Tuacheni Kujipa Moyo, Ndoa kwa Kizazi cha Sasa ni Gereza la Mateso

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,900
TUACHE KUJIPA MOYO, NDOA KWA KIZAZI CHA SASA NI GEREZA LA MATESO.

Anaandika, Robert Heriel
Kuhani!

Soma Kwa Utulivu;
Linatesa Wanawake
Linatesa wanaume;
Lakini Kwa nini?
Ili ndoa iwe ndoa kweli sharti ifuate mfumo wa kizamani, hilo nimeshalieleza kila mara. Kwa sababu ndoa misingi yake imejengwa kizamani. Misingi hiyo ndio inaifanya ndoa iwe ya muhimu na lazima.

Kam utakuwa ukinifuatilia Kwa umakini Kwa Akili bila kuonyesha mihemko utagundua kuwa Taikon ninamawazo ya kizamani, na ninatumia mifumo mingi ya kizamani.

Wengi wa wanausasa huniona kama kijana mwenye mitazamo ya mfumo dume, mchukia Wanawake, mkatili na mwenye mambo ya kikoloni.

MTU yeyote anayetumia mifumo ya kizamani Ndoa haiwezi kumsumbua, matatizo sijui ya nguvu za kiume hayawezi kumpata, Kwa sababu mifumo ya kizamani inasuluhu ya mambo ya sasa.

Ndoa Kwa vile ni mfumo wa kizamani umejengwa katika misingi Mikuu ifuatayo;

1. Ndoa lazima ifuate muundo huu wa Familia (Family Structure)
a)Baba ndiye Mtawala.
Kiongozi, msemaji wa mwisho, mtafutaji, mtunzaji na mlindaji wa Familia.
Baba anauwezo wa kuamua jambo lolote pasipo kuingiliwa.

b). Mama ndiye Msaidizi
Mlezi wa familia Kwa kupika, kuhakikisha usafi WA nyumba, kuwafundisha Watoto heshima na adabu, kufanya shughuli ndogondogo za uzalishaji ambazo hazitampunguzia wajibu wake Mkuu wa nyumbani kama Mama.

C) Watoto Kama matunda ya familia.
Watoto ni Mali ya Familia, hasahasa Mali ya Baba kwani Baba ndiye Mtawala, Mfalme na Kiongozi.
Watoto watafuata sheria zote za familia na ukoo bila kujali umri wao, hata wakiwa Watu wazima, watabaki kuwa Chini ya maamuzi ya Baba Yao.

Kama itatokea utengano baina ya Baba na Mama, Watoto watakuwa Mali ya Baba, na ukoo wa Baba. Hivyo ndivyo ilivyokuwa na ndio msingi wa Ndoa ulipo.

Ukiangalia msingi huu Kwa kizazi cha sasa umevunjwa, n automatically ndoa inapoteza nguvu kumaanisha inakosa umuhimu. Siku hizi Mtoto sio Mali ya Baba tena ni Mali ya Mama. Wanawake wanang'ang'aniza umiliki WA watoto, hata Baada ya kuachana.

Ieleweke kuwa Kiasili mtoto ni wababa lakini anayekulia katika tumbo la Mama.ndio maana Mama anaweza kuzaa Watoto wa asili nyingi tofauti tofauti kama vile Wahindi, wasukuma, Wachina kulingana na Baba zao lakini mwanaume Han uwezo wa kuzalisha mtoto Aina tofauti na asili yake, yaani kama Mwanaume ni Mpare basi Watoto atakaowazaa automatically watakuwa Wapare. Hata angezaa na Wanawake WA mataifa yote Duniani.

2. Wajibu na Majukumu
Huu ni msingi WA pili Baada ya muundo wa Familia. Mgawanyo wa majukumu katika familia haukuwekwa Kwa bahati Mbaya. Uliwekwa na watu wazima wenye Akili zao. Mgawanyo huo ulizingatia mambo Makuu yafuatayo;

i. Hulka, Akili na Maumbile ya Binadamu.
Mwanamke anahulka,Akili na maumbile yake na Mwanaume anahulka, akili na maumbile yake.
Majukumu ya Mwanamke na Mwanaume hayawezi kuwa Sawa Kwa sababu wanatofautiana katika tabia, Akili na maumbile Yao.

