Tofauti kati ya Yesu na Nabii Issa
Kutokuwa na mwingine hakumaanishi kuwa ni jambo kubwa mpaka nyinyi mkaamua kumuita Mungu.

Hivi ukitazama suala la kiumbe ambacho kipo hai mpaka muda huu mpaka itakapo karibia kiama unafikiri ni Yesu pekee ?

Lakini uhai,sio kwa Yesu bali kuna viumbe viko hai huko makaburini vinaendelea kuruzukiwa na Allah aliye juu.

Sasa sijaona hata hoja za uongo za kuwafanya nyinyi mumfanye Yesu kuwa ni mungu zaidi ya ujinga na kuchupa mipaka.
Wewe umesema hana Baba, Tumekubaliana Yusufu sio Baba wake wa Kumzaa, Japo alipaswa kutumia hata jina lake basi. Siamini hata alipoenda shule aliitwa Yesu Mariam.

Yeye anasema Baba Yake Yuko Mbinguni Alikotoka yeye. Yeye na Huyo Baba yake ni Kitu Kimoja. Kabla ya Kuja kwa njia ya Mariam, Alikuwa Yu namna ya Mungu sawa na Baba yake, Ameanza Kuwa na Baba kabla hata mariam hajazaliwa. Maana anasema kabla ya Ibrahim mimi niko.

Sasa unasemaje hapo.

Unakubali kuwa Anaye Baba, na Ni Mwana wa Mungu ambaye ni Mungu kwa mujibu wa Bibilia Yohana 1, Na ni mwana wa Mungu kabla ya Mariam Kuzaliwa wala adam kuumbwa.

karibu tutafakari pamoja.
 
najaribu kuweka huwenda ili nikusaidie kufikiri bila jazba za kidni.
Ila Yesu Kuwa Mungu hilo halina mjadala.
Mada kama hizi ni kutafuta kutoboa kona za mioyo Yenu ili mfikiri upya kwa nini Yesu na Sio Muhammad, na Bibilia na sio Quran.
Narudia tena '' Wenda'' ukajua
Yesu ndio ni mungu kwa mujibu wa baadhi ya wakristo ila si wakristo wote.
 
Yesu hakuhitaji hayo maana ndiye aliyewaumba Adam na Hawa wakiwa na Baba Yake. Baba Yake Haitaji Kumzaa wotenwapo milele

Sasa kama Yesu ni mwana wa Mungu,vipi aliwaumba Adamu na Hawa ? Ina maana waliahirikiana na baba yake ?

Na kama hoja ni mwana,hawa mbona ni wana lakini hamuwaiti Miungu ? Soma hapa,nanukuu :

Biblia inasema kwamba: 1. Bwana asema hivi, Israeli ni mwanangu mimi, mzaliwa wa kwanza wangu. (Kutoka 4:22). 2. Daudi ni mwana wa Mungu, yeye pia ni mwana wa kwanza. (Zaburi 89: 26-27). 3. ....maana mimi ni baba wa Israeli na Efraim (Ibrahim) ni mzaliwa wa kwanza wangu. (Yeremia 31:9). Hawa wana wa Mungu wote, kila mmoja wao ni mzaliwa wa kwanza kwa Mungu.

Kwanza itakuwaje watoto wote watatu wawe wazaliwa wa kwanza kwa Mungu. Pili kwa nini hawa wazaliwa wa kwanza wasiitwe miungu? Na kama hawa watatu wakubwa hawawezi kuwa miungu wala hawaabudiwi, basi mtoto mdogo Yesu pia hana haki yoyote ya kuitwa Mungu wala hana haki ya kuabudiwa. 4. Suleimani ni Mwana wa Mungu. (Mambo ya Nyakati 22:9-10). 5. Wapatanishao wameitwa Wana wa Mungu. (Mathayo 5:9). Oo! siyo tu bali katika Biblia baadhi ya watu wameitwa miungu.

Tena hakuna Mkristo ambaye anawaita miungu wala hawaabudiwi. Kama Biblia inavyosema kwamba: A. Yesu akawajibu, Je! haikuandikwa katika Torati yenu ya kwamba, mimi nimesema, ndinyi miungu? (Yohana 10:34). B. Bwana akamwambia Musa angalia, nimekufanya wewe kuwa kama mungu kwa Farao na huyo ndugu yako Harun atakuwa Nabii wako. (Kutoka 7:1).

Ila sijapata kuona washirikina kama nyinyi Wakristo.
 
Yesu ndio ni mungu kwa mujibu wa baadhi ya wakristo ila si wakristo wote.
Hata waislam wote hawaamini mtume ni nabii wao wa mwisho ndio maana mnabaguana shia, hamadiaya, sunni etc.
sio hoja yangu.
Wakristo kukataa Yesu ni Mungu mfano JW haimzuii Kuwa Mungu, Haimpori sifa zake.

