Saikolojia: Sababu zinazosababisha magonjwa ya akili ambazo wengi hawafahamu. (psychological disorder)

Education Mentor

JF-Expert Member
Oct 26, 2016
396
687
“Know yourself is beginning of all wisdom” <Aristotle>

1. MWANZO
upload_2018-3-27_0-44-17.png

Kwanza ningeliweka wazi hili suala kabla ya kuendela na makala hii fupi Ijapokuwa magonjwa ya akili ni magonjwa tu kama mengine ya mwilini na mengi tu yanatibika.

Nakumbuka kuna ndugu mmoja wa karibu kabla sijaenda kusomea saikolojia chuoni nilikuwa nashindwa muelewa hasa tabia zake hakuwa na mood stable kabisa. lakini baadaye nikajafahamu alikuwa na dalili za Biporal disorder, lakini namuanza vipi kumuambia? Sababu kumuambia mtu ana ugonjwa wa akili katika jamii zetu ni “tusi” umemtukana kama yeye mwenyewe hakujigundua kwa hilo.

Na mara nyingi sababu kubwa sana zinazokuwa zinatajwa zinatokana na magonjwa ya akili na wengi huwa wanazifahamu ni tatu (i)Kulogwa (ii)Matumizi ya madawa ya kulevya na vilevi.(iii) Radhi ya mzazi hasa mama

Ni kweli Madawa ya kulevya ni sababu kubwa mojawapo na hata katika hiyo ya kulogwa inaweza kuwa kweli sababu ulimwengu wa giza shambulizi mengi huwa katika fikra za mtu. Sina lengo la kuzichambua sababu hizo tatu

Katika mada hii Nimejikita katika kuangazia sababu ambazo jamii myingi huwa imezipuuza.

2. UCHUNGUZI KIFANI (Case study).

MFANO

Kulikuwa kuna mtu mmoja marekani alieitwa “Andrew Laeddis” baada ya kutoka kupigana vita ya pili ya dunia (World War Two) alirudi nyumbani marekani kama ilivyokuwa taratibu hasa wamarekani vijana mara nyingi waliporudi kutoka katika kutimiza majukumu ya kulinda na kupigania taifa lao. Aliamua kuoa Mwanamke aliempenda alieitwa Dolores Chanal na akawa anafanya kazi ya Upolisi ambao wanafahamika kama Marshall yaani kwa mazingira ya huku nyumbani tungewaita askari kanzu au wapelelezi (Katika kutekeleza majukumu yao huwa hawavai uniform kama wengine)

Maisha yakawa yanaenda na alikuwa anampenda sana mke wake na wakafanikiwa kupata watoto watatu Wawili wakiume na wa mwisho wakike. Ijaapokuwa kutokana na kazi aliyokuwa akiifanya ilimpa majukumu mengi sana kiasi kukosa kuwa na muda na familia yake.Wakati Binti yake mdogo akiwa na umri wa miaka 4-6 mara kwa mara alikuwa anapokea mashtaka kutoka kwa binti yake sana kuhusu mama yake.

Kumpa ripoti ya nyumbani (nini huwa kinaendelea wanapobaki na mama yao) kuhusu mama yao tabia zake zilikuwa hazieleweki (ni kawaida baba kuwa na uhusiano wa karibu na binti yake au zake kuliko kwa watoto wa kiume). Lakini Andrew hakuwa sana na muda na hilo na aliipenda familia yake sana labda pengine ndilo lilomsukuma sana kutofuatilia habari hasi (negative) kuhusu mke wake.

Siku iliyombadilisha kabisa maisha yake Bwana Andrew Laeddis kama kawaida arirudi nyumbani baada ya wiki nzima kuwa busy au kutingwa na majukumu ya kazi. Ilikuwa jumamosi akafika kwake “Honey I’m Home” (Ni msemo wanaopenda kutumia Wazungu wanapokuwa wamerudi majumbani kwao) lakini hakusikia kuitikiwa akawa napita sebuleni akatoke jikoni akatoa kwenda uwani kwake (Nyumba yake ilikuwa karibu na Mto) akamuona Mke wake kakaa kwenye bembea peke yake huku anaimba. Na Mke wake alipomuona jambo la kwanza alilofanya alimkimbilia mme wake kumpokea kwa upendo mkubwa tu kama kawaida (wazungu huwa wana kiss) kama msisitizo wakati wanabadilishana maneno kwa dakika 1 Ndipo akauliza kwani watoto wako wapi? (Sababu alizoea kupokewa na famila yake yote).