Sisi wanaume kimaumbile tuna misuli yenye nguvu ndio maana kazi za nguvu zinatuhitaji lakini Wanawake maumbile Yao ni nyoronyoro na nyororo hivyo kazi za nguvu sio Haki kwao kuzifanya, ingawaje wapo wanaojilazimisha lakini matokeo yake tunayaona wanapoteza Ile asili Y utukufu wao wa kike.

Mwanaume akifanya kazi za nguvu atazidi kuvutia na utukufu wa uanaume wake utazidi kushamiri.
Lakini Kwa Mwanamke atadhoofika na itakuwa kumuonea tuu.

Akili ya mwanaume Imeumbwa kufikiri na kukabiliana na mambo makubwa na mazito. Huku Akili ya Mwanamke Imeumbwa kufikiri na kukabiliana na mambo madogomadogo na Mwepesi.

Wanawake wako Very Sharp kuwaza na kukimbizana na mambo madogo madogo hata yawe Kumi na moja Kwa wakati mmoja. Lakini Jambo zito moja kubwa Kwa kweli wasingependa kulikabili.

Hata hivyo Kwa Sisi wanaume Akili zetu hazipo sharp kukimbizana na mambo madogo madogo Kwa wakati mmoja Ila tupo vizuri katika Jambo zito moja kubwa kulikabili.

Hii ni kusema, Chemistry hiii ndani ya familia ikitumiwa vizuri ndio huzalisha Maendeleo. Ukiwa na Mkeo ndio mnaanza Maisha ni rahisi kufanikiwa hasa ukimfuatisha katika mambo madogo madogo alafu naye akikufuatisha Kwa mambo makubwa makubwa. Ni ngumu Sana kuingia hasara ikiwa mtakubaliana katika tofauti zenu za Kiakili.

Bado hujamuelewa Taikon? Subiri utanielewa. Wakati Mwanamke anawaza kununua Jiko la Gesi, sahani za udongo, mapazia mazuri, n.k. Kwa mwanaume mambo hayo anaweza kuyapuuza asinunue Kwa sababu yeye anafikiri mambo makubwa kubwa kama kununua Gari, kiwanja, au kujenga nyumba.

Msipokuwa Makini katika utofauti wenu wa Kiakili mnaweza kujikuta mkipiga mark-time pasipokufanya Jambo zuri lolotendani ya Nyumbani.

Taikon ninashauri, Kwanza jueni ninyi ni mwili mmoja lakini mna hulka, Akili na maumbile tofauti, hivyo timizeni mambo ya familia Kwa utofauti wenu bila kuathiriana. Wekeni vikao na mijadala kisha muweke mipango na malengo yenu.

Mfano, Ndio mmeanza Maisha. Hamna kitu chochote. Mwanaume elewa kuwa Mkeo Akili yake na tamaa yake zinapishana, ni kweli anatamaa na vitu vikubwa kama umiliki WA nyumba na magari lakini Akili yake Kwa muda huo itawaza vitu vidogo vidogo.

Elewa kuwa Mwanamke ofisi yake ya Kwanza ni hapo nyumbani Wakati kwako mwanaume nyumbani ni sehemu ya mapumziko tuu. Hiyo pekee inatosha kukuambia upo utofauti.

Ikiwa Kwa Mkeo nyumbani ni Ofisini, basi hakikisha zana na vyombo vyote vya kazi zake vipo, na hapa nazungumzia vyombo vya Kisasa vitakavyomrahisishia kazi na majukumu yake.

Ni mateso makubwa kuoa Mwanamke na kumuweka nyumbani pasipo kuyatengeneza mazingira ya ofisi yake kuwa mazuri.

Unajua Mwanamke anapenda kupika kwaajili yako, mnunulie Majiko mazuri, vifaa ya Upishi kama Brenda, Mashine ya kufulia, pasi, Fridge, N.k.

