6 Pack
JF-Expert Member
- Apr 17, 2022
- 2,852
- 6,057
Niaje waungwana,
Kiukweli mimi sio mwanasiasa, wala mfuatiliaji wa mambo ya siasa hapa JF. Hivyo nimesukumwa tu na uzalendo wangu mwenyewe kuandika haya niliyoandika. Kwa kawaida nchi yetu ina mawaziri zaidi ya ishirini na manaibu wake (hapo sijazungumzia makatibu wakuu na manaibu). Kikawaida na kikatiba kila Waziri ana wizara yake, na lengo la kuteuliwa kwake ni kuisaidia nchi na wananchi kulingana na kanuni na muongozo wa wizara husika.
Sasa cha kushangaza Mawaziri wengi wamekuwa hawafanyi lolote la maana kuisaidia nchi wala wananchi. Unakuta nchi ina wizara mbalimbali, lakini yanayofanyika ndani ya nchi utafikiri labda Raisi bado hajaunda baraza la mawaziri. Wananchi wapo wanaona, bunge lipo linaona na raisi ambae ndio mkuu wa nchi yupo anaona lakini hakuna hatua yoyote anayochukua kuhusiana na uzembe wa baraza lake la mawaziri.
Ufisadi umetamalaki katika wizara nyingi, utendaji wa kazi wa mawaziri hao umekuwa mbovu, wa kusua sua na wa kukatisha tamaa wananchi, miradi mingi ya maendeleo inakwamishwa na wizara hizo, lakini mamlaka ya juu wote kimya wanaangalia tu mambo yanavyokwenda shagala bagala kama vile nchi haina raisi wala viongozi wanaoweza kutoa muongozo kwa mawaziri hao.
Sasa pamoja na uozo wote huo, tunashangaa raisi amekuwa akitumia uozo huo wa Mawaziri wake kuwaadhibu wakuu wa mikoa na wilaya. Hakuna siku tuliwahi kuona raisi anaadhibu mawaziri fulan kwa uzembe, ufujaji wa fedha za serikali, ufisadi nk. Kila siku yeye ana deal na wakuu wa mikoa na watendaji wengine wa chini ambao hawana tija yoyote katika nchi.
Kwangu mimi ukimtoa waziri Dkt Dorothy Gwajima, Silaa na Jafo yule wa enzi za "Tamisemi", waliobakia wote ni mizigo inayotafuna kodi zetu bila kufanya kazi yoyote ya maana katika ofisi zao.
Ushauri ni kwamba raisi asiwe busy tu kuangalia makosa ya wakuu wa mikoa na wilaya bali awe anafuatilia pia na yale yanayofanyika katika baraza lake la mawaziri lililojaa wachumia tumbo wengi uongozini.
Usiku mwema.