Cannabis

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
8,943
25,284


Baada ya kipande cha video kinachowaonesha watoto wa shule za msingi wakicheza wimbo wa msanii Zuchu ‘Honey’ wilayani Tunduma kusambaa mitandaoni, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda ameagiza walimu wakuu wawili wa shule hizo wavuliwe vyeo.

Amesema hayo nje ya Bunge jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu video hiyo ambapo pia amepiga marufuku wanafunzi kucheza nyimbo zisizo na maadili na kuwataka walimu kuwa wasimamizi wa maadili pindi wanafunzi wawapo shuleni.

“Tumeshatambua shule yenyewe iko Tunduma, kulikuwa na kikundi kimeenda kutoa msaada shuleni pale, baada ya kutoa msaada ule kikaweka na muziki halafu wanafunzi wakacheza, na maudhui ya muziki wenyewe kila mtu ameusikia sina haja ya kuurudia,” amesema Profesa Mkenda.

Ameongeza, “tumeongea na wadhibiti ubora wapeleke taarifa kule, mkurugenzi awaondoe walimu wakuu wa shule mbili; moja shule ya Tunduma na nyingine ambazo ni kama shule pacha, waondolewe madaraka ya ukuu wa shule watafutwe wakuu wengine wa shule. Tunafanya hivi ili kutuma ujumbe, walimu wakuu tusaidieni msiruhusu vitu kama hivi viingie mashuleni.”

Kwa upande wake Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima amempongeza Profesa Mkenda kwa kukemea kitendo hicho na kutoa wito kwa watoa huduma wote na wanaohudumia watoto kusimamia malezi na makuzi ya watoto.
 
Chadema walikuwepo Tunduma

EhdtAtyXgAEcFv6.jpg
 
Leo nimeona video ya wimbo wa Whozu ft Billnass na Mbosso unaitwa Umeyatimba,
Kipande anachoimba Mbosso kuna sehemu anasema "Nyoooo na Nyokoooo", pia ile video inaonesha anambaka Mwanamke chumbani huku Wanaume wapo sitting room wanashangilia, anampaka hadi mafuta ya nazi....

Nimeshindwa kuelewa mamlaka husika hawajaona haya lakini na hawa wasanii kwanini wanafanya hivi, lengo lao hasa ni nini kutoa nyimbo za namna hii huku wakijua wahanga wakubwa ni watoto na vijana wadogo!??
 
Mmh najaribu kutafakari na kuona kosa la walimu mpaka kuvuliwa nyadhifa zao sioni.

Tujiulize haya!

1.Je kosa ni kurekodiwa na kuwekwa katika social media au

2. Mziki kupigwa maeneo ya shule na watoto kucheza.

3. Je ingekuwa siku ya mahafali ya Darasa la saba na wimbo huo ukapigwa na wanafunzi wakaucheza je mwalimu angevuliwa nyadhifa yake?

Kiukweli tunakemea mmomonyoko wa maadili katika jamii yetu lakini mpaka wimbo umepita basata walichuja wapi na kuona utatumika kwaajili ya wakubwa tu na watoto hawata sikiza wimbo huo?

Watoto wanavyoimba inaonesha wanaujua wimbo tangu awali, this means kwamba kwa siku hiyo tu mwalimu mkuu hajasababisha mmomonyoko wa maadili kwa wanafunzi.

Kumvua cheo mwalimu mkuu ni Kuiambia BASATA kuwa walikosea kuruhusu wimbo huo.
Kwa maoni yangu mwalimu mkuu hana makosa ya kumvua cheo chake.

Yani Kiukweli mawaziri hukurupuka sana katika maamuzi, sijui ni poor kantiri ndo maana na mindset zetu zipo kama hali yetu ya uchumi.

Honeeey.
 
Mimi kama mwalimu mzoefu nachelea kusema kuwa waziri kakurupuka,shuleni sio mahali pa kujifunza ya darasani tu,kuna extra curriculum ambayo inajumlisha mambo hayo,huo wimbo wa kawaida sana,wasitake kutufanya walimu tuishi kama panya mashinoni

Kama wazirianaona hii comment imemkela na mimi anifukuze kazi,niko shule ya msingi mpigamiti wilaya ya liwale
 
Kwa kweli watoto wadogo tena wengine hata chekechea hawajaanza huimba nyimbo za wasanii zinazo trend. Basata walizembea kuacha kuupiga ban wimbo huo uliojaa mapenzi waziwazi. Kingine ni hao show maker wanapoenda kutoa misaada mashuleni wawe wanachagua nyimbo za heshima zisizochochea mapenzi waziwazi wala kutukuza ulevi na uhuni
 
Mimi kama mwalimu mzoefu nachelea kusema kuwa waziri kakurupuka,shuleni sio mahali pa kujifunza ya darasani tu,kuna extra curriculum ambayo inajumlisha mambo hayo,huo wimbo wa kawaida sana,wasitake kutufanya walimu tuishi kama panya mashinoni


Kama wazirianaona hii comment imemkela na mimi anifukuze kazi,niko shule ya msingi mpigamiti wilaya ya liwale
Sawa kabisa. Ila kabla hajakufukuza awatafute waliotoa jina la hiyo shule unayofundisha na awape adhabu kwa kosa la kutumia jina hilo kwa vile linatia kichefuchefu kwa sisi wazazi.
 
Back
Top Bottom