Tofauti kati ya Yesu na Nabii Issa
Ungejibu Kwanza swali ndipo uulize hayo maswali yako.

Lengo la Quran lilikuwa kuwaambia Waarabu kuwa Mungu ni mmoja na waache kuabudu miungu kwenye like Jiwe Jeusi ilipokuwa miungu 360. Zaidi ya hapo Quran haina jipya hata Kwa Waarabu wenyewe. Kwani mengine yote yalikuwa utamaduni WA Waarabu.

Sasa tusitoke kwenye mjadala.

Nioe hoja tatu kubwa zinazokufanya uamini Yesu ndiye ISA
Ndiyo maana nimekuuliza ikiwa umewahi kuigusa QUR'AN,ungekua umeigusa QUR'AN usingeandika ulichoandika, waarabu waliupiga Vita uislam sababu ulikua kinyume na utamaduni wao,ama kuhusu issa na yesu naiamini Qur'an,siyo biblia ambayo habari za yesu zimeandikwa miaka 100 baada ya yesu kuondoka,huku ikijichanganya na kuwa na maandiko yanayopingana kimantiki
 
Sasa mbona Umeeleza vizuri lakini umeshindwa kui-drive Yeshua mpaka ifike Kwa Isa( eisa) wa Quran.

Uelewe pia hapa unazungumzia Fonetiki ya Lugha Kwa hiyo kama huna utaalam wa Lugha ni Bora uomne msaada uelezewe.
Ni Kwa nini Jesus iwe Yesu, au Yeshua kiebrania iwe Iesus Kwa kigiriki.

Mambo ya kusema Biblia ilibadilishwa ni uzushi kama hauna Biblia halisi ambayo haijabadilishwa.
Toleo la biblia la kiswahili la impremanto wewe umeliona!?..kaulize kanisani wakupe,toleo la biblia tulilotumia 1990s mwishoni tu limebadilishwa,maneno Kama swaumu, sikukuu ya IDD,kuwatawadha miguu wanafunzi yametolewa na kuweka mengine mfano kuwaosha miguu wanafunzi nk, nimekwambia kiebrania yesu akiitwa y'shua, kiebrania Ishmael wakati kiarabu ismail, tofauti ya sh na s, kwenyewe y'shua toa sh weka s ili upate kwa kiarabu jina litatamkwa vipi,au Ishmael siyo ismail!?..vizuri umeweka kigiriki hapo,linatamkwaje kigiriki kwa mujibu wa ulivyoandika?
 
Yeshua ni kiaramaic.... Kiebrania ni Yahushua
Aramaic ni ya wasyria wakati Hebrew ni waisrael,zote ni semitic zenye misamiati sawa,ni Kama kisukuma na kinyamwezi,na hakuna herufi 'e' kwenye hizo lugha,herufi hiyo inawekwa na watu wa ulaya kufuata lugha zao
 
Huu ni uongo..... Kiebrania inatamkwa kama Yahushua.......kama mtu anayetoa na kuvuta pumzi , ukitaka yi, unavuta au kutoa pumzi?
Acha kudanganya watu.
Jielimishe babu acha kubandika watu sifa ya uwongo, google tu 'jesus' name ni Hebrew' halafu uje uniambie
 
Jielimishe babu acha kubandika watu sifa ya uwongo, google tu 'jesus' name ni Hebrew' halafu uje uniambie
Sasa unabisha?
Aya google kama watakuletea yissaya sijui....
Wayahudi walikuwa Wana mtindo wa kuita watoto majina ya kuwakumbusha kuwa YHWH ni Mungu wao.
 
Aramaic ni ya wasyria wakati Hebrew ni waisrael,zote ni semitic zenye misamiati sawa,ni Kama kisukuma na kinyamwezi,na hakuna herufi 'e' kwenye hizo lugha,herufi hiyo inawekwa na watu wa ulaya kufuata lugha zao
Nimekuambia jina lake ni Yahushua kwani Kuna e apo?
 
Uzuri ni kuwa Imani ya uislamu haitaji approval kutoka Kwa watu wa dini nyengine. Amini utakavyoamini lakini Imani yako haibadilishi chochote juu Imani ya uislamu. Uislamu utakuwa vilevile.
 
Sasa Baada ya hayo maelezo jibu hoja za huu Uzi hata Moja ili Watu wajifunze.
Mimi nikiamua kujibu hakuna hoja hata moja ya nguvu uliyoitoa isipokuwa sikuwa na makusudio ya kuchangia mjadala huu, ila ukinitaka nichangie naweza na nitaanza kama ifuatavyo.

