Spika Tulia: Walimu waliosimamishwa kisa "honey" warejeshwe

mtwa mkulu

JF-Expert Member
Sep 11, 2013
8,098
9,994

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson ameishauri Serikali kuwarejesha kazini Walimu wakuu wa Shule za Msingi zilizopo Tunduma Mkoani Songwe waliovuliwa vyeo baada ya kusambaa kwa video ikiwaonesha Wanafunzi wakicheza wimbo wa Msanii Zuchu uitwao ‘Honey’.

Spika amesema kama Walimu hao hawakuwepo Shuleni wakati wa tukio linatokea na Mamlaka ya nidhamu imechukua hatua kabla ya kuwasikiliza iwarejeshe kwenye nafasi zao na kama walikuwepo Mamlaka iendelee na utaratibu wake.

Hoja hiyo imeanza kwa kuibuliwa na Mbunge wa Viti Maalum, Husna Sekiboko aliyehoji kuhusu nyimbo zinazostahili kupigwa kwenye Taasisi za Elimu na hatua zinazopaswa kuchukuliwa na kuiomba Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kutoa mwongozo wa nyimbo gani zinastahili kupigwa na zipi hazistahili.

Akijibu hoja hiyo leo November 6 2023 , Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema nyimbo ambazo hazistahili kupigwa kwenye Taasisi za Elimu ni pamoja na zile zinazohamasisha ngono, ulevi au sigara aidha ameongeza kuwa sio kila kinachokubaliwa uraiani kinakubaliwa Shuleni na kama Wizara ina wajibu wa kusimamia suala hilo.

Pia soma Tunduma: Wakuu wa shule wavuliwa nyadhifa kisa wimbo wa Zuchu (Honey)
 
1.Walimu walionewa kwa hatua ile iliyochukuliwa.

2.Ila hiyo haiondoi ukweli kuwa miziki ya sasa ni ya hovyo sana kimaadili.

3.Mamlaka zije na agizo maalumu kuhusu miziki inayofaa kupigwa mashuleni, na Prof.Mkenda asibezwe kwa nia yake ya kulinda maadili.
 
Kuna wanafunzi wa sekondari wanacheza miziki kinyege nyege sana. Tukiwatongoza na kuwapiga miti mnatukamata na kutufunga. Kwanini ilhali wao ndo wanatupa mzuka wa kuwatongoza?
 
Kwenye mahafali upigwe wimbo was taifa, Tanzania, Tanzania nakupenda kwa moyo wote. Baada ya hapo waimbe za mchakamchaka na sherehe iishie hapo.Make kutoka Bongo flavor sioni wimbo wenye maadili.

Kwa upande wa nyimbo za kina Ney na Roma serikali inasema ni uchochezi!
 
Walimu waliokuwa wamesimamishwa kazi kutokana na wanafunzi wa shule yao kucheza nyimbo ya haniiii ya msanii wa miondoko ya bongo flava zuchu warudishwa kazini hii ni kutokana na spika wa bunge kusema warejeshwe kazini na kupewa fursa ya kuhojiwa maana nyimbo waliokuwa wanacheza na wanafunzi haijafungiwa na BASATA.
 
Walimu waliokuwa wamesimamishwa kazi kutokana na wanafunzi wa shule yao kucheza nyimbo ya haniiii ya msanii wa miondoko ya bongo flava zuchu warudishwa kazini hii ni kutokana na spika wa bunge kusema warejeshwe kazini na kupewa fursa ya kuhojiwa maana nyimbo waliokuwa wanacheza na wanafunzi haijafungiwa na basata
Ac ha Uongo hakuna mwalimu aliyesimamishwa kazi,.waliondolewa madaraka...ukuu wa Shule ! Jambo huna taarifa nalo Kwa Nini unakuwa na kimbelembele Cha kuanzisha Uzi!
 
Ac ha Uongo hakuna mwalimu aliyesimamishwa kazi,.waliondolewa madaraka...ukuu wa Shule ! Jambo huna taarifa nalo Kwa Nini unakuwa na kimbelembele Cha kuanzisha Uzi!
Binafsi nikahisi labda taarifa ya mwanzo sikuielewa.
 
Ac ha Uongo hakuna mwalimu aliyesimamishwa kazi,.waliondolewa madaraka...ukuu wa Shule ! Jambo huna taarifa nalo Kwa Nini unakuwa na kimbelembele Cha kuanzisha Uzi!
Hakusoma vizuri chanzo kilichompa habari hii au hajui kuna tofauti kati ya kuondolewa madaraka/kushushwa cheo na kufukuzwa/ kuondolewa kazini
 
Back
Top Bottom