Nitajie tarehe yako na ya mwenza wako nikwambie mpo vipi na hatima yenu, siri yake n.k

Rakims

JF-Expert Member
Jun 4, 2014
4,982
4,478
Habari zenu wana ndoa na wenye ndoto za ndoa,

Yawezekana umewahi kusikia kauli maarufu sana inasema;
"Kosea yote usikosee ndoa"

Katika thread hii nitakupa maana halisi na siri iliyojificha nyuma ya kauli hiyo hivyo ukiweza kunitajia tarehe yako na ya mwenza wako na herufi zenu za mwanzo,mchumba,mpenzi na mwanandoa nitakupa taarifa zako na zake na siri zake kimapenzi hivyo utakachojua hapa ni kitu kitakachokusaidia kuimarisha mahusiano yenu au kuyaharibu kabisa.

man-and-woman-zodiac-compatibility-in-love-and-relationship.jpg


Yafuatayo nitakutajia;
  • Tabia zake
  • Sehemu yake ya hisia
  • Jinsi ya kumfanya azidi kuwa karibu na wewe
  • Mtizamo wake kwako
  • Mtizamo wako kwake
  • Unachopenda akufanyie
  • Udhaifu wake
  • Na vingine vya ziada
MATOKEO:
Kwa asilimia 90 nitakayokwambia ni ya kweli kama sivyo basi kuna mmoja kati yenu alidanganya tarehe kwa mwingine,

MFANO WA KUANGALIZIWA
Ili niweze kukuangalizia vizuri andika hivi;

Mimi mwanaume Jina langu (Herufi ya kwanza);
Nimezaliwa tarehe: 14 December mwaka
Mwezi wangu Jina lake (Herufi ya kwanza)
Kazaliwa tarehe: 24 April mwaka

(Kisha unaweza kusema upande gani nikazie zaidi japo sio lazima)

MEMBER WA KWANZA
Ke 24/4 P

Me 14/12 E

Matokeo yake:

MTIZAMO WAKO KWAKE;

Wewe ni mtu mwenye tabia za maji na yeye ni mtu mwenye tabia za udongo kwa mjumuiko huu unaonyesha kabisa nyinyi kuendana ni vigumu na hata kama mnapendana vipi itakuwa dhoruba tu ndani.

Kwa mtizamo anaonekana yeye ni mtu wa kupenda utawala na ukubwa kwa kuongoza mambo/kupelekesha- ambapo wewe unaonekana sio mtu wa kupelekeshwa na hautakubali hilo.

Pia, wewe ni mtu wa kuhitaji mabadiriko,anuwai,matukio ambapo hayo humfanya yeye kujihisi tofauti na wewe kwa kuwa yeye ni mtu wa ambaye hujifanya ni mjuaje na incharge wa mambo yanavyokuwa yanakwenda katika miliki yenu na kujiona ni mtawala mzuri wa tabia za nyumbani na hujiona ni mwenye hekima na heshima na imani zaidi kuliko wewe. Yeye anakuwa ni mtu wa kutaka kufanya mambo ambayo teyari yana uhakika na kutaka kufanya mambo yenye uhakika, wakati wewe unakuwa upo teyari kufanya chochote kinachowezekana.

Na pia wewe ni mtu wa kusema chochote kinachokujia na nimtu wa kumdondoshea maneno tu randomly yanayokujia kichwani kwa fikra yako ambayo humfanya kuanza kujawa na hasira taratibu. Pia kuna tatizo la pesa katika mahusiano yenu, hiyo ni sababu wewe unataka kuzalisha pesa kwa yanayowezekana leo hali ya kuwa yeye anawaza kuhusu mambo ya kesho (ukifa unaniachaje). Mna muda mfupi sana kwenye mahusiano yenu.

MTIZAMO WAKE KWAKO:
Mapenzi yenu yanaweza kwenda kama tu ataweza kujikaza vizuri kuwa na wewe au kukuvumilia kwa maana mtizamo wake kwako wewe ni mtu ambaye huvumiliki. wote mnavutiwa zaidi kwa muonekano wa mwenzi wake, kwa tamaa zake yeye alizonazo katika kufanya tendo anakuwa anavutiwa zaidi na ufanyaji wako.

