Wana CCM naomba mhalalishe picha hizi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wana CCM naomba mhalalishe picha hizi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jan 2, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jan 2, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Serikali ya CCM chini ya Rais Kikwete ambaye anatarajiwa kuwa mgombea wa CCM mwaka huu imehalalisha na kukubali matumizi ya karibu shilingi bilioni 3 kujenga upya nyumba mbili kwa ajili ya maisha ya kifahari ya Gavana wa Benki kuu na manaibu wake. Wamefanya hivyo kwa sababu mikataba ya hawa watumishi inawataka wapatiwe vitu hivyo vinginevyo wangegoma kufanya kazi BoT. Mastahili ya hayo yanazidi yale ya Magavana wa Benki kuu za Uingereza na Marekani!

  [​IMG]

  [​IMG]

  Hizi ni picha zilizochukuliwa katika wodi ya kina mama waliojifungua wakiwa wanapumzika pale Hospitali ya Temeke. Ni hali ndiyo ilimfanya mwanamapambo Naomi Campbell..

  [​IMG]

  [​IMG]  [​IMG]

  SWALI: NANI ANASTAHILI ZAIDI KATI YA GAVANA WA BENKI KUU ILIYOGUBIKWA NA UFISADI ULIOKUBUHU NA KINA MAMA HAWA NA WACHANGA WAO?
   
 2. Wacha

  Wacha JF-Expert Member

  #2
  Jan 2, 2010
  Joined: Nov 23, 2006
  Messages: 856
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Chama Cha Majambazi hawana aibu, tena wote akina Kikwete na genge lake la wahuni walisomeshwa bure na pesa ya walipa kodi.
   
 3. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #3
  Jan 2, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Mwanakijiji,

  Gavana anastahili alale kwenye kitanda cha sufi, na mashuka ya silk, paa lake na nyumba yake inapaswa inukie kama keki na kalamati, huku maji yanatiririka kama maporomoko ya Pangani na nuru ndani ya nyumba yake ni kama vile jua limehamia ndani ya nyumba yake na kuipatia nishati!

  Gavana ana umuhimu sana kwa maana asipopata malezi haya bora, je unafikiri ni nani atakaa na kutafakari mbinu mpya za kiuchumi kwa Taifa letu? Unafikiri hawa kina mama na Watoto wao wana uwezo hata wa kuelewa jinsi kalamu ya risasi inavyofanya kazi au utamu wa kulalia mashuka ya hariri?

  You are damn right kuwa CCM ina kipaumbele naye ni ni Gavana!
   
 4. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #4
  Jan 2, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  Hao wakina mama wanafiki wakubwa......
  Tatizo lao ni elimu na kujitambua kuliko umasikini....
  Mbona kwa waganga wa kienyeji wananunua mbuzi na kuku wanapeleka???
  Au ni imani kuwa hospitali ni bure na ni kazi ya serikali.....

  Bottom line ni kuwa sio wote wanaoenda hospitali za serikali
  ni maskini kupita kiasi......
  Ni mazoea tu.........

  Halafu hao akina mama..
  Hizo mimba walizipataje????
  Hao wanaume waliowapa hizo mimba
  hawana kazi kabisa??????
  Walihongwa nini kabla ya kufungua miguu
  yao kwa hiyari????
  Mbona hizo khanga wanazovaa ni mpya mpya
  na bei ya khanga moja sasa ni sh 5000/??????

  Serikali ina mambo mengi ya kulaumiwa but sio
  hao ya akina mama wa mjini......

  Nitailaumu serikali kwa huduma za afya vijijini.
  But hoa wa mwananyamala na amana na temeke.
  Hell no.
  Kwani lazima kuishi mjini na kuzaa kama uwezo huna???????
   
 5. ChaMtuMavi

  ChaMtuMavi JF-Expert Member

  #5
  Jan 3, 2010
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 333
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tunatofauti gani na wakimbizi kule ngara au Darfur-Tafauti ni kwamba hawa wamama wazazi wamo kwenye kuta za jengo imara.

  Kuwa mkimbizi siyo lazima nchi iwe na vita ya kutumia silaha za moto. Hata ufisadi ni vita inayowaacha wazawa kuwa wakimbizi nchini kwao kama hawa wazazi na watoto hawa.

  Mungu ibariki Tanzania.
   
 6. U

  Ujengelele JF-Expert Member

  #6
  Jan 3, 2010
  Joined: Jan 14, 2008
  Messages: 1,256
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Ulichoandika n kweli kabisa. Idadi kubwa ya Watanzania wanaishi maisha yanayofanana kabisa na ya wakimbizi ndani ya nchi ambayo inasemekana ina amani. Na hili linasababishwa na Viongozi waliopo madarakani kuweka mbele maslahi yao ya kutajirika kwa haraka.
   
 7. MwalimuZawadi

  MwalimuZawadi JF-Expert Member

  #7
  Jan 3, 2010
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 643
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mkuu Boss
  mmmh...nothing special!!!
   
