Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 10,129
- 35,148
Asante sana TLS.Mnamo tarehe 19 Machi 2021, aliyekuwa Makamu wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, aliapishwa kuwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, kufuatia kifo cha Raisi Dr. John Pombe Joseph Magufuli. Kuapishwa kwake kunaibua suala la msingi la kikatiba juu ya kuendelea au kutoendelea kuwapo kwa Baraza la Mawaziri lililoteuliwa na Hayati Raisi John Magufuli...
Mmetupa mwongozo murua.
Hii ndio tunataka kuona inafanyika Tanzania. Wataalamu wa fani husika wawe mstari wa mbele na huru kutoa maoni, mapendekezo na ushauri kulingana na jambo husika linalotatiza nchi.
Kwa kifupi kabisa, kisheria kwa sasa hatuna waziri mkuu, hatuna baraza la mawaziri.