Tofauti kati ya Yesu na Nabii Issa
KwaMujbu wa ndugu zetu waislam Yesu ni mtu tu kamaibrahim . ndio tunahoji hapa kama ni mtu kwa nini baba awe mariam? Angalau basu awe issa IBn Yusuf baba mlezi.

Allah anasema baba mzazi ya issa ninani? Kama hana Baba basi sio mtu huyo, mariam ilikuwa ni njia tu
Unaonekana husomi Bible na kwahiyo unadhani miraculous birth ipo kwa Yesu peke yake!! Kila mmoja anafahamu simulizi ya Kitabu cha Mwanzo, endapo hata baada ya Malaika kumtokea Sarah na kumwambia atazaa mtoto wa kiume, ilibidi Sarah acheke kwa sababu alishakuwa biologically infitile! Kuwa biologically infitile ni kwamba asingeweza kupata mtoto! Lakini kwa uwezo wa Mungu, Sarah akazaa mtoto wakati alishakuwa beyond expiration date!

Kipo kisa kingine ambacho kimesimuliwa na 2 Wafalme 14-17. Wakati Eliah (anayefahamu hiki kisa anisahihishe kuhusu jina), anahoji "sasa afanyiwe nini mwanamke huyu" Gehaz akajibu "Kwa kweli hana mwana, na mumewe ni mzee!" Aliah akaomba huyo mwanamke aitwe kisha akamwambia "mwaka ujao wakati huu utakuwa unamkumbatia mwana" Lakini yule mwanamke kwa kujua mume wake hakuwa tena na uwezo wa kuzalisha, akamwambia yule mtu wa Mungu "Hapana Bwana wangu, ewe mtu wa Mungu, usimwambie uongo kijakazi wako!"

Pamoja na hayo, 2 Wafalme 17 ikamaliza mjadala kwa kusema "Hata hivyo, mwanamke huyo mwaka uliofuata akapata mimba na kuzaa mwana!" Kwamba, pamoja na kwamba mume wa huyo mwanamke alishakuwa less reproductive lakini kwa uwezo wa Mungu, huyo mwanamke akazaa!!

Na kwa nyongeza tu, baadae mtoto aliyezaliwa alikufa, na haraka haraka yule mwanamke akarudi kwa yule mtu wa Mungu na kumkumbusha jinsi ambavyo alimtahadhalisha asimpe a false hope! Mtu yule wa Mungu akarudi kwa yule mwanamke na kufanya maombi kisha uhai ukarejea kwa mtoto!!

Kwahiyo jenga hoja ya u-Mungu wa Yesu kwa kutumia vigezo vikingine lakini sio cha miraculous birth, kwa sababu Yesu hakuwa wa kwanza kuzaliwa kimiujiza!!
 
Kama lengo lilikuwa ni kumtofautisha kabisa Yesu na binadamu wengine basi Mungu alikuwa na uwezo wa kumshusha moja kwa moja pasipo kupita hata kwenye tumbo la binadamu.
Zurri

mkamuita Issa ibn Mariam badala ya Issa Ibn Yusuf ambaye angalau ni baba mzazi.
Kitendo cha kumuita Bin Mariam hamuoni mnakubaliana na Yesu kuwa Yeye sio wa dunia hii wala chanzo chake sio mariam mariam ilikuwa kamamdaraja la kuwafikia wanadamu

Huoni hapo kuna jambo mnalificha nmalijua. Kuwa Yule hakuwa binadamu wa kawaida hivyo ni makosa kunmasibisha na Baba yake wa kuf
 
Chanzo cha Binadamu yoyote ni Kuzaliwa ukiacha adamu ambaye aliumbwa kwa udongo na mkewe.
Yesu anasema '' Kabla hata ya Babu wa wayahudi hajazaliwa Yeye Alikuwepo''. Wayahudi wakaelewa anasema yeye ni Mungu maana anakana kuwa source yake sio Mariam. na hajaanzia pale.

Kwa hoja hizi, unaweza kuniambia Yesu alianza kuwepo lini?