Mkewe akamjibu wameenda shule, Andrew Laeddis akashtuka Shule? Mbona leo jumamosi, Mkewe akamjibu Shule yangu (Huku akicheka). Sasa Bwana Andrew Laeddis ndipo akaangalia upande wa mto uliopita kwao anawaona watoto wote watatu miili yao ikiaelea juu ya Maji. Kwa kuhamaki anatoka mbio kuelekea sehemu hiyo na anajitupa ndani ya maji anaivuta miili ya watoto wake nje anaenda ilaza ufukweni na kujaribu kuangalia kama bado ina uhai. Anagundua ameshachelewa na wakati huo mke wake anaendelea kucheka.

Ndipo anamvaa kwa nguvu na kumuuliza Kwanini!? kwanini umefanya hivi!? (Huku kamkamata mabega). Akili ya mke wake Bi Dolores Chanal inakua kama imerudi sasa na kugundua ni nini alichofanya. Anamuambia mume wake nasikia kama nina mdudu kichwani huku akilia hivyo anamuomba sana wakati huo hamuweke huru amuue. Bwana Andrew akiwa kachanganyikiwa anampiga mke wake risasi ya tumboni anaanguka palepale na kufariki dunia.

Bwana Andrew Laeddis ndio anazidi kupagawa anashindwa amshike yupi amuache yupi sababu tayari chini kuna miili ya watu wanne Mkewe aliempenda sana Binti yake wa pekee na watoto wake wa kiume wawili.

Haikuishia Hapo yakamshinda mabaya yale kuvumilia maisha yake yalibadilika kabisa akijisikia hatia juu ya binti yake aliyemtahadharisha hali ya mama yake lakini halimpuuza, na jinsi alivyomuua Mkewe mtu aliempenda sana maishani kwake.

Kwa kuwa alikuwa na Marshal baada ya Muda akaanza kumtafuta Yule mhusika aliyewaua Mkewe na Watoto wake. Baada ya kuota ndoto mara kwa mara Mke wake na binti yake wakimtokea na tena wakimsihi akalipe kisasi kwa mtu aliyeitwa “Andrew Laeddis” kwa mauaji yale aliyowatendea na wakati huo kumbukumbu mbaya za aliyoyaona wakati wa kuikomboa kambi ya wafungwa wakiyahudi na wakivita katika kambi ya “Dachau” (Dachau concentration camp) wakati wa vita ya pili ya dunia hivyo vyote vikimsumbua akili yake.

Hivyo anaandaa Mission binafisi ya kumfuatilia muuaji wa mke wake na watoto wake (ambaye ni yeye mwenyewe) wakati huo na yeye akiitwa “Edward Teddy” na sio tena “Andrew Laeddis”(Kalibadili jina lake kuishinda dhamira yake)).

Walichofanya Idara ya Polisi alipokuwa akifanya kazi walimpeleka Hospitali ya Wagonjwa wa akili ili kumsadia askari mwenzao kurejesha akili zake tena. Na aweze ku-cope na hali aliyoipitia kimaisha.

3. UTANGULIZI

Nafikiri kuna kitu utakuwa umejifunza tiyari kuhusu Bwana “Andrew Laeddis” Kisa cha maisha yake na hadi kuugua Ugonjwa ya akili.

Nimeleta hivi kwa makusudi ili tupaje kujifunza hasa katika Ulimwengu wa leo ambapo kutokana na hali za kimaisha wengi wamejikuta wakiangukia katika matatizo hayo.

Wapo baadhi ijapokuwa sio wote wameonekana Makanisani wanamapepo kumbe ni hali kama hizo zimewakuta (Mfadhaiko wa akili) kutoka na nyakati flani tofautitofauti wanazozipitia maishani ambazo ngumu



4. FAHAMU KINACHOSABABISHA MAGONJWA YA AKILI , KANSA AMBAZO WENGI HAWAFAHAMU

(Nimejumuisha Uzoefu na Tafiti halisi)

i. KUTOJISAMEHE AU KUSHINDWA KUJISAMEHE

Nimekutana na clients wa namna hii Yapo mambo mengi yanatukuta unaweza kufanya jambo la kutisha kwa mtu mwingine au kumjeruhi na namna nyingine lakini Dhamiri yako inapokushinda (Kushtaki) Ukajua kabisa ulikosea suala hilo halafu ukajipiga kwenda kuomba msamaha. Msamaha pengine ukakataliwa au kwa namna nyingine ikukute Case ya mazingira ya kama Bwana “Andrew Laeddis” ambaye moja ya chanzo la tatizo la akili alilolipata ilikuwa ni kukataa Kujisamehe tu.