Bismillah, kwa ufupi mkubwa mijadala ya kumtofautisha issa mwana wa mwaryam alayhi ssalaam na yesu imekithiri siku za karibuni, na malengo ya mijadala hii ni kupindisha ukweli kwa makusudi baada ya kushindikana kuvunja hoja kuwa uislamu umemtukuza masihi issa alayhi ssalaam na kumpa heshima kubwa kuliko ukristo uliomtweza na kumfanya msulubiwa tena aliyedhalilishwa mbele za watu.

Jambo la pili, mijadala hii pia imekithiri baada ya kuwa kule kuonekana masihi issa amani juu yake ndio uzi mwembamba baina ya uislamu na ukristo hivyo wahafidhina wakaona bora kusema huyu si yule ili kuhafifisha hoja za wapinzani wao, maana tukikubaliana sio mwana wa mungu na tukikubaliana hajasulubiwa kama uislamu ulivyoeleza basi hakuna ukristo tena.

Tukirudi kwenye mada, binafsi sio muumini wa hearsay's hivyo mapenzi yangu ni kutoa hoja kutoka kwenye certified source ni mamoja iwe kutoka kwenye maneno ya allah yaani Qur'an au hadithi sahihi za mtume swala na salaam ziwe juu yake zilizoshuhudiliwa na wanawachuoni wakubwa wa fani ya hadithi juu ya usahihi wake, kwa sababu hiyo hoja za kutoka upande huu zitabaki zenye nguvu zaidi daima kutokana na usahihi wa kule zinapotoka.

Masihi issa mwana wa mariam ni mtume wa allah na ndie mtume wa pili kutoka mwisho na baina yake yeye na mtume muhammad swala na salaam ziwe juu yao ni miaka 600 takriban, yeye alitoa bishara ya kuja mtume muhammad na nabii ibrahiym alayhi ssalaam aliomba dua allah awapatie mtume pale alipoacha kizazi chake yaani mkewe haajar na mwanae ismail alayhi ssalaam, hivyo yeye mtume muhammad ni bishara ya ndugu yake issa mwana wa mariam na dua ya baba yake ibraahiym, manabii wote ni watoto wa baba mmoja na mama zao mbalimbali, juu yao swala na amani,

Turudi nyuma kidogo bila kurefusha sana maneno, nabii zakariyyah alayhi ssalaam alikosa mtoto kwa muda mrefu mpaka akafikia uzee na yeye ndio alikuwa mlezi na muangalizi wa mariam bint imraan mama yake na nabii issa, wakati fulani aliyaona mambo yasiyo ya kawaida kwa mariam na habari hii imeelezwa vizuri katika Qur'an pale allah aliposema.

"Hakika allah alimteua adam na nuhu na ukoo wa ibrahim na ukoo wa imran juu ya walimwengu wote."

"Ni kizazi wao kwa wao,na allah ni mwenye kusikia na mwenye kujua."

"Aliposema mke wa imran, mola wangu mlezi! nimekuwekea nadhiri kilichomo tumboni mwangu kuwa wakfu, basi nikubalie! hakika wewe ndiye mwenye kusikia mwenye kujua."

"Basi alipomzaa alisema: mola wangu mlezi! nimemzaa mwanamke! na allah anajua sana aliyemzaa, na mwanaume si sawa na mwanamke, na mimi nimemwita mariam, na mimi namkinga kwako, yeye na uzao wake, uwalinde na shetani aliyelaaniwa."

"basi mola wake mlezi akampokea kwa mapokeo mema na akamkuza makuzo mema, na akamfanya zakariyyah kuwa mlezi wake, kila mara zakariyyah alipoingia kwake alimkuta na vyakula, basi alimwambia: ewe mariamu! unavipata wapi hivi? naye akasema: hivi vinatoka kwa allah, na allah humruzuku amtakaye bila ya hisabu."

"basi hapo zakariyyah akamwomba mola wake, akasema: mola wangu mlezi! nipe kutoka kwako uzao mwema, hakika wewe ndiye mwenye kusikia maombi."

"Basi akamuita yeye malaika na hali ya kuwa amesimama akiswali kwenye mihrabu "hakika allah anakubashiria {kupata mtoto aitwae} yahya, atakayekuwa mwenye kusadikisha neno litokalo kwa allah, ni bwana na mtawa na nabii kwa watu wema."