''Alifanyika Binadamu'' Yohana 1.
Kitendo kile cha uzaliwa kwa mfumo ambao hadi sasa unawachanganya watu humu kwa Lugha rahisi ni Incarnation kitendo cha Mungu kufanyika mwanadamu ndio maana akaitwa jina lingine Emmanuel (Mungu pamoja na wanadamu)
Huo ni uzushi wenu katika bibilia.

Bibilia hio hio inasema kuwa yeye sio kama Binaadamu wengine, kwa maana ya kuwa yeye ni binaadamu ila sio sawa na sisi, kwa vile yeye hakuzaliwa na baba na mama bali alizaliwa kwa kun fayakun tu.

Wewe tuhtibitishie kuwa Yesu alikuwepo kabla ya mababu wa mayahudi, halafu tuzungumzie na aya za kwenye bibilia ambazo zinakwenda kinyume na uaminicho.

Yesu alianza siku alozaliwa na Mariam.

Waislam hatujachanganyikiwa na concept yenu ya kuwa mungu aliingia kwenye mwili wa binaadamu. Ni concept ambayo haileti maana ya kiungu kabisa. Mungu the All powerful vipi aweze kuhimiliwa na kiumbe dhaifu kama mwanadamu? Kuzaliwa ni udhaifu wa mwanadamu, kuumbwa kwa udongo ama chochote ni udhaifu wa kiumbe yenye kuleta maana kuwa it can not sustain itself.

Yesu alikuwa mtume na hata bibilia inaonesha ivo.

Bibilia yenu wenyewe inawapinga mnachoamini!
 
Mkuu mbishie Yesu mwenyewe " kabla ya Ibrahim kuwako, mimi Niko" na ndani ya Yesu umesitirika uungu wote. Hii huitaji PhD. Alipoonekana kama mwanadamu alionekana dhaifu tu kuliko hata wewe
 
Kama lengo lilikuwa ni kumtofautisha kabisa Yesu na binadamu wengine basi Mungu alikuwa na uwezo wa kumshusha moja kwa moja pasipo kupita hata kwenye tumbo la binadamu.
Hata yeye Yesu anasema alishuka kutoka juu. Mariam ni njia aliyopitia kushuka sio chanzo cha Yesu.
 
Unaonekana husomi Bible na kwahiyo unadhani miraculous birth ipo kwa Yesu peke yake!! Kila mmoja anafahamu simulizi ya Kitabu cha Mwanzo, endapo hata baada ya Malaika kumtokea Sarah na kumwambia atazaa mtoto wa kiume, ilibidi Sarah acheke kwa sababu alishakuwa biologically infitile! Kuwa biologically infitile ni kwamba asingeweza kupata mtoto! Lakini kwa uwezo wa Mungu, Sarah akazaa mtoto wakati alishakuwa beyond expiration date!

Kipo kisa kingine ambacho kimesimuliwa na 2 Wafalme 14-17. Wakati Eliah (anayefahamu hiki kisa anisahihishe kuhusu jina), anahoji "sasa afanyiwe nini mwanamke huyu" Gehaz akajibu "Kwa kweli hana mwana, na mumewe ni mzee!" Aliah akaomba huyo mwanamke aitwe kisha akamwambia "mwaka ujao wakati huu utakuwa unamkumbatia mwana" Lakini yule mwanamke kwa kujua mume wake hakuwa tena na uwezo wa kuzalisha, akamwambia yule mtu wa Mungu "Hapana Bwana wangu, ewe mtu wa Mungu, usimwambie uongo kijakazi wako!"

Pamoja na hayo, 2 Wafalme 17 ikamaliza mjadala kwa kusema "Hata hivyo, mwanamke huyo mwaka uliofuata akapata mimba na kuzaa mwana!" Kwamba, pamoja na kwamba mume wa huyo mwanamke alishakuwa less reproductive lakini kwa uwezo wa Mungu, huyo mwanamke akazaa!!