Unajua kabisa Mkeo kuna muda atahitaji kupumzika hivyo lazima umuwekee Luninga, Sabufa, Feni au AC, muwekee vitabu vya simulizi ajisomee, Unga bando la ving'amuzi Mkeo ajisikie Raha, Nunua makochi au masofa mazuri na kitanda, Zulia na mito. Ili akichoka apumzike akikusubiri.

Kwa sababu ili mwanaume apumzike vizuri akirudi nyumbani sharti Mwanamke awe amepumzika vyema.

Sio mwanaume mzima unafungia TV na Deki ndani ATI ili Mkeo asiangalie, Huo ni uchizi, na wewe ni Mwendawazimu, na nitashangaa Mwanamke akikubali kuishi na kichwamaji.

Tabia ya Mwanamke na Mwanaume zinapishana Kwa kiwango kikubwa. Kupishana Huko ndiko kunafanya majukumu na wajibu kutofautiana.

Hakunaga usawa WA kiwajibu na kimajukumu baina ya MKE na Mume. Hiyo haipo. Ukitaka kuharibu familia yako basi weka huo usawa.

Nakupa Mfano, ni Hulk ya Mwanamke kutaka kupendwa, Wakati ni hulka ya mwanaume kutaka kuheshimiwa.
Ni hulka ya Mwanamke kutaka kusifiwa, Wakati Kwa mwanaume ni hulka yake kutaka kutukuzwa.

Mfano, umerudi nyumbani umemkuta Mkeo kajiliza, Mchana kutwa alikuwa akijishughulisha na kazi ya usafi na Kupanga nyumba.

Hata kama umechoka vipi ni jukumu lako kumsifia Kwa kazi nzito na nzuri aliyoifanya Mkeo. Utaangaza macho Kwa kustaajabu, ukiangalia huku na huku katika nyumba kisha utamtazama Mkeo na kumwambia;

Hakika hapa nimeoa Mwanamke, pamependeza mno, yaani pakitoka Mbinguni Kwa uzuri basi panafuata hapa nyumbani kwetu. Kisha unamfuata unamsiriba mabusu yakutosha.

Usijesema Taikon ni mchawi jinsi mambo yenu yatakavyowaendea vizuri. Ni vitu rahisi vinavyojulikana Sana Ila vilivyopuuzwa na Wengi.

Lakini wewe umerudi, ni kweli umetoka kazini, ni kweli umechoka, sasa unataka uonewe huruma za kijinga kama litoto lijinga, au uambiwe Pole, pole ya nini.

Mwanaume hautakiwi kutafuta pole za ajabuajabu. Usilazimishe mapenzi, pole ni sehemu ya kujali, kujali ni sehemu ya mapenzi, mapenzi yapo kwaajili ya Wanawake.

Mwanaume unatakiwa utoe Kwanza mapenzi ili urudishiwe kibaba cha heshima na mahaba.

Msingi huu umevunjwa katika Zama za Leo. Wanawake wanatafuta heshima badala ya kupendwa. Huku wanaume wanatafuta kupendwa badala ya kuheshimiwa.

Hapo automatically ndoa haina umuhimu wowote Kwa minajili hiyo. Kwani itageuka uwanja WA mateso makubwa.

Unataka ule hela za Mkeo alafu unategemea Mkeo akuheshimu? Unataka Mkeo atunze familia alafu unategemea heshima hapo? Taikon nazungumzia Uhalisia hapa.

Njia nzuri ya Kula hela za Mkeo au Wanawake ni kuwapenda, Full-stop. Na kuwapenda ni gharama zaidi ya Pesa watakazokupa😂😂 ingawaje Kwa MTU mwenye True love hatoona kazi.

Elewa kuwa Mwanamke anachotafuta Kwa mwanaume ni upendo tuu. Hivyo ni jukumu la mwanaume kuhakikisha anaiteka Imani na Akili ya Mwanamke Ione upendo wake(mwanaume).

Hata hivyo weka Akili kuwa Mwanamke kama hakupendi ni hakupendi tuu! Pia elewa kuwa Wanawake pia wanatamaa za miili Kam walivyowanaume hivyo anaweza kukukubalia Kwa sababu ya tamaa yake lakini hiyo tamaa ikiisha utaonja joto la jiwe.

