Wajua Tanzania Haijawahi Kuwa na Katiba ya Wananchi?. Katiba Hii Iliyopo ni ya CCM!, Pongezi Katiba ya Samia, Ndio Katiba ya Kwanza ya Wananchi!.

Wajua Tanzania Haijawahi Kuwa na Katiba ya Wananchi?. Katiba Hii Iliyopo ni ya CCM!, Pongezi Katiba ya Samia, Ndio Katiba ya Kwanza ya Wananchi!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
57,101
Reaction score
128,716
Wanabodi,
Makala yangu kwenye gazeti la Mwananchi la leo,
Katiba Mpya ya Samia Ndio Katiba ya Kwanza ya Wananchi.jpg


Utangulizi:
Bandiko hili ni bandiko la manifestation ya Katiba mpya, japo hata mchakato wa Katiba mpya bado haujaanza, bandito linatoa pongezi kwa Katiba mpya ya Samia!, hii ni kufuatia kushindikana kwa mchakato wa Katiba mpya ya Warioba, hIvyo kutumia powers za manifestation kuwezesha Katiba mpya ya Samia kuwezekana.


Hii ni kufuatia michakato yote ya Katiba Nchini Tanzania, kukumbwa na mitafaruku na sintofahamu. Mwalimu Nyerere ndiye aliyeanzisha mfumo wa chama kimoja, ila kukana na mgombea binafsi. Kwenye uchaguzi wa Mwaka 1965 Jimbo la Mbulu, wana kijana wao Herman Sarwak, wananchi walimuomba agombee kupitia chama cha TANU, huku rafiki wa mwalimu, Chief maarufu wa kabila la Wagorowa Chief Amri Beo Dodo, anataka kugombea, Mwalimu Nyerere akalazimisha Sarwak akatwe, TANU ikamtea Chifu Amri Dodo, Sarwak akagombea kama mgombea binafsi, Nyerere akcja Mbulu kumpigia kampeni rafiki yake Chief Amri Dodo, haikusaidia kitu, Wana Mbulu, wakampiga Chini Chifu na kumchagua Kijana Sarwak, ndipo Nyerere akapiga marufuku mgombea binafsi.

Kitendo cha kufanya mabadiliko ya katiba bila kuruhusu mgombea binafsi, kilimkera Mwalimu, mwaka 1995 akakemea wazi wazi kushindwa kurekebisha hilo, hivyo tukaingia uchaguzi wa vyama vingi kwa Katiba ile ile ya CCM ya chama kimoja.

JK akataka kutuletea Katiba mpya, akaunda Tume ya Warioba, likakusanya maoni ya Watanzania, akaunda Bunge Maalum la Katiba, likaja na Katiba pendekezwa, ila muda haukutosha, hivyo mchakato ukaingizwa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2015-2020. Akaingia Mwamba akasema "Katiba sio kipaumbele changu".
kwanza tukauliza, Kitendo cha Kukiuka Ilani ya CCM Bila Kikao Chochote, Sio Udikiteta? kisha tukatoa hoja hii Trends, Visions: Watanzania msitatizwe na kauli zake kuhusu Katiba, baada ya Nyerere, ni Magufuli ndiye ataacha legacy kubwa ikiwemo Katiba Mpya!
Kwa bayati mbaya Mwamba akatwaliwa kabla ya kutupatia Katiba mpya.

Hivyo alipoingia Rais Samia nikashauri Hongera Sana Rais Samia kwa Miaka Miwili Madarakani. Japo Umefanya Mengi, Makubwa, Mazuri, Lakini Bado! Linalowezekana Leo, Lisingoje Kesho!, Rais Samia akamaliza miaka yake 4, bila kutekeleza hili.

Hata hivyo hoja ya Katiba mpya ikawekwa kwenye Dira ya Taifa na Ilani ya CCM, na Rais Samia akaahidi mchakato wa Katiba mpya kuanza ndani ya siku zake 100 za kwanza, ndio hizi zinafiki na sio dalili, hivyo inatubidi kutuma manifestation kufanya hili la katiba liwezekane, hivyo neno katiba ya Samia na pongezi kwa Rais Samia kwa kutupatia Katiba mpya ya Samia, ni manifestation ya Katiba mpya, bila kufanya hivi, kutatokea tena kitu, Katiba ikaendelea kiwa hadithi. Tusiruhusu!.

