The Radar Scandal: Investigation & Progress

Wewe Kama Nani Unamchunguza Mamlaka Hayo Na Ruhusa Hiyo Nani Kakupa - Nani Mfadhili Wako ? Chadema ? Cuf ? Au Shirika La Transparency ?

Na wewe hebu tuondolee upuuzi wako hapa! Hivi moderators huyu jamaa mnamlealea wa nini? Naamini katika uhuru na kustahimiliana lakini kuna wengine wanachefua mno, mfano ni huyu jamaa anayejiita Shy!
 
Hii Ndio Tunataka Kusikia na naonesha Msisitizo.

Maana Nimeshaona Hapa Habari Za Mtoto Kula Kichwa Cha Mtoto Mwenzie Muhimbili Inaanza Kutaka Kufunika Hoja Tata Za Mafisadi Ikiwemo Ya Chenge Vijisenti Na Issue Ya Ticts Ambapo Watu Tunahoji Inakuwaje Kampuni Kuongezewa Mkataba Mpya Kabla Ya Mkataba Wa Awali Haujaisha?


Na ni nani aliyetunga clause ya kusema kwamba Nchi haitaruhusiwa kuingia Mkataba na Kampuni nyingine yeyote hadi pale idadi ya Makontena itakapozidi Laki 7 kwa maana Ticts itakuwa haina uwezo wa kumudu kazi hali ya kwamba kila mtu shahidi wa Mlindikano wa Makontena pale bandarini
 
Na wewe hebu tuondolee upuuzi wako hapa! Hivi moderators huyu jamaa mnamlealea wa nini? Naamini katika uhuru na kustahimiliana lakini kuna wengine wanachefua mno, mfano ni huyu jamaa anayejiita Shy!

Mhh,

Hii nilikuwa sijaiona. Mwl Kithuku naona nawewe huyu Shy amekusinya (kuchosha kwa kiswahili cha kenya) kabisaaaaa.
 
Wewe Kama Nani Unamchunguza Mamlaka Hayo Na Ruhusa Hiyo Nani Kakupa - Nani Mfadhili Wako ? Chadema ? Cuf ? Au Shirika La Transparency ?

mamlaka hiyo nimejipa mimi mwenyewe kama raia wa Tanzania.. do you have a problem with that..? I didn't think so.
 
acheni hizo jama! sasa mnalalamika nini tena?, waziri si kasema wanamchunguza? mbona mnalia lia, kuweni objective jamani siyo kuwa against kila move serikali inayofanya. tusiwe kama watoto wadogo ukiwa na njaaa unalia, ukilishwa chakula bado unalia. ala!

Kinacholiza watu ni historia...kila siku uchunguzi unafanyika..matokeo hatuoni..afu kama unakumbuka,mkubwa wa awamu ya tatu..bwana MKAaPAle alipewa orodha ndefu tu ya hawa jamaa..MAFISADI et al..akadai kwamba ataifanyia kazi...lakini mpaka anaondoka... kimya.. tulichoambulia ni kusikia kwamba wadau wake wa karibu sana..ndio wameipamba hiyo list kwa majina yao yenye umaarufu wa kutisha...hivyo basi kulalama huku ni reaction ya yale ambayo tumeyazoea na tunayatarajia...ila tunapoelekea si pabaya sana..kama wamefikia hatua ya kutema nyadhifa..basi huenda mambo yakabadilika pia...
 
Ni ikulu ipi inamsurubisha Mzee Chenge? ni ile pale Feli ama? hebu yale mabilioni ya EPA ndiyo tumenyamaza au? jamanisijui Tanzania inakuaje kweli watu wanajichukulia wanavyotaka wao, wanasahau kule kijijini watu wanakula mlo mmoja, daa!!!1

Hapa ni usnii tu hamna kitu, hawasemi anachunguzwa na nani, haya ndo yaleyale ya pesa za EPA zinazorudishwa na mizimu bila kuonekana, serikali kweli imeona watanzania hawana akili, hivi ni nani atamchunguza chenge Hosea, Manumba, RO, au Mwanasheria mkuu wa serikali?

