Ushauri: Nataka kutumia mchango wa harusi kujenga nyumba

vanmedy

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
2,579
2,000
Kwa nongwa za wajumbe, ukifanya huo mchakato halafu ikatokea mbeleni huko (MUNGU AEPUSHE HILI) kwamba umepata labda changamoto za kiafya zinazohitaji tafu utajikuta "ulilichuma janga na wakati huo utastahili kula na wa kwenu"
 

SeliSelina

JF-Expert Member
Jun 27, 2014
252
1,000
wewe husemi kweli kabisaa, at least ungesema umepata michango ya harusi milioni 20, ingeingia akilini. lakini milioni 42 unatudanganya tuu hapa na kutupotezea muda.

lakini kwa nini watu ukiwaambia nichangie nijenge wanakuwa wagumu sana, lakini ukiwaambia nichangieni nifanye sherehe inakuwa sio ngumu? nalo neno hilo.

akili zetu zimedumaa kwa mambo yasiyo na tija na kuleta maendeleo.

mfano,
ndugu anaumwa tatizo sio kubwa sana lakini kuchangiwa akatibiwa mtu hawezi kuuza kishamba chake ili amtibu ndugu yake, lakini tatizo likiwa kubwa na ishara ya kuwa haponi tena au kufa watu wanaanza kutapatapa huku na kule, michango ya mazishi hutolewa hapa na ghrama kubwa tuu, ambazo zingeweza kumsaidia kutibiwa wakati alipokuwa hai.

au

Mtoto wa ndugu anahitaji hela ili aendelee na masomo hatutaki kumchangia kabisaa, ikiwa wakike akizurura mitaani kuhangaika huenda akapata mimba ohoooo kelele nyingi sana kwa mama mzazi wa mtoto na mtoto mwenyewe, au kama wa kiume akija kuharibikiwa wakati alikufuata umsaidie au unamuona ana akili sana lakini mazingira anayokaa ni mibaya sana na una uwezo wa kumtoa pale na kumpeleka boarding school ili apate elimu zaidi na utulivu wa akili, hutaki kumsaidia unaona hela yako itapungua kwa kumsaidia yeye huwezi kumpa kabisaa kwa roho mbaya tuu.

Hayo yawe kwenye familia au nje ya familia, kusaidiana kuleta maendeleo zaidi tupo wagumu sana. Mfano mwengine unakaa katika mtaa watu wanahangaika kutafuta maji, wewe una uwezo wa kujenga kusima ili watu wapate maji, hutaki kutoa hela, utadhani hilo hila utazikwa nazo ukifa zoote au unasahau kuwa yule alokupa alikwambia pia uwe unatoa, ila wewe unajitoa fahamu kabisa.
ni mengi tuu
 

ommytk

JF-Expert Member
Jul 30, 2015
247
500
wewe husemi kweli kabisaa, at least ungesema umepata michango ya harusi milioni 20, ingeingia akilini. lakini milioni 42 unatudanganya tuu hapa na kutupotezea muda
Natamani nikutumie mkeka uone hapa nawaza kikwazo mweka hazina tu.

Ukiwa unachangia watu nawewe una gangues mkuu mimi hapo kimenibust hela nyingi marafiki ofisi mbali mbali nilizofanya kazi na pesa Za vyama vya urafiki na marafiki pia toka nje nchi
 

Imalamawazo

Senior Member
Jul 27, 2021
120
250
Jenga nyumba lakini waambie ukweli, atakaye kudai mwambie akupe muda umrudishie mchango wake. Usisingizie korona inaweza kupita nawe kikweli kweli
 

kitali

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
1,477
2,000
Wadau ebu naomba ushauri wenu nitarajia kuchukua jiko sasa michango imefika 42 millin na point kadhaa na watu bado wanatoa

Imenijia wazo hizi hela nifanye jambo lingine nina kiwanja Bunju nikajenge nyumba fasta ya japo 35m nipate kustirika kikao cha mwisho sitokei natuma mjumbe mjomba akaaawambie wajumbe kuwa corona hakuna mikusanyiko naoa kimya kimya na watu wachache tu

Naomba ushauri
ucthubutu mkuu. kuna jamaa alifanya hvyo pale kkoo. amefiwa na mwanae juz kati kajikuta yeyd na mkewe tu. usichezee hisia za watu mkuu. hela zipo tu na utajenga. ningeweza kukushaur cheza na mhazin mbane kidogo bajet angalau zibak kidogo.
 

cariha

JF-Expert Member
Apr 9, 2015
18,043
2,000
wazo zuli Sana Mkuu, japo tegemea upinzani Kwa wana kamati lkn pambana. Ni ulemavu wa akili kufanya harusi ya M5. wakati wanandoa wanaenda kupanga tena Kwa Maisha ya kuunga unga
Nakuunga mkono ndoaa zenyewe hizi zinavunjik kilaa siku sometime Ili utoke kimaisha lazima uwe na maamuzi magumu we kajengee tu half trehe ya kikao unaenda lazwa muhimbili corona
Acheni mawazo ya kimaskini angekuwa hataki ndoa asingechukua michango au angetengeneza kadi za kuomba mchango wa ujenzi
 

luckyline

JF-Expert Member
Aug 29, 2014
12,464
2,000
Unasubiri nini sasa? Wewe jenga fasta tunza mil 15. Siku ikifika nenda kaode mavyakula na pombe waambie bi harusi alihairisha ndoa wakati ushalipia vitu imekubidi uwafurahishe kwa hicho kidogo. Usiruhusu maswali mengi sana. Hakuna atakae kupeleka police maana vyakula vitakuwepo wavile waondoke.
 

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
9,753
2,000
Wadau ebu naomba ushauri wenu nitarajia kuchukua jiko sasa michango imefika 42 millin na point kadhaa na watu bado wanatoa

Imenijia wazo hizi hela nifanye jambo lingine nina kiwanja Bunju nikajenge nyumba fasta ya japo 35m nipate kustirika kikao cha mwisho sitokei natuma mjumbe mjomba akaaawambie wajumbe kuwa corona hakuna mikusanyiko naoa kimya kimya na watu wachache tu

Naomba ushauri
Ukitaka kuitwa tapeli la mjini kula hiyo hela yangu!
Mimi nimkuchangia ili niserebuke aafu wewe unataka kuila!
Kula alafu fiwa na mtu wako wa karibu haafu ita mchango tena, utazika mwenyewe.
 

chapwa24

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
1,115
2,000
Ukitaka kuitwa tapeli la mjini kula hiyo hela yangu!
Mimi nimkuchangia ili niserebuke aafu wewe unataka kuila!
Kula alafu fiwa na mtu wako wa karibu haafu ita mchango tena, utazika mwenyewe.
mzee walevi wameshaanza kukurukia, kuwa makini. nilikwambia jenga nyumba wenye akili watakuelewa, alfu hamsini kwa mtu aliyeamua kuachana na kupanga nyumba ajenge yake unaweza samehe. ila walevi kama huyu patachimbika, jiandae.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom