Walokole wengi wana magonjwa ya afya ya akili?

Walokole wengi wana magonjwa ya afya ya akili?

Kachina95

Member
Joined
Mar 7, 2019
Posts
60
Reaction score
210
Wanajukwaa sina mengi ya kueleza, lakini itoshe kusema hawa watu wanaosali makanisa ya kilokole kwa asilimia kubwa wanamatatizo makubwa ya afya ya akili!

Mama yangu ni mlokole, Imagine back then 1998 aliachana na baba sababu baba kakataa kuokoka, baba kafanyiwa matukio mpaka akakimbia familia. Guess what? Mama aliuza nyumba na kiwanja, pesa zote kapeleka kwa mchungaji(Moses Kulola).

Baada ya hapo tuliishi maisha ya shida sana, taabu mno! Huku akitujaza sumu kwamba baba katutelekeza, baba ni mbaya, baba hamjui yesu, anavuta sigara na mengine mengi!

Mungu si Athumani tumekua tukamtafuta baba(kwa sasa ni marehemu).

Sasa tunauona moto alioukimbia baba!

Nilijiapiza kutokuoa mwanamke mlokole, hata wife siku akirenda tu kwenye makanisa ya kilokole, it is over!

Nawasihi sana vijana wenzangu, usithubutu kuoa mlokole!

USISEME HUKUAMBIWA
 
Sio walokole tu, iwe mkristo au muislam au Imani yoyote, mtu yeyote akishika dini kupindukia uwezo wake wa kufikiri kawaida inapungua. Mambo mengi anaanza kuyatazama kiimani zaidi wakati mambo ya kawaida kwenye maisha ya mwanadamu.
 
Sio dini tu, hata siasa.

Imagine mtu anagawa pikipiki nchi nzima ili umchague, wewe mchaguaji HUJIULIZI KITU?
 
Tatizo kubwa ni kwamba IMANI hua haitaki matumizi sahihi ya AKILI (logic)

Kadiri unavyozama kwenye imani ndivyo na matumizi ya akili unaweka pembeni
Sio walokole tu, iwe mkristo au muislam au Imani yoyote, mtu yeyote akishika dini kupindukia uwezo wake wa kufikiri kawaida inapungua. Mambo mengi anaanza kuyatazama kiimani zaidi wakati mambo ya kawaida kwenye maisha ya mwanadamu.
 
Wanajukwaa sina mengi ya kueleza, lakini itoshe kusema hawa watu wanaosali makanisa ya kilokole kwa asilimia kubwa wanamatatizo makubwa ya afya ya akili!

Mama yangu ni mlokole, Imagine back then 1998 aliachana na baba sababu baba kakataa kuokoka, baba kafanyiwa matukio mpaka akakimbia familia. Guess what? Mama aliuza nyumba na kiwanja, pesa zote kapeleka kwa mchungaji(Moses Kulola).

Baada ya hapo tuliishi maisha ya shida sana, taabu mno! Huku akitujaza sumu kwamba baba katutelekeza, baba ni mbaya, baba hamjui yesu, anavuta sigara na mengine mengi!

Mungu si Athumani tumekua tukamtafuta baba(kwa sasa ni marehemu).

Sasa tunauona moto alioukimbia baba!

Nilijiapiza kutokuoa mwanamke mlokole, hata wife siku akirenda tu kwenye makanisa ya kilokole, it is over!

Nawasihi sana vijana wenzangu, usithubutu kuoa mlokole!

USISEME HUKUAMBIWA
KUOKOKA NI LAZIMA. USIPOOKOKA NI KUANGAMIA. KUOKOKA NI KUUPATA UZIMA WA MILELE. UKIMPA BWANA YESU MAISHA YAKO UNAKUWA NA UHAKIKA WA MAISHA HAYA NA YALE YAJAYO, YA MILELE PAMOJA NA BWANA. WATU WOTE TUSEME AMEN.

Jesus is Lord & Savior
 
Hata mimi aisee mwanaume mlokole simtaki.
Watu wanamtukuza mchungaji kama Mungu wao. Halafu wachungaji wenyewe aina ya kiboko ya wachawi na wale wengine wapuuzi..!!

Muda mwingi wanautumia kushinda kanisani na kwa mchungaji kuliko muda wa kutafuta pesa na kuangalia familia zao..!!
 
KUOKOKA NI LAZIMA. USIPOOKOKA NI KUANGAMIA. KUOKOKA NI KUUPATA UZIMA WA MILELE. UKIMPA BWANA YESU MAISHA YAKO UNAKUWA NA UHAKIKA WA MAISHA HAYA NA YALE YAJAYO, YA MILELE PAMOJA NA BWANA. WATU WOTE TUSEME AMEN.

Jesus is Lord & Savior
Mkuu vipi kuhusu issue ya mleta mada kwa Mama yake kuuza Nyumba na kiwanja kisha pesa zote akapeleka kwa mchungaji,
hili unalizungumziaje?
 
Walokole hasa wa makanisa ya mabati/majamvi au yaliyokuwa hivyo hamna kitu,bora mpagani.
Kuna dogo anaishi na mke wake kwenye kiwanja changu ananilindia. Sasa kuna kifaa nilihifadhi kwa huyo dogo nikawa nakihitaji nikafanyie kazi.

Nikamcheki dogo kwenye simu ili aniletee mahali nilipo, akasema hayupo nyumbani na mke wake simu yake imeharibika, hivyo ikabidi niende nyumbani kwake. Kufika hapo kwa dogo nikakuta wanasali (walokole kama 10 hivi)ile kijumuiya nadhani ilikuwa asubuhi. Nikapiga mahesabu kusubiri mpaka wamalize kusali nitakuwa nimechelewa kazi yangu. Nikanyata mdogo mdogo mpaka wanaposali nikakatisha ibada nikasema samahani kwa usumbufu za asubuhi, hakuna alieitikia, waliniangalia kwa hasira na dharahu, miguuni nilikuwa na vumbi. Basi mke wa dogo akawa ameniona nikamwambia anipe kifaa.

Nakiri kukosea kwa kukatisha ibada lakini kwa watu wa Mungu kweli walitakiwa wanisikilIze kwanza bila kuonyesha hasira na dharau maana pengine nilikuwa nahitaji msaada mkubwa kwao,pengine kuna ajali nahitaji msaada.
 
Huyo alirukwa na akili
Bora yule alirukwa akili, wa saivi ni vichaa kabisa, wanapotezwa na the so called miujiza, "nilikuja hapa mwezi wa 12 mkesha wa vuka na chako, saivi nina nyumba tatu, biashara naenda China, na sasa na mpango wa kufungua tena manini nini" watu wanalipuka shangwe mojaa😀😀😀 mtu anatoka hapo naakili ya maombi kachanganyikiwa, ni maombi na sadaka ya kujimaliza humwambii kitu ohooo miaka inakata yeye na kanisa, mpaka msongo wa mawazo maana hapati cha kutolea ushuhuda kumbe wenzie ndumba, kazi sana, kudanga saana, kupangwa sana watoe ushuhuda ohooo
 
Back
Top Bottom