Matokeo yake anajaribu kuitoroka Nafsi na Roho yake anatengeneza nyingine bila yeye kujua ndani ya mwili huo huo na anatengeneza mission ya kujitafuta yeye mwenyewe na tena akimaanisha kabisa kulipa kisasi cha damu kwa ajili ya mauaji ya famila yake.


upload_2018-3-27_0-44-59.png

(Picha hii ilipigwa na Mpiga picha Kevin Cartel 1960-1994 (Kushoto juu) 1993 na baadaye ilimpa tuzo ya kimataifa ya Pulitzer Prize lakini kutokana na tukio hilo liligusa hisia za ulimwengu kuhusu hatima ya mtoto na inaonesha Kevin hakufanya lolote kuhusu maisha ya mtoto huyo zaidi ya kumpiga picha tu, Baadaye mwaka uliofuatia Kevin alikutwa amejiua.)

Ni kawaida sana wengi wamejikuta wakiugua Magonjwa ya akili kwa kukataa kujisamehe, na wengine wamechukua hatua ya juu zaidi ya kujiua ili kujaribu kukimbia hatia katika ulimwengu wake mwenyewe. Pengine wakidhani ndio suluhisho la pekee la kuwaweka huru.

i. KUKATAA KUKUBALI UKWELI (FACING REALITY)

“..Tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru...” <Yohana8:32>

Neno la Mungu linasema Mtaifahamu kweli kisha itawaweka huru.

Mwanadamu anaepitia nyakati hizi kwenye saikolojia tunawaingiza katika kundi la watu wenye kuhitaji Crisis Counselling. Wapo watu wengi sana baada ya kuambukiwa VVU au kugundua anaumwa Kansa au kupatwa na tukio baya labda kuondokewa na Mtu aliyempenda au kufeli shule na sababu nyingine nyingi. Kwa kawaida huwa ni kipindi kigumu sana.

Wapo nimewahi kuwaona ambao walifikia hali si nzuri kabisa kiakili hata kwenda kulazwa Wodi ya watu wenye Magonjwa ya akili “Muhimbili Psycho ward” baada ya kupatwa kuambukizwa VVU sababu tu kuendelea kukataa kukubaliana na hali iliyompata.

Na wapo Wanafunzi hasa katika ngazi baada ya kufeli (Discontinuous) au kushindwa endelea na masomo wakijaribu kujiua kwa kujirusha magholofani vyuoni kwao.

Huu huwa ni mgogoro mkubwa sana wa nafsini na mbaya zaidi unaposhinda upande mbaya (Kukataa hali) au Negative side ndipo yapo maamuzi mabaya yanafuatia.

Wakati wote unapokutana na hali yoyote jifunze kujikabidhi kwa Mungu hasa unapokabiliana na hali ngumu za kimaisha kuna mwanafalsafa mmoja alisema “Ni ujinga pale mtu unapokataa kuwa hatuna nyakati za kupita gizani katika maisha” hivyo ni muhimu hatua ya kwanza ya kutoka katika hali ya msongo au katika hatari ya kuelemewa katika fikra zako.

Jifunze kubaliana na ukweli wakati wote kwa lolote lililokutokea na hiyo ni hatua ya ushindi katika changamoto yoyote utakayokabiliana au tatizo lilokupata.

ii. UCHUNGU BITTERNESS

"..Samehe kwa faida yako si ya aliyekukosea.."
Uchungu kama Sababu ya kimaumbile
.

Wanaume wanapokutana na mazingira ya yenye kusababisha uchungu au stress wao huzitoa nje yao (External) kwa njia ya uharifu au tabia zinazojumuishwa kama (Antisocial) au matumizi ya vilevi (Substance abuse Disorder)

Lakini Wanawake wao maumbile yao uzikabili ndani yao (internal) hivyo ujikuta wapo sana katika hatari ya magonjwa ya akili ambayo ni zao la Uchungu mfano Eating disorder, Mood Disorder na anxiety disorder na mengi ikiwemo zaidi kansa.

Katika tafiti iliyofanywa miaka ya karibuni wanasayansi wamegundua asilimia 69 kama sikosei chanzo mojawapo cha magonjwa ya kansa au sababu ya watu kuugua kansa ni tabia ya kuwa na uchungu labda wenye kutokana na kutosamehe kuhifadhi kisasi na vitu vingine kama Hasira na imedhibitishwa kabisa.si hivyo tu magonjwa ya moyo, Kisukari, Pressure ya (Kupanda na kushuka).

