The Radar Scandal: Investigation & Progress

The Radar Scandal: Investigation & Progress

So if at any time one of our leaders is alleged that he/she has been involved with something deemed inapprop[riate or they failed to protect our Land, Constitution and National Interest, will the President issue a public clemency by stating "mwacheni Mzee wa Watu"?

Isn't that covering mabaya na rushwa kwa kutumia rungu la madaraka?

Why is JK defending Mkapa? Why not let Mkapa face the public and come out in clear?

Kama JK atafanya hivi, je atajisikiaje Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Tarafa wakianza kutumia nafasi yao "kuepusha" uchunguzi wa tuhuma kwa kusema "mwachieni huyo"?
 
Rev. Kishoka,
That's a good question!
Waandishi wetu wako wapi?
 
Rev,
You have asked a very fundamental question. Kwenye CCM kuna culture ya kulindana na ukichanganya na mchakato mzima wa kupatikana mgombea swali lako linakuwa na kina zaidi.
 
na hii nayo:

[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif][SIZE=+1]Obbo was right on BAE scandal[/SIZE][/FONT]
[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif][SIZE=-1]
[/SIZE][/FONT]
[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif][SIZE=-1]Charles Onyango-Obbo's article on the purchase of the BAE radar system by Tanzania (The EastAfrican, February 19-25) was spot on.[/SIZE][/FONT]
[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif][SIZE=-1]
[/SIZE][/FONT]
[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif][SIZE=-1]I heard the BAE Systems radar story break in 2001 as a major item on the BBC radio news in the morning. Clare Short was interviewed and she pulled no punches in her condemnation of BAE Systems and Barclays Bank. [/SIZE][/FONT]
[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif][SIZE=-1]
[/SIZE][/FONT]
[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif][SIZE=-1]In the early afternoon of the same day, I was in a taxi driving across London while listening to the BBC news and heard not a squeak about the scandal. Nothing. Not even Clare Short - never a shrinking violet - fulminating further about the outrageousness of the scandal. [/SIZE][/FONT]
[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif][SIZE=-1]
[/SIZE][/FONT]
[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif][SIZE=-1]It was obvious to me what had happened. A weighty individual - most probably Blair's chief Downing Street
[/SIZE][/FONT]
[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif][SIZE=-1]spin doctor, Alistair Campbell - had been on the phone and told Ms Short to shut up in no uncertain terms. The story died rapidly. [/SIZE][/FONT]
[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif][SIZE=-1]
[/SIZE][/FONT]
[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif][SIZE=-1]Six years later, life was breathed back into it because of yet another scandal involving BAE Systems. Blair ordered the termination of an investigation into allegations of corruption by people associated with BAE Systems in securing the largest ever arms deal in history: the Saudi Arabian Al-Yamamah project of the 1980s.[/SIZE][/FONT]
[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif][SIZE=-1]
[/SIZE][/FONT]
[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif][SIZE=-1]I am sure any right-thinking person will agree wholeheartedly with you, Charles. Corruption is all about scale. Paying $1,000 to a greedy black fellow in darkest Africa is beyond the pale. [/SIZE][/FONT]
[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif][SIZE=-1]
[/SIZE][/FONT]
[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif][SIZE=-1]Approving shady activities where billions of pounds are involved is just good business. After all, Britain needs to maintain its status as the world's fourth richest country.[/SIZE][/FONT]
[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif][SIZE=-1]
[/SIZE][/FONT]

[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif][SIZE=-1]Gitau G. [/SIZE][/FONT]
[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif][SIZE=-1]via e-mail[/SIZE][/FONT]

http://www.nationmedia.com/eastafrican/current/Opinion/opinion2602074.htm
 
Vituko vya rada: Noti zamwagwa

2007-02-26 16:03:01
Na Mwandishi Wetu, Jijini


Wakati uchunguzi juu ya sakata la rada ya bei mbaya iliyonunuliwa na Serikali ya Tanzania kichwa-kichwa baada ya kupigwa `changa la macho`na Kampuni ya Uingereza ya BAE System ukiendelea huko ughaibuni, sakata hilo hapa Bongo limeibuka maajabu mapya!

Mfanyabiashara mmoja maarufu hapa nchini amemwaga mapesa kibao na kutangaza rasmi namna Watanzania wanavyoweza kuyachangamkia.

Mfanyabiashara huyo, Bw. Jaffar Sabodo ametangaza dau la Sh. 100,000 kwa watu 10 wa kwanza watakaochangia vizuri hoja juu ya ununuzi wa rada.