Ili Mkeo au Mwanamke yoyote akuheshimu na kukurejeshea mahaba lazima uwe Mwanaume kweli. Usimamie misingi ya kiume.

ii) Mwenye Umiliki.
Mwenye Umiliki ndiye anatakiwa kuwajibika zaidi kuliko asiyemiliki. Hiyo ni kanuni ya Asili. Kwenye Ndoa au familia, mwanaume ndiye mmiliki wa Mke, Watoto na mali.

Hivyo yeye majukumu yake lazima yawe makubwa kuliko Mwanamke. Wanawake wote Duniani wanajua kuwa wakiolewa wanaenda kumilikiwa au kuwa Chini ya umiliki WA mwanaume. Kwao huo ni ufahari hasa wakimilikiwa na wanaume wanaowapenda.

Wajibu wa Mwanamke Kwa mwanaume ni mdogo Sana ukilinganisha na wajibu wa mwanaume Kwa Mwanamke.

Ni sharti mwanaume umvalishe Mkeo, umlishe, akiumwa umpeleke hospitali, Watoto halikadhalika.
Ila sio wajibu wa mwanamke kukufanyia hayo. Umiliki ndio Sababu kuu ya Jambo Hilo.

Ndoa kama mfumo wa zamani umejengwa katika mfumo huo wa umiliki. Kizazi cha sasa kimevunja msingi huo ndio maana ndoa imegeuka mateso makubwa Kwa Zama za leo.

Wewe unataka kuoa au umeoa, alafu umvalishi Mkeo, humlishi chakula kizuri, Watoto wanahangaika, alafu bado unataka heshima Kwa Mkeo huoni hapo kuna tatizo Pande zote mbili.

Unamtesa Mkeo kimwili, Kiakili na kihisia Kwa kushindwa kummiliki Kwa sababu ni Haki ya Mwanamke kumilikiwa ili ajihisi kupendwa.

Na pia ni mateso kwako mwenyewe(mwanaume) Kwa kutokuheshimiwa kwani utaishi Maisha ya TAABU ukidhani unadharauliwa na Wanawake(including Mkeo)

Hauwahudumii Watoto, Watoto wanatunzwa na Mama Yao alafu unataka Haki ya umiliki Kwa hao Watoto, come on! Huko ni kutesana tuu.

Ni vizuri, kama kweli mmeamua kuoa na kuolewa mfuate mifumo ya kizamani ili kulinda furaha, Amani na Mustakabali wa familia na kizazi chenu.

3. Kuvurugika Kwa utamaduni
Sisi ni waafrika, kuanzia asili yetu, ngozi zetu, Akili zetu na hata bara tunaliishi ni Afrika. Tuna tamaduni zetu ambazo ndoa na familia zilikuwa na nguvu.

Ujio wa tamaduni za kigeni kupitia dini ya kiarabu(Uislam) na Dini za Wazungu( Ukristo) umezifanya ndoa zetu kuwa magereza ya mateso.

Hatuwezi kuendesha ndoa zetu Kwa mifumo ya kigeni na kuacha mifumo yetu ya Asili. Kadiri tunavyojiingiza kwenye mambo ya kigeni ndivyo kunavyoiangusha Taasisi ya Ndoa zetu za kiafrika.

Mfumo wetu wa kiafrika hatuambui kitu kiitwacho Single mother, wala pasingekuwa na single mother, lakini mfumo wa Kiafrika unatambua Mwanamke Mjane basi,

Sheria, miiko, Mila na desturi zilijengwa katika mifumo ya kuhakikisha kuwa mwanamke anaolewa Kwa namna yoyote Ile tena Kwa asilimia kubwa akiwa Bikra.

Mfumo wa Kiafrika hajitambui kitu kinachoitwa ushoga, na hakukuwepo na ushoga na kama ingetokea dalili yoyote ya ushoga basi kijana huyo angekula Chuma akafie Mbele.

Mfumo wa kizamani ni ngumu Sana mambo ya ushoga kutokea Kwa sababu majukumu ya mwanaume ni makubwa, kazi zake na Chakula chake anachokula hazimfanyi afikirie upuuzi upuuzi, lakini mfumo wa Kisasa WA kijana muda wote amekaa kaa tuu, anajiangalia kwenye Kioo siku nzima, anajipodoa kama Mwanamke unategemea nini kama sio kutaka Kufirwa Huko.