Kutokana na kitu kama uchungu ambacho ni suala la kihisia (Emotional) na tafiti ya masuala ya akili inadhibitishwa wanawake ndio watu ambao ni wenye hisia sana. Na asilimia kubwa wanaougua kansa wanajikuta wa jinsia hiyo. Mfano kansa ya Matiti, Milango ya uzazi nk.


iii. KUMKATAA MUNGU AU KUTOTAKA KUWA KARIBU NA MUNGU

“..Waliomwambia Mungu, Tuondokee; Tena, Huyo Mwenyezi aweza kutufanyia nini?”<Ayubu 22:17>

Zipo tafiti nyingi zimethibitisha watu wanaoishi kwa miaka mingi ni wale wanaohudhuria sana katika ibada.

Sababu kuwa karibu na Mungu kunampa mtu afya Nzuri ya akili hata kama ni Mgonjwa lakini fikra chanya zinazotokana na Neno la Mungu zinamsaidia mtu kuweza cope na changamoto za maisha, kuwa na tumaini, imani na upendo ni tiba ya akili nzuri kwa nafsi ya mwanadamu.

Sababu Mausia na Maonyo yanayotokana au kutupa mwenendo unaofaa mfano kuepuka tabia uzinzi “Sexual immorality” Ulevi Kisasi na kutosamehe nk. ni sababu tosha kudhibitisha kwanini wanao mcha Mungu wanadumu kiafya ya akili na hata kimwili kwa muda mrefu kuliko asiyejihusisha na Mungu.
upload_2018-3-27_0-48-35.png


(Muigizaji wa Hollywood Marekani Marilyn Monroe aliwahi kufuatwa na Billy Graham kumuhubiria akamjibu “Simuhitaji huyo Yesu wako” licha kuwa Maarufu ulimwenguni pote na kuwa tajiri miaka hiyo. Marilyn alijiua kutokana na Ugonjwa wa akili “Msongo wa Mawazo” au “depression” kwa mujibu wa Daktari wake binafsi aliyekuwa akimtibia)
Hupo utafiti unaeleza kuwa wengi wanahojishughulisha Na shughuli za kiimani Na dini zimewapunguzia hatari ya kupatwa Na matatizo ya Msongo WA mawazo, Kujiua na kufariki mapema tofauti na asiyejishughulisha na masuala ya imani kwa Muumba wake.


iv. MTINDO WA MAISHA HASA WATOTO WANAOLELEWA NA MZAZI MMOJA. (SINGLE PARENTHOOD)

“..Uimara wa taifa unaanzia kwenye uadilifu Nyumbani...” <Confucius>
upload_2018-3-27_0-49-4.png

(Kushoto ni Joseph Stalin wa Soviet Union na Kulia ni Adolf Hitler wa Nazi Germany wanafanana kimaisha hasa wakati wakiwa wadogo wakipitia maisha ya kunyanyaswa na kuishi kwa kulelewa na mzazi mmoja )

Imekuwa ni aina flani ya staili ya maisha. Mara kwa mara hasa wadada (Sihukumu) kuamua kutafuta Mwanaume wa kuzaa nae mtoto baada ya hapo kila mtu anachukua 50 zake. Lakini zipo tafiti mbalimbali zimekwisha kufanywa namna kuna athali ya aina gani pale mtoto anapolelewa na Mzazi mmoja (bila baba) (Tafiti imejumuisha pia matokeo ya kutalikiana kwa wazazi au malezi ya mzazi mmoja asiyejari kutoa huduma ya matunzo kwa mtoto wake).

Ijapokuwa si watoto wote lakini tafiti zinabainisha kuwa.

Matokea ya utafiti huo ilikuwa kama hivi wa watoto wanaolelewa na mzazi mmoja hasa mama tu au kutokuwa na ukaribu na baba mzazi (Biological father):

· 70% ambao wanaoamua kuacha shule wenyewe bila kufukuzwa au sababu yoyoye (School dropout)

· 90% ya watoto wanaokimbia makwao na kwenda kuishi mitaani (Street Children)

· 71% ya wasichana 12-19 wanaopata ujauzito (Teenager Pregnancy)

· 63% ya vijana wanaofanya maamuzi ya kujiua (Teenager suicide)

· 70% Vijana wadogo wanaoishia jela za watoto au vituo vya kurekebishia tabia (Juvenile delinquency)

· 80% Wanaojikuta wabakaji (Rapist)

· 85% ya watoto wanaokutwa na matatizo ya kisaikolojia (Psychological disorder)

· 79% ya vijana wanaojikuta katika matukio ya uharifu na mauaji (Adolescent murders)



Labda Kama ukuwahi kusikia pia Adolf Hitler katokea single parent (Bila baba), Dictator Joseph Stalin, Saddam Hussein ni wengi kama nikiwataja.

