TLS: Kwa Mujibu wa Katiba, sasa Tanzania haina baraza la Mawaziri, Rais Samia atakiwa kuteua Waziri Mkuu ndani ya siku 14

Kutokuwa makini ni utamaduni wetu watanzania. Kuanzia kuandika mpaka kufanya kazi. Sijui tumefikaje hapa. Watu ni wazembe wa kupiliza. Unajua nini? ukishindwa kuzingatia mambo madogo madogo (basics) makubwa pia huwezi. Makosa kwenye maisha yapo lakini yakizidi mno inakuwa ni uzembe.
Katiba inasema endapo Rais aliyepo madarakani anakoma kuwa Rais basi na baraza la mawaziri nalo linavunjika papo hapo?
 
Well, hiyo katiba inasema waziwazi kuwa endapo Rais aliyepo madarakani anaacha kuwa Rais kwa sababu yoyote ile, ikiwemo kifo, basi baraza la mawaziri nalo linavunjika?

Manake kama haisemi waziwazi, inaacha mwanya wa kutafsirika ki namna mbalimbali.

Mambo kama hayo inapaswa yatamkwe waziwazi na katiba pasipo kuacha mwanya au mianya ya tafsiri.
Mkuu, kama Waziri mkuu akifariki baraza linavunjika itakua Rais?

Mama Samia ni Rais wa Awamu ya Sita haendelezi awamu ya 5, sasa kwanini aendeleze serikali ya awamu ya 5?
Ofcoz kama anataka kuendelea na baraza hilihili anapaswa kumteua tena Majaliwa na hao mawaziri upya.

Mbona kuna mantiki hapa bila ukakasi?
 
Ukishasema hii ni serikali ya awamu ya 6 ina maana kuna mabadiliko ya serikali uliyoikuta. Ukirndeleza serikali ileile bila kuivunja inaonekana bado una kaimu Nafasi ya urais uliyemkuta.

Leo Samia amekaa na baraza la awamu ya 5 kama Makamu Rais na sio Rais.

Kama anawataka hawa warudi kwenye awamu yake, afanye uteuzi upya.

Sijui kama kuna wanasheria wanamsaidia...
Nchi za wenzetu, wanasheria washafungua kesi mahakamani kupata ufafanuzi
 
Mkuu, kama Waziri mkuu akifariki baraza linavunjika itakua Rais?

Mama Samia ni Rais wa Awamu ya Sita haendelezi awamu ya 5, sasa kwanini aendeleze serikali ya awamu ya 5?
Ofcoz kama anataka kuendelea na baraza hilihili anapaswa kumteua tena Majaliwa na hao mawaziri upya.

Mbona kuna mantiki hapa bila ukakasi?
Waziri mkuu ni jambo jingine. Katiba ikon clear kabisa kuwa waziri mkuu akiondoka/akiondolewa na baraza linavunjika. Hili la rais halina kifungu kama cha waziri mkuu. Ila nadhani ufafanuzi wa TLS uko sahihi.
 
Sawa kabisa mkuu hii iko very clear bila cheenga
 
Haisemi chochote. Ila ukisoma huo ufafanuzi TLCS una mashiko japo pengine kunaweza kuwa na njia nyingine ya kuelezea hii issue.
See!

Inapaswa iseme waziwazi. Hakuna ugumu wowote ule kuliweka hilo waziwazi.

Hakuna haja ya tafsiri wala miongozo kwenye mambo mepesi kama hayo.

Weka mambo waziwazi. Basi.

Hii katiba yetu sijui iliandikwa na nani tu? Ina mapungufu kibao.

Sasa hapo leo mtu anaweza kweli kumshutumu Mama Samia kuwa kavunja katiba?

Sidhani.
 
Waziri mkuu ni jambo jingine. Katiba ikon clear kabisa kuwa waziri mkuu akiondoka/akiondolewa na baraza linavunjika. Hili la rais halina kifungu kama cha waziri mkuu. Ila nadhani ufafanuzi wa TLS uko sahihi.
Wangeweka wazi na kuhusu Rais.
 
Shukrani sana TLS Kwa mwongozo huu.
Imani yetu rais ameapa kuilinda na kuitetea katiba yetu, naamini pia atakiishi kiapo chake, kama hakutakua na mashinikizo yalio juu ya uweza wake kwa wakati huu.
 
Kwa mujibu wa muongozo wa TLS upo sahihi, waziri mkuu na baraza lote la mawaziri wanatakiwa kuteuliwa na kula kiapo mbele ya rais (aliye wateua).

Hivyo kwa sasa hakuna cha PM, waziri wala naibu waziri yoyote yule.

Sent using Jamii Forums mobile app
Yaani kwa Sasa Majaliwa hatakuwa na usingizi mnono kama kawaida especially kama alikuwa anajiona na mkubwa kuliko Makamu.
 
See!

Inapaswa iseme waziwazi. Hakuna ugumu wowote ule kuliweka hilo waziwazi.

Hakuna haja ya tafsiri wala miongozo kwenye mambo mepesi kama hayo.

Weka mambo waziwazi. Basi.

Hii katiba yetu sijui iliandikwa na nani tu? Ina mapungufu kibao.

Sasa hapo leo mtu anaweza kweli kumshutumu Mama Samia kuwa kavunja katiba?

Sidhani.
Ni kweli. Pengine huyu mama atasikiliza kilio cha katiba mpya na uchaguzi ujao tutakuwa nayo. Mradi tu asikubali kusikiliza ''makombo ya Magufuli'' yaliyobaki. Na aanze kuifumua TISS yote. Ni aibu sana kumwacha rais kufa kwa covid wakati ishara zilikuwa wazi kabisa baada ya wasaidizi wake wa karibu kufa. Magufuli alikuwa mjeuri lakini ni nini kazi ya TISS?
 
Asante kwa waraka huu, umetufumbua macho mathalani kwamba kumbe kutakuwa ba Waziri Mkuu mpya au kuteuliwa tena upya. Nisichokipata sawasawa ni kwa nini Mhe Nshala anasema hii ni AMRI. Ni amri ya nani kampa nani? Mbona mlengwa hajatajwa kwenye Dear Sir, au kwa jina? Ni ushauri mzuri, no doubt about that, lakini AMRI? Si kuna Attorney General ni mwanasheria mkuu wa srkali, kwani hili halijui? Au tuseme kuna kipengele cha sheria kinawapa TLS madaraka ya kutoa amri kwa serkali? Historia ya hivi karibuni ya TLS, ya kukumbatia wasaliti kina tundulissu na fatmakarume, imepunguza sana imani ya Watanzania kwenye taasisi hii. It is good advise, hilo halina ubishi, lakini ushauri ni ushauri si amri. Lawyers are very expensive, akitoa ushauri wa bure kwa AMRI, who foots the invoice?
 
Lile siyo Baraza la Mawaziri. Ni kikao tu cha marafiki. Ndiyo maana kina Abbas alihudhuria wakati siyo wajumbe wa Baraza
Msigwa hakuongea ukweli mbele ya kadamnasi kuualifu imma kuwa muheshimiwa rais anakwenda kuendesha kikao Cha Baraza la mawaziri ikiwa hoja yako Ni kweli
 
Back
Top Bottom