Hapo sioni hata mmoja wa kufanya kazi hiyo, huku ni kuendelea kulindana, lakini wananchi sasa wameamka 2010 tutawauliza vijisenti vya chenge alivipata wapi?
 
Revealed:Vithlani to spill the beans on radar deal

-More heads expected to roll as radar agent seeks to avoid prosecution

THISDAY REPORTER
Dar es Salaam

CONTROVERSIAL radar agent Shailesh Vithlani is said to have cut a deal with British investigators to avoid criminal prosecution by spilling the beans on senior Tanzanian government officials who received illegal kickbacks to approve the dubious 2002 transaction.

THISDAY can now reveal that the fugitive businessman, wanted for multiple charges of perjury and lying to an investigating officer in Tanzania, has now offered to cooperate with UK detectives in exchange for his freedom.

According to well-informed sources, Vithlani - who initially denied receiving an illegal $12m (approx. 15bn/-) commission from the radar manufacturer BAE Systems � has notified investigators from Britain's Serious Fraud Office (SFO) that he is now willing to admit his guilt, in part to avoid criminal prosecution.

''It appears the SFO people have accepted Vithlani's offer to cut a deal, and he has since been fully cooperating with the ongoing investigation,'' the sources confirmed to THISDAY.

The agent of the 28 million pounds sterling (approx. 70bn/-) radar deal is believed to have used the illegal commission from BAE Systems to bribe a number of top Tanzanian politicians and senior officials in the third phase government of ex-president Benjamin Mkapa, and get them to approve the deal.

The sources say Vithlani, who grew up in Tanzania but holds a British passport, has agreed to break his silence on the deal in return for an amnesty from criminal prosecution and the possibility of serving a jail sentence.

It is understood that thanks to Vithlani's cooperation, SFO investigators were recently able to discover the offshore bank accounts belonging to former attorney general and cabinet minister Andrew Chenge.

There are allegations that at least $1m of the funds traced to Chenge's offshore bank accounts in Jersey, Britain originated from BAE Systems, the company that supplied the military radar system to the Tanzanian government through the controversial agent.

Although there is an international arrest warrant out for Vithlani, he is reported to be living quite comfortably in Switzerland while continuing to cooperate with the British investigators over the radar deal.

''The investigators are keen to get more information from him on illegal conduct by BAE Systems in connection with the transaction�including possible outright corruption,'' the sources told THISDAY.

They added: ''If Vithlani does go ahead and reveal all he knows about the radar transaction and all those who were involved in it, we could very well witness more high-profile casualties in government.''

Chenge was recently forced to resign as infrastructure development minister after being implicated in the radar deal, which was concluded during his tenure as the country's attorney general.

He was effectively the first 'casualty' of the ongoing investigation.

However, it is understood that with Vithlani's help, investigators are now expecting to expose the involvement in this particular corruption scandal of other prominent government officials from the Mkapa era.

According to THISDAY findings, the team of British and American lawyers hired by Chenge to defend him against the radar corruption allegations have already gone to some length to apportion blame on other government departments.

Maintaining that their client was not involved in the deal, the lawyers have hinted in writing that the then ministry for communications and transport and ministry for defence and national service were the chief promoters of the deal.
 
Serikali ya JK si inamtafuta Vithlani? Mwaka huu ni mwaka wa hasara kwa MAFISADI

Kwani walikuwa wanamtafuta kweli ama walikuwa wanafunika kombe ili mwanaharamu apite? Sasa naona SFO wataharibu dili lote la kufunika kombe na kila kitu kitaanikwa hadharani.