Qur'an 3:33-39

Mpaka mwisho wa habari hii, nimeleta aya hizi kwa makusudi kuonesha ufanano wa matukio ya zakariyyah, maryam, yahya na issa mwenyewe amani iwe juu yao, watu hawa kamwe haiwezekani kuwatenganisha kwasababu kwa uhakika hasa hilo haliwezekani.

Torati, injili, na zaburi vyote ni vitabu vimetoka kwa allah na ni maneno yake na si ya mwanadamu katu, ila tu hivyo vilivyotangulia vimeingiliwa na mikono ya watu wakayabadili mengine na mengine wakayafuta, na uwezekano wa kuyafuta yote ni mdogo ndio maana utaona tofauti ya majina ya kihebrania lakini yanawiana na yaliyotajwa kwenye Qur'an kwasababu yote ni majina ya kiajemi, na issa mwana wa mariam atarudi mwisho wa zama na atakufa kama wanavyokufa wanadamu wengine.

"Na mayahudi wanasema uzeir {ezra} ni mtoto wa allah, na wakristo wanasema, masihi {yesu} ni mtoto wa allah, hiyo ndiyo kauli yao kwa vinywa vyao, wanayaiga maneno ya waliokufuru kabla yao, allah awaangamize! vipi wanageuzwa? {kuacha ukweli kuuelekea uongo}."

Qur'an 9:30

Nahofia kurefusha zaidi faida ikawa ndogo, tuanzie hapa.
 
Uislamu hauwezi kujenga hoja bila kumng'ang'ania Yesu kuwa na Isa

Uislamu haujakamilika

Kupitia Quran huwezi kupata historia full ya Yesu

Kwenye Biblia kuanzia vitabu vya manabii unaanza kuona picha halisi ya Yesu

Mfano Mika alitabiri eneo sahihi la Yesu atakapozaliwa

Isaya ndiye katabiri mengi kuhusu Yesu

Daudi kupitia zaburi katabiri mengi Sana

Mfano Zaburi 22

Sasa vitu Kama hivi huwez kuvipata kwenye Quran

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nikiamua kujibu hakuna hoja hata moja ya nguvu uliyoitoa isipokuwa sikuwa na makusudio ya kuchangia mjadala huu, ila ukinitaka nichangie naweza na nitaanza kama ifuatavyo.

Bismillah, kwa ufupi mkubwa mijadala ya kumtofautisha issa mwana wa mwaryam alayhi ssalaam na yesu imekithiri siku za karibuni, na malengo ya mijadala hii ni kupindisha ukweli kwa makusudi baada ya kushindikana kuvunja hoja kuwa uislamu umemtukuza masihi issa alayhi ssalaam na kumpa heshima kubwa kuliko ukristo uliomtweza na kumfanya msulubiwa tena aliyedhalilishwa mbele za watu.

Jambo la pili, mijadala hii pia imekithiri baada ya kuwa kule kuonekana masihi issa amani juu yake ndio uzi mwembamba baina ya uislamu na ukristo hivyo wahafidhina wakaona bora kusema huyu si yule ili kuhafifisha hoja za wapinzani wao, maana tukikubaliana sio mwana wa mungu na tukikubaliana hajasulubiwa kama uislamu ulivyoeleza basi hakuna ukristo tena.

Tukirudi kwenye mada, binafsi sio muumini wa hearsay's hivyo mapenzi yangu ni kutoa hoja kutoka kwenye certified source ni mamoja iwe kutoka kwenye maneno ya allah yaani Qur'an au hadithi sahihi za mtume swala na salaam ziwe juu yake zilizoshuhudiliwa na wanawachuoni wakubwa wa fani ya hadithi juu ya usahihi wake, kwa sababu hiyo hoja za kutoka upande huu zitabaki zenye nguvu zaidi daima kutokana na usahihi wa kule zinapotoka.

Masihi issa mwana wa mariam ni mtume wa allah na ndie mtume wa pili kutoka mwisho na baina yake yeye na mtume muhammad swala na salaam ziwe juu yao ni miaka 600 takriban, yeye alitoa bishara ya kuja mtume muhammad na nabii ibrahiym alayhi ssalaam aliomba dua allah awapatie mtume pale alipoacha kizazi chake yaani mkewe haajar na mwanae ismail alayhi ssalaam, hivyo yeye mtume muhammad ni bishara ya ndugu yake issa mwana wa mariam na dua ya baba yake ibraahiym juu yao swala na amani.

