Barua ya wazi Kwa wanawake: Usiolewe na mwanaume mpumbavu na mwoga!

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,339
51,864
USIOLEWE NA MWANAUME MPUMBAVU NA MWOGA!

Kwa Mkono wa RObert Heriel.

Leo nitakaanga wapumbavu wote na waoga bila kupepesa. Iwe ni Mimi mwenyewe, wewe au Yule. Andiko hili halitamkwepa mwanaume yeyote Mpumbavu na mwoga bila kujali nafasi yake, hadhi yake, na umri wake.

Aidha andiko hili natanguliza tahadhari ikiwa moyo wako ni mwepesi hautavumilia maonyo haya ni Bora uishie kusoma hapahapa. Endapo utakaidi ukaendelea kusoma basi nisihesabike wala nisipewe lawama Kwa madhara yatakayokupata.

Niite Taikon wa Fasihi, mkaangaji.

Mwanaume yeyote asiyemjali mke wake ni Mpumbavu.
Mwanaume yeyote asiyejali familia yake ni Mpumbavu.
Mwanaume yeyote asiyefanya kazi ni Mpumbavu.
Mwanaume yeyote asiyeweza kujitetea jamii yake ni mshenzi na Mpumbavu.
Mwanaume yeyote anayedhalilisha wanawake ni Mpumbavu.
Mwanaume yeyote anayeharibu watoto wa wenzake ni mshenzi na Mpumbavu tuu!

Enyi kina Dada, mabinti na wanawake wote, kamwe usiolewe na Mwanaume Mpumbavu.
Usimuendekeze Mpumbavu.
Usifikiri atabadilika, wapumbavu ni ngumu kubadilika.


Mwanaume yeyote mwenye aibu ya kufanya kazi ni Mpumbavu.
Usikubali hata akuongeleshe, akikufuata mtemee mate, akikuzingua mlete Polisi hapa tutakusaidia kukupa mawakili afikishwe mahakamani afungwe, apeleke upumbavu wake Jela huko.

Uliona wapi mwanaume akasikia aibu kufanya kazi. KAZI ndio inampa hadhi mwanaume yeyote.
Mwanaume habagui kazi ILIMRADI ni halali.
Mwanaume anayechagua kazi asikuoe IPO siku mtalala njaa.

Ogopa mwanaume aliyeiweka akili yake kwenye kazi moja. Mkimbie Kama ukoma. Huyo lazima akufanye uwe masikini dunia ingalipo.

Mwanaume mwoga usikubali akuoe.
Mwanaume mwoga hataweza kukulinda.
Kumbuka kuna woga na Heshima.
Kama Mwanaume woga anauita heshima mtemee mate kisha ukimbie, akikukimbiza akupige mlete kwetu tumfundishe adabu ili siku nyingine zimkae sawia.

Mwanaume anayedhulumiwa huyo usikubali akuoe. Huo ni mkosi katika familia yenu.
Usikubali kuolewa na Mwanaume anaemuchia Mungu. Mtakuwa Masikini, mtaonewa, watoto wako watateseka.

Usiolewe na Mwanaume asiyeweza kuwa hata na nyumba au Shamba, huyo atakuachia Mateso Duniani, atatesa watoto wako. Atawaacha watoto wako pasipo Urithi. Likikutongoza limwanaume la namna hiyo liliulize swali linashamba au kiwanja, Kama halina liulize utaishije na Mimi kama huna Shamba au kiwanja. Likikujibu bado linahangaika au mjini viwanja bei ghali liambie likuonyeshe Shamba au kiwanja huko kijijini. Halina litemee mate kisha toka nduki.
Usicheke na limwanaume lipumbavu litakutia mikosi na kukuzalisha Matoto ya hovyo hovyo.

Olewa na Mwanaume sio uolewe na mtu mwenye Cover/motherboard ya kiume alafu ndani ni jike jenzako.

Hakuna cha huruma hapa!
Usiolewe na Mwanaume anayependa kuhurumiwa hurumiwa, huyo ni mpuuzi.
Wanaohurumiwa ni watoto, wanawake na Wazee.
Ukiolewa na Mwanaume apendaye kuhurumiwa utaishi maisha ya kutia huruma mpaka unye mavi Kwa upuuzi wako.