Na kwa nyongeza tu, baadae mtoto aliyezaliwa alikufa, na haraka haraka yule mwanamke akarudi kwa yule mtu wa Mungu na kumkumbusha jinsi ambavyo alimtahadhalisha asimpe a false hope! Mtu yule wa Mungu akarudi kwa yule mwanamke na kufanya maombi kisha uhai ukarejea kwa mtoto!!

Kwahiyo jenga hoja ya u-Mungu wa Yesu kwa kutumia vigezo vikingine lakini sio cha miraculous birth, kwa sababu Yesu hakuwa wa kwanza kuzaliwa kimiujiza!!
Adam ni source ya mwanadamu.
Aliumbwa na mchakato mzima umeandikwa.
Hao wengine woote umekoseakosea kuwataja walizaliwa kwa tendon la ndoa kama wanadamu wote...

Yesu alikuja, hakuanzia tumboni mwa Marian humo alipitia tu. Ndio maana nawaambia Waislam Baba Wa Yesu ni Yule ambaye hata Yesu alimkumbushaga " Baba unitukuze ktk ule utukufu wangu niliokuwa nao kabla,".

Yohana mbatiZaji mnamuita yahaya alijua yote haya ninayokuambia. Anamzidi Yesu umri kwa miezi 6 lkn anasa "huyu amekuwepo kabla ya mimi kuwepo". Inawezekanaje mkuu?
 
Wapi nimemtaja Adam?! Tendo la ndoa lisilo na rutuba tangu lini likazalisha mtoto?! Inaelekea unajua sana Bible! eleza hapa ni wapi nimekusea kuhusu uzazi wa Isihaka na wapi nimekosea kuhusu hiyo 2 Wafalme 14-17? Eleza hapa kinyume chake unathibitisha madai yangu kwamba huijui Bible na ndo maana umeongea kijumla jumla tu wakati mimi nimekutajia vitabu husika!

Taja nilipokosea kosea hao watu kwa kutumia vitabu unavyoviamini!
 
usijali mkuu naona umekuja juu sana.
hujakosea maana uliomba kama umekosea ukosolewe yule sio eliya ni Elisha wa 2King 14-17.
Pole kama yale maneno yamekukwangua kidogo. Nisamehe.

Turudi kwenye Mada.
Wote hao uliowataja wamezaliwa Biologically na mimba imetungwa Biologically.
Hadi leo wapo wanawake wanaopata Ujauzito umri umevuka menopause. Mungu anaweza kureverse mifumo maana yeye ndio kaiumba.
Yule mama alikuwa Tasa, Mungu aliyeumba anaweza kureverse utasa na kuwa fertile.

Kwa Mariam sio hivyo na haifanani kabisa na hizo case.
Ni kitu supernatural nje ya binadamu na mifumo ya kibinadamu kilihusika kupita kupitia huyo mwanamwali.
Jambo la ajabu Mungu alikuwa ameshatabiri kupitia isaya miaka zaidi ya 500 iliyopita. Atapata Mimba atakayezaliwa sio mtu. ni (Mungu pamoja na wanadamu) yaani Emmanuel.

Kama tumekubaliana Yesu hana Baba, Yeye anasema anaye. Ni Kweli Sio Yusufu Bali ni Mungu Baba.
Na hakuanzia kwa mariam bali pale alipita tu katika process inaitwa Incarnation.
 