 8. M

  Moelex23 JF-Expert Member

  #8
  Jan 3, 2010
  Joined: Oct 8, 2006
  Messages: 497
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mbaya zaidi hiyo ni hospitali ya wilaya DAR ES SALAAM.

  Can U even imagine hospitali ya wilaya say LINDI, MTWARA hali ikoje???

  Hivi sisi watanzania hata aibu hatuna kweli kununua mashangingi zaidi ya 1,000 kila mwaka ambayo nina uhakika pesa hizo zingeweza kabisa kuondoa tatizo la angalau vyumba vya dada zetu kuweza kujifungulia salama.

  May God Bless Tanzania
   
 9. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #9
  Jan 3, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Eti na huyu mjinga anajifanya kuwa kwenye kundi la great thinker. Nachelea kutoa tusi. Mungu nisaidie nipe uvumilivu..............
   
 10. m

  mmakonde JF-Expert Member

  #10
  Jan 3, 2010
  Joined: Dec 26, 2009
  Messages: 967
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Wazungu wakitutukana sisi Manyani tusilalamike!Hawaamini kuwa tunaweza kusort out hili tatizo!Tuko tayari kununua Phd fake,kuendesha FWD ,na corruption./ufidadi etc!

  Hata wakinamama Wabunge ndio hovyo kabisa.Mwanamke ana moyo,lakini no body cares plight ya wanawake wenzao hapa.CCM inanunua magari zaidi ya 200!
  Hizi pesa zinaweza kununua vitanda,hata kujenga maternity wards !
  Shame on me,shame on you ,i am sick to death watu wanalia crocodile tears kwa kifo cha Kawawa!
  Niko tayari kutoa machozi kwa hawa akina mama watanzania wenzetu ambao hawana
  uwezo!
   
 11. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #11
  Jan 3, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Alafu sikiliza hotuba zao zilivyojaa majigambo. Kwa ushahidi ni hotuba ya juzi tu ya JMK. Hawana aibu hawa! naomba hizi picha ziwekwe kwenye magazeti!
  Ajabu utasikia watu wakiandamana kuiunga hotuba hiyo mkono, na wengi watakuwa wakina mama.
  hivi wa tz tumelogwa?
   
 12. b

  bnhai JF-Expert Member

  #12
  Jan 3, 2010
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,207
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Boss
  yr comments are not polite na ninadhani hawastahili.
  Kwanza sio wote wanaokwenda kwa mganga wa kienyeji tafadhali.
  Pia wanahaki ya kuzaa kama wewe na mwingine.
  Sasa km bei ya khanga moja ni elfu 5 unajua wanazo ngapi?
  Nani alisema mjini ni kwa jamii fulani.
  Binafsi naona ni kukurupuka kuwalaumu hawa maana hawakuwezesha kama ulivyokiri hawana elimu.
  Hili ni tatizo la utawala wetu kuanzia tangu uhuru mpaka sasa. Na it will take yrs. Tuifanye serikali iwajibike kwa wananchi. Mf Gharama za nyumba ya gavana zilikuwa zinaepukika na kungeweza kutengeneza zahati nzuri au hata kuweka vitanda. Na sie wananchi pia hebu tuchangie tuachane na ubinafsi, tuwaone na wenzetu ambao hawana wanastahili kupata basic needs.
   
 13. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #13
  Jan 3, 2010
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Niliposoma mwanzo kuhusu unafiki wa akina mama hawa nikajua labda point inayofuata ni kuwa wao ndiyo wapo mstari wa mbele kuhakikisha CCM inashinda baada ya kupewa vipande vya Khanga za "CCM NAMBARI WANI" kila uchaguzi unapowadia.

  Ila lawama zako hazina msingi hata chembe, Wewe ulitakaje?
  1. Unapofika muda wa kujifungua waende Hospitali na vitanda vyao siyo?
  2. Waache kupanua miguu kwa hiyari yao hata katika ndoa zao halali?
  3. Wanaume zao wajenge hospitali kwa ajili ya wanawake zao hata kama wanakatwa kodi zao kila mwezi na serikali?
  4. Kazi ya serikali ni nini hasa kama siyo kuhakikisha usalama kwa raia wake, kusambaza "Public goods" ikiwamo huduma bora za afya hata kama ni kwa kuchangia kiasi fulani?
  5. Je kina mama hawa waliambiwa kuchangi huduma ya afya wakagoma? baada ya serikali kuweka mazingira mazuri ya wao kujipatia kipato chao halali?

  Ukijibu maswali haya nitajua kweli wewe una-uchungu na serikali yako isiyojali majukumu yake ya msingi kwa wananchi wake.
   
 14. M

  Moelex23 JF-Expert Member

  #14
  Jan 3, 2010
  Joined: Oct 8, 2006
  Messages: 497
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Halafu jamani wajenzi humu ndani, naomba msaada.