Lakini ni mtu inamuwia ugumu katika kuvumilia tabia yako ya kupepesa macho na kutizama mambo mapya(wanawake wa nje) wewe ni mtu wa kuchukulia kila jambo poa poa na rahisi rahisi inapokuja katika maswala ya mahusiano na tendo la ndoa wakati yeye ni mtu muda mwingi anataka kuwa serios kwenye mahusiano na kutawala. hali ya kuwa wewe ni mtu ambaye hutaki kutawaliwa kimapenzi na mtu yoyote hakuna baya kwenu lakini ni watu wenye kupishana mara kwa mara uhawara kwenu inakuwa ni starehe kuliko ndoa. maana mnaweza kukaa kwenye uhawara miaka ila mwezi tu ndoa ikawa ndoana.

Mahusiano yenu ya ndoa yatakuwa ni vichekesho tu.

SEHEMU ZAKE ZA HISIA:
Sehemu zake za hisia ni shingo na koo ndio maeneo ambayo kuna hisia zake kubwa za kiwazimu ikiwa;- utagusa eneo hilo,kumbusu na kutomasa eneo hilo hata kama umekaa nae basi utampandisha kwa kasi sana hisia zake na hasa ukiwa umekaa karibu nae ukawa unamgusa hapo chochote unachosema kinaingia kwenye akili yake na roho yake moja kwa moja kuhusu wewe.

Ukimbusu eneo hilo vizuri na kumng'ata kichokozi akiwa kalala chali na kwenye koo lake basi utaona maajabu. Fanya mbinu hii pia itakuongezea umaarufu kwake. Mfanyie massage hii ili kuweza kumfanya siku yake yote ajihisi yupo kwenye raha:

(1)Akiwa kalala kwa mgongo wake muwekee mitetemo kwenye shingo yake karibu na mizunguko ya masikio yake kwa kutumia vidole vyako tumia miondoko ya taratibu sana kwa maana sio punda huyu kama kina fulani huyu anataka vitu sensitive rudia hivyo hadi uone vipele vimesimama kwenye mikono yake. (Be very gentle kuzunguka sehemu ya pipe za hewa kwenye shingo vinginevyo utamniga).

(2) Kumbuka ni mtu mwenye kupenda zaidi kufanyiwa hivyo akiwa kalala kwa tumbo lake hivyo fanya hivyo hadi kukaribia eneo la muunganiko wa uti wa mgongo lakini usitoke nje ya shingo maana umeme utakatika halafu ataona unamtembezea wadudu.
Ukianza kuona vinyweleo vimesimama na vipele basi jua chini hali si shwari wacha niishie hapa na Ramadhan hii nisije nikafanya mambo magumu masaa yamebaki machache.

Ikiwa utamgusa au kumfanyia manjonjo sehemu za shingo yake basi ni mtu mwenye kupata hisia za kiwazimu na wewe ikiwa atajua kucheza na mapaja yako yako basi ataweza kukupeleka mbali sana kihisia hisia zako siwezi kukwambia sana kwa maana wewe unamtizamia yeye.

UTAMVUTIA VIPI:-
Yeye kwanza sio mtu wa papara ni mtu anapenda kama ni utafiki ama mahusiano basi yaanze taratibu kama vile unajenga nyumba mapenzi kwake anataka uanzie msingi kwanza hivyo inakutaka kuwa ni mtu mwenye subira kuweza kummudu kimapenzi na subira wewe muda mwingine ni kitu huwa,

Mbinu;
kwanza kabisa kama ndio unaanza nae basi hakikisha kuwa unakuwa ni mtu wa kwanza kumtafuta na usiende nae kwa pupa kama hujagusa katika kujifanya ni mtu mwenye subira sana basi moja kwa moja hutampata kwa maana kama ni wa dada wazamani huyu atakwambia nisubiri miezi 9 nikufikirie.

Muonyeshe kuwa upo radhi kuwepo muda wote pale anapokuwa anakuhitaji na ujionyeshe kuwa wewe ni mtundu mtundu. Yeye hupenda mtu anaekuwa taratibu taratibu na kama unaweza kumsababisha kucheka cheka basi huna muda mrefu unayoyataka utapata. Pia utaanza kumuona nae ni mtu anautundu utundu na kupenda utani utani na anapenda mtu mwenye kumvutia kwa yale anayoyafikiria akilini kwake yaani unatakiwa kujipendekeza kuuliza unataka niwe vipi?

Tabia zake za kero ndogo ndogo ni mategemeo yake uzifurahie na ujifanye kucheka anapoongea upumbavu au jambo lisilo na maana kwako.