Leo naendelea na makala za historia ya Katiba Tanzania, ambayo tulianza wiki iliyopita, tuliangazia katiba 4 za mwanzo za Tanzania, kuanzia katiba ya uhuru, 1961, katiba ya Jamhuri, 1962, Katiba ya Muungano 1964 na katiba ya mpito ya mwaka 1965. Leo tunaiangazia hii katiba iliyopo sasa ambayo ndio Katiba ya kwanza ya Kudumu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya mwaka 1977.

Katiba hii ya sasa, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ni katiba ya tano, lakini nayo pia haikushirikisha wananchi. Katiba hii ilipatikana kupitia Tume ya Rais Nyerere, wakati huo nchi ikiwa chini ya mfumo wa chama kimoja, huku chama kikiwa ndio kimeshika hatamu za kuongoza serikali, Rais Nyerere ambaye pia Mwenyekiti wa chama cha TANU, aliteua wajumbe 20 (10 toka kila upande wa Muungano) ikiongozwa na Sheikh Thabit Kombo Jecha na Katibu wake akiwa Pius Msekwa. Tume hii ilifanya kazi ya kutunga Katiba ya CCM ambayo ilizaliwa baada ya kuunganisha vyama vya Tanganyika African National Union (TANU) na Afro-Shirazi Party (ASP) tarehe 5 Februari 1977. Katiba hii ya CCM ndio iligeuzwa kuwa Katiba ya JMT ya 1977, na ilijikita katika misingi mikuu mitatu ambayo ni urais wa kifalme, mfumo wa chama kimoja cha siasa na muundo wa serikali mbili kuelekea serikali moja. Katiba hii ilipitishwa na Bunge la chama cha Mapinduzi, CCM, kwa kujigeuza kuwa Bunge Maalum la Katiba na kuipitisha katiba hiyo ndani ya muda wa dakika 30 tuu!.

Katiba hizo. Zote tano, hazikushirikisha wananchi. Mchakato wa kwanza wa kushirikisha wananchi ni ule wa Tume ya Jaji Warioba na Bunge Maalum la Katiba, lakini mchakato huo haukukamilika, hivyo mchakato wa Rais Samia kuelekea katiba mpya, ambao utashirikisha wananchi, na hatimaye kama katiba itapatikana, hii itakuwa ndio katiba ya kwanza ya wananchi, kwa nchi ya Tanzania, hivyo na heshima ya Rais Samia, napendekeza katiba hii iitwe Katiba ya Samia, baada ile Katiba ya Warioba kushindikana.

Katiba ni Nini?. Katiba ni mkataba kati ya watawala na watawaliwa, ndio mamlaka kuu ya nchi inayopaswa kuheshimiwa na wote, na kwa Tanzania yetu, hakuna yeyote aliye juu ya Katiba, ndio maana viongozi wetu, tukiisha wachagua, au kuteuliwa, wanakula kiapo cha utii wa katiba, kuilinda, kuiheshimu, kuitetea na kuitekeleza.

Katiba ni ya Kazi Gani. Katiba ndio msingi Mkuu na muongozo wa uendeshaji wa nchi yetu, ambapo sheria zote, taratibu zote na kanuni zote, za kufanya kila jambo, lazima zitokane na katiba.

Misingi ya Katiba- Katiba yetu imeweka misingi mikuu 4 ya katiba ambayo ni uhuru, haki, udugu na amani.

Misingi hiyo yaweza tu kutekelezwa katika jamii yenye demokrasia ambayo serikali yake husimamiwa na Bunge lenye wajumbe waliochaguliwa na linalowawakilisha wananchi, na pia yenye Mahakama huru zinazotekeleza wajibu wa kutoa haki bila woga wala upendeleo wowote, na hivyo kuhakikisha kwamba haki zote za binadamu zinadumishwa na kulindwa, na wajibu wa kila mtu unatekelezwa kwa uaminifu.

