Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,580
- 23,915
Napenda kumwomba anayejiita Boss achukue time out kidogo kwani kadiri anavyoendelea kutoa ufafanuzi kwa kile alichoandika mwanzo ndivyo anavyozidi kudhihirisha ulimbukeni wake. Eti anashangaa kwa nini hawa kina mama wanaenda kujifungulia kwenye hospitali za serikali wakati za binafsi zipo. Sijui umri wake wala kisomo chake lakini hili dai lake ni dhihaka na tusi kwa wananchi wote kwa ujumla wao linaloweza kutolewa tu na chizi, ndio nasema chizi. Je, kulingana na kichwa cha hii thread, anahalalisha hali hii kwa sababu haoni umuhimu wowote wa sekta ya afya kuimarishwa badala ya nyumba ya Gavana. Je, kwa nini angependa kuona hao watu anaodai wana uwezo wakienda kutibiwa katika hospitali za binafsi hadi awatukane na kuwakejeli kwa kwenda Muhimbili. Je, anawaambiaje na hao watoto wanaokaa sakafuni au juu ya matofali bila madawati, na wao waende shule za international za binafsi. Kwa mtindo huo si ajabu akawashangaa wanaolala njaa kwa kukosa chakula majumbani na huku hoteli zipo.