John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,373
Kauli za Wakili Fatma Karume kuhusu hatua ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe kufutiwa mashitaka yake katika Mahakama Kuu, Machi 4, 2022 ambapo alikuwa yeye pamoja na wenzake watatu ambao wote wamefutiwa mashitaka yaliyokuwa yakiwakiabili.
"Ukitazama historia ya siasa, haijawahi kutokea hata siku moja njia ya kutumia fikra au mfumo wa kuendesha mashtaka ya makosa ya jinai kukomoa wanasiasa wenzako, njia hii haijawahi kufanya kazi, mfano ni Nelson Mandela alikaa jela miaka 27 na akaja kuwa Rais.
"Niliona tu itafika mahali kwamba Freeman Mbowe ni lazima wamtoe tu, kwa sababu hatokoma. Kama walitaka kumvunja moyo, sasa wamemzidisha kuwa shujaa.
"Kazi ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali (DPP) ni kuendesha mashtaka hadi mwisho, anapoendesha mashtaka ni kwamba ameangalia ana ushahidi wa kutosha, kinachonishangaza ni kwamba DPP amemaliza ushahidi wake na Jaji amesema Mbowe ana kesi ya kujibu, kisha DPP anajitoa.
"Katika kesi ya Freeman Mbowe, mahakama na Mwendesha Mashtaka wa Serikali (DPP) wote wamejivua nguo, ni fedheha pia kwa sababu hawakufuata utaratibu wowote wa kisheria ninaoujua mimi.
"Jaji alipaswa kutoa sababu mara baada ya kusikiliza ushahidi na kisha kusema Mbowe na wenzake wana kesi ya kujibu, kwamba ushahidi wote aliousikiliza na kuwasilishwa ulikuwa umefika lengo la kutokuwa na shaka yoyote.
"Niliwahi kumuuliza Jaji Mkuu mmoja kwamba, wewe huna kinga ya kutoshtakiwa, je ukishtakiwa uko tayari kushtakiwa katika mahakama zako hizi? Je, una imani na mfumo unatokana nao utakutendea haki?”
Source: Dar Mpya