Mfanyabiashara huyo ametangaza dau hilo kupitia kwenye vyombo vya habari.

`Watu 10 watakaochangia hoja hii vizuri watazawadiwa kila mmoja Sh. 100,000,` ikasema sehemu ya taarifa ya mfanyabiashara huyo.

Ukitaka kuibuka na pesa hizo, taarifa hiyo ikasema, unachotakiwa kufanya ni kuandika hoja yako ambayo hata hivyo hakuna masharti ya urefu na kuituma kwa M.R.J Sabodo wa S.L.P 730, Dar es Salaam.

Sakata hilo la rada lilipamba moto baada ya kuibuka madai kuwa rushwa ilitumika katika uuzaji na ununuzi huo.

Sakata hilo lilipamba moto baada ya watu mbalimbali kushupaa wakitaka hatua zichuliwe dhidi ya wajanja waliolamba `cha juu� katika uuzaji wa rada hiyo.

Mwezi uliopita, Rais Jakaya Kikwete alikaririwa akisema Tanzania itafarijika iwapo pesa za ziada zilizoongezwa kwenye bei halali ya rada hiyo zitarejeshwa.

SOURCE: Alasiri

Hii issue inazidi kunishangaza...nasindwa kusahau ile story ya MAZINGAOMBWE aliyotuletea MKJJ hapa....hebu niambieni huyu bwana nia yake nini?? Au ni hoja zipi anazonizungumzia yeye ambazo bado mpaka leo hajazisikia???

Hizo hoja zielekezwe kwenye kuilaumu serikali, kuunga mkono au kupinga manunuzi ya rada, kuilaumu BAE, uk governments au hoja ziwe na malengo gani?? Most of all akishapata hizo hoja yeye atazifanyia nini..kama nani???

Tafadhalini naomba tuchangie kidogo background ya huyu bwana maana ninavyojua mimi ni mtazania bilionea zaidi ya hayo simjui...!! Anaweza kweli kuwa na solusion ya uozo huu uliotokea hapa??

Naomba kutoa hoja.
 
Mengi tutasikia kuanzia wana mtandao kuongoza mikutano ywa JK wakiwa Dar na yeye ugenini hadi wafadhili wa wanamtandao kutaka kuficha ukweli .Poleni sis Wadanganyika .
 
Mwambie aje achukue bure hoja Jamboforums. Na yeye ni msanii tu na anataka kutuonyesha mazingaombwe yake
 
Hiyo habari imeandikwa kifupi mno...ni vizuri huyo mwandishi aende tena shule ya uandishi.
 
Huyo bwana, Mhindi mzawa, hudai kuwa mpenzi mkubwa wa Mwalimu na wakati mwingine huiumbua serikali. Amewahi kuwakemea Wahindi wenziwe kwa ubaguzi hapa nchini. Kwa kiasi amekuwa akijipambanua kuwa mzalendo. Anamiliki, pamoja na mali nyingine, Dar Cinema, ambayo imo ndani ya eneo aliloliita Nyerere Art Gallery, hapo Mwenge. Kwa heshima ya Nyerere alijenga sanamu ya Nyerere hapo hapo Nyerere Art Gallery, lakini mjenzi akamkosea (akashindwa kumpatia) Nyerere na hivyo wakaamua kuifunika sanamu ile. Ni yeye aliyetoa zawadi nyingi, kama si zote (magari, matrekta nk), kwa ajili ya bahati nasibu ya Mwalimu Nyerere Foundation kama njia ya kuusaidia mfuko.

Alianzisha programu ya kuwafadhili wanafunzi kwa elimu ya juu Tanzania na India. Amekuwa pia akihamasisha uandishi wa insha mbalimbali ikiwa ni pamoja na zile za kuhusu Mwalimu na mambo mengine ya kitaifa kama jinsi ya kupambana na rushwa na huwazawadia washindi maelfu ya pesa.

Ukimsikiliza utaona ni mkereketwa wa nchi yetu. Huyo ndiye Sabodo.
 
Ila Jamani mbona huyo Mramba hajadiliwi.Wakati counterpart wake Brown akiihurumia Tanzania kuhusu ununuzi wa Rada yeye alitetea hadi akawatukana watanzania.Je,hana hoja ya kujibu sasa?
 