  Zile bilioni 2.5 za nyumba 2 za BOT, zingeweza kuondoa tatizo la vitanda na wodi za kujifungulia kwenye hizi hospitali 3 tu za TEMEKE, MWANANYAMALA na ILALA??

  Kama zinaweza then vyama vya upinzani, jamani cha kuongelea ni hicho tu kwa picha ili sisi Watanzania wajinga na wavivu wakufikiri angalau hizo picha za nyumba ya Gavana na hizi za kina mama kulala chini zipenetrate ukuta mgumu unaoziba ubongo wetu.
   
 15. A

  August JF-Expert Member

  #15
  Jan 3, 2010
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Hivi je nchi za wenzetu ambako wana facilities, mbona hawa waulizi hao akina mama, Waume zenu wapo wapi, ulifunguaje miguu nk nk , ni thi thi tu ndio tunasubiri Naomi aje alie tupewe hata X-ray machine wacha Scan, Leo nenda Singida uugue na uhitaji Scanner, sharti nduguzo watafute njia ya kukutoa huko iwe kwa tractor, bicycle, pick-up, nkn kn kukuleta DSM au kukupeleka KCMC, lakini nguvu ya kununua/kujenga nyumba ya Governor. Unataka kusema ni Jukuma la kila mtu akienda hospitali aende na kitanda?
  Au ni jukumu la watu kwenda na X-ray zao hospitali?
  Au hujao hiyo picha kwamba wanashare vitanda au nafasi haitoshi , maana jengo ni dogo?
  Unataka kumaanisha leo hii wewe ukiugua utakwenda na chumba chako hapo Mwananyama, au Amana Ilala au Temeke.
  Nafikiri umesoma na unaelewa majukumu ya Serikali na hata ukiwa huja soma bado utaelewa haki zako.
   
 16. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #16
  Jan 3, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Maisha ni safari ndefu ndugu yangu angalia usije ukawa wewe au mkeo hawa hawakuitaka hii hali, hakuna mtu asiyependa raha au anayependa kuteseka.

  Mie ndio maana nilisema katika thread nyengine kuwa Ndullu angelikuwa ameona mbali asingelihamia katika hiyo nyumba maana watanzania tunamchukia sio siri. Msomi kama yeye alieingia kwa mikwala kuwa atakomesha ufisadi na kuirejesha imani kwa wananchi kwenda kuishi katika jumba la gharama kama hilo is unjustifiable hata kama watatoa risiti zote. Hizo angelijengewa robo au nusu yake nyengine zikatumika kwa taifa.

  Hivi huyu jamaa anajua kijijini ukiumwa hata dawa ya malaria hakuna!!!! inabidi upande taksi kwenda mjini kununua just dawa ya malaria. Tunakoelekea Tanzania kwakweli tutakuja kucharazana bakora haki ya nani tena!!!!
   
 17. Rufiji

  Rufiji JF-Expert Member

  #17
  Jan 3, 2010
  Joined: Jun 18, 2006
  Messages: 1,710
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 160
  Mwanakijiji,

  Asante sana mzee kwa hizi picha nilikuwa naomba kama ikiwezekana ile picha ya kwanza na jengo la gavana ziwekwe pamoja. Hii inatosha kuonyesha Tanzania mbili, moja ambayo watu wengi wanaifahamu nyingine inayofuraiwa na wachache.

  Kitu kingine kinachoniumiza kichwa hawa wapinzani wako wapi? Hizi ndio hoja za kushikia bango! Waachane na operesheni sangara ambazo ni vigumu kwa mwananchi wa kawaida kuelewa.
   
 18. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #18
  Jan 3, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  You have to be serious man...!! The matter here is are we setting our priority correctly as a country? Ability to give a birth is not a certificate that you are economically capable. Remember nature has no medicine.
   
 19. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #19
  Jan 3, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  nilichojaribu kusema ni kuwa
  watu wachukulie kuwa afya zao ni muhimu
  kuliko kununua khanga au hereni za dhahabu...
  zipo dispensary nyingi za binafsi za bei nafuu.....

  sio lazima kila mtu akasuburi huduma
  ya bure mwananyamala au amana.

  mimi binafsi nawajua wamama kadhaa ambao
  wana uwezoa kwenda kwenye dispensary
  za binafsi za bei nafuu,but wanaenda
  hospitali za serikali kwa kila tatizo lao.

  wapo kweli masikini wasio na uwezo
  but sio wote,wengine ni mazoea ya
  huduma za dezo.
   
 20. Facts1

  Facts1 JF-Expert Member

  #20
  Jan 3, 2010
  Joined: Dec 23, 2009
  Messages: 308
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Jamani mimi ni mgeni humu JF niliambiwa na rafiki yangu nijiunge na JF kwasababu kuna watu wanatoa changamoto zenye mantiki, kama ndizo hizi eeehee nimechoka kabisa NO COMMENT.
   
Loading...