Hapo shida sio mama bali ni baba, kwa nini alikimbia mji? Pia baba alikuwa si mpambanaji ndo maana akatawaliwa na mkewe. Mama ni maamuzi yake kuuza au kununua kitu kwa sababu ametafuta mwenyewe, we tafuta vyakwako mkuu na utoke hapo nyumbani usije ukajaza mimba mabeki tatu.
Kwanza kabisa ujue sipo nyumbani.
Baba baada ya kuzidiwa na vimbwanga vya mother aliondoka akaenda kuoa mke mwingine akajenga na akaendelea na maisha yake!
Mama tangu auze mali zote na kuenda kutoa zote kanisani, hadi leo amekuwa ni mtu wa kutangatanga tu, sisi watoto ilibidi tulelewe na ndugu tu(wajomba) kwa kutanga tanga vile vile, humiliations tulivumilia tukakua!
Baada ya sisi kumsaka na kumpata baba, mama alianza kupambana kurudiana na baba, baba alikataa vibaya mnoo, kwa kuapa ni bora afe kuliko kurudiana na mama! Mimi kama mwanae ilibidi ni muulize baba tatizo hasa ninini?
Alinijibu "mama yako alikuwa mke mwema sana kabla hajaingia kwenye hiyo dini yake, hiyo dini imemharibu siwezi kuishi naye tena".
Mimi kama mtoto wa kiume tangu 2021 nimejaribu sana kumuwezesha mama atoke kwenye haya maisha ya fedheha!
Sina uwezo mkubwa sana, life langu ni la ku struggle sana, so mara moja moja nimekuwa nikipata pesa naongea nae like "mama angalia kwenye shughuli zako, fanya tathmini nikutafutie mtaji walau tuboreshe mazingira yako na kipato chako"
Mama ukimpa pesa leo asubuhi let's say 1M, kwanza anasafiri kwa wapendwa kwenda kuwaonyesha jinsi Mungu alivyomuinua, na sasa watoto wake wanampa mamilioni, hapo anoenda kuwatambia wananyumba zao yeye kapanga hata kodi tu hana uhakika wa kulipa, akitoka huko anapita kwa mchungaji wake anamnunulia suti, watoto wa mchungaji anawanunulia nguo nzuri, na mama mchungaji ananunuliwa gauni, then anarudi nyumbani hana hata mia, after 1 week anakupigia simu kuomba umsaidie hela ya kula.
Mdogo wangu alimtengenezea mradi wa nguruwe, kamlimia mazao ya chakula na msimu ukakubali haswa, lengo baada ya mavuno, na nguruwe wakikua tumnunulie site tumjengee walau atoke kwenye upangaji, ikayokea harambee ya ujenzi kanisani, mama alitushangaza na kutu katisha tamaa sana kwa alichotufanya!
Ndipo nilipokumbuka maneno ya marehemu baba.
2024 niliamua kuoa, sasa vita anayopelekewa mke wangu ni balaa, kwanza nalaumiwa kwanini sijoa binti wa kilokole, pili, zile projects nilizokuwa namtengenezea anavuruga kwa kupeleka kwa watumishi wa Mungu kwa sasa zimepungua! Juzi nilisanuliwa na mdogo wangu mama amefunga maombi ya siku saba kuombea ndoa yangu ivunjike, hamtaki mke wangu sababu, sio mlokole!
Brothers, hata kwa ncha ya upanga sitaoa mlokole na najuta kuzakuzaliwa na mlokole wa aina hii, kwa sababu matatizo aliyotusababishia kama familia, traumas alizotusababishia na mambo anayoendelea nayo ni unexplainable, ni aibu na ni fedheha.