Olewa na Mwanaume ambaye anapambana Kama Mwanaume. Akikosa mjini basi apate shambani. Akikosa shambani apate mjini. Sio limwanaume lililokosa bara na Pwani. Hilo usikubali kuolewa nalo. Ni ishara ya mwanaume Mpumbavu asiyeweza tumia akili yake vizuri

Usiolewe na Mwanaume anayekuhonga laki tano alafu halina hata kiwanja, utateseke wewe mpaka ukome. Huyo Hana akili nzuri no mwehu tuu anaweza fanya hivyo.
Labda umtumie kumchuna pesa zake ili lifilisike litie Akili.

Nasisitiza usikubali kuolewa na Mwanaume asiye na uwezo wa kuacha Urithi Kwa watoto atakaokupa. Utazaa mitoto itakayohangaika hapa Duniani mpaka ikome.

Lazima uchague mwanaume anayejua nyakati, na mazingira. Akiona mjini vitu bei ghali basi akanunue nje ya mji huko kijijini vilipo rahisi.
Sio limwanaume linalong'ang'ania kujenga mjini linakusanya pesa zisizojaa, mwisho linakosa bara na Pwani.

Usiolewe na Mwanaume anayejipenda kimwili kukushinda, yaani mtanashati kukushinda wengi uwezo wao wa kufikiri ni mdogo, wengi ni wabinafsi, utashindia kanga moja Kama Sanda ya maiti, vitoto vyako vitavaa marapurapu wala Baba Yao halitajali.
Wanaume watashanashati kupitiliza wanatabia ya aidha ubinafsi au ushoga Kati ya hizo tabia lazima moja umkute nayo.

Hujawahi ona limwanaume limependeza lakini mkewe na Watoto wamevaa hovyo?? Ndio matokeo ya kuolewa na wanaume wapumbavu.

Usiolewe na Mwanaume Mlafi, na mwenye kujipenda mwenyewe. Huyo hawezi kujitoa kafara Kwa ajili ya Familia. Huyu anaweza kuwalisha Dagaa wa chukuchuku wewe na watoto lakini lenyewe linakunywa Bia na supu huko nje. Haya unayakuta yamenenepa na kukuza vitambi alafu wake zao dhoofu ilhali.


Usilivumilie! Likimbie! Hata Kama halijakufukuza ndani ya ndoa liache hapo, usiishi na Mwanaume Mpumbavu ndani ya nyumba.

Mara nyingi nawasema wanawake wapumbavu kuwa tusiwavumilie lakini leo nasi wasituvumilie.

Wewe jitu likulishe Dagaa miezi nenda Rudi aalafu lenyewe linakula nje na kunenepeana bado unalichekea.
Hakuna kulirekebisha, hiyo sio kazi yako, Kama halikurekebishwa na wazazi wake huko basi liende kanisani au msikitini huko ndio wanalipwa zaka na Sadaka Kwa kazi za namna hiyo. Hakuna kuchekeana na wapumbavu.

Mwanaume atakayekupiga bila sababu zile kubwa kubwa Kama kukutwa unataka ku-cheat, au ukiwa una-cheat, au mwanamke mwenyewe kutaka kupigwa maana wapo wanawake wanakuwaga wanawashwa washwa.

Lakini jitu limekukosea unaliambia Kwa adabu alafu linakupandia na kukupiga. Usilichekee. Piga chini. Usicheke na Mwanaume Mpumbavu.
Yaani lije limechelewa nyumbani, linanuka pombe, linatukana hovyo hovyo, ukiliuliza imekuwaje linajibu kipumbavu "hapa ni kwangu" na majibu ya mengine ya hovyo. Kisha likakojoe huko chooni au kutapika hovyo hovyo, bado likupige, loooh! Hakika ukiishi na Mwanaume WA hivyo nawe ni Mpumbavu tuu.

Kupenda upumbavu ni Dalili ya kichaa.

Mimi huwaga nawaambia Dada zangu na pia nitawausia binti zangu hayo wasiyachekee. Wasicheke na Kima, mwanaume Mpumbavu hachekewi muwashie Moto mpaka aone dunia chungu. Usimuhofie, akizingua mlete kwetu tumnyooshe kisheria.