Mama hakuwa tasa bali mume alikuwa mzee beyond reproductive age!! Soma upya hiyo aya!
Kwa Mariam sio hivyo na haifanani kabisa na hizo case.
Unaona haifanani kwa sababu umejikita kwa Mariam kuzaa bila kuingiliwa na mwanaume huku ukisahau msingi wa kuzaa bila mwanaume; kwamba Mungu anaweza kufanya yale yasiyowezekana katika hali ya kawaida ili kuthibitisha uwezo wake! Kama ambavyo alifanikisha Sarah kuzaa wakati biologically alishakoma! Kama ambavyo alifanikisha kuzaa kwa yule mwanamke wa 2 Wafalme 14-17 wakati mumewe hakuwa na biological capacity ya kuzalisha! It's all about God's Miracle kuwadhihirishia waja wake kwamba hakuna kwake kinachoshindikana! Kama ambavyo aliweza kuwapa wana wale ambao walikuwa biologically expired ndivyo alivyoweza kumpa mwana Maria bila kuingiliwa na mwanaume!!
Ni kitu supernatural nje ya binadamu na mifumo ya kibinadamu kilihusika kupita kupitia huyo mwanamwali.
Mtu kama Sarah kuzaa wakati alikuwa ameshakoma hata siku zake unaona sio supernatural?! Unaona jambo kama hilo lipo ndani ya uwezo wa mwanadamu?! Hujiulizi kama nalo lipo ndani ya uwezo wa mwanadamu ni kwanini hata nae alitokewa na malaika na kuambiwa "utazaa"? Hivi hujiulizi ni kwanini hata yule mwanamke wa kwenye 2 Wafalme 14-17 nae ilikuwa ni baada ya kuthibitishiwa na Mtu wa Mungu?! Na kama umeisoma hiyo aya kwa mapana na marefu, utaona kule Mungu akisema "Mungu alinificha" kufuatia lile tukio la mtoto kufa!!
Jambo la ajabu Mungu alikuwa ameshatabiri kupitia isaya miaka zaidi ya 500 iliyopita. Atapata Mimba atakayezaliwa sio mtu. ni (Mungu pamoja na wanadamu) yaani Emmanuel.
Hapo utakuwa unapotoka ndugu yangu unless kama una mashaka mashaka juu ya uwezo wa Mwenyezi Mungu! Kuna uajabu gani kwa Mungu "kutabiri" jambo lililo ndani ya uwezo wake?! Btw, tangu lini Mungu akatabiri?! Mungu anasema na kutenda, PERIOD!
Kama tumekubaliana Yesu hana Baba, Yeye anasema anaye. Ni Kweli Sio Yusufu Bali ni Mungu Baba.
Na hakuanzia kwa mariam bali pale alipita tu katika process inaitwa Incarnation.
Hili siwezi kulielezea kwa sababu nisingependa kuongea mambo yanayolenga kusema ni nani aliye sahihi kati ya anayeamini hayo unayosema au yule asiyeamini! Lakini kwavile wewe unaamini hivyo, well and good!
 
Mkuu mbishie Yesu mwenyewe " kabla ya Ibrahim kuwako, mimi Niko" na ndani ya Yesu umesitirika uungu wote. Hii huitaji PhD. Alipoonekana kama mwanadamu alionekana dhaifu tu kuliko hata wewe

Usiwe na wasi, sina haja ya kumbishia Yesu. Tunatumia kitabu ambacho mnasema kinatoka kwake Yesu.

Acts 3:13 Mungu wa Abrahamu, Isaka na Yakobo, Mungu wa baba zetu amemtukuza Yesu mtumishi wake. Yeye ndiye yuleyule mliyemtia mikononi mwa wakuu na kumkataa mbele ya Pilato hata baada ya Pilato kuamua kumwacha huru.

Apo juu tayari bibilia inasema Yesu alikuwa mtumishi tu. Hii Haihitaji ata elimu ya chekechea kujua kuwa mtumishi sio Mungu
 
mkuu naona kama unahamahama.
nilitegemea uje na hoja ya kumbishia Yesu kuwepo kabla ya kuzaliwa na mariam. Unakuja na hoja mpya ya utumishi wake.
Huoni kama unapungukiwa nidhamu ya mjadala.