Na kama akisema kwa utani ukajibu kwa utani basi moja kwa moja anakufungulia moyo wake na kuona hakuna mtu kama wewe duniani hapa na anaweza kukuganda kama kupe pia utani wa kimwili kama kumgusa mwili na kumminya minya ni vitu anapenda kama ni mke wako basi jaribu leo hata akinuna ukifanya hivyo anakaa sawa. Ni mtu kama unataka kumtoa basi anapendelea sehemu za hadhi ya juu kidogo na anapenda sehemu anayoenda kuwe kuna watu wanaojua nini wanafanya hasa wapishi. Mnunulie kinyaji kisichokuwa na kilevi ndio mapenzi yake kama sio mlevi lakini kama ni mtumiaji basi utakuta ni mpenzi wa wine.

Mazingira ya nyumbani ukimpikia hata chochote tu hujihisi special sana na hataskia la mtu kuhusu wewe valia mavazi ya kupika unapomuandalia chakula na hakikisha muonekano wako uwe ni safi mfanyie hivyo hata mara moja kwa mwezi utaanza kuona anatoa machozi

Ikiwa mazungumzo yanachelewa basi jitahidi asikushinde kimaongezi na wala usikwame katika kuzungumzia mnayoyapenda hasa akianza kuongelea pesa muhimu tabaka hili ni mwanamke mwenye kupenda pesa na kuigiza hajali pesa.

Pia tengeneza account mbili tatu za bank ili akitizama aone kabisa ni mtu mwenye kushughulika na mambo ya saving hata kama huna pesa atatambua ukipata utatunza.

Usihodhi mazungumzo. anapoanza kuzungumza usimkatishe na usiwe mzembe katika kutoa sifa akifanya kitu hata cha kipuuzi nyumbani,kwenye gari yake,mapambo ni watu wenye kupenda kusifiwa wanapofanya mambo madogo.

UCHAMBUZI WA KINA:
Habari wacha nikujibu kwa upendeleo na faida ya wengine pia nadhani niliishia kwako

Nakujibu kwa uchambuzi mpana size ya kati na mwenye kutaka full atalipia pia wacha nikupe mfano;

Nge & Kaa Chumbani na urafiki wa karibu Utangamano wenu:

Nyota yako kwanza kabisa inahusiana na kifo na kila aina ya jambo baya kwa maana ina tawala mlango wa nane (House of dealth and regeneration). na vile vile wenye nyota yako sifa hizi mbaya huja kutokana na hisia kali ulizonazo na pia ukandamizaji wako katika tendo la ndoa,
Kwenye mahusiano yeye (Kaa) mara nyingi ni mwenye kukuelewa zaidi hasa linapokuja suala la kuelezia hisia zako nzito kwake na kwa mambo mengine pia. Unatarajiwa kuwa na giza kubwa sana la wimbi la ngono hata kama utakuta unajizuia vipi. Na hii hupelekewa pale yeye atakaposhindwa au kuogopa kuhimili mikiki mikiki yako ya chumbani, vile vile mahusiano yenu kingono ni mazito sana na matamu kuliko kawaida unless uwe na matatizo ya kisaikolojia ila kama kati yenu hakuna mtu mwenye matatizo basi mahusiano kati ya Nge na kaa ni mahusiano ambayo watu wengi wanatamani kuwa nayo kwa maana ukiskia moja kati ya real love ndio hii couple.

Mahusiano haya ya nyota hizi mbili za asili ya maji yaani maji ya moto na maji ya bahari ni yenye kuvutia na kupendeza machoni kwa watu kwa jinsi mnavyokuwa hata mbele za watu. Kwa hapa hujakosea kama hujafunga ndoa basi nenda hata kafunge kesho.

Hii ni zawadi kubwa kuwa na mahusiano haya. Yeye(Kaa) ni mpenzi hasi na wewe (Nge) ni mpenzi chanya na vile vile kuna moto mkali wa mahaba unaotoka kwako kwenda kwake katika wimbi la kiroho ambao unapelekea mahusiano haya kuwa madhubuti. Joto la chumbani pia ni habari nyingine hapa mnafaana na kuendana sana.
Joto hilo la chumbani huamsha hisia kali na hupelekea kichochezi cha wawili nyie kuoneana wivu wa kupindukia.
Wewe ni mwenye kumjanza nguvu na ulinzi wa hali ya juu na yeye ndicho kitu ambacho anatafuta zaidi kwenye mahusiano kwa maneno mengine anaweza kukuita soul mate. Yeye ni mwenye kwenda sawa na kila mtu ni mtu wa watu na mwenye kupenda watu wote sio mbaguzi na anapokuwa na wewe hili huwa dhahiri kwake, na ni kitu ambacho wewe unapenda kukiona kiwepo kwa mwenza wako. Nyie wawili mnaendana kama mkate na Jam.

