TLS: Kwa Mujibu wa Katiba, sasa Tanzania haina baraza la Mawaziri, Rais Samia atakiwa kuteua Waziri Mkuu ndani ya siku 14

Mfano mwiguli nchemba kahamishwa wizara.lakini kesho ataapa tena.kwanini asiendelee nakazi Bila kuapa?
Yule kabadilishwa wizara kwahiyo kwenye kiapo Kuna sehemu ambayo unataja nafasi utakakotumikia kwahiyo lazima aape maana alikuwa hajaapa Kama waziri wa fedha na mpango
 
Sawa mtaalam.samahani.
Pole kwa kukuita mjinga , Ila nilikuwa najua unajua kuwa waziri akihama wizara anaapa upya.
Hivyo mwigulu ni sahihi kuapa upya
Nimekuwekea mfano hapa chini, mahiga na kabudi walivyohalishwa wizara waliapa upya.
Screenshot_20210331-235932_1.jpg
 
Utaapa tu endepo utabadilishwa nafasi ya kiuongozi. Ila wanao salia na nafasi zao hawaapishwi upya. Mfano kuna wakuu wa wilaya, wakurugenzi, wakuu wa mikoa na vyeo vinavyo fanana na hivyo walirithi kutoka awamu zilizo tanguliwa na bado walitambulika kwa nafasi zao.

Ikiwa Waziri Mkuu atatakiwa kuapa basi teuzi zote za JPM kuanzia mawaziri, wakurugenzi, wanyeviti wa board na wote walioapa mbele yake wanavyeo batili.
 
Mnamo tarehe 19 Machi 2021, aliyekuwa Makamu wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, aliapishwa kuwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, kufuatia kifo cha Raisi Dr. John Pombe Joseph Magufuli. Kuapishwa kwake kunaibua suala la msingi la kikatiba juu ya kuendelea au kutoendelea kuwapo kwa Baraza la Mawaziri lililoteuliwa na Hayati Raisi John Magufuli.

Baraza la Uongozi la TLS, kwa kutambua wajibu wake wa kisheria chini ya Kifungu cha 4 cha Sheria ya Tanganyika Law Society Act Sura ya Namba 307 wa kutoa ushauri kwa Serikali, Bunge, Mahakama, na Umma linapenda kutoa mwongozo wa nini kinatakiwa kufanywa kutokana na tukio kubwa la kihistoria ya nchi yetu la kupata Raisi mpya baada ya Raisi wa nchi kufariki.

Katika kutoa Mwongozo huu Baraza la Uongozi lilijiuliza swali lifuatalo:

Je, Katiba inalazimisha au inamtaka Raisi aunde na aapishe Baraza la Mawaziri pindi anapotwaa madaraka baada ya Raisi kufariki?


Kujibu swali hili mtu analazimika apitie ibara mbali mbali za Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ya Mwaka 1977 kama ilivyorekebishwa ili kuweza kupata mtiririko wa kisheria na kimantiki. Ibara moja haitakiwi kusomwa peke yake bali moja baada ya nyingine ambazo zinawiana. Hivyo kanuni ya uwianishaji/ulinganishaji (harmonization) lazima itumike.

1. Kwa mujibu wa ibara ya 37(5) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania pindi Raisi:
a. anapofariki;au
b. kujiuzulu; au
c. kupoteza sifa za uchaguzi; au
d. kutomudu kazi zake kutokana na maradhi ya mwili; au
e. kushindwa kutekelezwa kazi na shughuli za uraisi;

basi Makamu wa Raisi ataapishwa na atakuwa Raisi kwa muda uliobaki wa kipindi cha miaka mitano.

2. Makamu wa Raisi hawi Raisi kutokana na kiapo chake cha kwanza alichoapa wakati anaapishwa kuwa Makamu wa Raisi bali pale anapoapishwa kutwaa madaraka baada ya kutokea kwa moja kati ya mambo matano yaliyoanishwa hapo juu.

3. Baada ya hapo Raisi mpya (aliyekuwa Makamu) ana jukumu la kumteua mtu mwingine baada ya kushauriana na chama chake kuwa Makamu. Mteule huyu lazima athibitishwe na Bunge kwa kura zisizopungua asilimia 50 ya wabunge wote wa Bunge hilo.

4. Makamu wa Raisi mteuliwa kwa mujibu wa Ibara ya 30(5) naye anatakiwa kuapishwa na Jaji Mkuu, kama ilivyo kwa Makamu wa Raisi aliyechaguliwa kuwa Makamu pamoja na Raisi wakati wa uchaguzi mkuu kwa mujibu wa ibara za 42(5) na 49; au aliyeteuliwa na kuthibitishwa kuwa Makamu wa Raisi kwa mujibu wa Ibara ya 50(4).

