Tundu Lissu: Kufuta kesi ya Mbowe sio kuingilia Uhuru wa Mahakama

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
Makamu Mwenyekiti wa chama cha CHADEMA nchini Tanzania Tundu Lissu anayeishi uhamishoni Ubelgiji ameeleza azma yake ya kurudi nchini Tanzania wakati wowote.

Lissu alisema hayo katika mahojiano maalum na VOA baada ya kukutana na rais wa Tanzania Samia suluhu mjini Brussels Jumanne.

Akizungumzia dai lake la kutaka kesi ya mwenyekiti wa chama cha Chadema Freeman Mbowe ifutwe, Lissu amesema jambo hilo sio kuingilia uhuru wa Mahakama na kwamba kesi hiyo “haina maslahi yoyote na afanye kama alivyofanya kuhusiana na kesi ya mashekhe wa Uamsho wa Zanzibar ambao walifutiwa mashitaka baada ya kukaa gerezani miaka 9 hakuna cha kuingilia mhimili wowote hapa”

Akisisitiza kwamba hajamwambia Rais aongee na Jaji bali mwendesha mashitaka ambaye ni mteule wa Rais na anafanya kazi kama sehemu ya utawala sio sehemu ya Mahakama.

Pia kiongozi huyo wa upinzani na mgombea Urais mwaka 2020 amemwambia Rais kuhusu suala la Serikali kutaka kuwafukuza kwa nguvu wananchi wa wilaya ya Ngorongoro kutoka eneo la mamlaka ya hifadhi kuwa ni jambo la hatari na linaweza kuchafua nchi na akasema Rais amemwambia amelizuia.

Lissu pia amegusia Uhuru wa vyama vya siasa kufanya kazi akisema amemweleza Rais Samia kuhusu zuio aliloliita haramu la vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara na maandamano na madai ya hitaji la katiba mpya nchini humo na mfumo mpya wa uchaguzi.

Itakumbukuwa mbunge huyo wa zamani na mgombea urais kwa tiketi ya Chadema mwaka 2020 alinusurika katika shambulizi baya la risasi na watu wasiojulikana mwaka 2017 na amemtaka rais ahakikishe anatendewa haki kwa mambo ambayo alinyimwa baada ya shambulizi hilo, mwaka 2019 alivuliwa ubunge na mpaka sasa gari yake iko mikononi mwa Polisi.

Akizungumzia kuhusu sakata la Spika wa bunge Dr.Tulia Ackson juu ya wabunge wa CHADEMA amemwambia Rais kwamba spika Ackson asiwafundishe CHADEMA namna ya kuendesha chama chao yeye anatakiwa afanyie kazi maamuzi ya chama kama wanavyompa taarifa na walishamwambia hao si wabunge wa CHADEMA na yeye kuwaambia mpaka mchakato ukamilike “hayo hayamhusu kabisa Spika huyo na hata kama haujakamilika hawa sio wanachama wa Chadema na kwa maana hiyo kama sio wanachama wa Chadema hawatakiwi kuwa bungeni hata kwa siku moja zaidi” alisisitiza Lissu.

Lissu amesema Rais Samia amewamwambia amemsikia na atayafanyia kazi hayo madai yake.

Lissu pia amesema kuna mazuri yananayofanywa na utawala wa Rais Samia, akisema hasa kurejesha uhusiano na mataifa ya nje na kurejesha mapambano dhidi ya Covid lakini angependa kuona mengi zaidi kama kubadilisha sheria na taratibu ambazo zimeumiza watu wengi nchini humo.

Lakini anasema kwa ujumla hali ya jumla imebadilika tangu aingie madarakani lakini hali hiyo peke haitoshi. Lakini atamuuunga mkono ikiwa atakubali kwamba nchi inahitaji uponyaji aiongoze kuiponya nchi hiyo aliongeza.

