TLS: Kwa Mujibu wa Katiba, sasa Tanzania haina baraza la Mawaziri, Rais Samia atakiwa kuteua Waziri Mkuu ndani ya siku 14

Asante TLS kwa kutoa ufafanuzi huu. Kama nimeelewa vizuri andiko hili, Ina maana kikao Cha leo alichoendesha Mh. Madame President na Baraza la mawaziri baada ya Kula kiapo Ni batili? Yaani null and Void. TLS please fafanua hili.
Hiki cha leo ni kama kikao cha kupiga stori tu maana as long as the PM is not legit basi hakuna baraza la mawaziri
 
Iko hivi
1.Raisi akila kiapo cha uraisi waziri mkuu anaacha kuwa waziri mkuu immediately-Rejea Magufuli alipoapishwa the second time, siku hiyo akamwambia PM kuwa siyo PM tena mpaka alipomwapisha tena some few days later (Kifungu kipo itafute kwenye katiba)

2.Na waziri mkuu akiacha kuwa waziri mkuu basi baraza la mawaziri linavunjika - rejea kujiuzulu kwa Lowasa kuliondoka na baraza lote la mawaziri, Kikwete alikuja kuliunda upya baada ya kumwapisha Pinda)

Kwa hiyo kuingia kwa Samia Suluhu Hassan, huyu ni Rais Mpya na kiapo kipya.

Ni kweli Kiongozi, narejea 16 Nov 2020 wakati Rais John Magufuli alipomuapisha Kassim Majaliwa baada ya yeye Magufuli kuapa kuwa Rais kwa kipindi cha pili baada ya matokeo ya Uchaguzi wa Oktoba 28, 2020

Raisi MAGUFULI akimuapisha KASIMU MAJALIWA kua waziri mkuu wa Tanzania 16 Nov 2020

 
Lakini, kwa mkutadha huu, nikwamba. Mawaziri wanapaswa kuapa kwa rais aliyeko madarakani! Sasa hawa waliapa kwa rais Magufuli!! hivi wakula kiapo cha utii kwa nani? si rais aliyeko madarakani.
Wanasheria wako sawa!!

Ndio maana wameambatanisha vifungu vingi. Kumbuka hata mwenyekiti wa tume ya uchanguzi, wakati anamtangaza Magufuli, alitumia vifungu zaidi ya kimoja kuharalisha hio mamlaka yake!!

Sent from my TECNO B1p using JamiiForums mobile app
 

16 Nov 2020

HOTUBA YA RAIS MAGUFULI BAADA YA KUMUAPISHA WAZIRI MKUU NA MAWAZIRI WATEULE

 
TLS kwa mara ya kwanza nimeona mmetekeleza wajibu wenu wa kisheria kwenye nchi hii. Mawaziri wote ikiwemo waziri Mkuu inabidi waambiwe, na wasiendelee kutokea kwenye nafasi zao kwani kwa sasa hakuna baraza la mawaziri. Nimemuona Majaliwa akiendelea kutambulishwa kama waziri Mkuu, wakati kikatiba hana uhalali huo. Tungekuwa na vyombo vya habari vinavyotekeleza wajibu wao walipaswa kulitangaza hili wazi wazi kuwa kwa sasa hakuna baraza la mawaziri, na waziri yoyote aliyekuwa kwenye baraza lililopita asiendelee kuingia ofisini au kutumia mali za ofisi kama gari nk, wakati hana uhalali huo.
Kwamaana hiyo basi mara baada ya Rais mpya kula kiapo Baraza la Mawaziri la zamani automaticaly linavunjika?? Kama ndivyo mbona mara baada ya Rais npya kula kiapo alikwenda kufanya kikao na Baraza la Mawaziri wa zamani?? Je kikao kile kilikuwa halali au batili??
 
Kwenye mazishi ya viongozi wa juu serikalini waziri mkuu ndiye mwenyekiti wa kamati ya mazishi katibu wake ndiye katibu wa mazishi wajumbe ni waziri wa fedha wa bara na visiwani na baadhi ya mawaziri, hivyo kama katiba haiwatambui kama mawaziri na katiba hiyohiyo inawapa hayo majukumu ya kushughulika na maziko basi kwa upande huo katiba inahitaji marekebisho.

Hiyo katiba ni so outdated hilo halina mjadala, hata hivyo kwenye hiyo katiba hao viongozi uliowataja wamepewa hayo majukumu kikatiba, au ni utaratibu umefanyika sasa kutokana na kutokufahamu katiba? kumbuka hapa hatuongelei viongozi wa juu, bali ni rais kufariki akiwa madarakani. Hao mawaziri watoke ofisini kwa mujibu wa katiba, ili wasimuwekee mama Kiwingu wakati wa kuunda baraza jipya la mawaziri. Kama ni kuingia kwenye hizo kamati za mazishi, waingie kama watu maalum na sio kama mawaziri.
 
Kwa maana hiyo hata hawa kina Pole pole walioteuliwa kuwa wabunge na rais Magufuli nao inatakiwa wasiwe wabunge tena?

Hapa hawa TLS inaonekana nao hawana wanachojua
Hawa TLS Wana ajenda yao!! Si uliona ameshaanza kutoa mwongozo wa kushughulika na corona wakati si eneo lake! Hawa ni majanga matupu. Watumie ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali kutoa mwongozo wa kikatiba kuhusu namna ya kuanza mama yetu kwenye hukumu la Urais. Hawa TLS ni wanaharakati!
 