Ewe binti usiyaogope maisha ikiwa unamikono na miguu na akili timamu. Ni Bora uishi mwenyewe kuliko kuishi na Lofa na lipumbavu likakuchosha mwili na Akili.

Mtu Kama hakuheshimu wa nini?
Mtu Kama hajiheshimu Kwa nini umheshimu?
Mwanaume sio Mungu, Ila ni mungu mdogo endapo atafanya wajibu wake Kwa hekima na akili.

Usitishwe na Motherboard yake Kama ndani yake ni Mwanamke.

Binti zangu, msitishwe na wanaume wapumbavu wasiojielewa. Bali Tishweni na wanaume wema, wenye akili na hekima, wanaojiheshimu na kuwaheshimu, wanaomheshimu Mungu. Hao wakiwaoeni hao watiini na kuwasujudia ikibidi Kwa maana HAO ni Kama mungu kwenu.

Lakini hawa Mbuzi wasiojielewe msipoteze muda nao. Msiwakawize, wawashieni moto mpaka waelewe.

Kama nilivyowaandikia na Kuwafunza ndivyo mtakavyofanya.

Mimi Baba Yenu,

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa, MBEZI BEACH, DAR ES SALAAM
 
USIOLEWE NA MWANAUME MPUMBAVU NA MWOGA!

Kwa Mkono wa RObert Heriel.

Leo nitakaanga wapumbavu wote na waoga bila kupepesa. Iwe ni Mimi mwenyewe, wewe au Yule. Andiko hili halitamkwepa mwanaume yeyote Mpumbavu na mwoga bila kujali nafasi yake, hadhi yake, na umri wake.
Braza hongera sana kwa fasihi kumbushi na fundishi sana, nadhani viewers watakuwa wengi kuliko wachangiaji ila usijali watu kama wewe tupo tunajiita "progress enthusiasts" and "liberals". Hii dawa ni kali but no way out lazime tuitumie ili tupone. Mambo ya uhuru na kusonga mbele ni mazuri sana!
 
Braza hongera sana kwa fasihi kumbushi na fundishi sana, nadhani viewers watakuwa wengi kuliko wachangiaji ila usijali watu kama wewe tupo tunajiita "progress enthusiasts" and "liberals". Hii dawa ni kali but no way out lazime tuitumie ili tupone. Mambo ya uhuru na kusonga mbele ni mazuri sana!


Nashukuru Sana Shemeji
 
Pale inapotokea kupendwa na mpenzi wako na akakupa mahaba na kusahau yote sasa ole akusaliti na akupe maumivu yale ambayo hata dawa yake haijagunduliwa we eee asikwambie mtu utaimba bia taam na kuja kuedit ulichooandika na kutafuta gunia la mkaa maisha hayaa

Ila ubarikiwe alie juu tunakungojachini
SGN_11_26_2021_1637934876563.jpg
 
USIOLEWE NA MWANAUME MPUMBAVU NA MWOGA!

Kwa Mkono wa RObert Heriel.

Leo nitakaanga wapumbavu wote na waoga bila kupepesa. Iwe ni Mimi mwenyewe, wewe au Yule. Andiko hili halitamkwepa mwanaume yeyote Mpumbavu na mwoga bila kujali nafasi yake, hadhi yake, na umri wake.

Kwa Sasa, MBEZI BEACH, DAR ES SALAAM
Mkuuu ,Naomba kwanza nikukosoe .Uzi wako ni nzuri Mno Ila kuna Mambo matatu umeshindwa kuyatambua 1.Binadamu anabadilika kulingana na mazingira ( Human being is dynamic not sysmatic)) 2.mwanaume yeyote ili awe na Maisha yaliyonyooka Kwa asilimia Mia ni lazima awe na mke na watoto ( familia Kwa ujumla ) 3.hakuna binadamu anaependa Kuishi Maisha ya kipumbavu ila hii ni dunia tunaishi katika mazingira yafuatayo a.folish age b.umaskini ndani ya familia c.ukosefu WA elimu ( fikra na maradhi ) na mwisho Ni elimu dunia kututawala....NI mtazamo wangu
 
Back
Top Bottom