Turudi nyuma kidogo bila kurefusha sana maneno, nabii zakariyyah alayhi ssalaam alikosa mtoto kwa muda mrefu mpaka akafikia uzee na yeye ndio alikuwa mlezi na muangalizi wa mariam bint imraan mama yake na nabii issa, wakati fulani aliyaona mambo yasiyo ya kawaida kwa mariam na habari hii imeelezwa vizuri katika Qur'an pale allah aliposema.

"Hakika allah alimteua adam na nuhu na ukoo wa ibrahim na ukoo wa imran juu ya walimwengu wote."

"Ni kizazi wao kwa wao,na allah ni mwenye kusikia na mwenye kujua."

"Aliposema mke wa imran, mola wangu mlezi! nimekuwekea nadhiri kilichomo tumboni mwangu kuwa wakfu, basi nikubalie! hakika wewe ndiye mwenye kusikia mwenye kujua."

"Basi alipomzaa alisema: mola wangu mlezi! nimemzaa mwanamke! na allah anajua sana aliyemzaa, na mwanaume si sawa na mwanamke, na mimi nimemwita mariam, na mimi namkinga kwako, yeye na uzao wake, uwalinde na shetani aliyelaaniwa."

"basi mola wake mlezi akampokea kwa mapokeo mema na akamkuza makuzo mema, na akamfanya zakariyyah kuwa mlezi wake, kila mara zakariyyah alipoingia kwake alimkuta na vyakula, basi alimwambia: ewe mariamu! unavipata wapi hivi? naye akasema: hivi vinatoka kwa allah, na allah humruzuku amtakaye bila ya hisabu."

"basi hapo zakariyyah akamwomba mola wake, akasema: mola wangu mlezi! nipe kutoka kwako uzao mwema, hakika wewe ndiye unayesikia maombi."

"Basi akamuita yeye malaika na hali ya kuwa amesimama akiswali kwenye mihrabu "hakika anakubashiria {kupata mtoto aitwae} yahya, atayekuwa mwenye kusadikisha neno litokalo kwa allah, ni bwana na mtawa na nabii kwa watu wema."

Qur'an 3:33-39

Mpaka mwisho wa habari hii, nimeleta aya hizi kwa makusudi kuonesha ufanano wa matukio ya zakariyyah, maryam, yahya na issa mwenyewe amani iwe juu yao, watu hawa kamwe haiwezekani kuwatenganisha kwasababu kwa uhakika hasa hilo haliwezekani.

Torati, injili, na zaburi vyote ni vitabu vimetoka kwa allah na ni maneno yake na si ya mwanadamu katu, ila tu hivyo vilivyotangulia vimeingiliwa na mikono ya watu wakayabadili mengine na mengine wakayafuta, na uwezekano wa kuyafuta yote ni mdogo ndio maana utaona tofauti ya majina ya kihebrania lakini yanawiana na yaliyotajwa kwenye Qur'an kwasababu yote ni majina ya kiajemi, na issa mwana wa mariam atarudi mwisho wa zama na atakufa kama wanavyokufa wanadamu wengine.

"Na mayahudi wanasema uzeir {ezra} ni mtoto wa allah, na wakristo wanasema, masihi ni mtoto wa allah, hiyo ndiyo kauli yao kwa vinywa vyao, wanayaiga maneno ya waliokufuru kabla yao, allah awaangamize! vipi wanageuzwa? {kuacha ukweli kuulelekea uongo}."

Qur'an 9:30

Nahofia kurefusha zaidi faida ikawa ndogo, tuanzie hapa.
Una Torati ,zabri na Injili ambazo hazijaharibiwa tufananishe na hiz ambazo zimeharibiwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uzuri ni kuwa Imani ya uislamu haitaji approval kutoka Kwa watu wa dini nyengine. Amini utakavyoamini lakini Imani yako haibadilishi chochote juu Imani ya uislamu. Uislamu utakuwa vilevile.
Uislamu una matobo Sana ,mfano hii hoja ya Isa sio Yesu ,unaona inavyoshindwa kujitetea

Kwenye Biblia mfano Mika aliishi miaka 700 kabla ya Yesu, lakini anatabiri exactly kuhusu Yesu,