Kwamaana hiyo basi mara baada ya Rais mpya kula kiapo Baraza la Mawaziri la zamani automaticaly linavunjika?? Kama ndivyo mbona mara baada ya Rais npya kula kiapo alikwenda kufanya kikao na Baraza la Mawaziri wa zamani?? Je kikao kile kilikuwa halali au batili??

Kikao kile kwa mujibu wa katiba ni batili, ifahamike hali hii ni mara ya kwanza kutokea kwenye nchi hii, na uzoefu unaonyesha watu wengi ikiwemo viongozi, huwa hawajui katiba inasemaje bali huendesha nchi kwa mazoea. Kumbuka hata rais Samia juzi alitangaza maombolezo ni siku 14, wakati kikatiba ni siku 21, na leo amerekebisha kosa lile.

Jambo baya kupita yote hata Muhimili wa mahakama haujui mambo haya, na huwa mahakama inasubiri viongozi waseme na wao ndio watekeleze. Kama jambo haliwauzi viongozi, basi mahakama hutekeleza kwa kufuata utashi wa viongozi.
 
16 Novemba 2020

Rais Magufuli: Cheo cha Waziri Mkuu hakina ‘uhakika’​

Majaliwa alikuwa Waziri Mkuu katika kipindi chote cha miaka mitano ya kwanza ya utawala wa Magufuli uliokamilika mwezi uliopita.

OFISI YA WAZIRI MKUU, TANZANIA: OFISI YA WAZIRI MKUU, TZ
Rais wa Tanzania John Magufuli hii leo tarehe 16 November 2020 amemuapisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa awamu ya pili na kumtahadharisha kuwa nafasi yake haina uhakika wa kuwa nayo kwa miaka mitano.

Rais Magufuli amemsifia Majaliwa akisema ni mchapakazi na muadilifu na anastahili nafasi hiyo, japo si sahihi kwa watu kuhesabu kuwa atasalia kwa kipindi chote cha miaka mitano ijayo.

“Baada tu ya kumchagua kuwa Waziri Mkuu naona kuna watu wanasherehekea na baadhi ya magazeti yanaandika kuwa atakuwa Waziri Mkuu kwa miaka 10. Hilo si sahihi.”

Rais Magufuli ameeleza kuwa ni Waziri Mkuu mmoja tu Fredrick Sumaye (1995-2005) ambaye amedumu katika wadhifa huo kwa miaka mitano na wengine wote walikaa kwa vipi fi vifupi zaidi.
Majaliwa alihudumu kama Waziri Mkuu katika miaka mitano ilopita ya awamu ya kwanza ya Magufuli.

''Guarantee (uhakika) pekee alokuwa nao (Majaliwa) ni wa miaka mitano ilopita. Miaka mitano ijayo linaweza kutokea lolote...Huo ndio ukweli. Kitu pekee kitakachomfanya abaki hapo ni utendaji kazi wake...Majaliwa ni mtendaji mzuri na ndio maana sikupata shida kumchagua tena,'' ameelezea rais Magufuli.

Kwa upande wake, baada ya kula kiapo katika ya Ikulu Chamwino, Waziri mkuu Majaliwa amesema:
''Namshukuru sana rais kwa kunipa nafasi tena, Mh. Rais utaunda Baraza la Mawaziri muda mfupi ujao jukumu langu ni kusimamia utendaji kazi wao, nitapita kila wizara na kuwataka waweke mpango kazi wa yale yaliyoanzishwa kwenye Ilani na kwenye hotuba yako''.

Bwana Majaliwa ameonesha atakayoyapa kipaumbele ikiwemo kupanda kwa bei ya saruji na kuahidi kulitafutia ufumbuzi suala hilo.

''Tulipokuwa kwenye kampeni, kumeibuka kupanda kwa bei ya saruji bila sababu ya msingi, hatutarajii saruji kuwa na bei kubwa...sasa naanza na hili la saruji'', amesema Bwana Majaliwa.
 
Kwa maana hiyo hata hawa kina Pole pole walioteuliwa kuwa wabunge na rais Magufuli nao inatakiwa wasiwe wabunge tena?

Hapa hawa TLS inaonekana nao hawana wanachojua

TLS hawajui sheria au katiba ni mbovu, wao TLS wameweka vifungu vya sheria ndani ya katiba, ww unawapinga kwa hisia za uzalendo uchwara na mifano irrelevant. Hao akina Polepole huo ubunge wameapa mbele ya rais au kwa spika? Siasa za kutegemea madaraka ya rais bila kufuata katiba ndio yanawatesa. Halafu mkiambiwa katiba ina mapungufu ifanyiwe mabadiliko, hamtaki mnaona mtatoka madarakani!
 
16 November 2020
Mh. Kassim Majaliwa Majaliwa akila kiapo mbele ya hayati Rais John Magufuli, alipoteuliwa tena kuwa waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mara ya pili. Hili ni takwa la kikatiba na kisheria waziri mkuu na mawaziri kula kiapo kwa Rais "aliyewateua" .

Mhe. KASSIM MAJALIWA AAPISHWA KUWA WAZIRI MKUU WA TANZANIA



1. Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) Kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

2. Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), kuwa Waziri wa Fedha na Mipango

3.Mhe. Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi(Mb), Kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
 
Back
Top Bottom