Kuhus Utumishi. Alikuwa anaongea na wayahudi na Kweli Yesu aliacha utukufu wote na kuja kuwa kama mtu wa kawaida akitumikia watu kwa kipindi cha miaka 30 hivi Kisha akarudi na kutwaa utukufu wake. Umeenda mbali huko matendo ungesoma kauli yake mwenyewe '' sikuja kutumikiwa bali kutumika'.
 
yesu mwana wa mungu ni nafsi ya pili katika kumkamilisha uungu mungu baba , mungu mwana , na ungu roho mtakatifu,
na tazama malaika akamshukia mariamu na kumwambia tazama utachukua mimba kwa uweza wa roho mtakatifu nawe utamzaa mwana jina lake yesu ama emanueli yaani mungu pamoja nasi huyu alikuja kuwa nasi ili atufundishe hapo sasa utaona mungu baba alimtuma mwana duniani akisaidiwa na mungu roho mtakatifu kuja kutufundisha yaliyo mema kumcha yeye aliye babayetu
asante
 
Mama hakuwa tasa bali mume alikuwa mzee beyond reproductive age!! Soma upya hiyo aya!
1138874

Huyu muhindi anaitwa Ramit Raghav kapata mtoto akiwa na miaka 94. Shida ilikuwa ni Mama kupita Muda wa Menopause mababu wanazaa tu mkuu.

naona haifanani kwa sababu umejikita kwa Mariam kuzaa bila kuingiliwa na mwanaume huku ukisahau msingi wa kuzaa bila mwanaume; kwamba Mungu anaweza kufanya yale yasiyowezekana katika hali ya kawaida ili kuthibitisha uwezo wake! Kama ambavyo alifanikisha Sarah kuzaa wakati biologically alishakoma! Kama ambavyo alifanikisha kuzaa kwa yule mwanamke wa 2 Wafalme 14-17 wakati mumewe hakuwa na biological capacity ya kuzalisha! It's all about God's Miracle kuwadhihirishia waja wake kwamba hakuna kwake kinachoshindikana! Kama ambavyo aliweza kuwapa wana wale ambao walikuwa biologically expired ndivyo alivyoweza kumpa mwana Maria bila kuingiliwa na mwanaume!!
Uwezo huo wa Mungu unaoutetea ndio huohuo uliomuwezesha mwana wake ambaye alikuwa na uungu wote kuzalowa kwa aibu kamammwanadamu.
Ndio maana hadi sasa nimejifunza Yesu hakuwa na Baba duniani. Maana yeye anaye Baba yake huko Juu ambaye wanaishi naye milele na kutawala naye milele, na yeye sio Kiumbe ni Muumba kwa Mujibu wa Bibilia Yohana 1.
Muujiza huu wa kupitia mariam mbona hata shetani kauiga kuna story nyingi sana katika dini za kioagani za zamani middle east za mwana wa muungu kuzaliwa na kuja kwa umbo la wanadamu. Soma matendo ya Mitume Paulo alipofika Listra wapagani wale walilia na kutaka kumuabudu wakisema ni Mungu kawajia kwa umbo la wanadamu. Hao walikuwa wazungu wa Ugiriki.

Hapo utakuwa unapotoka ndugu yangu unless kama una mashaka mashaka juu ya uwezo wa Mwenyezi Mungu! Kuna uajabu gani kwa Mungu "kutabiri" jambo lililo ndani ya uwezo wake?! Btw, tangu lini Mungu akatabiri?! Mungu anasema na kutenda, PERIOD!
Kuhusu Mungu Kutabiri nadhani soma tena Bibilia. Mungu ndiye aliyetabiri kuwa Utakuja utawala wa Umedi na Uajemi na Kiongozi wake ataitwa Koreshi akamtaja hadi jina na ndivyo ilivyokuwa. Soma Isaya mkuu. Pia Hutoa utabiri kupitia manabii wake. Kimsingi sifa yake ni Kujua Mwisho kabla ya mwanzo, mjuzi wa Yote. Alijua atazaliwa Mungu kwa kupitia mwanadamu Maria (Emmanuel Mungu pamoja na mwanadamu), akawawekea kwenye maandishi wayahudi ili wampokee lakon cha ajabu wakamkataa kama unachofanya humu rafiki.