Yasema si mali ya serikali

KAMPUNI ya BAE Systems ya Uingereza iliyoiuzia rada Tanzania, haimilikiwi na serikali ya nchi hiyo, ubalozi wa Uingereza mjini Dar es Salaam umesema.
Taarifa iliyotolewa jana na ubalozi huo, na kutiwa saini na ofisa wake wa habari, John Bradshaw, inaikana kampuni hiyo, ambayo awali ilielezwa kuwa inamilikiwa na serikali ya Uingereza.
"BAE Systems si kwa ujumla wake au kwa sehemu, haimilikiwi na serikali ya Malkia, na si wakala wa serikali. BAE Systems ni 'taasisi ya umma' ambako serikali haina maslahi ya kifedha au katika uongozi wake," taarifa hiyo ilisema.
Hata hivyo, ubalozi huo umesema ili kulinda usalama wa taifa hilo kutokana na kampuni hiyo kutengeneza na kuiuzia Uingereza silaha muhimu za kijeshi kwa ulinzi wa nchi, serikali inamiliki hisa 'maalum' tu.
Ilisema hisa hizo 'maalum' zinaiwezesha serikali kuwa na udhibiti wa watu wanaoteuliwa kuwa wajumbe wa Bodi wasiokuwa raia wa Uingereza, na kuweka kiwango cha watu - mmoja mmoja au vikundi vya wasiokuwa raia wa nchi hiyo - kutomiliki zaidi ya asilimia 15 ya hisa za kampuni hiyo.
Taarifa hiyo ilisema ubalozi huo umelazimika kutoa ufafanuzi huo kufuatia taarifa zilizoandikwa katika vyombo vya habari vya hapa nchini hivi karibuni, kwamba kampuni hiyo iliyoiuzia rada Tanzania, inamilikiwa na serikali ya Uingereza.
Ununuzi wa rada hiyo umezua utata mkubwa, ikidaiwa kuwa wakala aliyesimamia ununuzi wake alizidisha bei kwa mabilioni ya shilingi, hali ambayo imezua dhana kuwa kuna harufu ya rushwa katika ununuzi wa mtambo huo.
Kutokana na hilo, kitengo cha uchunguzi wa hujuma mbaya cha serikali ya Uingereza, kimeanzisha uchunguzi dhidi ya kampuni hiyo ili kubaini ukweli kama ilitapeli katika uuzaji wa rada hiyo.
Kufuatia kuibuka kwa utata huo, Rais Jakaya Kikwete, alipokuwa ziarani nchini Uingereza hivi karibuni, alikaririwa akisema katika mahojiano kuwa anavyojua BAE Systems ni kampuni ya serikali ya Uingereza, na ikithibitika kuwa imeitapeli Tanzania katika uuzaji huo wa rada, serikali ya Tanzania itaomba kurejeshewa fedha zake zilizozidi.
 
Ni UONGO MTUPU. Hakutegemea itagunduliwa.Alifikiri wote ni illiterate na wajinga.Simple as that;and dont look for scape goats in his staff.Wonder if he is abreast with todays world of the internet or he is also one of those who is proud to say he is BBC ie BORN BEFORE COMPUTERS.
 
Wanabodi,
Haikuhitaji balozi wa Uingereza kusema ndipo watu waamini hili. BAE ipo ktk soko na investment zake zinajieleza wazi unless watu bado wanafikiria neno Public company ni mali ya serikali... Hii lugha lini itaondoka kwa wajamaa?..
Tembelea site yao utaona kuwa kampuni hii imejipanua hadi Marekani na kuna watu kibao Marekani wamenunua hisa.
 
Mkandara, ilinichukua siku moja tu kuonesha kuwa alichosema Muungwana si kweli. Labda kwa vile wameandika "Uhuru" watatilia maanani. Ila sitashangaa akienda mahali pengine na akarudia maneno hayo hayo walisema "sikio la kufa..."
 
Habari za leo Ndugu wana Forum, Leo nimekuja na hii habari kutoka gazeti la wapinzani wetu kuhusu bwana Lipumba katika hili sakata la rada. Japokuwa linawasema viongozi wangu vibaya lakini duh!! THATS THE TRUTH

Lipumba afichua siri mpya ya rada


74162.jpg

Ibrahim Lipumba

Kutoka gazeti la 'wapinzani wetu' Tanzania Daima,
na Asha Bani


SIKU chache, baada ya Rais Jakaya Kikwete kumkingia kifua Rais mstaafu Benjamin Mkapa, kwa kuwataka Watanzania waache kumhusisha katika sakata la ununuzi wa rada, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, ameibuka na tuhuma nzito dhidi ya serikali.