Mkapa ambaye alikuwa amegoma kuongea itafika mahali itabidi aseme tu. Hapa ndipo ambapo unaanza kujiuliza kwamba hivi PCCB, TIS na Polisi huwa wanafanya kazi gani? Yaani uchunguzi makini hauwezi kufanyika mpaka waje SFO kutusaidia? Aibu gani hii? Yaani UK ndiyo wana uchungu zaidi ya hela za walalahoi wa Tanzania kuliko watanzania wenyewe?

Ballali mpaka leo kimya na hakuna kinachoendelea. Sana sana wameishia kuwasimamisha wale wafanyakazi 5 wa BoT na huku aliyekuwa Gavana na ndiyo mwenye maamuzi ya mwisho akiwa ameacha anapumzika. Hapo kweli haki itatendeka? Kwa kuwa vyombo vya nje havitahusika utasikia wale staff wa BoT waliosimamishwa watafukuzwa kazi na huku mhusika mkuu akiwa huru na mabilioni yamepotea. Yote hayo yanafanyika ili kuficha uozo ulio kwenye serikali ya CCM ya awamu ya tatu, lakini this time lazima mambo yamwagwe hadharani maana nina uhakika SFO watakuja hard evidence na ndiyo maana mawakili wa Chenge wameishaanza kuwanyooshea vidole waliokuwa kwenye wizara zilizokuwa zinahusika kwa karibu na ununuzi wa radar.

Kila la Heri SFO labda mtatusaidia kufichua uozo wa serikali. Na hao wachache watakaopatikana labda nao watawataja wenzao waliohusika kwenye ma-deal mengine ya ununuzi wa ndege ya rais pamoja na 10% ya mambo mengineyo mengi zaidi!
 
Maintaining that their client was not involved in the deal, the lawyers have hinted in writing that the then ministry for communications and transport and ministry for defence and national service were the chief promoters of the deal.

Who are these two freaks? And what was their involvement? I think we need to involve the likes of SFO in BOT investigations. They appear to be good in turning the cards than the Manumba's and the TAKUKURUs.

Asha
 
GAZETI LA MWANANCHI JUMATANO APRIL 2008

-NI YULE WA MAREKANI

-ADAI ATALIPUA MABOMU YA WANASIASA NCHINI

-ASEMA YUKO TARAYARI KUMTETEA POPOTE DUNIANI

-IKULU YATHIBITISHA KUTOA KIBALI KUMCHUNGUZA



WAKILI ANAEMTETEA FISADI ALIEKUWA WAZIRI WA MIUNDO MBINU MHE A.CHENGE J.LWEISKY MADOSKY AMESEMA ANASUBIRI KWA HAMU MTEJA WAKE AFIKISHWE MAHAKAMANI,,MADORSKY AMBAE NI MARA YA KWANZA KUZUNGUMZA NA VYOMBO VYA HABARI KWA NJIA YA SIMU ALITAMBA MAHAKAMANI HUKO NDIKO KWENYE KILA KITU NA UONGO AU UKWELI UTABAINIKA
NIMEWASILIANA NA CHENGE AMENIPA MBINU ZOTE ZINAZOTUMIWA NA BAADHI YA WANASIASA KUMWANGAMIZA

TUNASUBIRI KWA HAMU SERIKALI AU TAASISI YOYOTE IMFIKISHE MAHAKAMANI NA MIMI NITATOA USHAHIDIAMBAO UTAITISHA DUNIA NZIMA...MMMHHH PATAMU HAPO,,

KAULI HIYO YA MADORSKY IMEKUJA SIKU MOJA BAADA YA WAZIRI WA UTAWALA BORA SOPHIA SIMBA KUELEZA UWEZEKANO WA CHENGE KUFIKISHWA MAHAKAMANI KAMA USHAIDI UTAPATIKANA

WAKILI HUYO AMEIDHIIRISHIA DUNIA KWAMBA YUKO TAYARI NA MPAMBANO WOWOTE NA KUONYA HATOMWACHA MTU WALA KUMWOGOPA HATA AKIWA MKUBWA KIASI GANI,,