Lakini kuvurugika Kwa utamaduni imekuwa chanzo kikuu cha kuifanya ndoa kuwa uwanja wa mateso.
Ndio maana nikasema sehemu Fulani kuwa wenye Kampeni ya kukataa Ndoa wanazohoja za msingi tena kubwakubwa.

Kijana au Binti, Oa au Olewa na kijana au Binti anayefuata mifumo ya kizamani lakini mwenye Akili za kisasa alafu utakuja kunishukuru.

Taikon ngoja nipumzike, watakanielewa wanielewe. Watakaonipinga wanipinge. Tumalize zamu yetu, tuwaache wanaokuja.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Mimi nadhani ambao watataka kuingia ktk ndoa waowe wanawake form four & six au hata la saba coz hawa wanakuwa hawajakutana na zile pilika pilika za kuchangamana na wenzao vichwa vibovu huko mavyuoni pia hii itapunguza speed ya wao kuzidiwa kipato na wake zao hadi watake huruma ya kutunzwa au kusaidiwa maisha na mwanamke.

Wanawake wanaopita vyuoni huwa na experience kubwa sana ktk mahusiano,ile kuwa wameachiwa bora liende na wazazi wao ndani ya miaka 3 au minne wengine hujiingiza ktk mahusiano ya ndoa zile za chuoni fikiria amekaa miaka 2½ na mwanaume wakamaliza chuo ndoa ikafa then ndani ya hiyo ndoa haramu kukawa na matokeo mabaya kwake arudi mtaani akutane na kijana msamaria mwema asiyejua A wala B ktk ndoa huku kipato hana mke amemzidi kipato au kijana anawaza mke amsaidie maisha unadhani patakalika hapo?

Vijana badilikeni familia anaendesha mwanaume haijawahi kuandikwa popote kwamba mke amsaidie mwanaume kigezo cha kipato cha mwanamke siyo kigezo ktk kuanzisha familia owa asiyekuwa na elimu kubwa pambana wewe umpe shughuli ya kufanya.

NB;sijasema wenye elimu wasiolewe ila unaetaka kuowa mwenye elimu muwe mmeanza wote kabla au mkiwa wote huko vyuoni.
 
Robert nakuunga mkono.

Ni kweli NDOA za sasa naziita za New Age au 'NWO' ni majanga, misingi mikuu ya NDOA kwanza zimepitwa na wakati na hakuna wa kuipa promo ili isimamiwe.

Wachungaji wa kizazi kipya wanatumia majukwaa yao (mimbari/vimbweta) kujipatia umaarufu kwa clip za vichekesho, (foolish) ili kujipatia wafuasi, wenye NDOA nao wamemkimbia Muumba wao na kumuona hana jipya na No change in their life.


NDOA imekuwa gereza la mateso, kunyongea mmoja wa wanaNDOA na moja ya hatari ambayo hata mwenyezi Mungu kupitia mitume alisema ni kujikweza kwa mmoja wa wanaNdoa na kusahau majukumu yake muhimu na kutaka kuchukua majukumu yasiyo yake.

Siipingi NDOA ila ni kutokana na mienendo ya binadamu, nowadays wanakimbilia adhabu kabla ya tukio linalopelekea kupewa adhabu.
 
Shida inaanzia pale kuoa mwanamke msomi

Katika wanawake wasomi 100 wenda angalau akapatikana wife material 1 na ni bahati kwelikweli (most of them are naturally feminist)

Pili kuoa mwanamke ambae ana kazi hasa kuajiriwa, kidogo angalau awe anafanya biashara ambayo umemuanzishia mwenyewe japo nayo inaweza kuwa sumu pia huko mbeleni itategemea

Kingine kama ulichokisema wanaume wapumbavu nao kuwa na tamaa na vitu vya wanawake


Mimi msimamo wangu ndoa hata kwasasa bado ni muhimu ila ni kwa wanaume wenye akili tu.
 
Back
Top Bottom