Vivyo hivyo kwa Yeremia,Isaya ,Daudi , Ezekiel ,n.k

Hata Yesu kwenye kuwabana Wayahudi alikuwa anarejea Sana Maandiko ya hao manabii

Mfano Zaburi 22 Ni full kuhusu Yesu

Isaya 61 ,53 zinamuhusu Yesu

Utaona Wanamtabiri Kama mwana wa Daudi ,atatokea kwenye huo ukoo ,

Hadi Yesu anakuja ,Kuna mlolongo mkubwa unathibitisha habari zake

Lakini Quran haipo hivo imeokotaokota na kubumba habari

Manabii wa zaman walieleza had kwann Yesu ataitwa Hilo jina Yehoshua au Joshua

Quran haisemi chochote ,

Maana ya Jina Isa kwa kiarabu Ni Wekundu

Yehoshua /Joshua /Jesus/Yesu ni Mwokozi

Hilo jina linasadifu had aliyokuja kuyafanya huyo Yesu

Hivo kwa hoja lukuki ISA SIO YESU

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ama kuhusu issa na yesu naiamini Qur'an,siyo biblia ambayo habari za yesu zimeandikwa miaka 100 baada ya yesu kuondoka,huku ikijichanganya na kuwa na maandiko yanayopingana kimantiki
Koran imeandika habari za Isa baada ya miaka mingapi baada ya Isa kuwepo?

Tafadhali jibu kama swali nilivyoliuliza
 
Koran imeandika hanari za Isa baada ya miaka miangapi baada ya Isa kuwepo?

Tafadhali jibu kama swali nilivyoliuliza
Qur'an ni wahyi(ufunuo toka kwa Mungu mmoja asiye na mshirika,hakuzaa Wala kuzaliwa,Hana mwana Wala baba,ana wivu)...miaka mingapi baada ya issa kuwepo Hilo Sina hakika,Ila Wana historia wanadai Isa aliondoka duniani akiwa na miaka 33 wakati Muhammadi kapata utume 610AD
 
Ndio maana nikakuambia hata mambo Subiri wakubwa wako wajadili.
Nimejadili jina Yeshua etymological, asili yake nikakuambia ni tofauti na isa.
Kisha nikaelezea maana ya jina Yeshua ni Mwokozi, Semantically ambayo ni tofauti na ISSA.
Nikikuambia ueleze maana ya jina Issa Kwa mujibu wa Quran utaeleza?
Hayo maelezo umetoa kwenye chapter gani ya biblia?

Nina imani hata haufahamu herufi za kiarabu zinazounda hilo neno hadi likatoa Isa kwenye kiswahili. Ngoja nikupe shule ya bure herufi zinazounda likapatikana neno isa kwa kiswahili kuna ع ain ambalo kwenye kiswahili wala kingereza matamshi yake hayapo.

Kuna ي kwenye mfumo wa consonant ni y na kuna س inawakilisha kama S kwenye lugha zingine ndiyo likazaa neno
عيس. Kurahisisha kwa kiswahili likapatikana neno Isa.
Nataka nikuelewe kichwa chako kigumu wapi kwenye matamshi neno Isa au linavyoandikwa.

Kuna mchezaji wa Yanga Jesus au Arsenal angalia majina yanavyosomwa lakini muundo huo huo mmoja.
Kwa hiyo kijana uache ukilaza kwa hoja ya jina au matamshi.

Croatia kwenye wakristo wengi anaitwa Isus. Au mchungaji kakuongopea mapepo yanatoka ukitamka Jesus, Yesu na Yeshua ndiyo maana umekuwa king'ang'anizi.
 
Una Torati ,zabri na Injili ambazo hazijaharibiwa tufananishe na hiz ambazo zimeharibiwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapana hakuna na baadhi ya maneno ndio hayo yako kwenye hiyo inaitwa biblia, na kwa kubadilishwa huku sisi tumetoshelezwa na Qur'an kwasababu imekuja kutueleza baadhi ya habari za torati na injili na zaburi pia, bali hizo zilikuwa sheria za wana wa israeli sisi ni umma na zama nyingine wala zisitufae tena, baadhi ni kama aya hii.

"Na hakika tulikwishaandika katika zaburi baada ya dhikr, ya kwamba ardhi watairithi waja wangu walio wema."

Qur'an 21:105

Na mfano wa habari hizo kwenye Qur'an ni nyingi tu, kwa ajili hiyo sisi tukafundishwa mtu akitujia na habari akadai ni sehemu katika torati au injili au zaburi basi tuseme sisi tumeamini yaliyoteremshwa kwenu na yaliyoteremshwa kwetu, ili tusije kukanusha kumbe ni sehemu katika hayo, na tusije kukubali kumbe ni yale yaliyobadilishwa.
 
Back
Top Bottom