HATA HIVYO ALIVYOULIZWA SWALA LA KIASI GANI ANALIPWA NA CHENGE ALISEMA SIWEZI KUMWAMBIA MTU INAWEZEKANA NAMFANYIA BURE AU ANANILIPA MABILLION AU PESA NDOGO SANA..KAZI IPO JIBU UNALO MSOMAJI..ALISEMA ANATUMAINI TUHUMA ZA CHENGE ZINA MKONO WA SIASA KUTOKANA NA BAADHI YA WATU KUMBAMBIKIZIA ALISEMA MTEJA WAKE WAKATI AKICHUNGUZWA ALIKUWA ANAJUA KILA KITU ..ALIPOULIZWA KWAMBA ANA HABARI MTEJA WAKE KUPEKULIWA ALISEMA HAKUNA ASICHOKIJUA ANA TAARIFA ZOTE NA HUWA ANAWASILIANA NA CHENGE KILA SIKU....

KWENU WAPENDA NCHI NA OLE WENU VIONGOZI MTAKAOTAJWA MTAMFWATA HUYO CHENGE KWA GHARAMA HATA KAMA AWE RAISI WA NCHI..KARIBU MADORSKY UTUFUMBUE MACHO WATANZANIA TUMEPIGWA NA BUTWAA KUMBE KUNA ZAIDI YA HAYO

KWENU WANANCHI
 
Afadhali Umfundishe Field Marshall Natumaini Hawa Ndio Waliokuwa Wakigombania Ukiranja Kila Kukichwa Na Wanakosa...msamehe Maana Namwona Hata Kwenye Mada Ya Said Kubenea Amekosa Cha Kuongea Matokeo Yake Wanamfedhehesha
Si Kosa Lake Kosa Inawezekana La Wazazi Wake ..pacha Na Chinga Huyu Tusijibishane Nae...shy Soma Ukiwa Na Hoja Jibu Hoja Na Si Vioja
 
Fieldmarshall Msameheni Mtu Kama Huyu Ndio Maana Kama Umesoma Habari Z
Saidi Kubenea Amechoka Na Hoja Analeta Vioja Si Kosa Lake
Ushauri Jibu Hoja Na Si Vioja
 
Si Kosa Lako Shy Rudi Kaatoe Hoja Kwa Kubenea
Field Marshall Tumsamehe Nenda Kasome Mada Ya Kubenenea
Uone Vioja Vyake .....soama Mada Ukishindwa Toa Hoja Na Si Vioja
 
Acha wafunuane. Uzuri wa shetani atakufichia siri wee lakini huwa lazima ifike mahala akuumbue. Sasa muda nafikiri umefika kwa hawa jamaa kuumbuliwa na shetani na huko CCM kutakuwa hakukaliki! Kwa mara ya kwanza anayeumia hapa sio nyasi, ni hayohayo matembo!
 
Ni wakati tunaousubiri maana hata kama JK atakataa kumshitaki tayari wananchi tumeshajua kuwa kama ushaidi upo na hawataki kumshitaki basi watakuwa wanaficha kitu ambacho watanzania tutakitafuta wenyewe.

Lakini vilevile mkumbuke hawa watu hawana chochote zaidi ya kutishia ili serikali isimpeleke mahakamani, statement ya kuishangaza dunia, ina maana kubwa inawezekana serikali yote ni wezi na wameifadhi pesa zao offshore accounts ambazo huyu mkuu anazijua, au anawatisha wasifikirie kumpeleka mteja wao mahakamani aendelee kura pesa ya wadanganyika vizuri.

Ujasiri wa JK sasa utajifunua ndani ya miaka hii miwili iliyobaki, hapo ndo ataamua kunyoa au kusuka, aachie kiti ndani ya miaka mitano au ateketeze mafisadi wamuumbue na yeye, maana naona hawa watu wanacofidance kubwa sana.
 
Back
Top Bottom