Katiba ni ya Nani? Katiba hii ni katiba ya wananchi, au katiba ya watu, na imetungwa na Bunge maalum kwa niaba ya Wananchi, kwa madhumuni ya kujenga jamii kama hiyo, na pia kwa ajili ya kuhakikisha kwamba Tanzania inaongozwa na Serikali yenye kufuata misingi ya demokrasia.

Hivyo kwa mujibu wa katiba hii, kitu muhimu kabisa kwa Taifa la Tanzania, ni watu!, Watanzania, hawa ndio wenye katiba!, katiba ni mali ya Watanzania. Ni watu hawa Watanzania, walioweka misingi mikuu minne ya katiba yetu, uhuru, haki, udugu na amani. Msingi mkuu wa kwanza wa katiba yetu ni uhuru, wa pili ni haki. Hivyo vitu vitu viwili vikuu vya katiba yetu ni uhuru na haki, bila uhuru, hakuna haki, bila haki hakuna amani!.

Katika uendeshaji wa nchi, tuna mihimili 3 ya Dola inayoendesha nchi yetu, mihimili hii ni Serikali, Bunge na Mahakama. Ili kuendesha nchi kuna watu muhimu sana, ambao wanatajwa na katiba ili kuhakikisha katiba inafuatwa, hawa ni wanasheria.

Licha ya viongozi wetu kuapishwa kuilinda na kuitetea katiba ya JMT, lakini baadhi ya viongozi wetu ni wasoma katiba wasioielewa katiba, wanaapa kuilinda katiba wasioielewa na mwisho wa siku, badala ya kuilinda na kuitetea katiba, wao ndio kwanza wanakuja kuikanyaga na kuivunja katiba bila wao kujijua, kwasababu hawajui watendalo kuwa ni kinyume cha katiba!.

Licha ya viongozi wetu kuapishwa kuilinda na kuitetea katiba ya JMT, lakini baadhi ya viongozi wetu ni wasoma katiba wasioielewa katiba, wanaapa kuilinda katiba wasioielewa na mwisho wa siku, badala ya kuilinda na kuitetea katiba, wao ndio kwanza wanakuja kuikanyaga na kuivunja katiba bila wao kujijua, kwasababu hawajui watendalo kuwa ni kinyume cha katiba!.

Mhimili wa Serikali, tuna wanasheria serikalini, tuna wanasheria Bungeni na tuna wanasheria Mahakamani, ambao ndio walipaswa kuijua katiba kindakindaki!, lakini kwa bahati mbaya sana, baadhi hawa wanasheria wetu, nao pia hawaijui katiba yetu!. Matokeo yake ni Serikali yetu, inatunga miswada ya sheria ambayo ni batili kwa kwenda kinyume na katiba, hivyo viongozi wetu wa serikali wanajikuta wanavunja katiba bila wao kujijua.

Mhimili wa Bunge letu nao, licha ya kushehenezwa na wanasheria manguli, wabobezi na wabobevu wa sheria, wanaipokea miswada hiyo batili kutoka serikalini na kuitunga kuwa sheria, hivyo Bunge nalo linavunja katiba kwa kutunga sheria batili kinyume na katiba.

Mhimili wa Mahakama nayo ndio wenye jukumu la kutafsiri katiba na sheria, ambao imeshehenezwa majaji na mahakimu, ambao ni wanasheria manguli, wabobezi na wabobevu, ila wote hawa wameingia ganzi ya upofu (too blind to see) kushindwa kuona katiba inavunjwa, kwa serikali kutunga miswada batili kinyume cha katiba, Bunge linatunga sheria batili, huku mahakama ipo na inaangalia tuu.

Ujio wa katiba mpya, utayaondoa haya makandokando yote ya katiba hii iliyopo na Rais Samia, atakuwa ni Rais Shujaa wa kwanza wa Tanzania, kuwapatia Watanzania, katiba ya wananchi.

