Baraza la Mawaziri kukosa Mawaziri wenye exposure kuna mchango gani katika kukwamisha maendeleo endelevu Tanzania?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
876
4,101
Tofauti na George Mkuchika hakuna Waziri mwingine mzoefu wa mifumo na miundo ya serikali kisiasa na kiusalama.

Mawaziri waliobaki wote wanabase kwenye siasa wakati ambao hakuna nchi Duniani inakua kisiasa nchi zote uwekeza katika usalama kwa lengo la kuzaa maendeleo endelevu.

Serikali zote Duniani zimewekewa mifumo ya urasimu katika mambo yenye maslahi kwa umma. Tanzania mambo yote yenye maslahi kwa umma wameondoa urasimu. Matokeo yake kila jambo likishakuwa kwenye maono binafsi ya mwanasiasa halina room for critics badala yake wote mnapaswa kutekeleza.

Mfano; tumepangisha bandari kwa siri, tumeuza madini kwa siri, tumeuza gesi kwa siri, tumeuza Vitalu kwa siri, tunajenga kwa single source, tunaingia mikataba kwa siri......kila lenye maslahi kwa umma limevikwa usiri na hivyo kupelekea nia njema ya mmiliki wa wazo kukosa mikakati kinzani yakuliboresha

Haya yote ulyanatokana na kuwa na baraza la mawaziri ambalo nilakisiasa zaidi badala ya kuwa baraza lenye siasa, usalama na uchumi. Tumekosa watu wakimwambia Mhe. Rais hapo unapotea njia sahihi ni hii.

Mawaziri hawa wenye siasa pekee ndio wanashiriki kumtafuta Katibu Mkuu Kiongozi. Lakini pia wao ndio wanapendekeza wanataka nani awe katibu mkuu. Matokeo yake makatibu wakuu nao wamemezwa na siasa hivyo katibu wa baraza la Mawaziri ambaye ni Karibu Mkuu hapeleki mishale kinzani kwa wateule wake. Amebaki kuwa observer.

Hali hii ndiyo inapelekea ofisi ya karibu mkuu Kiongozi kustaafishwa kijana mdogo kwa maslahi ya umma bila kuwa na sababu yoyote kisha maamuzi hayo yanapelekea Mhe. Rais kuambiwa hapa hapana.

Kwa kuwa tuna baraza la mawaziri la kisiasa na makatibu wakuu waliomezwa na siasa; ni kawaida kabisa watu wa aina hii kufikia maamuzi yakutotekeleza maamuzi ya Mahakama na kumwona Mh. Jaji kama mtu asiye na uzalendo. Ni watu wa aina hii ambao watajieleza kupambana na Jaji badala ya kuimarisha mapengo yaliyoainishwa na hukumu ya leo dhidi ya DC mtumbuliwa.

Mwisho, nitoe mifano michache kuonyesha kwamba kama Taifa siasa ipo mbele kwenye baraza la Mawaziri kuliko uchumi na usalama.
Mara kadhaa tumesikia MH. Rais amekaa kwenye kikao cha baraza la Mawaziri. Lakini nani anaweza kuuambia umma Bazara lina msimamo gani dhidi ya
1. Mgawo wa Umeme
2. Changamoto ya kukosekana kwa sukari
3. Mrundikano wa meli bandarini
4. Uharibifu wa miundombinu uliopelekewa na mvua kubwa
5. Changamoto ya bima ya afya baada ya kutungwa kwa sera na sheria mpya
6. Wizi na ubadhirifu wa mali za umma
7. Kupotea kwa watu
8. Kupanda kwa dola na athari zake katika importation

Haya mambo yote na mengine hayakuwa foreseen kwenye mipango previously so hatutegemei kama nchi tusiwe na mikakati ya wazi. Lakini hadi sasa hakuna mikakati ya wazi kwa umma ya kukabiliana nayo.

Nchi za wenzetu katika hali hii lazima Mhe. Rais atamke kwa umma kupunguza matumizi yasiyo ya lazima. Lazima atamka adharani kubadili vipaombele, na lazima atamke adharani kwamba kwa haya na haya wananchi tuvumiliane hayapo ndani ya uwezo wangu tujikaze.

