Rais anaweza wote. Akiwa weak the hayo mashinikizo yatamsumbua.Shukrani sana TLS Kwa mwongozo huu.
Imani yetu rais ameapa kuilinda na kuitetea katiba yetu, naamini pia atakiishi kiapo chake, kama hakutakua na mashinikizo yalio juu ya uweza wake kwa wakati huu.
Abasi ni msemaji mkuu wa selikaliLile siyo Baraza la Mawaziri. Ni kikao tu cha marafiki. Ndiyo maana kina Abbas alihudhuria wakati siyo wajumbe wa Baraza
Katiba haijatamka waziwazi kuhusu suala la baraza la mawaziri na kifo cha Rais aliyekuwepo madarakani.Kwa maana hiyo hata hawa kina Pole pole walioteuliwa kuwa wabunge na rais Magufuli nao inatakiwa wasiwe wabunge tena?
Hapa hawa TLS inaonekana nao hawana wanachojua
naona unaanza kumfundisha kazi.. Sasa mh raisi.. Unadhani yeye na jiwe wanautofauti huyu yeye anafanya kimya kimya tofauti na aliepita aliekuwa anasemaa hadharani... Anaposema atailinda na kuisimamia katiba si katiba tu hata ba matakwa ya chama chake kibaki madarakani ni mpuuzi gani akubali arahisihe sheria ili CCM Ikose nguvu? never ever..Hawa lazima wabanwe, maana tunaanza upya na hii ni nafasi ya mabadiliko ktk masuala ya kisiasa na kijamii tuachane na "desturi au taratibu" za kuvunja katiba na sheria za nchi.
Ndio maana nikasema kwa wakati huuRais anaweza wote. Akiwa weak the hayo mashinikizo yatamsumbua.
Ndani ya siku 14 hakuna Waziri Mkuu wala baraza la mawaziriKama nimeelewa vizuri kana kwamba kwa sasa hatuna Waziri Mkuu wala Baraza la Mawaziri! Naomba kusahihishwa tafadhali
Kabisa mkuu.. Kwa mjibu wa TLS basi hata wakuu wa mikoa wote watenguliwe maana si walikula kiapo mbele ya magu?Katiba haijatamka waziwazi kuhusu suala la baraza la mawaziri na kifo cha Rais aliyekuwepo madarakani.
We umezungumzia kiapo wanachoapa.Akiapa raisi mpya harithi kiapo cha aliyemtangulia.
Magufuli alipoapa November 2020, uwaziri mkuu wa Majaliwa ulikoma siku hiyo, hata yeye alisema, Japo alikuja kumteua tena kuendelea nae
Alichagua sura za watu wachache watete kidogo. Ukiangalia vyema utaona sura za watu wasio mawaziri, labda watakuwa makatibu wakuu.Bado sheria ina ombwe kidogo,je ni kweli mh Rais aliendesha kikao cha Baraza la mawaziri ambalo halipo au aliwachagua watu alioona washauriane?
naona unaanza kumfundisha kazi.. Sasa mh raisi.. Unadhani yeye na jiwe wanautofauti huyu yeye anafanya kimya kimya tofauti na aliepita aliekuwa anasemaa hadharani... Anaposema atailinda na kuisimamia katiba si katiba tu hata ba matakwa ya chama chake kibaki madarakani ni mpuuzi gani akubali arahisihe sheria ili CCM Ikose nguvu? never ever..
Iko hiviSawa, hiyo ni kuhusu waziri mkuu.
Lakini, ni wapi panapotamka hivyo kuhusu Rais aliyepo madarakani?
Yale yaa kikahongeren TLS kwa kutimiza wajibu wenu sasa ni muda wa wahusiku kufanya yaliyoshauriwa 👏
Yale ya kikatiba yatafuatwa lakini yale aliyochomekea ya kiuanaharakati hayatafuatwa. Nimeiona sauti ya Tundu Lisu kwake! Amerukia kueleza taratibu za kufuata kwenye janga hili la korona! Hilo si eneo lake! Amwachie waziri mwenye dhamana hiyo!Asante sana TLS.
Mmetupa mwongozo murua.
Hii ndio tunataka kuona inafanyika Tanzania. Wataalamu wa fani husika wawe mstari wa mbele na huru kutoa maoni, mapendekezo na ushauri kulingana na jambo husika linalotatiza nchi.
Kwa kifupi kabisa, kisheria kwa sasa hatuna waziri mkuu, hatuna baraza la mawaziri.
Sawa.Iko hivi
1.Raisi akila kiapo cha uraisi waziri mkuu anaacha kuwa waziri mkuu immediately-Rejea Magufuli alipoapishwa the second time, siku hiyo akamwambia PM kuwa siyo PM tena mpaka alipomwapisha tena some few days later (Kifungu kipo itafute kwenye katiba)
2.Na waziri mkuu akiacha kuwa waziri mkuu basi baraza la mawaziri linavunjika - rejea kujiuzulu kwa Lowasa kuliondoka na baraza lote la mawaziri, Kikwete alikuja kuliunda upya baada ya kumwapisha Pinda)
Kwa hiyo kuingia kwa Samia Suluhu Hassan, huyu ni Rais Mpya na kiapo kipya.