Mungu Ibariki Tanzania

Paskali
 
Mratibu Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Wakili Onesmo Olengurumwa @olengurumwa2 , ameshauri tarehe 29 Oktoba iwe siku ya kumbukumbu rasmi ya kitaifa ili kuwakumbuka waathirika wa matukio ya siku hiyo na kuzuia historia isijirudie.

Kupitia ukurasa wake wa Mtandao wa Kijamii, Olengurumwa Olengurumwa amesema matukio kama hayo yanapowekwa kwenye kumbukumbu ya kila mwaka ni rahisi kuyazuia yasitokee Tena kwa kuonesha athari zilizotokea.

“Hata tarehe 29 Oktoba inapaswa kuwekewa kumbukumbu rasmi, makumbusho na mijadala ya kila mwaka ili kuzuia historia isijirudie tena.” Ameandika Olengurumwa.

Akizungumzia suala hilo Olengurumwa amerejea mifano ya matukio makubwa ya kihistoria duniani, ikiwemo mauaji ya kimbari ya Wayahudi yaliyofanywa na Wanazi chini ya Adolf Hitler, ambapo takribani Wayahudi milioni sita waliuawa (Holocaust).

Onesmo Ameeleza kuwa Januari 27 alifanikiwa kuhudhuria Katika maadhimisho ya Holocaust yanayofanyika kila mwaka ili kuwakumbuka waathirika wa matukio hayo.

“Wiki iliyopita, kama sehemu ya International Holocaust Remembrance Day, tulipata heshima ya kumkaribisha Tana Ross (aliyepo katikati), manusura wa Holocaust, msanii, na mtetezi wa haki za binadamu. Tulitazama filamu yake inayosimulia maisha yake akiwa mtoto mdogo katika kambi ya Theresienstadt, na jinsi alivyofanikiwa kutoroka hadi Sweden."

Olengurumwa kupitia chapisho lake, amesema wayahudi takribani milioni 6 kwenye tukio hilo waliuawa, huku sababu zilizotumika kuhalalisha mateso yao hazikuwa na mashiko yoyote.

“Waliteswa kwa kiwango kisichoelezeka, wakinyimwa utu wao, haki zao, na hatimaye maisha yao. Ukweli ni kwamba hawakuteswa kwa sababu walifanya kosa lolote la kibinadamu, bali kwa hofu, chuki, propaganda, na wivu uliochochewa na nguvu zao katika elimu, biashara na mtandao wa kimataifa." Ameandika.

Amefafanua kuwa historia kama hizi zinapaswa kuhifadhiwa na kujadiliwa kila mwaka kama kumbukumbu za kudumu.

"Kumbukumbu si kwa ajili ya kulia yaliyopita pekee, bali ni silaha ya kuzuia uovu wa kesho" amesema.
1770206760162.jpg
 
Katiba Hii Iliyopo ni ya CCM!, Pongezi Katiba ya Samia, Ndio Katiba ya Kwanza ya Wananchi!.
Samia hakuchaguliwa na wananchi, kwa hiyo Katiba yake haiwezi kuwa ya wananchi, hiyo ni yake na kundi lake.

Halafu, baada ya yale mauaji yake ya maelfu ya Watanzania MO29, chochote kwa jina lake hakiaminiki wala kukubalika.

Kama kuna nia njema Fufueni ile Rasimu ya Katiba ya Warioba, inajitosheleza na imesheheni maoni, matamanio na matakwa ya wananchi
 
Samia hakuchaguliwa na wananchi, kwa hiyo Katiba yake haiwezi kuwa ya wananchi, hiyo ni yake na kundi lake.

Halafu, baada ya yale mauaji yake ya maelfu ya Watanzania MO29, chochote kwa jina lake hakiaminiki wala kukubalika.

Kama kuna nia njema Fufueni ile Rasimu ya Katiba ya Warioba, inajitosheleza na imesheheni maoni, matamanio na matakwa ya wananchi
kigezo gani unatumia kusema samia hajachaguliwa na wananchi?
 
Back
Top Bottom