mitale na midimu
JF-Expert Member
- Aug 26, 2015
- 10,419
- 17,762
Kama ntajaribu kukufahamisha.Hapo ndio naona dini ni ujinga wa kiwango cha lami, kwani ni lazima Mungu amfanye laana Nabii wake ili kuwaokoa? kwani kwa uwezo wake yeye husema jambo likawa, iweje mtu atesweeee halafu aangikwe msalabani kwa taaabu mpaka afe ili nyie muokolewe? kwa nini asiseme "Mmeokolewa" basi mkaishi safi na wote mkawa dini moja, hakuna cha alshabab wala antibalaka? anakwama wapi huyo Mungu?
hiyo ni kesi sio suala la kutamka tu.
Mungu aliweka kanuni. Mwanadamu akiivunja atakufa. mwanadamu akavunja. Mungu sio kama viongozi wetu apindishe sheria, Sheria au ile kanuni inataka afe hakuna jinsi. Kama haitoshi shetani mshataki yupo anafuatlilia ili Mungu asitende haki alalamike ionekane Mungu ni mbaguzi.
Hakukuwa na Jinsi kati ya mawili. Mwanadamu aangamie milele au Mungu aliyemuumba afe kwa niaba ya mwanadamu kukidhi takwa la sheria inayodai mtu lazima afe maana kaivunja. Hawezi kufia Mbinguni lazima aje hukuhuku kwa wanadamu ambao anaassignment pia ya kuwaonyesha jinsi ya kuishi. Anawaonyesha pia model ya maisha. Kafa msalabani kwa niaba ya ulimwengu wote.
Hapa inqbaki kqzi mbili kukubali huo mbadala wa kifo maana hiyo aibu ulipaswa kubeba wewe yeye kafanya kwa niaba au umkatae Yesu na zoezi zima tena wengine wanapotosha kusema hakufa.
Hapo ndipo imelala hatma ya mwanadamu. Ndicho kinatufanya kukomaa hapa na ndugu zetu nao angalau wapate picha tunamaanisha nini tunaposema Mungu kaonekana mitaani hatimaye kasurubiwa uchi msalabani?