Joseph Stalin kutokana na sera zake na ugonjwa wa akili aliougua “Paranoia” alisababisha mauaji na vifo vya watu inakadiliwa milioni 40 hadi 60.

Adolf Hitler kutokana na sera zake ikiwemo na sera ya ubaguzi (anti-Semitic), chuki kwa wapinzani hasa wakosoaji wake na kuanzisha vita ya pili ya dunia hivyo alisababisha vifo vya watu milioni 17 hadi 20.

Hivyo fikiria mara mbili zaidi ni kizazi gani tunakitengeneza baadae kwa mfumo wa maisha ambayo tunauchukua (Single parenting style) hasa kutoka katika tamaduni hii.

Na si tu single parenting au masuala ya kutalikiana wazazi na kumuacha mtoto alelewe na mzazi mmoja.
upload_2018-3-27_0-50-11.png


(Kushoto Rashid Mberesero mtuhumiwa wa mauaji ya wanafunzi chuo kikuu Garissa Kenya, na kulia Nikolas Cruz mtuhumiwa mauaji shuleni Marjory Stoneman Douglas High School, Florida, Marekani, wote wanahistoria zinazokaribiana kufanana katika ukuaji na maisha yao awali)

Kama utakuwa pia una muda wa kufuatilia kajifunze pia kuhusu wale wanafunzi wanao waua wenzao mashuleni kwa bunduki nchini marekani, tukirudi kwa kijana Rashid Charles Mberesero Mtanzania aliyehusika na Mauaji ya wanachuo wa Garissa nchini Kenya.

Kisha jiulize mfumo mpya wa kimaisha tunaouchukua “single mother and dad” Tunatengeneza kizazi cha watu wa aina gani hapo baadae? tafakari jamii kubwa inapoamua kuchukua mfumo au mtindo wa maisha ya namna hii kwa tafsiri nyingine taifa halitakuwa salama.

‘..Mwanangu, yasikilize mafundisho ya baba yako, Wala usiiache sheria ya mama yako...” <Mithali 1:8>

v. KUPENDA TEGA SIKIO KUSIKIA UOVU, KUFUATILIA HABARI MBAYA (NEGATIVE NEWS OR INFORMATION).


Naweza kusema wanadamu wana aina mbili ambayo wanatakiwa wale vyakula ili wawe na afya nzuri ya kwanza ni Mungu alitupa mdomo kwa ajili ya kuutumia pale tunapo kula Chakula kusudi tuzidi kuwa imara kiafya na kuendelea kuishi.

Namna nyingine tunakula kupitia Nafsi zetu na tumbo letu ni akili zetu na udhabiti wa afya ni fikra. Muhimu Sana ufahamu Yale unayoyasoma iwe vitabu, majarida, magazeti kwa muda mrefu ndio yanatengeneza mfumo wako wa kufikiria mambo na wakati mwingine misimamo yako na maamuzi. Pasipo kusahau yale unayotega sikio lako kusikia pia.

Hivyo kuwa sana muangalifu na unachosoma na kusikiliza huwe na msimamo wa kuchagua sababu mbinu ya “Mind control” hapa ndipo hufanya kazi sana na watu wengi sana waliopatwa na shida za namna hii au wenye uchungu, hasira na baadhi ya magonjwa ya saikolojia huwa ninawashauri kujaribu sana kuchagua kusoma au kusikiliza habari chanya.

Kujifunza kujidhibiti katika hilo Ijapokuwa ni vigumu sana katika ulimwengu huu wa leo lakini Uchaguzi ni wako.

vi. MAWAZO MABAYA (HAJIONAVYO NAFSINI MWAKE NDIVYO HALIVYO)

Katika moja ya wananadharia wanaotumia mbinu ya kufanyia watu tiba za kitabia hasa magonjwa ya akili kama phobia, anxiety, depression na bipolar disorder nadharia hii inaitwa Cognitive behavioral therapy (CBT)

kundi hili wanaamini asilimia kubwa ya watu wanaopatwa na matatizo ya kisaikolojia hata kufikia uchizi au kupata magonjwa mengine ya kimwili chanzo chake kinaanzia katika mawazo ya mtu huyo (jinsi anavyojiwazia kutokana na vichochezi katika mazingira yake)