Baraza la Mawaziri

5. Sehemu ya Tatu ya Sura ya Pili ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania inazungumzia Baraza la Mawaziri. Ibara ya 51(2) inatamka ifuatavyo:

Mapema iwezekanavyo, na kwa vyovyote vile ndani ya siku kumi na nne, baada ya kushika madaraka yake, Rais atamteua Mbunge wa kuchaguliwa kutoka katika jimbo la uchaguzi anayetokana na chama cha siasa chenye wabunge wengi zaidi Bungeni au kama hakuna chama cha siasa chenye wabunge wengi zaidi, anayeelekea kuuungwa mkono na Wabunge walio wengi kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, naye hatashika madaraka hayo mpaka kwanza uteuzi wake uwe umethibitishwa na Bunge kwa azimio litakaloungwa mkono na wabunge walio wengi. (Mkazo umeongezwa)

Hivyo ni wazi kabisa kuwa Raisi wa nchi yetu awe wa kuchaguliwa ama wa kuapishwa kutokana na ibara ya 37(5) anatakiwa kumteua Waziri Mkuu ndani ya siku 14 baada ya yeye kuwa Raisi.


6. Ibara ya 51(1) ya Katiba inataka Waziri Mkuu aliyeteuliwa na Raisi kabla ya kushika madaraka yake kuapa mbele ya Raisi kiapo kilichowekwa na Bunge.

7. Aidha, Raisi baada ya kumteua Waziri Mkuu, na Waziri Mkuu huyo kuthibitishwa na Bunge na kumuapisha, ndipo anatakiwa kuteua mawaziri wengine na manaibu mawaziri kwa mujibu wa Ibara ya 55(1).

8. Ibara ya 56 ya Katiba inatamka:

Waziri au Naibu Waziri hatashika madaraka yake ila mpaka awe ameapa kwanza mbele ya Rais kiapo cha uaminifu na pia kiapo kingine chochote kinachohusika na utendaji wa kazi yake kitakachowekwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge. (Mkazo umeongezwa)

9. Ielew.eke kiapo hicho lazima kifanywe kwa Raisi aliyepo na si yule aliyeondoka madarakani kwani kiapo kwa Raisi mmoja hakimishwi kwa Raisi mwingine. Ndiyo maana hata aliyekuwa Waziri chini ya Raisi huyo huyo pindi akiteuliwa kuwa Waziri wa wizara nyingine tofauti na ile ya kwanza ni lazima aape upya.

10. Ibara ya 57(2) inazungumzia uwazi wa nafasi ya Waziri au Naibu Waziri kitu ambacho chaweza kutokea ikiwa mojawapo ya mambo yafuatayo:

a. Kujiuzulu au kufariki;
b. Kukoma kuwa mbunge;
c. Raisi atafuta uteuzi wake na kumuondoa kazini;
d. Akichaguliwa kuwa Spika;
e. Waziri Mkuu akijiuzulu au kiti cha Waziri Mkuu kikiwa wazi kwa sababu nyingine yoyote;
f. Unapowadia muda wa Raisi mteule kutwaa madaraka yake;
g. Iwapo Baraza la Maadili linatoa uamuzi wa yeye kukiuka maadili; (Mkazo umeongezwa)

11. Usomaji wa pamoja wa ibara ya 51(2) na ibara ya 57(2)(e) unatufanya tuseme, kwa kujiamini kabisa, kuwa mara tu baada ya Raisi kuapishwa kuwa Raisi anatakiwa kumteua Waziri Mkuu ndani ya siku 14 tokea kuwa kwake Raisi. Waziri Mkuu aliyepo wadhifani anahesabika kutokuwa Waziri Mkuu na hivyo Baraza la Mawaziri linakuwa limevunjika kutokana na Waziri Mkuu kutokuwepo “kwa sababu nyingine yoyote”. Sababu nyingine yoyote ni “kufariki kwa Raisi aliyemteua na kusimikwa Raisi mpya ambaye siye aliyemchagua.”

Baraza la Uongozi la TLS linaamini kuwa Mwongozo huu utaiwezesha nchi yetu kuweza kusonga mbele huku ikiwa imefuata kwa usahihi na uaminifu mkubwa misingi na matakwa ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania hivyo kuhakikisha kuwa Baraza la Mawaziri na uongozi wa nchi yetu una uhalali wa kikatiba na kisheria.



Umetolewa leo tarehe 19 Machi 2021 Jijini Dar es Salaam kwa Amri na Mamlaka ya Baraza la Uongozi la TLS.

Dkt. Rugemeleza A.K. Nshala

Raisi

[/CENTER]


Imagine unaandika yote haya kumbe UTUMBO MTUPU!!!!!
 
Back
Top Bottom