BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,376
- 8,120
Walimu wawili wakuu wa Shule za Msingi Mlimani na Tunduma TC zilizopo Halmashauri ya Mji Tunduma Mkoani Songwe ambao walivuliwa vyeo kutokana na video iliyosambaa mitandaoni ikionesha Wanafunzi wakicheza wimbo wa Msanii Zuchu wa Honey, wamerejeshwa kwenye nafasi zao.
Akiongea na @AyoTV_ kwa njia ya simu leo Jumanne November 07, 2023, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji Tunduma, Philemon Magesa amethibitisha kuwa Walimu hao wamerejeshwa “Ni kweli taarifa hizo ni sahihi Walimu hao wamerejeshwa vyeo vyao"
Alipoulizwa sababu za kurejeshwa vyeo Walimu hao, Mkurugenzi huyo amesema “Walimu hao walivuliwa vyeo kutokana na maelekezo ya Waziri wa Elimu na wamerejeshwa kutokana na maelekezo wa Waziri wa Elimu"
Jana November 6, 2023 akiwa Bungeni, Spika wa Bunge laJamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt, Tulia Ackson aliishauri Serikali kuwarejesha kazini Walimu hao.