Kwetu katika mazingira haya wanasiasa wote wanazungumza lugha ya kwamba nchi haina changamoto. Tunajidanganya na hakuna waziri anapewa sifa kwa kuonyesha mambo yanakwenda. Mawaziri wanasifika kwa kuja na suluhu kwenye mambo magumu kama haya.

Nadhani niwakati sasa wa kutafuta wabobezi kwenye biashara na serikalini na kuwapeleka wakagombee tupate mawaziri sahihi wanaoweza kusimama nakusema uchaguzi umepita na sasa tunapaswa kuacha kumsikiliza Rais badala yake tuumize kichwa na kumshauri ipasavyo na kwa ufasaha kama kiapo kinachotaka.

Mhe. Rais makala hii naiweka mbele yako na mbele ya viongozi wa upinzani. Shawishini watu sahihi waingie majimboni kwa lengo la kupata washauri sahihi. Tukipata wabunge sahihi 95 kati ya 300+ tutaweza kuwachezesha tupate right ministers katika kila angle. Tujaribu

Wakipatikana watu sahihi hata Karibu Mwenezi wa Chama hatoweza kujigamba kwamba anaweza kumwondoa Waziri; akisema hivyo nikumwambia Rais hawajui mawaziri wake ambao ukaa nao kwenye baraza always..........siyo kauli nzuri kwa Mhe. Rais ila ina ukweli ndani yake kwa safu tuliyonayo sasa ya wabunge.
 
Tofauti na George Mkuchika hakuna Waziri mwingine mzoefu wa mifumo na miundo ya serikali kisiasa na kiusalama.

is hawajui mawaziri wake ambao ukaa nao kwenye baraza always..........siyo kauli nzuri kwa Mhe. Rais ila ina ukweli ndani yake kwa safu tuliyonayo sasa ya wabunge.
Word!
 
Tofauti na George Mkuchika hakuna Waziri mwingine mzoefu wa mifumo na miundo ya serikali kisiasa na kiusalama.

Mawaziri waliobaki wote wanabase kwenye siasa wakati ambao hakuna nchi Duniani inakua kisiasa nchi zote uwekeza
, Prof Mkenda
 
Tofauti na George Mkuchika hakuna Waziri mwingine mzoefu wa mifumo na miundo ya serikali kisiasa na kiusalama.

uliyonayo sasa ya wabunge.
Uwaziri ni cheo cha kisiasa, wizarani kichwa anatakiwa kuwa Katibu Mkuu.

Waziri anapewa ajenda tu na kuisukuma.

Mtu anayeendesha wizara ni Katibu Mkuu.

Frankly tuko obsessed sana na uongozi wa juu kuliko kuangalia chini.

Uongozi wa juu hata uwe mzuri vipi, hauwezi kufanya vizuri kama chini hakuna watu makini wanaotoa feedback nzuri, wanao challenge, wanaoelimisha, wanaofanya follow up.

Kwa sababu mawaziri ni wachache sana, hawana brainpower ya kumaliza matatizo mengi.

Huku chini kuanzia kwa wananchi mpaka wafanyakazi wa serikali ndio kuna mengi ya kuangaliwa. Ukiweka vizuri huku chini, huko juu hata ukiweka waziri boya nchi itaenda tu.

Tatizo ketu sisi tumeweka mfumo ambao uko top heavy.

Ndiyo maana tunategemea sana mawaziri na hata rais.
 
Tofauti na George Mkuchika hakuna Waziri mwingine mzoefu wa mifumo na miundo ya serikali kisiasa na kiusalama.

Mawaziri waliobaki wote wanabase kwenye siasa wakati ambao hakuna nchi Duniani inakua kisiasa nchi zote uwekeza katika usalama kwa lengo la kuzaa maendeleo endelevu.
the tones of ur article tells everything about the side which the mindset of urz belongs
 
Back
Top Bottom