Lipumba, mmoja wa viongozi wa mwanzo kabisa wa kisiasa kuonya kuhusu kashfa hiyo ya rada iliyoligharimu taifa dola za Marekani bilioni 40, aliilaumu serikali kwa kumficha mhusika mkuu wa sakata hilo, ambalo katika miezi ya hivi karibuni limezusha mjadala mkali ndani ya Bunge la Uingereza na miongoni mwa Watanzania wadadisi.

Akizungumza na waandishi wa habari, ofisini kwake Buguruni, Dar es Salaam, Lipumba bila ya kumtaja kwa jina, alisema mhusika mkuu aliyeliingiza taifa katika kashfa hiyo ya rushwa ni kijana Mtanzania anayeishi nchini Uingereza, akiwa na pasi ya nchi hiyo hiyo.

Lipumba alieleza kushangazwa kwake na hatua hiyo ya serikali kufumbia macho ukweli huo, na kumwacha Mtanzania huyo aliyesema ndiye aliyevuna pato liliso halali linalofikia dola bilioni 12.

Alisema, uchunguzi uliofanywa na makachero wa Uingereza, umebaini kuwa aliyekula rushwa ya dola za Marekani mil. 12 kutokana na ununuzi wa rada hiyo, ni kijana wa Kitanzania na viongozi wa serikali wanamfahamu, lakini wameamua kufumba macho na wala hawataki kulijadili suala hilo.

“Serikali inamjua kijana aliyefanya udanganyifu huo wa kula rushwa, ni kijana wa Kitanzania mwenye kitambulisho cha uraia wa Uingereza. Wananyamaza, hawataki kumtaja ili achukuliwe hatua. Hii inaonyesha kuwa, Tanzania ni nchi iliyojaa rushwa,” alisema Prof. Lipumba.

Alisema hivi sasa Uingereza inamchunguza mtu huyo aliyeshirikiana na maofisa wa Kampuni ya BAE System waliouzia Tanzania rada hiyo kwa njia za rushwa.

Mwanasiasa huyo, aliyepata kuwa mshauri wa kiuchumi wa Rais wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi na Rais Yoweri Museveni wa Uganda, alisema jeuri ya viongozi ndiyo iliyosababisha wakatae kusikiliza ushauri aliotoa mapema mwaka 2000 na 2001 kuhusu ununuzi huo wa rada.

Alisema mwaka 2000, serikali ilipoamua kununua rada hiyo, alimwandikia barua Rais mstaafu Benjamin Mkapa na aliyekuwa Waziri Mkuu wake, Frederick Sumaye, akiwatahadharisha kuhusu uamuzi huo.

Lipumba alisema, pamoja na nakala ya barua hiyo kuiwasilisha kwa aliyekuwa Spika wa Bunge wakati huo, Pius Msekwa, bado serikali iliendelea na mipango yake ya kununua rada hiyo, ambayo sasa imegeuka na kuwa kashfa ya kimataifa.

Alisema katika barua yake hiyo, alieleza wazi msimamo wake na wa chama cha CUF, kupinga uamuzi wa kununua rada kwa bei kubwa ya dola bil. 40 za Kimarekani wakati nchi ikiwa katika lindi zito la umaskini.

Prof. Lipumba alisema mwaka 2002 aliandika barua nyingine kwa Mkapa na nakala akaipeleka tena kwa Sumaye, akiionya serikali kuhusu suala hilo hilo, na akaonya kuhusu kuwapo kwa vitendo vya rushwa katika ununuzi wake.

“Nilishangaa kuona Tanzania, kama nchi ‘chepe kama Abunuasi’, lakini imepata wapi uwezo wa kununua rada ya dola bilioni 40?” alihoji Prof. Lipumba.

Alisema pamoja na Serikali ya Mkapa kupuuza ushauri wake, hakuishia hapo, na hivi karibuni tena, wakati wa kikao cha Bunge kilichomalizika, aliandika barua ya tatu kwa wabunge wa chama chake na akampelekea nakala Spika Samuel Sitta, akiwataka waliwasilishe suala hilo bungeni.

Hata hivyo, kwa sababu ambazo hakuzitaja, barua yake hiyo pia iliwekwa kapuni, na Bunge likamaliza kikao chake bila ya ajenda hiyo kujadiliwa.

Alisema, Serikali ya Tanzania inapaswa kulaumiwa kwa kulea rushwa, na ili ijisafishe, ni lazima ichukue hatua dhidi ya kijana huyo wa Kitanzania, ambaye alichukua rushwa.