hatulazimishani imani mkuu.
tunapeana changamoto ili kama ikiwezekana tuuodate imaninzetu tushike lililojema na kweli.
Na ukweli ni Kwamba Yesu ni mwana wa Mungu aliyekuwa na uungu wote, kwa ajili ya kumuokoa mwanadamu ambaye ilibidi aangamie milele. Baada ya Kazi hiyo njema Yuko Mbinguni anatawala Na Baba Yake. Na Anasoma hata unachoandika. Ndiye atakayehukumu ulimwengu wote hata waislam wanajua ndiye atakayefufua wafu wote siku ya kiyama (nabii wa ufufuo). Sisi tunasema alipokuja miaka 2000 iliyopita alikuja kama nabii mko sahihi kabisa 100% ila Baada ya Kurudi katika enzi pomj na Baba Yake atakuja kuwachukua wanaomuamini kama Mfalme wa wafalme, Mungu wa Muungu, Bwana wa Mabwana. Manabii wote watamsujudia na kumtukuza
 
Wapo.Adam na Eva hawana baba wala mama.
hawa sio miungu na taarifa zao zipo. waliumbwa na Mungu. Na Yesu kama mwana wa Mungu ambaye anauungu wote ndani yake Bibilia inasema hakuna kilichofanyika ambachokilifanyika pasipo yeye wakiwemo hao wanadamu wa kwanza.

Yesu sio kiumbe, ni kiumba. alifanyika kiumbe ili akiokoe kiumbe dunia alipomaliza hiyo project alirudi tena kama muumba ktk enzi zake. Na siku sio nyingi atarudi kama Mungu sio yule tena tuliyezoea kumdhihaki.
 
mkuu naona kama unahamahama.
nilitegemea uje na hoja ya kumbishia Yesu kuwepo kabla ya kuzaliwa na mariam. Unakuja na hoja mpya ya utumishi wake.
Huoni kama unapungukiwa nidhamu ya mjadala.

Kuhus Utumishi. Alikuwa anaongea na wayahudi na Kweli Yesu aliacha utukufu wote na kuja kuwa kama mtu wa kawaida akitumikia watu kwa kipindi cha miaka 30 hivi Kisha akarudi na kutwaa utukufu wake. Umeenda mbali huko matendo ungesoma kauli yake mwenyewe '' sikuja kutumikiwa bali kutumika'.
Sijahama hama mkuu wala sijapungukiwa na nidhamu ya mjadala. Wewe umetumia hoja ya uwepo wake kabla ya mababu wa mayahudi ili kama uthibitisho kuwa yeye ni Mungu. Na mimi nimekuletea jibu la kukuonesha kuwa yeye sio Mungu kwaio huo mstari ulioleta umekuwa dhaifu.

Labda wewe ututhibitishie Yesu alikuwepo kabla ya kuzaliwa Mariam alikuwa akifanya nini na kama nani.

Kwenye Marko, haya ni maneno yake: Yesu akamjibu, "Mbona unaniita mwema? Hakuna aliye mwema ila Mungu peke yake. Sasa kama yeye mungu mbona anakataa kuwa yeye mwema?

By the way, Mungu hatumikii kiumbe chochote, ila viumbe ndio vinamtumikia Mungu. Kwaio kama unamtumikia Mungu kamwe huwezi kuwa Mungu. Msumari mwengine umejigongea mwenyewe "Sikuja kutumikiwa bali kutumika". Hata hii nalo haihitaji elimu ata ya chekechea kujua kuwa Yesu alikuwa ametumwa na mtumaji!
 
Ndo mana sisi tunaamini kwamba mwenye bibilia kuna maneno ya ukweli(machache)na mengi ya uongo ambayo hayana msingi.

Kwa hiyo unapotoa hoja za Uungu wa yesu ndani ya bibilia ujue hayo ni katika maandiko ya uongo ambayo yanafaa kutazamwa kwa jicho la pili..

Issa na mama yake mariamu kaelezewa ndani ya Qurani kiuadilifu kabisa pasi na kumtilia chumvi wala nini.