Hivyo Mawazo yanaathiri Hisia na Hisia zitaathiri Tabia na tabia itazidi weka madhara makubwa katika mawazo ya mtu huyo

Saa hali hiyo inapokuwa inajirudi jirudia ndipo inapozidi kupata nguvu ndani ya mtu huyo na madhara yananiongeza
upload_2018-3-27_0-51-36.png

(Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo)

Mfano baada ya mwanafunzi kufeli mtihani wake kwa mara nyingine tena labda pasipokujua tatizo linaweza kuwa aina ya usomaji wake) anaweza kusema tu mimi sina akili katika mawazo kwahiyo anapokutana na mitihani ya shuleni (hisia) zake zinatawala nitafeli kwahiyo anaanza kukimbia mitihani au hasomi tena (Tabia).

Kwa mfano huu hapo baadae anaweza kujikuta kamapata magonjwa ya kisaikolojia kama depression kwanini wengine wanafaulu lakini mimi nimesoma wewe lakini nimeshindwa kufaulu.

Hivyo magonjwa mengi sana yakisaikolojia yaanaanzia kwa namna wewe unavyojiwazia kwanza. Wakati wote kumbuka hajionavyo nafsini kwake ndivyo alivyo.

5. HITIMISHO

Nashukuru kwa kusoma makala hii fupi naamini umepata kitu naomba nikushirikishe kusaidia kuwafikia wengi kwa kushare.

Na makala hii natamani imfikie na hizidi kumtia nguvu jf member Candlelight na wengine wengi tofauti.

Education Mentor ana shahada ya Saikolojia, ni mwanasaikolojia anayeegemea kutambua uwepo na asili ya Mwanadamu inatokana na Mungu (Creation Theory).

Saikolojia: Fahamu tabia ya hasira, madhara yake na namna za kuishinda
 
Mimi binafsi nakumbwaga sana na Anxiety disorder ila Nashukuru Mungu kanipa upeo na Jf na internet najitahidi kujiweka sawa mpaka nakua sawa.

Mwaka juzi ndio kwa mara ya kwanza nilijigundua nmepatwa na anxiety disoder... miezi miwili akili yangu haikukaa sawa..ila hakuna watu wa pembeni walijua.
Ilianzia baada ya rafiki yangu kipenzi kuugua ukichaa gafla nikishuhudia... halafu na mm nna tatizo la hormone imbalance nikawa sifahamu
Maana ukiwa na tatizo hilo Inakua rahisi sana kupata anxiety disorders... sasa siku moja nilipatwa mshituko wa moyo.. hapo ndipo mambo yalipoanza nikawa nahisi kama na mm nachanganyikiwa ..ikaenda nikaanza kuumwa homa kali ,nikawa siwezi kula yani chakula kinaishia kooni kinarudi koo limefunga sasa nikiona ivyo nazidi kuchanganyikiwa nikilala naota ndoto za kuchanganyikiwa tu
Niliishi muda mrefu bila amani nilihangaika nikafika mahala nikawa naona dunia mbaya hakuna haja ya kuishi mbona wengine wanaishi kwa amani why me!? nikawa naogopa watu yani nikimwona mtu hasa wanaume moyo unashtuka nawaogopa bila sababu ,nikawa najiuliza huli ni pepo au ,basi nikijiuliza ivo nazidi kuchanganyikiwa.

Lakini nikaenda nikachunguza ,nikaunganisha This/That nikaga kugundua nna anxiety disorder.. kumbe tatizo ni Hofu/woga/wasiwasi

Yani huwezi amini nikajitibu tu akili yangu yani ni very simple.....
kumbe matatizo nilikua nayatengeneza mwenyewe kichwani kwangu ...halafu nayaogopa at the same time.

Mpaka leo naweza overcome moods mara nyingi,naweka kupanic halafu baada ya dk1 nikawa mpole gafla, natumia sana neno LET,let it be ,let my mind free,let let let

pia nasamehe kwa manufaa yangu,huwaga simsamehe mtu kwa manufaa yake ,hapana kwa manufaa yangu ili niwe na amani tu.

Ila nimebaki na tatizo moja tu maisha niliyoishi yameniathiri saikolojia mno hasa maisha ya shule .. kwahiyo sometimes huwa napata sonona ila sio muda wote.....

Asante kwa somo mkuu...
 
Back
Top Bottom