Akizungumzia hali ya uchumi wa taifa, Prof. Lipumba alisema, inazidi kuwa ngumu na mfumuko wa bei unazidi kuongezeka.

Alisema, mfumuko wa bei kwa bidhaa muhimu unaathiri kwa kiwango kikubwa maisha ya Watanzania, yanayoendelea kuwa magumu kiasi cha kuwafanya wazeeke zaidi wakati muda wa kuzeeka bado.

Alisema, bei ya mafuta nchini inazidi kupanda, bei ya bidhaa mbalimbali zinapanda pia wakati serikali iliahidi kupunguza bei ya mafuta.

Katika soko la dunia, alisema bei ya mafuta imepungua kutoka dola 75 hadi 60, lakini katika nchi ya Tanzania bei ya mafuta bado iko juu.

Prof. Lipumba alisema, wakulima wanapatwa na wakati mgumu kutokana na bei za bidhaa zao kuwa chini na kuwafanya kunyonyeka, huku serikali ikishindwa kuwatetea.

“Wakulima wa korosho walitangaziwa na serikali kuzidishiwa bei ya kilo ya korosho kutoka sh 300 hadi 600, lakini kwa sasa hali inazidi kuwa ngumu kwao, kwa kuwa wanauza korosho hizo kwa kilo sh 200 hadi 300 ambapo kwa mkulima anakuwa amekandamizwa,” alisema Prof. Lipumba.

Alisema, utafiti alioufanya amegundua wakulima wengi wa korosho wamezirundika korosho zao ndani wakisubiri bei mpya kutangazwa.

Prof. Lipumba, alisema kampuni za madini nyingi nchini zimeingia katika kutapeli uchumi wa Tanzania kutokana na kupata faida kubwa, lakini serikali haipati faida yeyote.

Akizungumzia suala la uchaguzi wa Jimbo la Tunduru, alisema chama chake kiko katika mazingira mazuri ya kushinda, hasa baada ya mgombea wake kuungwa mkono hata na baadhi ya wanachama wa chama tawala, CCM.
 
na hawa nao wachekeshaji.. yaani wanaogopa kumtaja mtu jina.. mbona hilo tulishalisema sisi huko nyuma na kuwaambia aliyefanya siyo Mtanzania ni Mwingereza.. Ukichukua uraia wa nchi nyingine unaupoteza uraia wetu.. Lipumba naye angejua hilo!!
 
kama asemavyo FD

hizo ndizo siasa................, nina hakika Prof analifahamu hili wazi kabisa!!
 
na hawa nao wachekeshaji.. yaani wanaogopa kumtaja mtu jina.. mbona hilo tulishalisema sisi huko nyuma na kuwaambia aliyefanya siyo Mtanzania ni Mwingereza.. Ukichukua uraia wa nchi nyingine unaupoteza uraia wetu.. Lipumba naye angejua hilo!!

Ni kweli lakini unasaba unabaki pale pale.Na huyu jamaa atatambulika kama Muingereza mwenye asili ya Tanzania.
 
Kampuni iliyoiuzia Tanzania rada yabwagwa mahakamani

*Yadaiwa kuwafanyia ujasusi wanaoifuatilia
*Yapewa wiki 2 itoe jina la anayewaibia siri

KAMPUNI ya British Aerospace (BAE Systems) inayoendelea kuchunguzwa kwa tuhuma kadhaa za kutumia rushwa kupata mikataba sehemu mbalimbali duniani ikiwemo sakata la ununuzi wa rada hapa nchini, imebainika kuwa sasa inatumia 'mchezo mchafu' kuwanyamazisha wanaoifuatilia.

Kampuni hiyo imehusishwa na matumizi ya ujasusi dhidi ya taasisi au watu wanaoonekana kufuatilia kwa karibu tuhuma za rushwa zinazoikabili.

Hali hiyo imebainika kufuatia taasisi moja ya mjini London inayojihusisha na kampeni dhidi ya Biashara ya Silaha (CAAT) Kubaini kuwa maofisa wa BAE walipata taarifa za siri za asasi hiyo iliyokuwa ikijiandaa kufungua kesi kuhoji uhalali wa Waziri Mkuu wa Uingereza, Bw. Tony Blair kusimamisha uchunguzi wa kashfa ya BAE nchini Saudi Arabia.

Mwenendo huo mpya wa BAE umevishtua hata vyombo mbalimbali vya habari nchini Uingereza vinavyoripoti zaidi kashfa za ununuzi wa silaha na rada.