VOA Swahili
 
amsamehewe
Kwa muktadha wa swala la Mbowe lilivyo, Haitaji msamaha, na wala sio sahihi kutumia neno msamaha sababu hana kosa alilofanya ambalo yahitajika aombe au aombewe msamaha.
Akifanya Lisu ana akili, akifanya Zitto ccm B. Acheni unafiki Zitto amewatangulia na hammuwezi.
Jaribu kuzitafakari hizi kauli mbili, Na utaona mantiki ya swala la Mbowe.
---
“mwenzetu hayupo hapa kwa sababu ana changamoto za kisheria, itafutwe namna, ASAMEHEWE” - Zitto Kabwe

“kesi ya mwenyekiti Mbowe ni 'ubatili mtupu na ushahidi ni wa uongo' na hailisaidiu taifa kwa lolote, IONDOLEWE
- Tundu Lissu

#76
 
Ngoja tuone next step hayo yote aliyomwambia Samia yatachukua muda gani kufanyiwa kazi kama alivyoahidiwa.

Kwa wale wanaolazimisha alichokifanya Lissu ndio alifanya Zitto waache kupoteza muda, Zitto alikwenda pale kama sehemu ya serikali hii ya CCM, asingeweza kusema yote kwa uwazi bila kupepesa macho kama alivyofanya Lissu, alikuwa na uso wa uoga na kujipendekeza, more over Mbowe haitaji msamaha, anahitaji kuwa huru bila masharti yoyote
 
Wanasiasa wenye akili kama za lissu wamekuwa adimu sana siku hizi, wengi ni wachumia tumbo wasioweza kujenga hoja
Kwani zito hakusema hayo?

Mbona hujampongeza na kupa hiyo hadhi wakatu Tundu ka cooy kwa zito?
 
Kama kuna kitu kinasikitisha kama mtanzania/mtanganyika ni hii hali ya kuacha hii "brain" ya Lissu ipotelee hewani badala ya kutumika kuijenga nchi yetu. Watu aina ya Lissu wanazaliwa mara chache sana. Hii ni "asset" kwa nchi.

Angekuwa kwenye nchi za wenzetu zisizo na ubaguzi wa kijinga wa kiitikadi zingemtumia vizuri pamoja na kuwa na itikadi tofauti na watawala. Ndio maana kila siku huwa napingana na watu wanaomsema vibaya spika wa zamani mama Makinda kwa sababu licha ya mapungufu yake kidogo kama spika lakini alikuwa anatumia watu wenye akili kutanzua mambo tata bungeni.

Makinda alikuwa anawatumia akili za akina Lisu, Chenge (pamoja na makando kando yake), na wengineo. Sasa hivi kukiwa na mambo tata bungeni watu wanotumika kutatua naona hata aibu kuwataja hapa.
 
.....Kuhusu suala la wabunge 19 sikubaliani na mtizamo wa Lissu

Ni mpaka pale uamuzi wa rufaa yao huko kwenye chama utakapohitimishwa

Wabunge 19 wa CHADEMA bado ni wabunge halali.. CHADEMA iache kutumia mabavu itumie haki na demokrasia. Lakini pia CHADEMA haiwezi kuwa mwamuzi wa mwisho dhidi ya wabunge .. baada ya uamuzi huo wabunge 19 wana uwezo wa kuwasilisha pingamizi mahakamani kama ilivyokuwa kwa Zitto Kabwe

Uzoefu unaonesha kuwa CHADEMA haizingatii hata utaratibu wa katiba yao ktk kumfuta mtu uanachama badala yake hutumia mabavu na maamuzi ya watu wachache waliojimilikisha chama

KUHUSU SUALA LA KUINGILIA MAHAKAMA UKWELI NI KUWA CHADEMA KTK HILI INAINGILIA UHURU WA MAHAKAMA.. KUFANYA EXTERNAL INFLUENCE JUU YA KESI ILIYOPO MAHAKAMANI NI KUINGILIA UHURU WA MAHAKAMA PIA. SEMA KWA SABABU JAMBO HILI LIMEWAGUSA WAO NA NDIYO MAANA INAONEKANA SIYO KUINGILIA UHURU WA MAHAKAMA

KWA mtizamo wangu naona kuwa suala la kesi ya Mbowe kwa kuwa tayari lipo mahakamani; tuwaachie mahakama kazi hiyo ya kutafsiri sheria na tuwaamini kuwa watafanya uamuzi wa haki.

Endapo maamuzi ya mahakama itaonekana kutoridhika upo utaratibu wa kukata rufaa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom