na uhai wa wapigakura,

2) Itatumia tekinolojia ya kisasa katika kuyatuma matokeo ya kura katika kila kituo cha uchaguzi na kuyapeleka kwenye tovuti ya Tume ya uchaguzi ikionyesha fomu ya matokeo ya kila kituo ikionyesha jina la kituo, wasimamizi wa kituo, mawakala wa kila chama cha siasa na wagombea binafsi kama wapo wote hawa yatakuwepo majina, sahihi zao na picha zao,

3) Tume ya uchaguzi haitakuwa na mamlaka ya kuwatengua wagombea kwa kukosa sifa za kujaza fomu za kugombea ubunge, udiwani au Urais bali kwa amri ya mahakama kuu tu,

4) Tume itakuwa na mtandao wa watendaji wao katika kila jimbo na kuacha mara moja kukasimu mamlaka yake ya kikatiba kwa chombo batili cha serikali za mitaa kupitia wakurugenzi wa majiji na Halmashauri zake,

Tutaendelea kuyapendekeza maoni mengine baadaye
 
ccm, JK, na Ukawa walitunyima fursa muhimu sana mwaka 2014! Rasimu ya Katiba ya Jaji Warioba ingepitishwa na kuwa Katiba ya Wananchi! Leo hii tungekuwa tumepiga hatua kubwa sana kwenye nyanja za kiuchumi, kijamii na pia kisiasa.
 
ccm, JK, na Ukawa walitunyima fursa muhimu sana mwaka 2014! Rasimu ya Katiba ya Jaji Warioba ingepita, leo hii tungekuwa tumepiga hatua kubwa sana kisiasa, kijamii na pia kiuchumi.
Isingetatua matatizo ya taasisi ya Rais kuteua tume ya uchaguzi.

Mapendekezo ya Warioba kutakuwepo na kamati ya uteuzi itakayoundwa na majaji wakuu na manaibu wao kutoka Tanganyika na Zanzibar, Mwanasheria Mkuu, Maspika na manaibu wao kutoka pande mbili za Muungano na mwakilishi mmoja wa vyuo vikuu.

Mwakilishi wa vyuo vikuu hakupaswa kuwepo kwa sababu wadau siyo wao pekee yao


Waliobaki ni wateule wa Rais kwa hiyo tume ya uchaguzi haiwezi kuwa huru kwa sababu haitokani na kamati ya uteuzi iliyo huru
 
Wameuza nchi, wamekuwa na kiburi, majivuno na madharau sasa wakati wa kuwatimua CCM madarakani ni huu na mwarobaini wao ni marekebisho ya katiba na sheria za uchaguzi.
Mkuu Ruta, Rutashubanyuma , hoja yako hii, "

Kwa muundo huu wa tume huru ya uchaguzi, CCM wataachia ngazi asubuhi na mapema kabisa hata kabla ya kura moja haijapigwa"​

CCM ukiachia ngazi, nafasi yake ndio aje nani?.
P
 
Mkuu Ruta, Rutashubanyuma , hoja yako hii, "

Kwa muundo huu wa tume huru ya uchaguzi, CCM wataachia ngazi asubuhi na mapema kabisa hata kabla ya kura moja haijapigwa"​

CCM ukiachia ngazi, nafasi yake ndio aje nani?.
P
Ninachojua wapigakura wameichoka CCM sasa wapigakura kwa kuikataa CCM watavichagua vyama vinginevyo waonavyo vinafaa.


Lengo ni kuwa na Tume huru ya uchaguzi itokanayo na kamati ya uteuzi huru kwa maana ya kutofungamana na taasisi ya Urais ambayo huunda tume ya makada wa CCM wakiwa na majukumu ya kuchakachua matokeo ya kila uchaguzi
 
Mkuu Ruta, Rutashubanyuma , hoja yako hii, "

Kwa muundo huu wa tume huru ya uchaguzi, CCM wataachia ngazi asubuhi na mapema kabisa hata kabla ya kura moja haijapigwa"​

CCM ukiachia ngazi, nafasi yake ndio aje nani?.
P
atajibu akiwa anacheka mwenyewe 🤓.

Kwa maoni yangu, Mbadala wa CCM hajazaliwa bado, nadhani hata kufikiriwa kuzaliwa bado
 
Nakukumbusha tu tume ya Uchaguzi haina uwezo wala mamlaka ya kumtangaza aliyeshindwa ni mshindi. Hapa ndio wengi wanakwama na wameshindwa kuuona ukweli huu, ni ukweli mchungu lakini acha usemwe tu ili kuliponya Taifa.

Kwenye nchi nyingine, upinzani upo imara lakini sio Tanzania. Upinzani wa nchi nyingine una agenda za kusimamia wa hapa hauna agenda. Kwa mfano mpinzani mkuu wa Rutto hapo Kenya Odinga, anasimamia agenda ya kupanda Kwa gharama za maisha na anakubalika kwa jambo hilo.

Hapa Tanzania ni tofauti. Hawana agenda kabisa wapo wapo na hata ikiletwa tume ya Kenya haiwezi ikabadili ukweli huu kuwa Upinzani wa Tanzania ni dhaifu sana. Jengeni kwanza sera zenu ili muwe na agenda za kueleweka bila hivyo CCM sio chama Cha mchezo eti hata Mzee Dovutwa au yule Mzee wa Ubwabwa anawaza kukitoa madarakani.

Mshindani wenu ana nguvu kubwa sana
 
atajibu akiwa anacheka mwenyewe .

Kwa maoni yangu, Mbadala wa CCM hajazaliwa bado, nadhani hata kufikiriwa kuzaliwa bado
Tunachodai si ni nani atawale bali kuweka mfumo utakaoheshimu haki ya mpigakura tu.
 
Back
Top Bottom