Haya ni mahusiano kati ya nyota mbili za maji ambapo mapenzi yenu kila mmoja anataka na kupendezewa kuona hisia kali kwa mwengine na ni kitu ambacho wote wawili kila mmoja yupo radhi kumgawia mwenzie bila choyo wala kumbania, Mnapoingia kwenye mahusiano basi mnakuwa na upendo usio na mipaka na urafiki wakaribu kwenu hushamiri na watu wengine hapa inategemea wa kike ni nani na wa kiume ni nani kwa maana kuna mmoja akiwa jinsia fulani basi mnaweza kuwa kama mtu na shoga yake yaani urafiki wenu hukithiri hadi kuanza matani ya kuonana mtu na shoga yake walioshibana.

Ingawa sasa nyota yako ya Nge ni nyota ya mtu ambaye ni sawa na mbalamwezi iliyodondoka ambayo mbalamwezi ni sayari ya nyota ya kaa kinajimu kwake wewe ni sawa na baba au mama kutegemea na jinsia yako. Sasa kama wewe hisia zako zikichanganyika na ukali basi mahusiano yenu yatakuwa ni sawa na mapenzi ya ugomvi wenye hisia za mahaba makali ndani yake yaani mnaweza kutukanana kisha mkacheka Isipokuwa baadae hii itakuja kumchosha yeye na vile uombaji wako wa tendo mara zingine umetawala mabavu na shari.

Kwa hivyo hapa mtakuwa mnaendana kwa asilimia 90%

Nge & Kaa uaminifu wenu

Wewe (Nge) unapopenda moja kati ya jambo kubwa kwenye mahusiano yako huwa ni Uaminifu, Ikifikia sehemu umejihisi kusalitiwa basi mara nyingi huonyesha wivu wako wote na uchungu sana bila kuficha na kila mtu aliyekaribu yako atajua kuwa umesalitiwa.
Lakini sasa kwa mwenza huyu (Kaa) anapoingia kwenye mapenzi yeye hupenda kuheshimu sana mpenzi wake na kumlindia kwa hali zote kumuhifadhia utu wake kwa maana moja kwa moja ni rahisi sana kwake yeye kujua kuwa hapa akicheza kitim tim chako ni kivumbi cha hatari kwenye wivu.

Na nyote vile ni wenye asili ya maji mara nyingi ni watu ambao usaliti kwenu kila mmoja ni kitu anachopenda kufanya japo ni wenye mapenzi ya dhati kila mmoja kwa mwenzie hivyo kwa ugumu kidogo mwanzo kwenye uaminifu mapenzi yatayumba lakini baada uaminifu huja kwa upana sana kwa maana kila mmoja kati yenu anajua ni jinsi gani mapenzi yanauma.
Moja kwa moja nyote wawili ni wenye kupeana ulinzi wa mahaba na wote mtajihisi kuhifadhika hapo baadae.

Hivyo linapokuja suala la uaminifu mnaendana kwa asilimia 95%

Nge na Kaa mawasiliano yenu na mazungumzo:
Wawili nyie ni wenye kuelewana hata kama pasipohitajika mazungumzo yaani sura tu huonyesha kujielezea kwa kila mmoja wenu. Hii pia huweza kuinfluence maisha yenu ya tendo la ndoa na kulifanya kuwa bora kuliko watu wengine. Lakini vile vile hii inaweza kuwa ni yeye kuleta mtafaruku kama mapenzi ya mwingine yataelemea katika kitu fulani tuchukulie mfano hajakupenda wewe na kapenda kile ulichonacho. Mazungumzo yenu ni mazuri sana kwa kuwa tu mara nyingi huhusisha hisia zenu. Na hata muda mwingine kwa wale wanaoanza urafiki utaona ni wepesi kila mmoja kumalizia sentensi ya mwenzie. Wote ni wenye kupenda kuzungumza mara kwa mara ingawa hili mwanzoni sio rahisi kuonekana na mara nyingi kwako wewe ni mwenye kupenda kujiweka hupendi maneno na una katabia ka kuexaggerate mambo.

Ikitokea yeye akaanza kukuona tofauti mwanzo basi moja kwa moja atashindwa hapo hapo mwanzoni kuendelea na wewe na atatafuta kila njia ili kila mtu ashike nafasi yake. Lakini hii ni ngumu kwa maana mkiwa pamoja kila mmoja wenu anatamani na kutaka kuhakikisha anamuweka mwenzie sawa vile anavyopenda aende nae yeye.