Maandiko yanayomsema yesu ni Mungu ni maandiko ya uongo ambayo hayaingii hata akilini, kwani hata baadhi ya hao wakristo wenyewe wanaukana Uungu wa yesu.
Mkuu mbishie Yesu mwenyewe " kabla ya Ibrahim kuwako, mimi Niko" na ndani ya Yesu umesitirika uungu wote. Hii huitaji PhD. Alipoonekana kama mwanadamu alionekana dhaifu tu kuliko hata wewe
 
Sijahama hama mkuu wala sijapungukiwa na nidhamu ya mjadala. Wewe umetumia hoja ya uwepo wake kabla ya mababu wa mayahudi ili kama uthibitisho kuwa yeye ni Mungu. Na mimi nimekuletea jibu la kukuonesha kuwa yeye sio Mungu kwaio huo mstari ulioleta umekuwa dhaifu.

Labda wewe ututhibitishie Yesu alikuwepo kabla ya kuzaliwa Mariam alikuwa akifanya nini na kama nani.

Kwenye Marko, haya ni maneno yake: Yesu akamjibu, "Mbona unaniita mwema? Hakuna aliye mwema ila Mungu peke yake. Sasa kama yeye mungu mbona anakataa kuwa yeye mwema?

By the way, Mungu hatumikii kiumbe chochote, ila viumbe ndio vinamtumikia Mungu. Kwaio kama unamtumikia Mungu kamwe huwezi kuwa Mungu. Msumari mwengine umejigongea mwenyewe "Sikuja kutumikiwa bali kutumika". Hata hii nalo haihitaji elimu ata ya chekechea kujua kuwa Yesu alikuwa ametumwa na mtumaji!
nilitamani umkosoe Yesu kwa Kauli zake. '' kabla baba yenu hajakuwako MIMI NIKO''

kwanza nakupongeza maana unahekima kuliko wale wayahudi walioambiwa hivyo maana wao waliona anakufuru kujiita Mungu yaani '' MIMI NIKO'' au kiebrania YHWH. hili jina hata wenyewe wanaogopa kulitamka halipo kwa utukufu wake. ytasikia Mungu wanamuita elohim, adonai, etc lkn sio yhwh.

Kitendo cha kutaka kujua alikuwa anafanya nini, ni ishara unaanza kukubaliana na yesu ambaye najua unamuheshimu sana kuwa hasemi uongo na yeye husema kweli tu. Alikuwa anatawala na baba yake huko juu. Na sio mara ya kwanza mungu kuja kama binadamu, alikuja sikuhile kwa ibrahimu na akala kabisa msosi, kwenye tanuru la moto la nebukadneza alishuka pia. Alipobadilika pale mlimani k

Kwa nini hataki kuitwa mwema?

Pamoja na yote, akiwa ktk umbile la binadamu aliishi akizielekeza sifa zote kwa baba yake. Na alitaka yule dogo aliyekuja atambue hilo wema ni kwa baba tu hata wewe jifunze hilo maana yule kijana inaonekana alikuwa anataka kumpambapamba au alikuwa anamkejeli.

JE KUSEMA HIVYO YESU HAKUWA MWEMA?
Yeye hakutenda dhambi, wala neno la udanganyifu halikusikika mdomoni mwake. 2 petro 2:22

Ili Yesu aonekane hana sifa hizo. Ndio sababu hakuja kama Mungu katika utukufu,uweza, mamlaka yake yote. Hii nimesema mara kadhaa na narudia..

Wafilipi 2:5
Muwe na nia kama ile aliyokuwa nayo Kristo Yesu;6 yeye kwa asili alikuwa sawa na Mungu, lakini hakuona kwamba kuwa sawa na Mungu ni kitu cha kush ikilia sana. 7 Bali alikubali kuacha vyote, akachukua hali ya mtumishi, akazaliwa na umbo la wanadamu.8 Alipochukua umbo la mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii mpaka kufa, tena kifo cha msalaba. 9 Kwa sababu hiyo, Mungu alimwinua juu kabisa, akampa jina ambalo ni kuu kuliko majina yote; 10 ili kwa jina la Yesu, kila goti lipigwe, mbinguni na duniani na kuzimu; 11 na kila ulimi ukiri kwamba Yesu Kristo ni Bwana, kwa utukufu wa Mungu
 
Back
Top Bottom