Tundu Lissu: Mashtaka dhidi ya Freeman Mbowe ni mepesi kuliko pamba, awaponda Waendesha Mashtaka

Laki sita inaweza kutumika kama kianzio cha kufanikisha uovu na baada ya hapo malipo kamili, hivi hili wanasahau vipi hao waharifu!
 
, ....ameahidi kushinda kesi hiyo ya kutunga mapema asubuhi .
......huyo Lissu uko mbeleni asije kuona kesi hiyo kuishinda ni sawa na kuona uzi wa JF wenye replies nyingi kuliko views! Mumueleze mapema hatutaki mambo ya presha kupanda sisi.
 
Kumbe unaelewa anything can come out? Basi usiidharau kesi.
Sasa kama anything can come out regardless what they do hata wakisema ni kesi serious itabdili nini? Mtu yeyoye mwenye ABC za sheria akisoma ile hati ya mashataka ataona kabisa wanamshtaki ni vilaza ambao hawajui wanachokifanya. Nyumbu kama nyie mnashabikia tu bila kujua kilichomo!
 
Hajakimbia kesi maana siku zote alikuwa na kesi hapa nchini. Kilichomkimbiza ni maagizo ya yule kiongozi muovu kuwa auwawe.

kwahiyo aliagiza auawe baada ya kushindwa uchaguzi na kukimbilia belgium!!!
 
Kesi ya Mbowe ni wazi imeichanganya Chadema vibaya sana. Kila kona ya Chadema wanapigana vikumbo. Siyo mitandaoni wala siyo mtaa wa Ufipa. Nasikia baadhi ya viongozi kwa sasa hawasalimiani. Huko Jamhuri ya Twitter pia kunawaka moto, ni matusi juu kwa juu. Viongozi, mawakili na wafuasi wao wanajaribu kujiaminisha wakiwa mbele ya umma kuwa kesi ni nyepesi na wataishinda. Mara eti laki sita ni ndogo kwa kesi ya ugaidi, mara hili mara lile. Nani aliwaambia kipimo cha madhara ya ugaidi ni kiwango cha pesa kilichotumika? Viongozi na mawakili wanajua hii si hoja yenye maana yoyote mahakamani.Pamoja na kuwaadaa watu wao kuwa kesi ni nyepesi, wakiwa wenyewe wanashika vichwa kuhusu ugumu wa kesi hii kwa sababu wanatambua ushahidi iliyo nayo serikali si ushahidi wa kitoto. Ni ushahidi unaoweza kumlambisha Mbowe mvua ya miaka 30 jela. Hii ndiyo maana kila kiongozi wa CHADEMA sasa anampigia magoti Rais ili aondoe kesi mahakamani bila kujali kuwa katika utawala wa kisheria, Rais hawezi kuingilia uhuru wa mahakama. Mikakati yote sasa inaonekana imekauka kwa upande wa Chadema. Mnyika alidai atakuwa akitangaza kila mara mikakati mipya ya kushinikiza kuachiwa kwa Mbowe. Iko wapi Huko Jamhuri ya twitter moja ya mikakati ilikuwa eti tuache kupanda mabasi, tuache kula, tuache kunywa soda na bia, tuache kuweka vocha kwenye simu zetu ili serikali ikose kodi. Hii nayo imebuma. Hakuna kiongozi au Taasisi yeyote duniani inayozungumzia kesi hii. Chadema imeachwa yenyewe na Mbowe wao. Mbowe pia ameachwa mwenyewe na familia yake. Kuna mengi ya kujifunza.
Tuanze na kuachwa Mwenyewe huo ni uongo viongozi wote wapo kazini Mnyika kila siku yupo mahakamani na leo kamwakilisha kwenye mazishi ya mama mkwe wake Arumeru. Maombi yanaendelea kila siku mikoa yote makanisani na leo Dr. Shoo kanongesha watamwombea kwa Mwenyezi Mungu.

Mh. Lissu yupo kwenye viunga vya Marekani kufanya mazungumzo na wale wanaotoa hela kwenye bajeti tegemezi miako yote 60 ya uhuru, Vijana wameandaa kongamano mkoani Mara la KatibaMpya.

Ninyi mmechanganyikiwa mpaka mnaomba poo mabalozi wasiende mahakamani.
 
Huwa nikisikia comments kama hizi mara moja huwa nahitimisha kwamba mtoaji comments ameshikiwa akili na ni mburula. Yaani ni mtu ambaye hana kabisa uwezo wa kutumia akili yake yeye mwenyewe kutafakari na kufanya hitimisho lake kwenye issues mbalimbali. Watu wa namna hii huendeshwa tuu kwa kufuata mkumbo wa kile wanachoelezwa kukiamini. Why kwa sababu mtu yeyote mwenye akili timilifu, na siyo akili ya kuvumia barabara au kwenda kukojoa , na wala si chuki za kijinga za kiitikadi au upuuzi mwingine, anajua fika nini hasa kilimkuta Tundu Lissu. Pia anajua fika uwezo wa Lissu kwenye eneo lake la sheria na ni kwa jinsi gani washindani wake wanamuogopa sana wanapokuwa naye mahakamani, kiasi kwamba ilifikia mahala wakaona hatakaa wamshinde mahakamani badala yake watafute njia ya mkato ya kushughulika naye.....
Huyo USSR, hajawahi kuwa na akili, hajawahi kuchangia kitu chochote cha maana. Kungekuwa na jukwaa kwaajili ya watu wenye uwendawazimu, would be the right place for him. Here, he is misfit.
 
kwahiyo aliagiza auawe baada ya kushindwa uchaguzi na kukimbilia belgium!!!
Alishindwa uchaguzi? ingia tovuti ya tume hata kama wanathubutu kuweka matokeo. Alipoagiza auwawe huko Dodoma alikuwa kwenye uchaguzi gani?
 
..Sikubaliani na TL.

..Ni kesi ngumu sana kwasababu mahakama zetu ni mali ya CCM.
Nyie jamaa bwana wababaishaji sana. Si mlisema Magufuli aliiweka mahakama mfukoni na mkafurahia kifo chake.

Mkafurahia DPP Biswalo kuondolewa, mkafurahia Sabaya kufunguliwa mashtaka na kesi, sasa haya ya Mahakama kuwa mali ya CCM yametoka wapi? Hivi mnajitambua kweli nyie watu?
 
Makamu Mwenyekiti wa Chadema Tundu Lissu , amechambua mashitaka yaliyosomwa Mahakamani yanayomkabili Mwenyekiti wake Freeman Mbowe , huku akiyaita duni , mepesi na ya UONGO.

View attachment 1906115

Amedai ana uzoefu wa kutosha kwenye kesi za uzushi na uongo kama hii kutokana na kazi yake ya Uanasheria aliyoifanya kwa miaka mingi , ameahidi kushinda kesi hiyo ya kutunga mapema asubuhi .

Hebu msikilize mwenyewe ufaidi uhondo .
Mwambie arudi aje amtetee aache kufugwa kama kuku wa kizungu huko kwa mabwana zake.
 
Back
Top Bottom