TLS: Kwa Mujibu wa Katiba, sasa Tanzania haina baraza la Mawaziri, Rais Samia atakiwa kuteua Waziri Mkuu ndani ya siku 14

Asante sana TLS.
Mmetupa mwongozo murua.
Hii ndio tunataka kuona inafanyika Tanzania. Wataalamu wa fani husika wawe mstari wa mbele na huru kutoa maoni, mapendekezo na ushauri kulingana na jambo husika linalotatiza nchi.

Kwa kifupi kabisa, kisheria kwa sasa hatuna waziri mkuu, hatuna baraza la mawaziri.
Na kama viapo haviamishiki makatibu wakuu wote waje wale viapo upya mbele ya mama samiha
 
Tanganyika Law Society muongozo wenu unanipa ukakasi Sana... Inamaanisha baada ya kifo Cha rais serikali yote inakoma?
Basi Makamu wa raisi aliendesha kikao Cha LEO Kimakosa maana aliendesha na Baraza ambalo limekwisha vunjika.
Nionavyo Mimi katiba yetu iliacha ombwe juu ya hii issue, ndio maana nchi nyingine wanaitisha uchaguzi ili kuunda serikali mpya.
Ninavyo sema hivi ninaona mbele yangu shida nyingi za kisheria, matharani uteuzi wa wabunge. Je wabunge walio ingia bungeni kwa tiketi ya raisi watatenguliwa ili Mama Samia akidhi takwa la kisheria la kuwa na nafasi 10?
TLs inaonaje hili ni awamu ya tano au awamu ya 6 ?
Karibuni kwa mtifuano
Ukijibiwa nijulishe mkuu!
 
Tanganyika Law Society wanasheria wa Ikulu Kama Ni wanachama wenu ninaomba wawe makini Sana kipindi hiki. Kitendo Cha kutangaza siku 14 za maombolezo kwa Tangazo la swali inaonesha muheshimiwa hakuandaliwa kabisa kisheria.
Aidha leo mama anapewa kalamu nyeusi, Ni tukio baya kisheria na kiusalama kwamba rais anatumia kalamu yoyote tuu mradi iwe eneo la tukio. Najua mnamaombolezo Ila tafadhari Jambo hili hatukulizoea na linaenda kutengeneza presedent lifanyike kwa umakini mkubwa mno!
 
17 Feb 2020
Samia Suluhu : "Napenda mawazo ya wapinzani, huwa wanajenga hoja vizuri, walini 'inspire' niingie siasa"

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amefunguka kuhusiana na historia ya maisha yake ambapo ameeleza siri ya mafanikio na chanzo kilichomvutia kuingia kwenye siasa. Samia Suluhu hoja za upinzani ni moto, walinivutia / inspire, mimi ni activist ...

Asanteni wanasheria!! sasa mmeanza kuitendea haki taaluma yenu, anashauri. kila mtaalamu aitendee haki taaluma yake, tuache unafiki tuliouanzisha to kipindi cha Magufuli.

Sent from my TECNO B1p using JamiiForums mobile app
 
Je vipi kuhusu Mwanasheria Mkuu wa Serikali?Na kwa nn leo kaitisha kikao cha Baraza la Mawaziri endapo baraza halina legitimacy?
 
Rais mwenyewe leo amekubali kuingia kwenye kikao cha baraza la mawaziri, na Rais huyo huyo mwanzo alitangaza siku 14 za maombolezo badala ya 21 zinazotambulika kisheria.

Hata wasaidizi wake nao wanaonekana bado wamelala, hawajui kama tupo kwenye utawala mwingine.
Well said!!!!!

Tunawaomba sana wasaidizi wa Mh. Rais mpya msituangushe. Maana inaonekana kama vile wamekuwa kama zoazoa vile, hawazijui protocol, yule mwingine badala ya kumletea Mh. Rais pen nyekundu analetewa nyeusi, hata yule mpambe wake alievaa nguo za kijeshi yule binti anatakiwa awe sharp asizibae maana nimeona wakati anaelekezwa na General Mabeo wakati President anakagua gwaride.

Chondechonde wasaidizi wa Mh. Rais msituangushe please!!!
 
Well, hiyo katiba inasema waziwazi kuwa endapo Rais aliyepo madarakani anaacha kuwa Rais kwa sababu yoyote ile, ikiwemo kifo, basi baraza la mawaziri nalo linavunjika?

Manake kama haisemi waziwazi, inaacha mwanya wa kutafsirika ki namna mbalimbali.

Mambo kama hayo inapaswa yatamkwe waziwazi na katiba pasipo kuacha mwanya au mianya ya tafsiri.
 
Well said comrade.

Ndio maana tunahitaji katiba mpya yenye clear-cut explanations haswa kwenye mambo nyeti kama haya
 
Nikweli kwa mujibu wa sheria kiapo hakiamishiki kutoka kwa MAGU kwenda kwa SAMIHA
Ushauri ni mzuri. Sitegemei kuona tena ukaidi kwenye jambo muhimu kama hili. Akikosea mwanzoni atakuwa ameshajijengea tabia ya kuendeleza ubabe. BTW siyo ''Samiha''.
 
Kwa maana hii kikao cha leo alichoobgoza mh rais samia ni batili, aache inaga katiba kama marehemu meko
 
Hongereni TLS.
Nahisi ndio maana mh Rais alisita kidogo kumtaja majaliwa kama waziri mkuu wa Tz wakati anatoa heshima zake kwa viongozi wengine kabla ya hotuba yake kwa wananchi.
Japo baadae alirudi kumtaja
 
Tanganyika Law Society wanasheria wa Ikulu Kama Ni wanachama wenu ninaomba wawe makini Sana kipindi hiki. Kitendo Cha kutangaza siku 14 za maombolezo kwa Tangazo la swali inaonesha muheshimiwa hakuandaliwa kabisa kisheria.
Aidha leo mama anapewa kalamu nyeusi, Ni tukio baya kisheria na kiusalama kwamba rais anatumia kalamu yoyote tuu mradi iwe eneo la tukio. Najua mnamaombolezo Ila tafadhari Jambo hili hatukulizoea na linaenda kutengeneza presedent lifanyike kwa umakini mkubwa mno!
Kutokuwa makini ni utamaduni wetu watanzania. Kuanzia kuandika mpaka kufanya kazi. Sijui tumefikaje hapa. Watu ni wazembe wa kupiliza. Unajua nini? ukishindwa kuzingatia mambo madogo madogo (basics) makubwa pia huwezi. Makosa kwenye maisha yapo lakini yakizidi mno inakuwa ni uzembe.
 
77 Reactions
Reply
Back
Top Bottom