Hivyo tunapokuja kwenye maelewano yenu mnaendana kwa asilimia 99%

Nge na kaa Hisia zenu:

Hii ni nyeti sana na tawala ya kimbinu sana kwenye mahusiano kama haya.
Yeye ni mwenye kupenda sana kuishia na hisia zake au kuzificha ikiwa ni zenye faida au hasara yeye hupenda kuficha sana hisia zake.Na pia hupenda zaidi na pia katika kutumia hisia zake katika maisha yake ya kila siku basi utakuta moja kwa moja yeye ni mwenye kukuletea ugumu kuelewa kwenda na hisia zake, kwa sababu ana uwezo mkubwa wa kupotezea na kuficha hisia zake.
na akili taka lake kihisia hashindwi kupata na ni mtu rahisi sana kucheza na hisia za mtu anaweza akakujaza kisha akakuacha kwenye mataa. Kitu kinachowasaidia kwenye mahusiano yenu ni ile hali ya kila mtu kuwa na uwezo wa kustahamili mwenzie na hisia ni vitu vinavyohitajika ili mahusiano yakue japo hazina nafasi sana ya kuingilia mafanikio ya uhusiano wenu kwa maana ni kitu wewe huwa unajiamini kuwa ni cha kupanda na kushuka.
Nyote wawili mnatakiwa kujifunza jinsi ya kuachia ngazi kwenye mahusiano ya utawala isiwe mmoja ni mwenye kung;ang'ania mahusiano ya utawala ulalie kwake tu. Hii itasaidia sana katika kukuza mahusiano yenu.

Kwa hali hii kwenye suala la hisia mnaendana kwa asilimia 70%

Nge na Kaa Thamani:

Linapokuja katika suala la kuthaminiana hapa huwa kuna mtiti kwa maana yeye ni mbinafsi katika suala la thamani na ni mwenye kutaka familia yenye kumtegemea yeye tu. kwenye familia huyu ni mbinafsi na bahili, Lakini kwenye familia wewe ni mtu wa kujiachia na inapokuja kwenye kuthaminiana wewe huthamini mwanzo wa thamani yenyewe kisha baadae kushusha kisha kupanda yani wewe kwake suala la thamani ni jambo la kupanda na kushuka. Ni ngumu na ugumu kwenu huja kwenye suala la kuthaminiana hata mjitahidi vipi ugomvi wenu mkubwa utakuwa ni kuchanganya maana ya neno thamani na kujali.
Mahusiano haya yana ubovu katika matumizi ya neno hunijali na hunithamini sawa na kulinganisha pumba na mchele time zote pumba utaona mchele na mchele utaona pumba na kusahau kuwa pamoja haviliki.

Hivyo kwenye thamani nawapeni asilimia 25%

Nge na kaa Kushirikishana

Kwenye suala la kushirikishana mambo litawalindia sana issue ya nyie kuthaminiana kwa maana ndio kama nilivyosema hapo mwanzo kwamba thamani na kujali mahusiano yenu hajajui maana yake ndio maana linapokuja suala la kushirikishana utaona mmoja kati yenu anasema kuna muda ananithamini na kuna muda hanithamini hapana hayo ni matumizi mabovu ya maneno haya mawili na elimu ya kutofautisha hili hata muwe ni waelewa vipi kwenye hili la kuthaminiana hamuwezi kuendana wala kuelewana.
Lakini kwenye issue ya kushirikishana na ushirikiano basi utaona kila mmoja wenu ni mwenye kujitoa kwa hali na mali katika kusaidia watu wanaomzunguka mwenza wake mfano yeye kujali ndugu zako na wewe kujali zake.
Yeye kutokana na hitaji lake la kimama kuwalinda watu anaewapenda, na wewe (Nge) ili kuweka mipaka mizuri juu ya kile uchofikiri ni sahihi.
Ikiwa mtaunda dunia yenu ndogo yaani (nyumba yenu) basi utaona ni watu ambao ushirikiano wenu ni sawa na mapacha.

Hivyo kwa ushirikiano hapana shaka mnaendana kwa asilimia 95%

Summarize:

Mahusiano kati ya wawili nyie yanaweza kupiga kila siku hatua kutoka hatua moja kwenda nyingine. Kiukweli ni watu wenye kuendana sana na mahusiano yenu hushamiri kama umeoa au kuolewa na mtu haeleweki na umempata huyu basi muache yule kaa na huyu lakini kama upo nae kwenye mahusiano tu basi oa leo kabla ya kesho, na kama ni mtu una mfukuzia usikate tamaa.

Rakims
 

Similar Discussions

15 Reactions
Reply
Back
Top Bottom