BAE wamekutwa na taarifa ya barua pepe inayohusu mawasiliano kati ya CAAT na mawakili wao kuhusu mbinu za kufungua kesi kuhoji mwenendo wa Serikali ya Blair inayoonekana kuiunga mkono kampuni hiyo ya silaha.

Kutokana na hali hiyo juzi, Jumatatu, Mahakama Kuu ya Uingereza ililazimika kutoa hukumu ya kwanza na ya kihistoria kuhusiana na masuala ya rada, rushwa na siasa, kwa kuibwaga BAE, kitendo kilichopokewa kama mwanzo mwema na wanaharakati wa masuala ya rushwa.

Kwa mujibu wa mtandao wa Forbes, katika hukumu hiyo iliyotolewa na Jaji King, BAE imepata pigo la kwanza katika harakati zake za kujisafisha na tuhuma za rushwa kwa kuamuriwa itoe hadharani jina la mtu aliyewapatia barua pepe inayoonesha mawasiliano binafsi katika ya CAAT na wakili wao.

" Jaji King ameipa BAE hadi Machi 12 mwaka huu ikabidhi maelezo yote na jina la mtu aliyewapatia barua pepe," ilinaeleza Forbes kuhusu hukumu hiyo.

Jaji alieleza kuwa barua pepe ambayo BAE walikutwa nayo, ilikuwa na taarifa ambazo zinakinga ya usiri ya kisheria na ilikuwa ikihusu masuala ya malipo na mbinu za kufungua kesi ambapo CAAT ingehoji uamuzi wa Taasisi ya Kuchunguza Makosa ya Ulaghai (SFO) wa kupokea maagizo serikalini na kusimamisha uchunguzi wa rushwa katika mauzo ya silaha kwa Serikali ya Saudia.

Hukumu hiyo pia imesisitiza kuwa BAE lazima wanajua waliipataje barua pepe hiyo ya watu ambao ni wapinzani wao kiutendaji, hivyo lazima watoe maelezo ya kina kuhusu hilo.

Wakili wa CAAT, Dinah Rose, alisisitiza kuwa kuhujumiwa kwa mawasiliano hayo na kuwafikia BAE katika mazingira ya kutatanisha, kumeibua hisia kuwa sasa majasusi wameanza kutumiwa kuzifuatafuata taasisi zinazopinga vitendo vya BAE.

" Kuna ushahidi mzito kuwa BAE imekuwa ikitumia majasusi kuifuatilia CAAT na imekuwa ikitumia pauni 120,000 kwa mwaka kwa kazi hiyo," alisema wakili huyo.

Katika hatua nyingine, imeelezwa kuwa wakati sakata la BAE na uuzaji wa silaha nchini Saudi Arabia likiendelea kuibua tafrani, SFO imekuwa ikiendelea na uchunguzi katika kashfa nyingine ikiwemo ya mawakala nchini Tanzania kulipwa kiasi cha sh. bilioni 12, kufanikisha uuzwaji wa rada ambayo hata hivyo imekuwa ikielezwa kuwa ni ya kizamani.

Rais Jakaya Kikwete tayari amekwishaweka msimamo wake bayana kuwa atalazimika kupeleka maombi rasmi kudai fedha iliyozidi iwapo itaonekana ununuzi wa rada uliofanyika mwaka 2001, uliongezewa 'cha juu.'

Pia Taasisi ya Kuzuia Rushwa hapa nchini (TAKURU) nayo imepewa jukumu la kuchunguza kama kuna maafisa wa hapa waliopokea rushwa kuchagiza ununuzi wa rada hiyo.

Kumekuwa na hisia kwamba kutokana na urafiki wa kidiplomasia ulioimarika hivi karibuni kati ya Tanzania na Uingereza, upo uwezekano wa uchunguzi huo nao kusimamishwa kama ilivyotokea Saudi Arabia.

Bw. Blair aliwahi kubanwa kwenye Bunge la Makabwela lakini akakwepa kujibu swali la kama anaweza kuzuia uchunguzi kuhusu rada ya Tanzania au la.

Hoja kama hiyo iliibuka tena kwenye Bunge la Mamwinyi lakini nako Waziri wa sasa wa Maendeleo ya Kimataifa wa Uingereza, Bw. Hilary Benn alikataa kuzungumzia kwa kina akiwaambia wabunge; " Masuala hayo yako chini ya uchunguzi wa SFO."
 
Back
Top Bottom