Ila yeye Ametuhakikishia siku ya kiyama kila kinywa kitakili, na kila Goti litapigwa.
Niafadhali uanze kumsujudia sasa kuliko umsujudie siku ukiwa umechelewa alafu ukubali kabisa kula fire maana utasema hata mitale na midimu aliniambia. Moyo ulisadiki lakni niliogopa dini yangu itanionaje nikikana imani?
 
Kutokuwa na mwingine hakumaanishi kuwa ni jambo kubwa mpaka nyinyi mkaamua kumuita Mungu.

Hivi ukitazama suala la kiumbe ambacho kipo hai mpaka muda huu mpaka itakapo karibia kiama unafikiri ni Yesu pekee ?

Lakini uhai,sio kwa Yesu bali kuna viumbe viko hai huko makaburini vinaendelea kuruzukiwa na Allah aliye juu.

Sasa sijaona hata hoja za uongo za kuwafanya nyinyi mumfanye Yesu kuwa ni mungu zaidi ya ujinga na kuchupa mipaka.
Kiumbe hai makaburini. Hii Kali ya quran
 
Hivi huwa huogop kusema uongo ? Nani amekiriya kuwa hakuna binadamu aliyezaliwa bila baba ?

Sasa Yesu mama yake nani ? Na kwanini Yesu iwe Mungu mkuu ndio baba ake ? Yaani baba ake kivipi ? Maana ubaba ni wa aina mbili :

1. Baba wa nasaba
2. Baba mlezi

Huu ubaba ake Yesu unaingia katika aina gani ?
Nionyeshe Binadamu Aliyezaliwa Bila Baba ukiacha Yesu ambaye anaitwa Immanuel (Mungu pamoja na wanadamu).
 
Yeye anasema Baba Yake Yuko Mbinguni Alikotoka yeye. Yeye na Huyo Baba yake ni Kitu Kimoja.

Hii sio yeye tu,yaani viumbe vyote Roho zao zinatoka mbinguni mzee.
Kabla ya Kuja kwa njia ya Mariam, Alikuwa Yu namna ya Mungu sawa na Baba yake, Ameanza Kuwa na Baba kabla hata mariam hajazaliwa. Maana anasema kabla ya Ibrahim mimi niko.
Alikuwa sawa na baba yake kimaumbile au kinguvu ?

Kipi kinachokufanya useme kuwa alikuwa sawa na baba yake ?

Naomba unipe hayo mandiko anayosema kuwa amesema yeye alikuwepo kabla ya Ibrahim kisha uyathibitishe kuwa ameyasema yeye ?

Tuendelee...
 
Hata waislam wote hawaamini mtume ni nabii wao wa mwisho ndio maana mnabaguana shia, hamadiaya, sunni etc.
sio hoja yangu.
Wakristo kukataa Yesu ni Mungu mfano JW haimzuii Kuwa Mungu, Haimpori sifa zake.
Ila yeye Ametuhakikishia siku ya kiyama kila kinywa kitakili, na kila Goti litapigwa.
Niafadhali uanze kumsujudia sasa kuliko umsujudie siku ukiwa umechelewa alafu ukubali kabisa kula fire maana utasema hata mitale na midimu aliniambia. Moyo ulisadiki lakni niliogopa dini yangu itanionaje nikikana imani?
HIYO NI KWA MUJIBU WA BIBLIA
 
Nionyeshe Binadamu Aliyezaliwa Bila Baba ukiacha Yesu ambaye anaitwa Immanuel (Mungu pamoja na wanadamu).

Ila unajichanganya sana ujue,hapa unakiri ya kuwa Yesu ni kiumbe na suala la kiumbe mwingine kuzaliwa bila baba hilo sijapinga. Ndio maana nikakuuliza ya kuwa kuzaliwa kwake bila baba ndio mkamfanya kuwa Mungu ? Lakini musa huo huo unasema baba yake ni Mungu ? Embu tuliza akili kisha uje upya.
 
Hata waislam wote hawaamini mtume ni nabii wao wa mwisho ndio maana mnabaguana shia, hamadiaya, sunni etc.
sio hoja yangu.
Wakristo kukataa Yesu ni Mungu mfano JW haimzuii Kuwa Mungu, Haimpori sifa zake.
Ila yeye Ametuhakikishia siku ya kiyama kila kinywa kitakili, na kila Goti litapigwa.
Niafadhali uanze kumsujudia sasa kuliko umsujudie siku ukiwa umechelewa alafu ukubali kabisa kula fire maana utasema hata mitale na midimu aliniambia. Moyo ulisadiki lakni niliogopa dini yangu itanionaje nikikana imani?
YESU NI MUNGU AU MWANA WA MUNGU?
 
