Wadada wenye akili, heshima na adabu ni ngumu sana kuolewa dunia ya leo. Ndoa zimebakia kwa micharuko tu

Tatizo ni kuwa too much selective. Zamani haikuwa kawaida binti kukosa mume. Siku hizi binti wengi wakiaona wamesoma kidogo wanajali material things na wanapokuja kugundua kuwa peke yake haziwezi leta furaha ndo wanaanza kuzitafuta ndoa. Bahati
mbaya wa kuwaona nao wanakuwa washakata tamaa. Ndo unaona mtu analeta post kama hii.

Unalopaswa kujua ni kwamba pamoja na kwamba mwanaume anaweza kusema wanawake ni wengi na akitaka muda wowote anaoa bado hata wanaume wana changamoto sana ya kupata wenza sahihi. Kwahiyo unavoona wanawake wengi wamekuwa micharuko, ni vivyo hivyo wanaume wanavyozidi kupata ugumu wa kuwapata wenza.
Halafu wengi wa hao wanatafuta ajira ya ndoa na sio ndoa.
 
Wewe kuwa na heshima, kwa hiyo hata mke wangu nyumbani ni mcharuko?

Hao uliowa-mention hapo ukitoa wenye adabu huwa wanatokea watu kwa wakati sahihi ili wawaowe ila wanakuwa macho juu juu kuchagua mara awe mrefu,awe six pack,awe mweupe na awe caring awe na pesa nyumba na gari na elimu nzuri mkiona wasiofanya machaguo kama nyie wanaolewa mnaishia kuwaita micharuko.

Acha kuchagua chagua hovyo uone kama hukuolewa kesho.
yaaani awe na magari sijui elimu ndo ke nipeleke kikwapa pale mwee!!...
Mwenye bahati ni yuleee aliye pata nae hivyo vitu.....
Sawa umepeleka kikwapa labda apate zaidi...akifilisika hee!! Utajiona una mikosi.
 
Kwa mtu kamili kuchagua lazima. Hata Mungu ana chagua wa kumbariki siyo hovyo hovyo tu!!

Watu tumeumbwa kwa mfano wake. Km huchagui wa kuolewa nae wewe si kiumbe wa Mungu nae mjua.
 
Halafu wengi wa hao wanatafuta ajira ya ndoa na sio ndoa.
wengine wana haja ya harusi na siyo ndoa. Wengi wao hufukiria ndoa ili kuwakoga wenzao na hawako tayari kwa majukumu ya ndoa.
 
  • Thanks
Reactions: RMC
Si kweli. Wanaume wengi wameoa wanawake ambao siyo machguo yao. Wengi wlitaka kupita kuonja lkn inatokea demu ana nasa mimba. Maisha ya ndoa yamaanzia hapo.

Nasema wengi, siyo wote.

Mm Sexless ni kungwi la kitaa. Nishaona na kusikia mengi.

Mkuu ukipata Nusu ujue umekosa Nusu - by Mwana FA

Kila jambo lazima linapande mbili, ila niamini mimi hao unaoona wamenasa mimba hawaolewi bahati mbaya,, Mwanaume anakuwa amepiga hesabu kati ya huyo aliyempa mimba na mademu wake wengine na hatimae huyo anaibuka kidedea.. Wangapi wanazalisha na wanakataa watoto au hawaoi kabisa..

Demu anayetangazwa kanisani au Msikitini ndio huwa mshindi na huwa hapatikani bahati mbaya..
 
Mdada Una post picha kila weekend uko hotelin..
Picha uko mwenyewe aliekupeleka hotelin haionekani
Haijulikan ni mtu mmoja au kila weekend una
Sponsor mpya wa bata
Kila kinacho trend upo nacho..
iPhone mpya unazo huku unasema unatafuta kazi..


Sasa nani anataka hizo stress?
Hahahahahahha unajitafta mabalaa kuoa mke kama huyo😅
 
Si kweli. Wanaume wengi wameoa wanawake ambao siyo machguo yao. Wengi wlitaka kupita kuonja lkn inatokea demu ana nasa mimba. Maisha ya ndoa yamaanzia hapo.

Nasema wengi, siyo wote.

Mm Sexless ni kungwi la kitaa. Nishaona na kusikia mengi.
Sidhani kama mimba tu inatosha kumbana mwanaume akuoe. Kama amaekubali kukuoa baada ya wewe kupata mimba ujue anakupenda pia. Wangapi wamezalisha halafu wanasema watalea mtoto?
 
Shida ipo kwa wadada wenye maadili. Wa kufanana nao hawapo. Wanaume walio wengi ni uso mkavu, kiatu kichafu kichwani hamna kitu
Tatizo kubwa ni kwa wanawake. Wanawake wengi wanapenda waume ambao kimuonekano na swaga zake itakuwa rahisi kumtambulisha kwa rafiki zake. Unaweza kuta mwanaume anafaa kabisa lakini bado binti anatafuta yule wa kuringishia kwa rafiki zake kama vile anaolewa kwa ajili yao.
 
Wdada waliojitunza na wenye kuishi kwa kufuata miiko na maadili hawaolewi. Kwasabb watu waovu ni wengi kuliko wema.

Dunia imejaa ubatili na hivyo wenye ubatili wametamalaki. Wakaka wengi wametawaliwa na tamaa za kishetani.

Akili zao ziko kwenye "kuonja", kuangalia makalio, shepu na rangi ya ngozi. Wanapuuza sifa za ndani ya mtu.

Hivyo kwa mdada mwenye maono, ndoto zake na mwenye kujitambua anaona bora atulizane tu. Acha micharuko iendelee kuolewa.

Mkuu, umeona mbali sana. Na hii unaikuta bongo tu 🤣 maana wanaume wa bongo asilimia kubwa hawajatulia mzee
 
Back
Top Bottom