AMEKAA KUUMENI KWA MUNGU BABA?
 
Yesu hawezi kuwa Mungu kwa sababu amezaliwa.

Halafu unasema kuwa ".... hakuna mwanadamu mwengine aliepitia huo" inamaana Yesu anasema yeye ni Binaadamu lakini sio sawa na binaadamu wengine 🙂
Chanzo cha Binadamu yoyote ni Kuzaliwa ukiacha adamu ambaye aliumbwa kwa udongo na mkewe.
Yesu anasema '' Kabla hata ya Babu wa wayahudi hajazaliwa Yeye Alikuwepo''. Wayahudi wakaelewa anasema yeye ni Mungu maana anakana kuwa source yake sio Mariam. na hajaanzia pale.

Kwa hoja hizi, unaweza kuniambia Yesu alianza kuwepo lini?

''Alifanyika Binadamu'' Yohana 1.
Kitendo kile cha uzaliwa kwa mfumo ambao hadi sasa unawachanganya watu humu kwa Lugha rahisi ni Incarnation kitendo cha Mungu kufanyika mwanadamu ndio maana akaitwa jina lingine Emmanuel (Mungu pamoja na wanadamu)
 
Naona umepata funzo la kuwa usiwe unaongea story za maskani katika mijadala ya kielimu,wenzako wanasoma wewe unaleta hisia usizo weza kuzitetea ? Acha kabisa tabia ya kuhisi hisi,soma uelewe.

Tuko pamoja.

Personal attacks na character assassination ni dalili kuu za watu wasio na upeo mkubwa kifikra. Mimi ni mtu huru kifikra na wewe ni ndege unaefurahia kukaa ndani ya CAGE, huwezi kujua ladha ya kuwa huru na lazma utauchukia uhuru. Usisahau kingine, sounding philosophical doesn't make you sound smart to people of my kind but the content and substance found within your words; I used to respect you from a far ila nikiri "you are a DISSAPOINTMENT kwangu leo".
 
adam ndie baba wa watu. labda niseme baba yake ni udongo labda unielew.
naomba baba yake yesu Vinginevyo sio mtu ukikoswa maelezo, maana wanadamu wote ambao wa kwanza ni ibrhm wanajulikana wanavyopatikanw
Adamu ni baba wa watu si pamoja na mama wa Yesu.
 
Ila unajichanganya sana ujue,hapa unakiri ya kuwa Yesu ni kiumbe na suala la kiumbe mwingine kuzaliwa bila baba hilo sijapinga. Ndio maana nikakuuliza ya kuwa kuzaliwa kwake bila baba ndio mkamfanya kuwa Mungu ? Lakini musa huo huo unasema baba yake ni Mungu ? Embu tuliza akili kisha uje upya.
Yesu sio Kiumbe.
Ni Mungu Mwana aliyefanyika Kiumbe kwa miaka takribani 30 na Baadaye akarudi katika enzi yake.
Anapofanyika mwanadamu ndipo nyie mnaishia na kuagia.
mnaacha mambo mengi mazuri sana.Mbona Yahaya (Yohana mbatizaji ) anaweka wazi '' Yeye ajaye ni mkuu kuliko mimi maana alikuwako kanla yangu''

Yohana 1:30
Huyu ndiye yule niliyewaambia ya kwamba, ‘Yuaja mtu nyuma yangu ambaye ni mkuu kuliko mimi kwa maana alikuwako kabla yangu.’

Yohana kama angejua Yesu ni Binadamu wa Miujiza ambaye sio Mungu na Birthday yake ninsiku ile aliyozaliwa Bethrehem maana alijua kwa sababu Yesu ni ndugu yake. Asingesema alikuwako kabla yangu wakati Yohana alizaliwa miezi sita kabla ua Yesu.

Mkuu Zurri na mosabiy hadi hapa unashindwa Kujua Baba wa Yesu ni nani na Yesu sio Mtu tu, Bali ni Mungu mwana aliyekuja kwa njia ya mwili wa mwanadamu.

Waislam ni watu wa reasoning, ukikwepa na hapa nitakushusha viwango mkuu wangu
 
Personal attacks na character assassination ni dalili kuu za watu wasio na upeo mkubwa kifikra. Mimi ni mtu huru kifikra na wewe ni ndege unaefurahia kukaa ndani ya CAGE, huwezi kujua ladha ya kuwa huru na lazma utauchukia uhuru. Usisahau kingine, sounding philosophical doesn't make you sound smart to people of my kind but the content and substance found within your words; I used to respect you from a far ila nikiri "you are a DISSAPOINTMENT kwangu leo".
umeandika kwa hekima...
 
Back
Top Bottom